Nusu Karne na CCM?

Plans zenu nzuri lakini hazijanyumbulishwa. Katika hali ya kawaida kupokea kuwa utaongeza bajeti kwenye sekta ya elimu na kuwaongezea mishahara haitoshi...meaning haina tofauti na propaganda za sisiemu.

May be kutaja kiwango cha chini cha mshahara kwa mwalimu, mahitaji ya vitabu ni kiasi gani na vitabu gani, nyumbani za walimu kiasi gani etc. Baada ya mnyumbulisho huo ukaja na kiwango kinachotakiwa kuongezeka katika bajeti ya sekta husika itafanya mtu aifikirie hiyo serikali yenu kuwa serious na kuitofautisha na hii ya sisiemu yenye maneno mengi bolded lakini utekelezaji hakuna kwa kukosa strategic planning,.
 
Hebu angalia msingi huu wa itikadi yetu. Haujibu matatizo ya ubinafsishaji? Watanzania, kwamba twalalamika tu is a myth! Tena sumu ambayo watu wanalishwa na CCM. Hii yote ipo katika tovuti ya CHADEMA www.chadema.net

CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.
 
Unaposema soko huru ina maana hakuna regulations zozote zile katika biashara?
 
This guided me to join Bomani Committee

CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.
 
Unaposema soko huru ina maana hakuna regulations zozote zile?

Soma msingi mzima, sio vipande. Naweka hapa

CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.
 
Plans zenu nzuri lakini hazijanyumbulishwa. Katika hali ya kawaida kupokea kuwa utaongeza bajeti kwenye sekta ya elimu na kuwaongezea mishahara haitoshi...meaning haina tofauti na propaganda za sisiemu.

May be kutaja kiwango cha chini cha mshahara kwa mwalimu, mahitaji ya vitabu ni kiasi gani na vitabu gani, nyumbani za walimu kiasi gani etc. Baada ya mnyumbulisho huo ukaja na kiwango kinachotakiwa kuongezeka katika bajeti ya sekta husika itafanya mtu aifikirie hiyo serikali yenu kuwa serious na kuitofautisha na hii ya sisiemu yenye maneno mengi bolded lakini utekelezaji hakuna kwa kukosa strategic planning,.

Nilitaka kuonesha Watanzania wenzangu kuwa mawazo ya Tanzania gani tunayo.......... inaweza kuwa hii ni skeleton. Ndio uwezo wetu ulipokuwa unaishia. Ndio maana twaomba Watanzania wengi zaidi wenye uwezo wa kunyumbulisha sera wajiunge nasi ili mwaka 2010 tuwe na sera bora zaidi. Kabla ya hapo mwaka 2009 tuwe na ilani nzuri zaidi ya jinsi ya kuendesha vijiji vyetu!
 
Nilitaka kuonesha Watanzania wenzangu kuwa mawazo ya Tanzania gani tunayo.......... inaweza kuwa hii ni skeleton. Ndio uwezo wetu ulipokuwa unaishia. Ndio maana twaomba Watanzania wengi zaidi wenye uwezo wa kunyumbulisha sera wajiunge nasi ili mwaka 2010 tuwe na sera bora zaidi. Kabla ya hapo mwaka 2009 tuwe na ilani nzuri zaidi ya jinsi ya kuendesha vijiji vyetu!

Pia mngelipa kipaumbele suala la kuungana. Hili Watanzania wengi tunadhani kwamba litawawezesha kuwa na chama kimoja chenye nguvu ya kuweza kupambana na CCM katika majimbo yote ya uchaguzi.
 
Nilitaka kuonesha Watanzania wenzangu kuwa mawazo ya Tanzania gani tunayo.......... inaweza kuwa hii ni skeleton. Ndio uwezo wetu ulipokuwa unaishia. Ndio maana twaomba Watanzania wengi zaidi wenye uwezo wa kunyumbulisha sera wajiunge nasi ili mwaka 2010 tuwe na sera bora zaidi. Kabla ya hapo mwaka 2009 tuwe na ilani nzuri zaidi ya jinsi ya kuendesha vijiji vyetu!


Kuwa hapa mtu kama mimi nimeshajiunga nanyi, kama msema chochote kuna vyenye manufaa utapata na kuna pumba utaacha. Watanzania wote wakijiunga kuja kutengeneza sera si itakuwa pashika nguo kuchanika.

By the way, I appreciate your good job, keep it up...you have a little while before 2010 and a lot have to be done. NYAMBULISHENI HIZO MIKAKATI ZENU
 
Hii ndio misingi ya itikadi yetu na hivyo imani za mwana CHADEMA. We are not an ampty party. Tatizo laweza kuwa 'communication strategy'! Lakini ataanza kusikiliza itikadi hizi katika masakata yote haya ya EPA. MEREMETA, Mikataba ya Madini nk?

Itikadi ya Chama

CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).


CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.


CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.


CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.


CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.


CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.


CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.


CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii.


CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.


CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.


CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.


CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.

Ndugu Zitto....Nakubaliana sana na sera za CHADEMA licha ya kwamba sina chama kwasasa....Posting zote za nyuma kusema ukweli nakubaliana na hoja na CHADEMA inakwenda na wakati....Mali za wananchi ccm warudishe pia na Taifa liwe Taifa na vyama vitupe sera na miongozo....Mungu na awabariki kwasbabu nia yenu ni nzuri.
Mwalimu alifanya makosa lakini nia yake nzuri ndiyo iliyomfanikisha kwa kiasi kikubwa.
Ni wazi kuwa hii ni awamu ya pili ya kugombea UHURU na ni wazi kuwa mnachukuwa hatuwa zilizo sahihi...

Hapa chini nilitaka kugusia jambo moja...
Quote:
Originally Posted by sheshe
nchi imeuzwa mirerani tunateseka lakini Tanzanite inasafirishwa na Tanzanite one kila siku.wazawa tunakufa,viongozi wajuu wanalijua ilo,sema ufisadi umewazidi.zito wewe ni kama Barack Obama.

Hapana. Mama yangu Mtanzania, Baba yangu Mtanzania. Sina bibi kontinenti lingine. Havent done my biography. Obama did 2.
This country has ceased to be the land of opportunities where the rich and the poor kids share the same desk at school and the rich and poor woman meet at the same clinic.

Are we being judged according to the content of our characters or according to the zeros in our bank accounts?

Hata hivyo maelezo mengine ya Injustices na Inequalities umelenga penyewe...God willing...The Patriots will emerge the victors.

Ndugu yetu Sheshe alipokufananisha na Obama hakumaanisha race wise ama continent..Nadhani alimaanisha ile imani na mwamko walio nao watanzania ni sawa na wewe ni Obama wao ukilinganisha siasa za marekani na Tanzania.
Kwasababu Obama na yeye ni kama mkombozi wa watu masikini na wenye hali ya chini hapa USA na dunia nzima kwa ujumla...Hivyo usijali kwasababu tu mama yuko contineti moja...As long as we have one cause...FOR THE PEOPLE...THEN WE HAVE SOMETHING IN COMMON...JUSTCE AND FREEDOM TO THE PEOPLE....
 
Pia mngelipa kipaumbele suala la kuungana. Hili Watanzania wengi tunadhani kwamba litawawezesha kuwa na chama kimoja chenye nguvu ya kuweza kupambana na CCM katika majimbo yote ya uchaguzi.

Sidhani kama idea ya kuungana n nzuri sana. Kinachotakiwa ni kuwa na chama chenye sera nzuri, zitakazowavuta wafuasi wengi zaidi na kipate ngucu kuba ya umma. Itakapotokea hivyo, vile vyama vingine visivyo na nguvu vitakufa kifo cha asili na wote watajikuta wapo pamoja. Hii ya kuunganisha vyama ambavyo 'vinadhani' kuwa vina nguvu ni vigumu sana kupata kitu kimoja chenye nguvu kwa sababu kila chama kitakachoingia kwenye muungano kitajiona kuwa chenyewe ndio zaidi, matokeo yake itakuwa ni kuendelea kuvuraga
 
Sidhani kama idea ya kuungana n nzuri sana. Kinachotakiwa ni kuwa na chama chenye sera nzuri, zitakazowavuta wafuasi wengi zaidi na kipate ngucu kuba ya umma. Itakapotokea hivyo, vile vyama vingine visivyo na nguvu vitakufa kifo cha asili na wote watajikuta wapo pamoja. Hii ya kuunganisha vyama ambavyo 'vinadhani' kuwa vina nguvu ni vigumu sana kupata kitu kimoja chenye nguvu kwa sababu kila chama kitakachoingia kwenye muungano kitajiona kuwa chenyewe ndio zaidi, matokeo yake itakuwa ni kuendelea kuvuraga

Hili la kutoungana linagawa kura katika vyama vya CHADEMA, CUF, TPL n.k. ambazo kama wangekuwa na chama kimoja zote zingeingia kwenye chama hicho, lakini kwa kuwa hawajaungana matokeo yake ni CCM kuchukua majimbo mengi na pia Urais. Kwa maoni yangu wataendelea kushindwa katika chaguzi zijazo kutokana na mgawanyiko wa kura hizo (Naweza kuwa nakosea) kutoingia katika hesabu ya chama kimoja.
 
