Nusu siku ndani ya jeneza

Nusu siku ndani ya jeneza

KAMA MNAKOSA MADA ZA KUPOSTI HAPA ACHENI SIKU NZIMA JAMVI LIPITE BILA MADA YOYOTE! Au Hamjaoa? Mada hii ni nzito zaidi ya mnavyofikiria! KATIKA MAISHA YA HAPO NYUMA NIMEBIKIRI WABINTI 5 songea 1, Kg 2 moro 1 na Geita 1, mke niliye naye akiwa wa sita (6) na wa mwisho kubikiri! Nasema kuwa mada hii siyo nzuri kwa kuwa wapo watu wengi wana wake ambao tayari walibikiriwa na watu wengine! na pia watu tunatofautiana katika kukabili matatizo! Hivyo hata leo mnaweza sababisha migogoro kwenye miji ya watu wengi kwa namna ninavyo fahamu wanaume wengi tulivyo na wivu! Aidha kwa wale wote ambao mmeoa wake waliobikiriwa na watu wengine! Waamini wake zenu si lazima amvulie huyo aliyembikiri na usiwe na haja ya kumwuliza nani kambikiri! Unaweza hangaisha kichwa chako bure! Mfano binti niliyembikiri Songea Lizaboni 2007 mwaka 2010 nilikutana naye akiwa bado hajaolewa lakini nilipomweleza juu ya hayo alikataa kata kata! Na huyu alikuwa bado hajaolewa je, akiolewa? Hata wa Morogoro nimekutana naye Tabora kwenye semina lakini kakataa! HIVYO HAPANA UKWELI HAPA LABDA MWANAMKE MWENYEWE AWE MUHUNI TU NA SI KIGEZO KUWA ULIMTOA BIKIRA!
NARUDIA TENA JAMANI MADA ZINAZO WEZA KUVUNJA USTAWI WA JAMII SIYO NZURI KUZIPOSTI HAPA!
HAKUNA KITU KINACHO KONDESHA KAMA KUKOSA AMANI KATIKA NGAZI YA FAMILIA NA ZAIDI KTK UWANJA HUU WA MAPENZI! AU HAMJAOA! FIKIRIA UNAPO POSTI MADA KWANZA KAMA NI YA KUJENGA! Isiwe kama kuna mtu unamlenga hapa! Unamdhihaki labda kaoa demu wako?

Thenkyuu!
 
NUSU SIKU NDANI YA JENEZA - 5-

ILIPOISHIA :
Wapo waliokuwa na mapembe mawili kwenye pande mbili za vichwa, pia kuna wengine walikuwa na pembe moja tu juu ya mapaji ya uso, hivyo kuonekana kama yule mnyama aitwaye faru.
Kusema ule ukweli walitisha sana, kama mmoja wao ningebahatika kukutana naye barabarani tena tukiwa wawili lazima hali ya hewa ingebadilika, kama si mimi kuanguka na kufa basi ningekimbia nikipiga kelele sana.
“Una swali?” yule kiumbe wangu aliniuliza.
“Mengi sana.”
“Uliza sasa.”
SASA ENDELEA…