Hili la kutoungana linagawa kura katika vyama vya CHADEMA, CUF, TPL n.k. ambazo kama wangekuwa na chama kimoja zote zingeingia kwenye chama hicho, lakini kwa kuwa hawajaungana matokeo yake ni CCM kuchukua majimbo mengi na pia Urais. Kwa maoni yangu wataendelea kushindwa katika chaguzi zijazo kutokana na mgawanyiko wa kura hizo (Naweza kuwa nakosea) kutoingia katika hesabu ya chama kimoja.

Mimi sipingi kuungana lakini muungano ninaouunga mkono ni tofauti na huu ambaow alijaribu kuufanya. Kijitokeze chama kimoja, kijijenge na kujikusanyia nguvu kiasi cha vyama vingine kujiua vyenyewe kwa wafuasi wake (ikiwezekana na viongozi) kuhamia chama hicho.
Huu muungano wa sasa ni kuwaweka mafahari mahali pamoja, lazima vumbi litatimka na hakutakuwa na kazi ya kujenga bali kubomoa
 
Mimi sipingi kuungana lakini muungano ninaouunga mkono ni tofauti na huu ambaow alijaribu kuufanya. Kijitokeze chama kimoja, kijijenge na kujikusanyia nguvu kiasi cha vyama vingine kujiua vyenyewe kwa wafuasi wake (ikiwezekana na viongozi) kuhamia chama hicho.
Huu muungano wa sasa ni kuwaweka mafahari mahali pamoja, lazima vumbi litatimka na hakutakuwa na kazi ya kujenga bali kubomoa

Kwa maana nyingine mafahari walioweka mbele maslahi yao binafsi badala ya yale ya Taifa. Bado tuna safari ndefu. Hata ushauri wa bure waliopewa na Waziri Mkuu wa Kenya bwana Odinga kuhusu umuhimu wa kuungana ili kuing'oa CCM madarakani hawaoni umuhimu wa kuufanyia kazi.

Process ya kusubiri chama kimoja kijitokeze na kuonyesha ndicho chenye nguvu kuliko vyama vingine na vyama vingine kufa inaweza kuchukua miaka mingi ukilinganisha na process ya kuamua kukaa chini na kuunda chama kimoja chenye nguvu ili kiingie madarakani na kulinda maslahi ya Tanzania na Watanzania ambayo sasa hayako salama.
 
Watanzania inabidi wabadilike, chama kimoja kikitawala kwa muda mrefu hugeuka kuwa dikteta. Maneno ya Chiligati ni dalili ya umaskini wa kutoa na kujenga hoja za kuwapa matumaini watanzania juu ya mustakabali wa Taifa lao. Umaskini wa hoja unapotokea matokeo yake ni maneno ya jazba yaliyojaa matusi au kejeli kama Ndugu Chiligati alivyofanya siku chache zilizopita. Na mara Matusi yanaposhindwa kufua dafu Nguvu za dola (Jeshi, Polisi & Usalama wa taifa) huingizwa kucheza rafu dhidi ya wananchi. Nguvu za dola zikishatumika matokeo yake ni maafa.

Watanzania badilikeni, kwa kuwa CCM ilitupatia uhuru kutoka kwa mkoloni mweupe mwaka 1961, zawadi tuliyoipa ya kutuongoza (au kututawala kama wengine wanavyodai) kwa miaka 47 inatosha!. La sivyo tutajikuta tumemwondoa mkoloni mweupe tumemweka mkoloni mweusi. Kwa maana nyingine tutakua tumeondoa kisiki na kuweka gogo barabarani. Haya tumeyaona Zimbabwe, Ethiopia, nk.

Tuendelee kujadiliana.
 

Process ya kusubiri chama kimoja kijitokeze na kuonyesha ndicho chenye nguvu kuliko vyama vingine na vyama vingine kufa inaweza kuchukua miaka mingi ukilinganisha na process ya kuamua kukaa chini na kuunda chama kimoja chenye nguvu ili kiingie madarakani na kulinda maslahi ya Tanzania na Watanzania ambayo sasa hayako salama.

hapo umegusa pale ninapopasema mimi-wasiungane kwa namna waliyojaribu kufanya. Kama wanaamua kuungana kwa namna ya kuua vyama vyao, wakaunda kimoja chenye nguvu inaweza kusaidia lakini inabidi wawe na msingi mzuri wanapoingia kwenywe hicho chama kimoja, si kutoka na sentiments za kwenye vyama vilivyouawa.
Wakiwa na mentality ya ummoja zaisdi kuliko ya ubinafsi, yote yanawezekana. Kwa maana hiyo wanatakiwa kuwa waangalifu zaidi kuwa wanajiunga pamoja wakiwa na msimamo gani wa pamoja na kila mmoja apimwe nafsi yake msimamo wake binafsi katika lengo hilo la pamoja ili kuwaondoa wale ambao wanaweza kuwadhani kwua muungano huo ni opportunity ya wao kuibuka
 
ITIKADI
NA SERA ZA
CHADEMA

ZIMEKUSANYWA NA
NIVOJ SUED
YALIYOMO
I. Falsafa, Itikadi, sera na madhumuni ya chama 4
1. Utangulizi katika katiba ya chadema 4
2. Falsafa ya chadema 5
3. Itikadi ya chadema 6
4. Madhumuni ya chadema 7
4.1 Madhumuni ya Kisiasa 7
4.2 Madhumuni ya Kiuchumi 7
4.3 Madhumuni ya Kijamii 8
II. Sera ya Afya 10
1. Hali ya afya Tanzania ikoje? 10
2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kuboresha huduma za Afya? 10
III. Sera ya Ajira 11
1. Hakuna Ajira, Watanzania tukale wapi? 11
2. Serikali ya CHADEMA itatengezena ajiri nyingi na hasa kwa vijana, kivipi? 12
IV. Sera ya Ardhi 12
1. Hali katika sekta ya ardhi ikoje? 12
2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kumilikisha Ardhi kwa Watanzania? 13
V. Sera ya Biashara 14
1. Kwa nini Tanzania inafanya biashara ya uchuuzi? 14
2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje kuimarisha biashara? 14
VI. Sera ya Utawala Bora 15
1. Hali ikoje? 15
2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje? 15
VII. Sera ya Demokrasia 16
1. Hali ikoje? 16
2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje? 16
VIII. Sera ya Elimu na Elimu ya Uraia 16
1. Hali ya Elimu yetu Tanzania ikoje? 16
2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje ili kuboresha Elimu ya Tanzania? 17
IX. Sera ya Kilimo 18
1. Kilimo chetu kidemorora, kwa nini? 18
2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini kurejesha hadhi ya kilimo na Wakulima? 18
X. Sera ya Uchumi - Sekta ya Kodi 19
1. Kodi nyingi na za kificho, hali gani hii? 19
2. Serikali ya CHADEMA itafanya yafuatayo kuboresha mfumo wetu wa kodi. 19
XI. Sera ya Madini 20
1. Hali ikoje katika utajiri wetu wa madini? 20
2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini Tanzania ifaidi utajiri wa Madini? 20
XII. Sera ya Maji 21
1. Hali ikoje? 21
2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini? 21
XIII. Sera ya Mazingira 22
1. Hali ikoje kwa mazingira yetu? 22
2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini kuboresha mazingira? 22
XVI. Mifugo 22
1. Mifugo yetu imesahaulika? 22
2. serikali ya CHADEMA itafanya nini kuboresha maisha ya wafugaji? 22
XV. Sera ya Miundombinu 23
XVI. Sera ya Rasilimali 24
XVII. Uchumi 26
1. Uchumi wa Takwimu, Umasikini kibao, kwa nini? 26
2. CHADEMA itafanyaje WATANZANIA WOTE wafaidi matunda ya kukua kwa uchumi? 27
XVIII. Ulinzi na Usalama 28
1. Hali ikoje? 28
2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje? 29
XIX. Sera ya Utawala 29
1. Utawala wa Ukiritimba na Urasimu, ukoje? 29
2. Serikali ya CHADEMA itaondoa ukiritimba na urasimu kwa kufanya yafuatayo. 30
XX. Vijana 30
1. Masikini Vijana wa Tanzania, kwa nini lakini? 30
2. Serikali ya CHADEMA na sura mpya ya Vijana wa Tanzania 31
XXI. Viwanda 31
1. Hali mbaya sana, kwa nini? 31
2. Serikali ya CHADEMA itatatua tatizo la Viwanda kwa kufanya yafuatayo 31

I. Falsafa, Itikadi, sera na madhumuni ya chama

1. Utangulizi katika katiba ya chadema

KWA KUWA ,Nchi yetu imeridhia mfumo wa Utawala wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kupitia sheria iliyopitishwa rasmi na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hivyo kutambulika rasmi na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyorekebishwa mwaka 1992, Sehemu ya Kwanza, Ibara ya Tatu, Kifungu cha Kwanza na cha Pili;

NA KWA KUWA , Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu tukiwakilisha wanachama wa Chama chetu, kama sehemu ya Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuona umuhimu wa kukuza demokrasia ya kweli yenye fikra mpya za kuwaendeleza Watanzania wote kiuchumi na kijamii bila kubagua kwa misingi ya rangi, ukabila, ukanda, jinsia, itikadi, umri au dini;

NA KWA KUWA, Tumetambua athari ambazo nchi yetu imekumbana nazo kutokana na mfumo wa Ki-imla uliotokana na Chama kimoja cha siasa na kusababisha kukosekana kwa uhuru na usawa wa mawazo sambamba na kukandamizwa kwa haki za msingi za kijamii na za kibinadamu kwa mujibu wa Tamko la Dunia la Haki za binadamu na kusababisha kudorora kwa uchumi pamoja na huduma zote za jamii;

NA KWA KUWA, Uzoefu wa miaka kumi na nne ya mfumo wa utawala wa vyama vingi umedhihirisha kutokuwepo kwa utekelezaji kwa vitendo, dhamira safi na nia ya kweli ya kuleta demokrasia kutoka kwa walio na madaraka.

NA KWA KUWA Tunatambua na kuamini kuwa itikadi na falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia itakayoleta jamii HURU na yenye AMANI YA KWELI;

HIVYO BASI, Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 13/8/2006, Mjini Dar es Salaam tumeamua kuifanyia mabadiliko Katiba ya 2004 ya Chama chetu cha Siasa kitakachoitwa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa FALSAFA yetu ya NGUVU NA MAMLAKA YA UMMA na Dira na Dhamira ya Chama
kuanzia 2006 na kuendelea.

Kuanzia sasa CHADEMA, kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya Chama vitavyotungwa kwa mujibu wa Katiba hii, ili kuimarisha kutetea, kudumisha, na kuendeleza DEMOKRASIA ya kweli, na HATIMAYE kuweza kuleta MAENDELEO ya kweli ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa jamii nzima ya
Taifa la Tanzania.


2. Falsafa ya chadema

FALSAFA YA CHAMA – ina maana ya imani na mtizamo wa chama kama ilivyoainishwa kwenye Katiba.

Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.

Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.

Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.

Historia inaonyesha kuwa “UMMA” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.

CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”.

Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.

CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.

Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya
kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.

Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

3. Itikadi ya chadema

ITIKADI YA CHAMA - ina maana ya mwelekeo wa chama kisiasa, kiuchumi na kijamii.

CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party). CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.

CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru,
utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.

CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote. CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.

CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki. CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa. CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii. CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.

CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu. CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi. CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.

4. Madhumuni ya chadema

Kuna madhumuni ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.
4.1 Madhumuni ya Kisiasa

(a) Kukuza, kulinda, kuelimisha na kutetea haki za binadamu katika misingi ya Tangazo la Ulimwengu la haki za Binadamu na miKataba yote ya Kimataifa inayolinda haki hizo na inayofutilia mbali ukandamizaji wa watu katika misingi ya rangi, jinsia, ukanda, umri au itikadi.

(b) Kuhakikisha kila mtu ana haki na uhuru wa kuabudu kwa minajili ya dini, madhehebu au imani yoyote anayotaka, bila kuathiri amani na/au utulivu wa mwenzake na jamii.

(c) Kuendeleza na kudumisha Demokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kujenga utamaduni wa demokrasia katika jamii kwa kutambua haki za wengi katika maamuzi na pia kutambua haki za wachache kusikilizwa, kuheshimiwa na kulindwa, sambamba na kukubali ushindani huru, wa haki na wa wazi katika uchaguzi.

(d) Kuhakikisha mtu ana uhuru wa kwenda mahali popote ndani ya mipaka ya nchi na kwamba anaweza kushirikiana na mtu yeyote ndani na nje ya nchi katika kuendeleza maslahi halali ya washirika na kuwa kuna uhuru wa kukutana na kuandamana kwa amani ili kuendeleza hayo maslahi kwa masharti ya sheria za haki.

(e) Kudumisha uhusiano wa kirafiki na mataifa jirani, Afrika na duniani kote; kuyaheshimu maamuzi yote ya kimataifa kulingana na kanuni zilizopo za kimataifa na miKataba ya Umoja wa Mataifa na ya nchi yetu na nchi zingine kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

(f) Kukuza na kuendeleza uraia mwema, Uzalendo na mapenzi ya nchi yetu.

4.2 Madhumuni ya Kiuchumi

(a) Kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na rasilmali zao.

(b) Kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti.

(c) Kujenga na kuimarisha kilimo, hususan cha umwagiliaji, na ufugaji katika lengo la
(d) kutosheleza Taifa kwa chakula na kwa ajiri ya masoko ya biashara ya ndani na ya nje ili kuboresha maisha ya wakulima na wafugaji na kuendeleza sera ya kulinda ardhi, maliasili na mazingira kwa manufaa ya kilimo na ufugaji endelevu.

(e) Kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la Taifa na hasa katika kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii zinazotumiwa na wananchi wote.

(f) Kujenga misingi imara ya ajira kwa kuongeza fursa na uwezo wa wananchi kujiajiri wenyewe, kujenga mazingira ya kupanuka kwa sekta binafsi na kuhakikisha kipato cha waajiriwa katika sekta rasmi za uchumi na huduma kinalingana na jasho au juhudi za muajiriwa.

(g) Kutoa mkazo katika Utafiti, Sayansi na Teknolojia na kusambaza matokeo yake kwa walengwa ili kuchochea maendeleo endelevu.

(h) Kutengeneza sera makini zitazowezesha kukuza maendeleo ya viwanda vya aina zote hasa vinavyotumia malighafi inayopatikana nchini kwa lengo la uzalishaji wa bidhaa kwa matumizi ya ndani na biashara ya nje.

(i) Kuimarisha miundombinu muhimu ya sekta ya usafiri na mawasiliano hususan barabara, reli, bandari, anga, na simu, mabwawa, mifereji ya maji na umeme.

(j) Kulipa kipaumbele suala la hifadhi na ulinzi wa mazingira katika mipango yote ya
(k) maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

4.3 Madhumuni ya Kijamii

(a) Kuendeleza juhudi za kuhakikisha haki za wanawake, watoto na wenye ulemavu kwa kuelimisha umma ili kuondoa fikra na mila potofu za ukandamizaji wa kijinsia, kuwanyima watoto haki za malezi bora na za kupata elimu ya kutosha, umuhimu wa kuwajali wenye ulemavu na kuwatimizia mahitaji yote ya msingi, pamoja na kutekeleza makubaliano na miKataba ya Kimataifa kuhusu haki za watoto, wanawake na walemavu.

(b) Kuboresha, kutunza na kutoa huduma za jamii, kwa mfano Afya, Elimu, Maji, Makazi na Usalama wa Raia, kwa ajili ya kukuza hali ya maisha ya watu.

(c) Kuhifadhi na kuboresha utamaduni wa Taifa ili kujenga hadhi na heshima ya Watanzania na kuendeleza nyanja zote za utamaduni, burudani, michezo, sanaa na historia ya nchi.

(d) Kutoa huduma za kukidhi maisha kwa wastaafu na makundi yasiyojiweza katika jamii
(e) hususan wenye ulemavu, watoto yatima na wazee,ambao hawapo katika mkondo wa kujipatia kipato cha kujitosheleza.

(f) Kuweka mikakati madhubuti ya kupambana na janga la Ukimwi (HIV/AIDS) sambamba na kutoa huduma muafaka kwa waathirika.



II. Sera ya Afya
1. Hali ya afya Tanzania ikoje?
(a) Serikali imekwepa jukumu lake la kutoa huduma za afya kwa wananchi, imelifanya kuwa la kibiashara kuliko huduma.
(b) Huduma za afya nchini zimezidi kupororoka siku hadi siku.
(c) Bajeti ya Wizara ya Afya haina mtazamo wa kijinsia kwani madawa mengi yanayoagizwa nchini ni ya magonjwa ya jumla.
(d) Mpango wa afya ya msingi umeshindikana – wananchi wenye uwezo wanatibiwa na wasio na uwezo wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kama malaria na kipindupindu.
(e) Wanawake wajawazito hawana uhakika wa maisha yao wakati wa kujifungua kwani katika kila wanawake elfu moja wanaojifungua sita hupoteza maisha yao kwa sababu ya mfumo mbaya wa afya usiojali kazi muhimu ya kuzaa.
(f) Ni wanawake 47 tu kati ya wanawake mia moja wanajifungulia hospitalini. Mafunzo kwa wakunga wa jadi hayatoshi na hakuna juhudi za kutatua tatizo hili.
(g) Maslahi ya wafanyakazi wa sekta ya afya ni finyu.
(h) Pesa za vita dhidi ya ukimwi zinaishia mifukoni mwa wajanja wachache.
(i) Upanuzi wa sekta ya afya haulingani na ongezeko la watu – Daktari mmoja anahudumia wagonjwa.
(j) Wagonjwa wachache sana wa Ukimwi wanapata madawa ya kurefusha maisha – madawa mengi yaliyotolewa kwa msaada yanaporwa na vigogo.
(k) Gharama za afya bado ni mzigo mkubwa kwa wananchi wa kawaida kiasi cha kupelekea kujitibu kwa matabibu wasiyofuzu ilhali viongozi wakitibiwa nje kwa kodi ya wananchi.
(l) Mzigo wa kulea wagonjwa wa Ukimwi limeachwa kwa akina mama majumbani peke yao bila msaada wowote wa serikali (serikali kuu na serikali za mitaa).