“
Sasa hawa ni akina nani?”
“Hawa ndiyo wale ambao nyinyi duniani mnawaita mashetani na kuwachora vibaya.”
“Sasa uhakika ni upi? Nyinyi ni wabaya au si wabaya?”
“Kwanza kabla sijakujibu naomba nikwambie kwamba muda umekwenda sana, kule duniani wameanza kushughulikia jeneza lako mapema sana.”
Nilishtuka sana kusikia habari hizo, kwamba jeneza langu limeshaandaliwa kabisa.
“Ndani kuna maiti?”
“Hakuna, maiti wewe upo hospitali.”
“Ni hospitali gani wamenipeleka?”
“Mwananyamala.”
“Halafu huku niliko?”
“Huku hakuhusiani na kule.”
“Ina maana kule wanaendelea na kuomboleza?”
“Tena wanalia sana kama ulivyokwishaona muda ule.”
Nilisikia uchungu sana.
“Sasa nikujibu, watoto waliozaliwa na uzao wa binadamu na malaika ndiyo hawa wenye maumbo ya kutisha.”
“Kwani kuna malaika na binadamu walizaa?”
“Hujawahi kusoma?”
“Popote pale?”
“Sijawahi.”
“Ni hivi, kuna wakati ulimwengu wenu ulikuwa na wanawake warembo sana, siku moja malaika walishuka wakawaona, wakawaingilia wale wanawake nao wakapata mimba na kuzaa.
“Wale watoto kwa wakati ule walikuwa na maumbo tofauti, wengi walikuwa warefu, wakubwa sana, wana maumbo ya kutisha.
“Wakati wa gharika la Nuhu, wale malaika walitaka kurudi kwa Mungu lakini walishindwa wakaishia kusikojulikana ndiyo hao vizazi vyao sasa.”
“Na malaika wanawake waliondoka na watoto wao waliowazaa na wanaume wa duniani?”
“Hakuna malaika wanawake.”
Aliposema hakuna malaika wanawake nikasimama vizuri, nikamwangalia kwa kumkazia macho na kugundua kuwa, yule kiumbe hakuwa anajua mambo kwa undani, asingeweza kusema vile. Nikamuuliza:
“Kwa nini hakuna malaika wanawake wakati sisi kule duniani mpaka matangazo, nyimbo za wanamuziki, maboksi ya sabuni yanaonesha kuna malaika wanawake?”
“Jiulizeni nyinyi binadamu, mmepata wapi hizo habari kwamba kuna malaika wanawake.”
Nilijikanyaga mwenyewe, nikashindwa kuthibitisha kwamba kuna malaika wanawake, lakini nikakumbuka wimbo wa Nakupenda Malaika ulioimbwa na wanamuziki mbalimbali wakiwemo Bony M.
“Labda nikwambie kwamba malaika wote ni wanaume. Kwenye vitabu vyenu mliandika kuna Malaika Gabriel, huyu kazi yake ilikuwa kupeleka habari kutoka kwa Mungu kwenda sehemu nyingine.
“Kuna Malaika Michael, huyu ni jemedari wa vita, alikuwa akipigana na maadui wa Mungu. Si ndiyo?”
“Ndiyo,” nilimjibu, akaendelea.
“Kama unakumbuka wakati wa Lutu, Sodoma na Gomora, malaika wa Mungu walipotumwa kwenda kwake, wale wakazi wa pale walimwambia wanataka kuwaingilia kimwili.”
Hapohapo nilipata cha kumuuliza.
“Sasa kama hakuna malaika wanawake hao wakazi wa Sodoma na Gomora walitaka kuwaingilia akina nani?”
“Hujasoma sifa mbaya ya Miji ya Sodoma na Gomora ilikuwa ya ulawiti?”
Nilitingisha kichwa kukubaliana naye kwani ni kweli nilisikia dhambi kubwa ya miji ile ilikuwa ni wanaume kuingiliana wenyewe kwa wenyewe licha ya kuonywa mara kwa mara na viongozi wa kidini.
Nilianza kumwamini yule kiumbe kwamba anajua mengi kuhusu ulimwengu na asili zake, nikamuuliza.
“Sasa wale malaika walioshindwa kwenda peponi walikwenda wapi?”
Kabla ya kunijibu alinisahihisha kwa kusema:
“Kwanza kabisa napenda kukwambia awali hao malaika hawakutoka peponi bali mbinguni.”
Nilimshangaa sana, nikamuuliza:
“Kwani kuna tofauti kati ya peponi na mbinguni?”
“Ipo kubwa tu.”
“Ipi hiyo?”
“Mbinguni ndiko kwenye makazi ya Mungu, peponi ni makazi ya watu wema.”
“Sijawahi kusikia hilo, lakini nimeamini sasa.”
Basi, sikuwa na maswali tena, nikaanza kuwaona wale viumbe wakihangaika huku na kule wakitweta kama vile wana jasho jingi kwa kazi kubwa waliyoifanya, hali zao zilikuwa za kutisha.
Niliweza kuwaona wakitoa meno marefu kiasi cha kuweza kuzidi urefu wa mkono wa binadamu, wengine masikio yao makubwa yalipita zaidi vichwani, ungeweza kusema wamejifunga miavuli vichwani mwao.
Karibu wote weusi wao ulifanana sana na wa jongoo, lakini meno yao yalikuwa meupe sana tena sana. Niliwaona wawili wakitembea, walikuwa kama watu wanene sana kwamba wanashindwa kutembea sawasawa kutokana na unene.
Baada ya hapo kiumbe alinishika mkono na kunipeleka sehemu nyingine bila kuniambia ni wapi na kuna nini, ikabidi mimi nimuulize.
“Huku tunakokwenda sasa ni wapi?”
“Utapajua tu tukifika.”
“Ni kama hapa tulipotoka?”
“Usiwe na haraka sana.”


Itaendelea .......
 
Mbn kimya kaka MziziMkavu mi natumia fursa nasubiri umalizie nshachukua pesa advance bongo muvi km mtunzi wa hadithi hii,hapa nulizwa napeleka saa ngapi script zilizobakia
 
Last edited by a moderator:
Kichwa kime knock natamani niuforwad muda ila ndio sina ubavu. U have drawn my full tention kaka.
 
NUSU SIKU NDANI YA JENEZA -6-


ILIPOISHIA:“Sasa kuna tofauti gani kati ya kule na hapa?” nilihoji huku najikinga na moto. Yule kiumbe aliniangalia kwa macho ya dharau kisha akaniuliza.

“Hakuna ila umbali tuliotembea ni mrefu sana. Lengo langu nataka kukuonesha ni namna gani watu wanaokuja motoni ni wengi sana kuliko wanaokwenda peponi.”

Alinitoa hapo haraka sana na kuniingiza kwenye chumba kikubwa sana ambapo kuna skrini kubwa sana, kuna majina ya watu yanapita toka upande mmoja kwenda mwingine.

SASA ENDELEA…

Hali ilikuwa hivi. Kila jina lilikamilika kwa maana ya kisheria. Yaani majina matatu, nilimuuliza yule kiumbe ndiyo akaniambia hivyo kwamba katika utawala wa sheria kila binadamu anatambulika kwa majina matatu.
Alisema: Duniani mnaishi kama mko gizani, mtu anaweza kushitakiwa kwa majina mawili lakini kusema kweli kiroho binadamu anatambulika kwa majina matatu. Kama unaitwa Hassan Juma lazima useme na jina la kati, mfano Hassan Juma Maulidi.
“Ndiyo maana kule kwenu Tanzania watu wa Zanzibar hutumia majina matatumatatu. Mfano mwingine ni kwenye kadi za kupigia kura au vitambulisho vya uraia, lazima yawe matatu.”
Basi, yalipita majina matatu yakiwa yameandikwa; Musa Soja Muambo, tarehe aliyokufa, aliyozikwa. Halafu yakatokea maelezo yake sasa. Yaliandikwa hivi:
Tarehe 25/12/1978 ulilewa, ukamchukua mwanamke wa mtu na kwenda kuzini naye huku na wewe una mke. Tarehe 12/2/1979, asubuhi uliingia ndani ya hoteli, ukaiba mkoba wa mzee mmoja anaitwa Sefu Rashid Mauzuliuzuli, alivaa kanzu.
Yalipita majina kama saba yakitoa maelezo mbalimbali halafu kila jina lilipopita likafuatiwa na picha za video zenye tukio zima mwanzo mwisho tena zinazoonekana kama vile unamwona mtu halisi maana skrini yenyewe ni kubwa sana.
“Una swali?” aliniuliza.
“Mengi sana.”
“Uliza.”
“Ile ni video?”
“Ndiyo.”
“Huku mna kamera za video?”
“Huku hatuna ila zinakotoka na sisi tunapata.”
“Wapi?”
“Unajua kwa Mungu ndiyo kwenye kila kitu cha maarifa. Unapoona ndege zinapaa, magari yanatembea, viwanda vinatengeneza kila kitu ni maarifa kutoka kwa Mungu na si kwingine.”
“Sasa ina maana kule duniani mtu akifanya dhambi anapigwa picha za video?”