2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kuboresha huduma za Afya?
(a) Kupanua mpango wa bima ya afya kumshirikisha kila Mtanzania. Mkazo utawekwa katika kusisitiza ‘lishe bora’ na siyo ‘bora lishe’ – miongoni mwa wananchi Mamlaka za serikali za Mitaa zitaunda mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa wananchi ili kuweka bima ya Afya kwa wananchi wengi vijijini.
(b) Mfumo wa Afya utajengwa kuanzia ngazi ya kijiji ili kupata mahitaji halisi ya madawa kutoka na historia ya magonjwa katika maeneo husika.
(c) Tutahakikisha bajeti ya wizara ya afya inakuwa na mtazamo wa kijinsia kwa kujali sana madawa muhimu kwa akina mama kufuatia masuala ya kimaumbile.
(d) Nguo za watoto wachanga kama nepi n.k hazitatozwa kodi VAT.
(e) Madawa yote muhimu kwa akina mama wajawazito na watoto hayatakuwa na kodi ya forodha na pia VAT.
(f) Ushuru wa forodha na VAT kwa vifaa vya hedhi utakuwa sifuri.
(g) Hamasa itatolewa kwenye utafiti, utumiaji na uboreshaji wa tiba zetu za asili.
(h) Elimu ya afya itatolewa ikiwemo kuhusu lishe ili kurekebisha mila na desturi ambazo zinaathiri afya ya jamii.
(i) Huduma zitakazolipiwa na serikali nje ya nchi ni zile tu zisizopatikana nchini na kwamba wananchi wote watapewa haki sawa ya kupata nafasi hizo.
(j) Vituo vya afya vitaanzishwa vijijini kuwapunguzia wananchi umbali wa kutembea kutafuta huduma za msingi.
(k) Itawajali na kuwahudumia Watanzania wenye kuishi na virusi vya ukimwi kwa kuweka mfumo bora utakaosimamiwa na serikali za Mitaa ili kuondoa mzigo wa kuhudumia wagonjwa kwa akina mama peke yao.
(l) Watanzania wote wenye kuishi na virusi vya ukimwi watapatiwa madawa {bure} na jamii kupitia serikali za vijiji na Mitaa na pia kupitia Asasi zisizo za kiserikali zitabeba jukumu la kuhudumia wagonjwa bila ubaguzi wa kijinsia.
(m) Tutatangaza malaria kuwa janga la kitaifa na tutoa huduma za afya kwa malaria bure.
(n) Huduma za afya zitatolewa bure kwa makundi maalum – waja wazito, vikongwe, wanafunzi, wenye kuishi na virusi vya ukimwi, watoto wachanga na walemavu

III. Sera ya Ajira
1. Hakuna Ajira, Watanzania tukale wapi?
(a) Watanzania wengi wanaishi kwa kubahatisha – Asilimia 28 ya vijana wanaoishi mjini hawana ajira.
(b) Wafanyakazi wanakandamizwa – mifumo ya ajira ya soko holela inawaminya.
(c) Wafanyakazi wanazidi kupunguzwa bila maslahi yao kuzingatiwa.
(d) Wafanyakazi wa Kitanzania wanalipwa mishahara midogo kuliko wa kigeni kwa kazi ileile.
(e) Mishahara na mazingira ya kazi bado ni duni.
(f) Hakuna juhudi mahususi za kutengeneza ajira kwa Watanzania.
(g) Hakuna takwimu sahihi za masuala ya ajira.
(h) Wawekezaji wanaajiri wageni hata kwa kazi ambazo kuna Watanzania wengi wanaweza kuzifanya.
2. Serikali ya CHADEMA itatengezena ajiri nyingi na hasa kwa vijana, kivipi?
(a) Tutaweka kipaumbele kuweka mazingira ya kuongezeka fursa za ajira
(b) Tutatengeneza ajira milioni moja ndani ya mwaka mmoja wa utawala wa CHADEMA kwa kuimarisha sekta za ujenzi, madini, kilimo, utalii na huduma za jamii (walimu, madaktari na manesi)
(c) Tutakomesha ubaguzi wa ajira kwa watu wenye ulemavu na tutatoa motisha kwa mashirika yatakayoajiri watu wenye ulemavu na kuwaendeleza kitaaluma.
(d) Tutaweka sheria kali kulinda haki za ajira kwa wanawake na mashirika na makampuni yatakayo ajiri wanawake zaidi yatapewa motisha katika kodi na hata zabuni za serikali.
(e) Tutaweka mifumo yenye kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi.
(f) Vyama vya wafanyakazi vitalindwa kisheria na kupewa nafasi kubwa katika kulinda maslahi ya wafanyakazi.
(g) Vyama vya wafanyakazi vitakuwa huru kweli kweli na itakuwa ni marufuku kwa serikali kuingilia utendaji wa vyama vya wafanya kazi.
(h) Tutasimamia wazawa na wageni wenye ujuzi unaolingana kulipwa sawasawa.
(i) Tutatunga sheria itakayohakikisha kuwa Wageni wataajiriwa pale tu hakuna mtanzania anayemudu kazi husika na kwamba Wawekezaji watafanya juhudi kufundisha Watanzania kumudu kazi hizo siku za mbeleni.
(j) Tutatoa msamaha wa kodi wa kiasi kwa kila atakaye ajiri mhitimu wa chuo mara baada ya masomo.
(k) Tutaweka kipaumbele umuhimu wa kurekebisha ajira na maslahi ya wafanyakazi.

IV. Sera ya Ardhi
1. Hali katika sekta ya ardhi ikoje?
(a) Watanzania wote ni wapangaji katika ardhi yao – sheria za ardhi hazitoi mamlaka ya kumiliki ardhi kama mtu binafsi ama vikundi.
(b) Sheria hizi zinampa mgeni mamlaka makubwa juu ya ardhi kuliko mwananchi.
(c) Mfumo dume umetawala katika kumiliki ardhi – wanawake na vijana hawajapata fursa ya kumiliki au ‘kukodisha’ ardhi.
(d) Wageni wanauziwa ardhi kama khanga.
(e) Mfumo mbaya wa ugawaji na umiliki wa ardhi pamoja na rushwa imesababisha utitiri wa migogoro ya ardhi.
(f) Wananchi wanaporwa ardhi zao kwa visingizio vya kuendeleza maslahi ya Taifa.
(g) Utaratibu uliyopo wa milki ya ardhi hautoi uhakika kwa wanyonge na maskini kumiliki ardhi yao.
(h) Kuna urasimu mkubwa unaoshawishi rushwa katika kutoa haki za kumiliki ardhi.

2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kumilikisha Ardhi kwa Watanzania?
1. Tutarejesha mamlaka ya asili ya wananchi kumiliki ardhi.
2. Hatima ya ardhi ya kijiji itaachwa mikononi wa mamlaka ya Serikali ya kijiji.
3. Rais hatokuwa na mamlaka ya kuhamisha ardhi kutoka kundi moja hadi jingine.
4. Wageni watapatiwa ardhi kwa masharti yafuatayo - kutoimiliki, kutoiuza, kutoipora rasilimali na kutoitumia kwa namna itakayoharibu mazingira.
5. Umilikaji wa ardhi kwa wanawake haitakuwa suala la mjadala tena. Mfumo dume wa kumiliki ardhi utatokomezwa na kufanywa historia.
6. Utawekwa utaratibu wa kisheria utakaowawezesha wanawake kumiliki ardhi bila bughudha wala hofu ya kuporwa.
7. Itaimarisha mabaraza ya ardhi ya vijiji na wilaya na kuhakikisha yanatoa haki kwa wananchi.
8. Utawekwa utaratibu wa serikali kuwawekea mawakili wananchi wasio na uwezo katika mashauri ya ardhi katika ngazi ya mahakama kuu na mahakama ya rufaa.
9. Tutatunga na kusimamia sheria zitakazo shughulikia uvamizi na ujenzi holela.
10. Itatoa maelekezo kwa halmashauri kuendesha mipango ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu za wananchi.
11. Itarejesha nyumba zote za serikali zilizouzwa kwa upendeleo.
12. Tutaunda baraza la Taifa la ardhi litakalowajibika kwa Bunge.
13. Mahitaji ya ardhi kwa jamii za vijijini yatapewa kipaumbele kuliko mahitaji ya wengine.
14. Tutalinda ardhi za vijiji dhini ya umegaji mkubwa ili kuepuka matatizo ya kijamii.
15. Itahakikisha vijiji vinakuwa ni vitengo vinavyojiendesha na kujitawala vyenyewe na tutawezesha wanavijiji kushiriki kikamilifu kuendesha masuala yote ya ardhi kupitia vikao vya mkutano mkuu wa kijiji.
16. Tutahakikisha wanyonge na maskini wanamiliki ardhi ya nchi yao bila ubaguzi wa jinsi wala umri.
17. Madaraka ya kutoa haki za kumiliki ardhi yatakuwa chini ya mikoa (majimbo).