“Si video tu hata picha za kawaida.”
“Lakini mpigaji haonekani?”
“Huwezi kumwona kwa sababu kwa Mungu kila kitu kiko wazi. Wewe huwezi kujifungia ndani ya nyumba halafu ukategemea unachokifanya Mungu hakuoni, si kweli.”
“Sasa hawa marehemu wanayajua haya matendo yao?”
“Mimi nikitaka sasa hivi naweza kukuonesha wewe video zako zote ambazo ulifanya dhambi.”
“Sasa anayepiga ni Mungu au?”
“Mungu anapiga lakini sisi tunaambulia kwa ajili ya kuweka ushahidi.”
“Mimi nina swali.”
“Uliza.”
“Lakini liko mbali na haya mambo ya hapa.”
“We uliza tu.”
“Mfano mtu kama Musa, alikwenda wapi baada ya kufa?”
“Aaa, mbona hata kwenye maandiko yenu duniani imeandikwa kwamba alikwenda mahali pazuri.”
“Si nasikia alimkera Mungu akiwa na wale watu wa Israel jangwani?”
“Kosa lake alilitubu. Kwani nyiye wanadamu mkitubu hamsamehewi?”
“Hivi huwa tunasamehewa?”
“Lazima, ila mnakosea sana namna ya kutubu. Wengi wanaamini dhambi ndogo hazimsumbui Mungu, si kweli. Mungu anasumbuka na dhambi zenu hata ikiwa ya kumwangalia mwenzako vibaya.
“Kinachomsumbua Mungu ni kwamba yeye ndiye aliyesema usiseme uongo lakini pia akasema usiibe na usizini. Nyinyi wanadamu mnadhani kusema uongo ni dhambi ndogo sana kuliko kuzini, mmesahau kwamba aliyesema usiseme uongo ndiye aliyesema usizini.”
“Loo! Kweli wewe unajua mambo mengi.”
“Sisi huku tunajua mambo mengi sana lakini hatuna uwezo au nafasi ya kutubu, kosa letu lilikuwa kubwa na lilishatolewa adhabu ya moja kwa moja, hakuna tena kujirudi.”
“Ina maana hata mkiomba msamaha?”
“Sisi hatuna mawasiliano tena na Mungu, nyinyi mnayo. Sisi Mungu alishaacha kutuangalia toka miaka na miaka na miaka. Tunawaonea wivu nyinyi ndiyo maana tunahakikisha kila siku tunawavuna kwa dhambi.”
“Mmepewa nafasi ya kwenda peponi bure lakini sisi huku tunawashangaa sana mnapotumia fedha kwenda motoni.”
“Kivipi?”
“Ukienda kanisani au ukiishi maisha ya kumpendeza Mungu kuna gharama gani?”
“Hakuna.”
“Sasa nyinyi wanadamu mnaenda kwenye muziki, mnatoa fedha kununua pombe, mnahonga wanawake, mnakodi teksi kwenda gesti, mkifika gesti mnatoa tena fedha kuchukua vyumba, vyote hivyo ni dhambi. Ndiyo manaa nasema mnatumia fedha kununua motoni wakati mnaweza kwenda peponi bure.”
Wakati anaendelea kunisimulia kwenye skrini palitokea jina na matendo halafu picha, akasema:
“Yule ni Kaini kaka wa Abel wa Adam.”
“Ha! Naye yuko huku?”
“Asingeweza kukwepa kwa sababu Kaini ndiye binadamu wa kwanza kuua tangu kuumbwa kwa ulimwengu.”
“Tena umenikumbusha, kule duniani kuna maneno kwamba Adam na Eva ndiyo watu wa kwanza kuishi bustanini duniani, si ndiyo?”
“Nyinyi ndiyo mnasema Adam na Eva ndiyo watu wa kwanza lakini sisi tunajua Adam ndiye mtu wa kwanza na si Eva.”


Ili kujua zaidi usikose kusoma baadae.....
 
Bonge la story... Kila wakati nachungulia thread kuona kama umeshaunga!
 
Mungu wangu! Eti Charty, hicho alichoandika KIRANGWA kimeingiaje kwenye thread hii?
I'm:A S-confused1:
Haloo, hata mimi kaniacha kabisa. Na sidhani kama mimi ni mbumbumbu kiasi hicho! Itakuwa haihusiani tu!!!
 
Mungu wangu! Eti Charty, hicho alichoandika KIRANGWA kimeingiaje kwenye thread hii?
I'm:A S-confused1:
Mkuu Alichoandika mkuu.@KIRANGWA sijamuelewa huyu mkuu.@Charty kuweka Comment ya mkuu KIRANGWA kwenye hii Thread yangu? Watu wengine kazi yao kuharibu Thread za wenziwao hiyo ndio kazi yao sijuwi wanachangia kitu gani kwenye hii Thread yangu? Sijawaelewa kabisa hawa watu.
 
NUSU SIKU NDANI YA JENEZA -7-

ILIPOISHIA :
“Eva hajatolewa au hajaumbwa, mbona unakosea sasa?”
“Eva hakuumbwa, Adam ndiyo aliumbwa. Mwanamke alitokana na mwanaume na si kweli kwamba mwanaume alitokana na mwanamke.”
“Ha! Eva hakuumbwa, kivipi sasa?”

SASA ENDELEA…
“
Hilo ni tatizo kubwa sana mlilonalo wanadamu, sisi huku siku zote tunajifunza na kujua maandiko yenu lakini nyinyi wenyewe hamko hivyo ni kwa nini lakini?
“Eva hakuumbwa, Mungu alisema na tuumbe mtu kwa mfano wetu, akamuumba Adam. Alipomaliza akampa uhai akwa bnadamu hai, kwa mfano wake. Lakini baada ya hapo Mungu alimuona Adam yuko peke yake akamlaza usingizi akachomoa mbavu moja ya kushoto akaifanya kuwa mwanamke, ndiye Eva.”
“He! Kwa hiyo Eva alitokana na mbavu ya Adamu?”
“Tena ya kushoto. Kwa sababu hiyo ndiyo maana wanadamu wote upande wa kushoto hamna nguvu kwa sababu mbavu moja ilichomolewa.”
“Tena kwa kukuongezea sasa sisi huku tunavyojua mwanamke si mtu bali ni kiumbe ndiyo maana pepo wachafu wanapenda kukaa kwako na kuwatesa kuliko wanaume.”
“Hapo una maana gani?”
“Maana yangu ni kwamba kutokana na udhaifu wao kama viumbe na si binadamu wanawake wanateswa sana na pepo wachafu. Nikuulize swali moja na wewe?”
“Kama nitaweza kulijibu.”
“Ukiwa duniani umewahi kwenda kwenye mikutano ya kiimani hasa ya watu wanaodai wameokoka?”
“Ndiyo nimewahi mara nyingi sana.”
“Hujajiuliza ni kwa nini wanawake ndiyo wanaanguka sana?”
Aliposema hivyo nikaanza kupata picha kwamba madai yake ni ya kweli kabisa, kwenye mikutano ya dini hasa ya walokole wanawake wengi hupiga mwereka na kuweweseka.
“Hivi ni kwa nini?” nilimuuliza kwa sauti yenye ujasiri nusu.
“Kwa sababu wao ni viumbe tu. Ndani ya matumbo yao sehemu ya uzazi huwa wanaishi mapepo ambao huwa wanawatesa kwa mambo mbalimbali. Kama una swali jingine uliza kabla hatujaondoka hapa.”
“Swali ninalo, ina maana sisi tunafanana na Mungu?”
“Kwa sehemu kubwa sana. Kasoro fikra na uwezo mwingine. Ndiyo maana maandiko yenu yanasema; upumbavu wa Mungu unapita hekima ya mwanadamu.”
“Sasa kama sisi ni sawa na Mungu kwa nini wengine maisha yetu si mazuri wengine mazuri?”
Nilimwona yule kiumbe akiachia tabasamu huku akiniangalia kama vile ananionea huruma. Akasema:
“Unajua binadamu mmepewa uwezo mkubwa sana lakini hamuutumii?”
“Kivipi? Mbona mimi sina uwezo mkubwa kama wengine?”
“Hujui kutumia neno.”
“Kwani uwezo huo upo kwenye neno?”
“Sana. Mungu alitumia neno kuumba, si ndiyo?”
“Ndiyo, hata mimi nilisikia hivyo.”
“Na nyinyi wanadamu mmeumbwa kwa mfano wake, si ndiyo?”
“Kwa ulivyosema ni kweli tuliumbwa kwa mfano wake.”
“Sasa mnashindwa nini kulifanya jambo lolote liwe kwa kutumia neno wakati mliumbwa kwa mfano wake?”