V. Sera ya Biashara
1. Kwa nini Tanzania inafanya biashara ya uchuuzi?
(a) Mitaji bado ni ndoto kwa wafanyabiashara na hasa wanawake na vijana kutoka familia za kimasikini.
(b) Kutishwa mzigo wa kodi kubwa.
(c) Ushindani usio sawa – Wafanyabiashara wa nje wanakandamiza wa ndani na wafanyabiashara wakubwa wanakandamiza wadogo.
(d) Bidhaa zenye ubora hafifu.
(e) Ukosefu wa soko la nje.
(f) Rushwa na Upendeleo kwa makusudi ya kisiasa.
(g) Wafanyabiashara wachuuzi.
(h) Wafanyabiashara wadogowadogo, Machinga, wananyanyaswa.
(i) Ushiriki hafifu katika mashirika ya kibiashara kama Jumuiya ya Afrika Mashariki.
(j) Serikali kujitoa COMESA bila kujali maoni ya wafanya biashara wa ndani na matokeo yake kusababisha hasara kubwa kwa nchi.
(k) Mikataba mibovu ya kimataifa bila kushirikisha wananchi.

2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje kuimarisha biashara?
(a) Tutaimarisha upatikanaji wa mitaji .
(b) Tutaondoa kodi zisizo za lazima hususan kwa wafanyabiashara wazawa.
(c) Tutatekeleza sheria ya ushindani sawa wa kibiashara.
(d) Tutaimarisha utendaji wa shirika la viwango la Tanzania ili kuongeza ubora wa bidhaa zetu.
(e) Tutaimarisha na kutoa nguvu zaidi za kifedha kwa shirika la SIDO ili liwezeshe vijana kujiajiri kwa kuanzisha biashara na viwanda vidogo.
(f) Tutaziagiza balozi zetu kuwa vituo vya biashara.
(g) Tutakomesha rushwa za aina zote katika utoaji wa leseni, zabuni na misamaha ya kodi.
(h) Itakuwa mwiko kwa wanasiasa kuingilia shughuli za wafanyabiashara.
(i) Tutarasimisha na kuwezesha Wamachinga kufanya biashara zao kwa uhuru.
(j) Tutaimarisha mashirika kama TCCIA, Chamber of Mines, CTI na mengineyo ili kuwa sauti ya sekta binafsi.
(k) Tanzania itajiunga tena COMESA kwa kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki kama chombo kikuu cha kujadiliana masuala ya kibiashara na mashirika mengine. Lakini Tanzania haitajitoa SADC ili kuimarisha ushirikiano wa kindugu na rafiki zetu nchi za Kusini mwa Afrika.
(l) Tanzania itafanya mashauriano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya (EPA) kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki kama sehemu ya COMESA.
(m) Majadiliano yote ya kibiashara yatawashirikisha wananchi kupitia Asasi Zisizo za Kiserikali na Asasi binafsi kama TANGO, TCCIA na CTI ili kuweka mbele masilahi ya nchi.

VI. Sera ya Utawala Bora
1. Hali ikoje?
(a) Rushwa na upendeleo vimekithiri katika nyanja zote - Rushwa sasa imekuwa utamaduni.
(b) Shughuli za vyama vya siasa zinafanywa na vyombo vya dola.
(c) Matumizi ya anasa ya viongozi ilhali wananchi wamezamishwa kwenye umaskini uliokithiri.
(d) Viongozi kutowajibika mbele ya wananchi.
(e) Wizi wa mali ya umma, ubinafsishaji holela na ufisadi.
(f) Uuzaji wa nyumba za Serikali kwa viongozi kiupendeleo.
(g) Mamlaka ya Umma imeporwa na tabaka la watu wachache.
(h) Ukosefu wa maadili ya Taifa.
(i) Viongozi wabovu wasiokuwa na dira.
(j) Viongozi wanakula njama na wageni kuhujumu rasilimali zetu.
(k) Hakuna morali.
(l) Ubinafsi umetawala.
(m) Uzembe umekithiri.
(n) Viongozi wasiojali nchi na watu wake.
(o) Mwizi ni yule anayekamatwa, asiyekamatwa ruksa.
2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje?
(a) Itafuta PCB na kuunda upya idara ya kupambana na rushwa chini ya idara ya Mkurugenzi wa makosa ya jinai.
(b) Idara ya Usalama wa Taifa itafanyiwa marekebisho makubwa ili ilinde maslahi ya nchi na sio ya wakubwa wachache.
(c) Tutaita Mkutano wa Katiba ndani ya mwaka mmoja wa utawala wa CHADEMA.
(d) Katiba kuwa na kipengele kitakacho ruhusu wananchi kuwawajibisha madiwani, wabunge na wawakilishi “recalling clause”.
(e) Itapiga marufuku uuzaji wa nyumba za Serikali na kurejesha zilizokwisha uzwa kiupendeleo.
(f) Matumizi yote ya gharama kubwa bila stahili kusimamishwa mara moja.
(g) Tutakomesha rushwa na atakayetoa au kupokea rushwa atahukumiwa adhabu kali.
(h) Upendeleo utapigwa vita.
(i) Viongozi wa CHADEMA watajali nchi na watu wake.
(j) Tutahamasisha maadili ya Taifa.