Nilijikuta najishika kichwa na kujikuna nywele kama vile nilikuwa sijamuelewa vizuri.
Kimsingi nilimwelewa kwamba kwa sababu sisi wanadamu tuliumbwa kwa mfano wa Mungu na yeye aliumba ulimwengu kwa neno basi na sisi tuna uwezo wa kufanya jambo liwe au lisiwe kwa neno.
Akaendelea:
“Wazazi wengi huko kwenu duniani wanayafanya maisha kuwa magumu au marahisi kwa maneno yao bila wao kujua. Ukiumwa, ukasema mwaka huu siwezi kupona kwa sababu ya ugonjwa huu kweli hutapona kwa sababu umekiumba kifo kwa neno.
“Sisi huku tunawaonea wivu sana nyinyi, mna uwezo mkubwa lakini hamjuia kuutumia. Utakuta mzazi anamwambia mwanae wewe akili zako wewe hata darasani utafeli. Kweli atafeli, maana mzazi ameumba kufeli kwa neno. Lakini matokeo yake mtoto akifeli kweli mzazi huyo huyo anasema mi si nilisema! Lakini si kwamba alisema bali aliumba kwa neno.”
Nilijishika kichwa na kukumbuka kuna siku moja niliwahi kusingizia kazini kwamba ninaumwa, sitakwenda. Baada ya wiki mbili nikaumwa kweli, nikamweleza yule kiumbe kuhusu hilo, akasema:
“Ndiyo inavyokuwa. Wapo wanadamu wanaporomoka kiuchumi kwa sababu ya kusema tu. Mfano, mtu anafanikiwa katika maisha, ana miradi au kazi nzuri, analipwa mshahara mzuri, unamtosha kuishi vizuri, amepata bahati amenunua gari, akikutana na mtu anayefahamiana naye na kumwambia hongera naona mambo yako yanakwenda vizuri utamsikia akasema mazuri wapi, tunahangaika tu.
“Haya maneno ni mabaya sana, lazima utahangaika kweli kwa sababu umeyatoa kinywani mwako.
“Twende huku sasa.”
Alinishika mkono mpaka kwenye jumba moja ambalo ndani tulikuta vyumba vingi, kila chumba kilikuwa na viumbe kama yeye, tuliingia kila chumba tulipotoka tukaenda kwenye chumba kingine hadi tukamaliza vyumba vyote kumi na moja. Tukarudi katikati ya chumba na kukaa kwenye viti ambavyo vilipangwa vitatu.
“Una swali lolote?” aliniuliza.
“Haliwezi kukosa.”
“Uliza.”
Niliangalia vile vyumba kwa zamu nikizungusha shingo hadi chumba cha mwisho. Katika kila chumba kulikuwa na alama mlangoni. Alama zenyewe zilikuwa kama si mbuzi, kondoo, kama si kondoo ng’ombe, mpaka wanyama wa porini pia walikuwepo kwenye kila mlango.
“Nauliza sasa.”
“Uliza.”
“Hivi ni kwa nini kwenye kila mlango kuna alama ya mnyama fulani?”
“Kila chumba chenye alama ya mnyama fulani ndani yake kuna wanaowasimimamia wanadamu kulingana na tabia za wanyama fulani. Mfano, kile chumba cha kondoo, ndani yake kuna wanaoshughulikia wanadamu wenye tabia ya kondooo.
“Unajua iko hivi, kila binadamu aliyezaliwa ana tabia inayofanana na mnyama mmoja aliyopo duniani.”
“Ha! Kweli?” nilishtuka sana.


Ili kujua zaidi usikose kusoma kesho jioni.....
 
Mkuu Alichoandika mkuu.@KIRANGWA sijamuelewa huyu mkuu.@Charty kuweka Comment ya mkuu KIRANGWA kwenye hii Thread yangu? Watu wengine kazi yao kuharibu Thread za wenziwao hiyo ndio kazi yao sijuwi wanachangia kitu gani kwenye hii Thread yangu? Sijawaelewa kabisa hawa watu.

tumpotezee tu. yawezekana alikuwa anatuma msg kwa mtu aliyemvuruga then msg ikapotea njia. simu za mchina nouma
 
Back
Top Bottom