VII. Sera ya Demokrasia
1. Hali ikoje?
(a) Nchi inaongozwa kiimla.
(b) Mfumo wa vyama vingi umegubikwa na mizengwe.
(c) Chama kimoja kimehodhi kila kitu.
(d) Sheria zinagandamiza uhuru na ukweli.
(e) Upeo mdogo wa wananchi katika masuala ya demokrasia.
(f) Vyombo vya uwakilishi kama Bunge na Baraza la madiwani havina meno.
(g) Mfumo mbaya wa uchaguzi usiothamini kila kura ya mwananchi.
2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje?
(a) Tutashirikisha wananchi wote kuandika Katiba upya.
(b) Tutaongoza kwa misingi ya sheria na haki za binadamu.
(c) Tutatoa fursa ya vyama vya siasa kujiimarisha.
(d) Tutabadili mfumo wa uchaguzi na kuwa na mfumo mchanyato wa uwiano wa kura na tulio nao sasa ili kuongeza usawa wa kijinsia katika Bunge na pia kuimarisha vyama vya siasa kama asasi muhimu katika ujenzi wa nchi. Chini ya mfumo mpya wa uchaguzi wagombea binafsi wataruhusiwa bila bugudha yeyote.
(e) Tutatenganisha bayana wajibu na mamlaka ya mihimili mitatu ya uendeshaji wa nchi – Bunge, Mahakama na Dola. Wabunge hawatakuwa mawaziri.
(f) Tutafuta sheria zinazobana Asasi za Serikali kufanya kazi zake.
(g) Tutaimarisha Asasi zisizo za kiserikali ili zifanye kazi zake kwa ufanisi na kwa uwajibikaji mkubwa.
VIII. Sera ya Elimu na Elimu ya Uraia
1. Hali ya Elimu yetu Tanzania ikoje?
(a) Elimu bado ni ya kikoloni inayozalisha watwana.
(b) Mitaala haiendani na hali halisi ya kidunia.
(c) Wanafunzi wanalazimishwa kusoma kila somo kupata vyeti wakati vipaji haviendelezwi.
(d) Mpango wa Elimu ya Msingi wa kudandia uliyogubikwa na rushwa – Maandalizi ya walimu ni duni na rasilimali hazifikii walengwa.
(e) Bajeti ya elimu finyu sana – asilimia 9 tu!
(f) Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mwisho duniani ambayo kiuwiano na idadi yake ya watu, ina idadi ndogo ya wasomi wa sekondari na vyuo.
(g) Elimu inawezeshwa kwa fedha za mikopo na misaada ya wahisani wakati fedha itokanayo na kodi atozwayo mwananchi inafanyiwa anasa tu.
(h) Gharama za elimu bado ni mzigo mkubwa kwa familia masikini.
(i) Mazingira ya elimu ni duni – madarasa, nyumba za walimu, maabara na vitabu.
(j) Mfumo wa Elimu hauna mtazamo wa Kijinsia hivyo hauweki mazingira mazuri ya kupata maarifa kwa wanafunzi wa kike na pia wanafunzi wenye ulemavu.
(k) Mazingira ya shule haya kidhi haja na sio rafiki kwa watoto wenye ulemavu wa viungo,wasioona na viziwi.
(l) Elimu ya teknohama hususan sayansi ya kompyuta haijaanzishwa.
(m) Mfumo wa elimu unaochelewesha kuhitimu – kuchelewa kuanza (miaka 7+) na kuchelewa kumaliza (2,7,6,3+)
(n) Elimu ya Uraia ni finyu na potofu.
(o) Michezo mashuleni imefutwa na hivyo kuziba vipaji vya watoto mfano UMITASHUMTA na UMISETA.
2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje ili kuboresha Elimu ya Tanzania?
(a) Itabadili mitaala ya elimu – Italenga mahitaji na maslahi ya Taifa, mitaala itakayochochea fikra, udadisi, ugunduzi na kuendeleza vipaji.
(b) Itatenga kwa sekta ya Elimu na Elimu ya Uraia asilimia 35% ya bajeti yote ya Serikali – italenga kuboresha mazingira ya elimu, ya ufundishaji na uboreshaji wa maslahi ya Waalimu na kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu kupata elimu bila vikwazo
(c) Kamwe elimu haitategemea misaada ya wafadhili na hatutakopa ili kusomesha Watanzania. Elimu italipiwa na fedha za ndani kutokana na makusanyo ya mapato ya kodi na pia mkakati utawekwa ili mapato yote yanayotokana na uchimbaji wa madini yalipie elimu ya watoto wa Tanzania.
(d) Tutajali walimu kwa kuboresha kipato, makazi na mafunzo yao.
(e) Mfumo wa elimu utarekebishwa kwa kiasi kikubwa na utakuwa na mtazamo wa kijinsia ili tuoe fursa sawa kwa wananfunzi wa kike na wenye ulemavu katika kujifunza.
(f) Elimu itatolewa bure kutoka CHEKECHEA mpaka SEKONDARI.
(g) Tutashirikisha wadau wote muhimu kuweka mfumo wa elimu unaowahisha kuhitimu – kuwahi kuanza (miaka 5) na kuwahi kumaliza (2,6,4,3+)
(h) Elimu ya msingi itakuwa mpaka darasa na tisa (Kidato cha Pili) na itakuwa ni lazima kwa kila mtoto anaeishi Tanzania.
(i) Ushirikishwaji wa jamii na wanafunzi katika uendeshaji wa shule utaimarika ili kuboresha ufundishaji na uwazi katika matumizi ya pato la shule.
(j) Elimu sahihi ya Uraia inayochochea kujitambua na uzalendo itafundishwa katika ngazi zote.
(k) Kila mwanafunzi wa sekondari atafundishwa somo la sayansi ya kompyuta na utumiaji wa kompyuta.
(l) Tutageuza majengo yote ya Serikali Dodoma kuwa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi kwa kuendelea na azma yetu ya kuachilia mbali mpango wa kuhamishia makao makuu kwenda Dodoma. Dodoma itakuwa ni jiji la vyuo na kitovu cha elimu cha nchi.
(m) Uendeshaji wa shule za msingi na sekondari itakuwa ni jukumu la Serikali za Mitaa na Serikali kuu itatunga sera, kusimamia utekelezajiwa sera na kugawa rasilimali kama fedha.
(n) Tutaelekeza kila halmashauri kwa kutumia rasilimali zao kuanzisha vyuo vya ufundi katika kila wilaya.
(o) Tutatoa kipaumbele katika elimu ya ujasiriamali ili Watanzania waweze kujiajiri baada ya masomo.
(p) Tutarejesha masomo ya biashara katika shule za sekondari ili kuwajenga vijana wa Kitanzania waweze kujiajiri.
(q) Tutao ruzuku kwa shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Tutabadili shule za serikali kuwa ni vituo vya ubora wa elimu ili kuondoa matabaka.

IX. Sera ya Kilimo
1. Kilimo chetu kidemorora, kwa nini?
(a) Watanzania wengi bado wanalima kwa kutumia jembe la mkono.
(b) Kilimo bado kinategemea huruma ya mwenyezi Mungu kupata mvua.
(c) Soko finyu la mazao ya kilimo – Mengi yanaozea shambani, au kuuzwa kwa bei ya kutupa.
(d) Mifumo mibovu ya kuhifadhi na kusindika mazao ya kilimo.
(e) Sera potofu za soko holela zimeua kabisa motisha ya wakulima wa mazao ya chakula na yale ya biashara.
(f) Bado tunategemea mazao ya biashara tuliyorithi kutoka kwa wakoloni.
(g) Barabara hazifiki vijijini na hivyo mazao ya wakulima kuoza kabla ya kufika sokoni.
2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini kurejesha hadhi ya kilimo na Wakulima?
(a) Kodi zote za pembejeo za kilimo zitafutwa ikiwemo VAT.
(b) Itatilia mkazo wa kipekee barabara zingiazo vijijini.
(c) Tutatumia mabonde yote, mito na maziwa katika kilimo cha umwagiliaji maji.
(d) Tutarejesha vyama huru vya ushirika na mali zake.
(e) Serikali itadhibiti ya soko holela ya mazao ya kilimo.
(f) Tutatoa ruzuku kwa wakulima wetu ili wazalishe chakula cha kutosha na pia kupambana na ushindani wa bidhaa hafifu kutoka nje.
(g) Tutatoa motisha kwa wakulima kuzalisha mazao mbadala ya biashara km maua, viungo, mboga.
(h) Tutatoa motisha katika sekta ya usindikaji ya mazao ya kilimo – maelekezo kwa halmashauri ya wilaya kuweka mazingira ya uwekezaji katika usindikaji wa mazao yapatikanayo ndani ya wilaya.
(i) Serikali itashirikiana na nchi zingine zinazoendelea kushinikiza nchi zilizoendelea kulegeza masharti ya kuuza bidha zetu za kilimo katika masoko yao.
(j) Tutalinda soko la ndani la bidha zetu.
(k) Tutatafsiri kilimo sio tu kuishia katika kulima na kuvuna bali kwenye kuzindika na kuongeza thamani ya bidhaa.
X. Sera ya Uchumi - Sekta ya Kodi
1. Kodi nyingi na za kificho, hali gani hii?
(a) Kodi nyingi ni za kificho au kinyemela – mfano sukari yaweza kuwa na bei ndogo sana iwapo kodi kadhaa katika bidhaa zitaondolewa au kupunguzwa.
(b) Viwango vya Kodi anazotozwa mwananchi ni kubwa mno.
(c) Mfumo mbovu wa kodi unaosababisha mianya mingi ya ukwepaji kodi.
(d) Wageni wanapewa misamaha ya kodi kiholela na kiupendeleo.
(e) Kiwango cha VAT kipo juu sana na mzigo kwa wananchi wengi hasa VAT katika vifaa muhimu vya afya na hasa kwa akina mama.
2. Serikali ya CHADEMA itafanya yafuatayo kuboresha mfumo wetu wa kodi.
1. Itaweka wazi kodi zote zinazotozwa – mwananchi lazima ajue kodi anayotozwa.
2. Tutapunguza VAT ili iendana na viwango vya nchi nyingine za Afrika Mashariki.
3. Tutaziba mianya ya ukwepaji kodi na kutoa misamaha pale tu itakapobidi na lazima iidhinishwe na bunge.
4. Tutapanua wigo wa kukusanya kodi.
5. Tutafuta kodi katika bidhaa zote muhimu kwa akina mama wajawazito na watoto wao na pia vifaa vya elimu na vyakula vinavyozalishwa ndani ya nchi.
XI. Sera ya Madini
1. Hali ikoje katika utajiri wetu wa madini?
(a) Tanzania imebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali.
(b) Katika kila shilingi mia inayopatikana kwenye madini Tanzania inapata shilingi tatu tu!
(c) Mapato yanoyopatikana kutokana na madini bado hayamfikii wala kumnufaisha Mtanzania
(d) Mikataba ya uchimbaji wa madini imetawaliwa na usiri mkubwa na inanuka rushwa.
(e) Vijana wa Kitanzania wafanyao kazi kwenye migodi ya wageni ni sawa na manamba na watumwa ndani ya nchi yao.
(f) Wachimbaji wadogowadogo wanafukuzwa na kunyimwa fursa ya kumiliki migodi.
2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini Tanzania ifaidi utajiri wa Madini?
(a) Si chini ya asilimia thelathini ya mapato yatokanayo na madini yatabaki nchini.
(b) Mikataba yote ya uchimbaji itapitiwa upya na kuwekwa wazi kwa wananchi.
(c) Kuwekwa sheria na utaratibu zitakazowalinda Watanzania wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini hususan wachimbaji wadogowadogo.
(d) Kugawa maeneo ya uchimbaji kulingana na mahitaji halisi ya wananchi ili kuzuia migogoro iliyopo hivi sasa.
(e) Kutoa mikopo na ushauri wa kitaalamu kwa wachimbaji wadogo na kujihusisha na utafutaji wa teknolojia ya kisasa ya uchimbaji.
(f) Wanawake wafanyao biashara za madini watajengewa uwezo zaidi ili kulinda biashara zao dhidi ya utapeli na pia kuwawezesha kujiendeleza zaidi na kupata masoko ya biashara zao.
(g) Wachimbaji wadogo wadogo wa Kitanzania watawezeshwa kumiliki maeneo ya uchimbaji kama mbinu ya kuzalisha ajira kutokana na sekta ya madini.
(h) Mamlaka za serikali za Mitaa ambayo migodi ya madini au visima vya mafuta vipo zitashiriki kwa kiasi kikubwa katika kuandaa mikataba ya uchimbaji wa madini na mafuta.
(i) Mapato yanayotokana na madini yatatumika katika kuwekeza katika elimu kwa vijana wa Kitanzania.
(j) Usafishaji wa madini angalau kwa hatua za awali ni lazima ufanyike Tanzania ili kutoa ajira na pia kuchangia ukuaji wa uchumi na pato la wananchi.
(k) Tenda zote za ugavi kwa makampuni ya madini kwa bidhaa zinazoweza kupatikana Tanzania zitatolewa kwa Watanzania tu. Makampuni ya kigeni hayataruhusiwa kufanya ugamvi wa vitu kama vyakula, kwa mfano!

XII. Sera ya Maji
1. Hali ikoje?
(a) Tanzania ni nchi ya maji – imezungukwa na maziwa makuu, bahari, mito, chemchem na maji ya mvua.
(b) Asilimia 95% ya wananchi hawapati maji safi, salama na kwa uhakika.
(c) Wananchi hawa, hususan wanawake, hutumia nguvu na muda wao mwingi kuyatafuta maji
(d) Kumekuwa na ahadi hewa za upatikanaji wa maji – Kwa miaka zaidi ya 30 wananchi wote wameahidiwa maji bila mafanikio!

2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini?
(a) Itawekeza katika uvunaji wa maji ya mito, maziwa, chemchem na mvua.
(b) Mamlaka ya Usambazaji ya maji itakuwa chini ya halmashauri za manispaa, miji na wilaya
(c) Itawezesha vijiji kutunza vyanzo vya maji ili visiharibiwe.
(d) Upatikanaji wa Maji kwa Wananchi itakuwa ni kipaumbele muhimu cha serikali ya CHADEMA.
(e) Itaingiza kwenye mitaala kuanzia shule ya msingi hadi sekondari dhana ya utumiaji na utunzaji wa maji.
(f) Tutaboresha na kukarabati miundombinu ya maji iliyopo ili kuzuia upoteaji wa maji.
(g) Tutahakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama katika kipindi kifupi iwezekanavyo.
(h) Hatutabinafsisha sekta ya Maji na makampuni yote yaliyobinafsishwa yatarejeshwa chini ya mamlaka za Maji katika Halmashauri za Wilaya. CHADEMA haitaweka MAJI chini ya mikono ya Makampuni ya kigeni, ni hatari kwa usalama wa Nchi.

XIII. Sera ya Mazingira
1. Hali ikoje kwa mazingira yetu?
(a) Mazingira ya mijini ni machafu sana – huduma za uzoaji taka na usafishaji miji ni hafifu, miundombinu ya maji taka haifai.
(b) Jangwa lazidi kujongea na mvua sio za uhakika tena.
(c) Wawekezaji hususan wa maeneo ya madini na viwanda, wanaharibu mazingira.

2. Serikali ya CHADEMA itafanya nini kuboresha mazingira?
(a) Itaanzisha mashindano ya usafi wa mazingira na bustani za mapumziko kwa halmashauri za wilaya.
(b) Itahamasisha kila Mtanzania apande na kulea mti mmoja kila mwaka.
(c) Sheria zatatungwa kulazimisha wawekezaji kutunza mazingira hususan, maeneo ya machimbo ya madini
(d) Utunzaji wa mazingira itakuwa ni jukumu la serikali za Mitaa na serikali kuu itashughulikia sera na kusimamia utekelezaji wa sera tu.
XVI. Mifugo
1. Mifugo yetu imesahaulika?
(a) Tanzania ni nchi ya tatu kwa wingi wa mifugo barani Afrika.
(b) Makabila ya wafugaji hayasaidiwi kuwa wafugaji wa kisasa.
(c) Mchango wa ufugaji katika pato la Taifa bado ni mdogo mno.
(d) Watalaam wa mifugo wanaozalishwa na vyuo vyetu hawakidhi haja na waliopo hawatumiki ipasavyo.
(e) Maeneo ya wafugaji yametelekezwa – hakuna huduma za kijamii kama maji, shule.
(f) Sekta ya usindikaji ya mazao ya mifugo imeuwawa.
(g) Uuzaji wa mazao ya mifugo nje ya nchi umedorora.

2. serikali ya CHADEMA itafanya nini kuboresha maisha ya wafugaji?
(a) Tutarejesha viwanda vyote vya usindikaji wa mazao ya mifugo – mfano Tangayika Packers.
(b) Tutafufua soko la nje la mazao yatokanayo na mifugo.
(c) Tutatoa motisha kwa watalaamu wa mifugo.
(d) Tutaboresha huduma za jamii katika maeneo ya mifugo.
(e) Tutaelekeza halmashauri za wilaya kujenga majosho.
(f) Tutatoa chanjo za mifugo bure.
(g) Tutaimarishaji uzalishaji wa kuku wa kienyeji katika mikoa ya kanda ya kati kukidhi hususan haja ya soko la utalii.



XV. Sera ya Miundombinu
Nchi yetu ina maeneo mbalimbali yenye bidhaa, neema na utajiri wa rasilimali tele zinazohitajika sana maeneo mengine. Karibu kila kitu kinapatikana hapa hapa nchini kwa ajili ya maisha yetu na ya wengine.

Lakini kutokana na kukosekana kwa miundombinu, maeneo mengi nchini yanakosa bidhaa kutoka maeneo mengine, na kisha kuathiri ukuaji wa soko la ndani na kuwafanya wananchi wakose mahitaji muhimu. Tunashuhudia watu wakiwa na njaa maeneo fulani ya nchi huku wengine wakiharibikiwa na mazao. Katika hali hii, uchumi wa nchi umekuwa ukidorora kwasababu ya kukosa miundombinu ya uhakika na kusababisha watu wengi kushindwa kuendelea.
1. Miundombinu inayotakiwa kujengwa, kuimarishwa na kupanuliwa katika nchi kavu ni barabara, reli na mabomba. Hivyo basi, wahandisi na makandarasi wa barabara na reli, watapewa zabuni za ujenzi kwa usimamizi wa vyombo vya kuchaguliwa na wananchi, yaani Bunge na halmashauri. Pia washindi wa zabuni watapitishwa na Bunge na Halmashauri kwa uwazi.
2. Hivi sasa upo mpango wa kujenga barabara kuu muhimu katika kiwango cha lami ambao utagharimiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAM). CHADEMA haitasubiri mpaka nchi tatu ziafikiane, ila itahakikisha kwamba barabara zote kuu zinaounganisha mikoa na kanda zinajengwa katika kiwango cha lami.
3. Sheria ya Usalama barabarani (Road Traffic Act 1973) itakuwa chini ya Wizara mpya ya Miundombinu badala ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Usalama wa barabara na magari utatofautishwa na usalama wa raia. Wahandisi wa magari na barabara ndiyo watahusika na ukaguzi wa magari na barabara badala ya askari polisi.
4. Kwenye miji mikubwa, na hususan Dar es Salaam, ujenzi wa barabara zinazopita juu (flying roads) utaanzishwa maramoja ili kupunguza msongamano wa magari na uchelewaji kazini.
5. Matumizi na ujengaji wa reli utaendelezwa pamoja na kurudishia reli iliyong’olewa ya Mtwara hadi Nachingwea. Njia nyingine mpya za reli zitatafitiwa, kupimwa na kujengwa. Maeneo ambayo yanafaa kujengwa reli haraka ni Mtwara hadi Songea kupitia Nachingwea na Tunduru; Makambako hadi Mbambabay kupitia Mbinga; Arusha hadi Musoma kupitia Serengeti; na Tunduma hadi Mpanda kupitia Sumbawanga.

Pia CHADEMA itaweka utaratibu wa kupanua reli ya kati kutoka Shinyanga hadi Bukoba kupitia Nyakanazi na Biharamulo; na Dodoma hadi Tanga kupitia Kondoa, Kiteto na Handeni. Maeneo mengine yanayohitaji reli ni Singida hadi Arusha kupitia Katesh; Tabora hadi Mbeya kupitia Chunya; Iringa hadi Singida kupitia Manyoni; Ifakara hadi Tunduru kupitia Mahenge na Liwale; na Dar es Salaam hadi Mtwara kupitia Lindi.
6. CHADEMA itaanzisha utaratibu wa kusafirisha mafuta kutokea Dar es Salaam au sehemu zenye mafuta kwenda mikoa iliyo mbali kama Kagera, Mwanza, Arusha, Musoma, Ruvuma, Tabora, Manyara, Rukwa, Singida na Kigoma kwa kutumia mabomba ya mafuta ili kuondoa gharama za kutumia usafiri aghali wa barabara au reli na hivyo kupunguza bei ya mafuta mikoani.
7. Serikali ya CHADEMA itaweka jitihada za makusudi kwa wafanyabiashara wazawa zitakazowawezesha au kuwapa nguvu za kuimudu biashara ya uchukuzi na usafirishaji majini.

Uwezo wa wazawa kuendesha bandari umejionyesha katika kitengo cha upakiaji na upakuaji katika bandari ya Dar es Salaam ambacho kilikuwa kinaleta faida ya shilingi bilioni 10 kwa mwaka tofauti na sasa ambapo kimeshuka hadi kufikia bilioni 0.4 baada ya kubinafsishwa na wageni.
8. Sera ya CHADEMA itakazania katika ujenzi wa viwanja vya ndege utakaoendana na kutangaza utalii na vivutio vya kitaifa. Serikali ya CHADEMA pia itanunua ndege kwa ajili ya kuwakodishia au kuwakopesha wafanyabiashara wazalendo ili kuwapa uwezo wa uendeshaji na ushindani katika usafiri wa uchukuzi wa anga.


XVI. Sera ya Rasilimali
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizojaliwa utajiri wa maliasili. Ni nchi yenye mito, mabonde, maziwa, vito vya thamani, wanyamapori, milima, misitu na vingine vingi ambavyo kama vitatumika vizuri vinaweza kuliletea taifa letu maendeleo ya haraka katika sekta karibu zote.

Lengo kuu la sera hii ni kurudisha rasilimali za nchi mikononi mwa wananchi wenyewe ili wawe na wajibu na haki katika matumizi, ugawaji na utunzaji wa rasilimali zilizopo kwa manufaa ya Taifa letu.

Kimsingi sera hii ya maliasili inalenga sekta kuu sita:
1. Sekta ya Wanyapori
1. Kuhimizwa kwa wananchi wenye nia na uwezo wa kuwekeza katika maeneo yafuatayo: Ufugaji wanyamapori; Kuendesha shughuli za safari za uwindaji; Kuendesha shughuli za upigaji wa picha za wanyamapori kitalii; and Kujihusisha na biashara ya bidhaa zitokanazo na wanyamapori.
2. Kuwapa kipaumbele wazalendo katika kujifunza na kufanya utafiti wa wanyamapori.
3. Itakuwa ni marufuku kwa wageni kusafirisha au kuhamisha wanyama walio hai, badala yake kazi hiyo itafanywa na wananchi wenyewe.
2. Sekta ya Uvuvi
1. Kuwawezesha wawekezaji wazalendo kupata teknolojia ya kisasa ili kuongeza pato la Taifa kwa kuongeza kiasi cha mazao ya uvuvi.
2. Kuweka mkakati utakaowawezesha wavuvi wadogowadogo kuwa na uhakika wa soko la mazao yao. Aidha Kuweka sheria itakayowalazimu wavuvi wakubwa hasa wenye viwanda vya usindikaji kununua toka kwa wavuvi wadogo wadogo.
3. Sekta ya Ufugaji wa Nyuki
1. Lengo la sera hii ni kufanya ufugaji wa nyuki kuendeshwa kibiashara zaidi, na hii inatokana na kwamba mazao yatokanayo na nyuki bado hayajapatiwa soko la uhakika ukizingatia kwamba aina ya nyuki wanaopatikana katika nchi yetu ndiyo wanaoongoza kwa utoaji wa asali nzuri katika soko la dunia.
2. Kutolewa kwa elimu muafaka juu ya ufugaji mzuri wa nyuki kibiashara.
3. Kuongeza juhudi za kutafuta soko la nje na kuchukua jitihada za makusudi katika kuitangaza asali yetu.
4. Sekta ya Misitu
1. Kufuta utaratibu holela wa uvunaji wa misitu iliyopo hivi sasa.
2. Kuweka upendeleo kwa wananchi kuvuna na kuuza mazao ya misitu.
3. Kuhimiza uwepo wa misitu ya kupandwa.
5. Sekta ya Nishati
Kufanywa kwa utafiti wa kina zaidi juu ya matumizi ya kuni vijijini ili kupata nishati mbadala na isiyo aghali, ili kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na kukatwa kwa miti.
1. Kuwekeza katika utafutaji wa mafuta katika mwambao wa nchi yetu na kuendesha uchimbaji wake iwapo itathibitika kwamba uchimbaji wake unaweza kufanyika kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake.
2. Kuchukuliwa kwa hatua za makusudi ili kupunguza bei ya umeme. Na hili litawezekana iwapo tutakuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika.
3. Sehemu za vijijini ambako umeme haujafika, CHADEMA kitaweka utaratibu maalum wa kusambaza vifaa vya kutumia nishati ya jua kwa gharama nafuu ili wananchi waweze kulitumia kama nishati mbadala.
6. Sekta ya Utalii
1. Kuchukua hatua za makusudi ili kuimarisha miundombinu yote inayoelekea sehemu za kitalii.
2. Kuhakikisha kwamba moja kati ya kazi za balozi zetu ni kutangaza vivutio vyetu vya utalii.
3. Kuboresha na kuimarisha vituo vya utalii wa mambo ya kale, ili kuinua mapato yanayotokana na eneo hilo.
4. Wananchi waishio katika maeneo yazungukayo sehemu za kitalii washirikishwe katika mipango yote ihusuyo maeneo hayo. Aidha mipaka ya sehemu zilizotengwa kwa ajili ya utalii ni lazima ikubalike na wananchi hao.

XVII. Uchumi
1. Uchumi wa Takwimu, Umasikini kibao, kwa nini?
(a) Uchumi umekuwa kwa matajiri na wageni. Kwa Watanzania walio wengi uchumi unazidi kudorora.
(b) Bei za bidhaa zinapanda kifalaki kila mwaka-Petroli ilikuwa shilingi 450 mwaka 1995, mwaka 2005 imefikia shilingi 1,100 na inazidi kupanda.
(c) Pesa imepotea mifukoni mwa wananchi wakati maisha yanazidi kuwa ghali.
(d) Sekta zinazokuwa kwa kasi ni madini, utalii na utoaji huduma ambazo zinamilikiwa kwa kiasi kikubwa na wageni - ugenishaji
(e) Umaskini umezidi kuongezeka - asilimia 60 ya Watanzania wote maisha yao ya kiuchumi ni duni kuliko 1992.
(f) Kati ya Watanzania mia moja ni arobaini na nne tu wana uhakika wa mlo MMOJA kwa siku.
(g) Tofauti kati ya wenye kipato na wasicho nacho inazidi kuwa kubwa.
(h) Tumegeuzwa soko (dampo) la bidhaa hafifu za nje.
(i) Gharama ya kulipia mikopo holela kutoka nje inazidi kuwa kubwa – mikopo ya miradi isiyotekelezeka na miradi hewa iliyotafunwa na wajanja.
(j) Serikali ya awamu ya tatu imesambaratisha thamani ya shilingi ya Tanzania - Shilingi 575 iliweza kununua dola moja mwaka 1995, mwaka huu utahitaji takriban shilingi 1,200.
(k) Uchumi wa nchi unashikiliwa na wanaume wachache na wanawake kuwekwa pembezoni kabisa katika umiliki wa uchumi. Walio masikini zaidi katika Tanzania ni wanawake na hasa wa vijijini.
(l) Mchango wa wanawake wa Tanzania katika kukuza uchumi hauthaminishwi, mfano mchango wa kukaa nyumbani na kulea watoto na kutunza nyumba haupewi thamani ya kifedha katika kukokotoa pato la Taifa.
(m) Uchumi unakua mjini ilhali vijijini unazidi kuzorota. Umasikini wa Tanzania una sura ya Kijiji.
(n) Masharti ya mikopo ya mabenki kwa wanawake ni magumu sana.
(o) Serikali imepuuza kilimo ilihali kinachangia asilimia 44% ya pato la Taifa na 80% ya ajira.
(p) Bajeti zinapendelea walionacho - mfano kufutiwa kodi mafuta ya ndege

2. CHADEMA itafanyaje WATANZANIA WOTE wafaidi matunda ya kukua kwa uchumi?
(a) Tutatunga na kutekeleza sera za uchumi zinazojali watu maskini (pro-poor economic policies).
(b) Tutahakikisha kuwa tunatoa kipaumbele kwa sekta zinazotengeneza ajira kwa watu wengi mfano kilimo.
(c) Tutatunga na kutekeleza sera ambazo zitaweka mazingira bora kwa Watanzania kufanya biashara na hasa biashara ya kimataifa ili kuongeza ajira na kukuza pato la mtu binafsi na pato la Taifa.
(d) Tutaweka mazingira ya Watanzania kumiliki uchumi wao wenyewe na kuwezesha wanawake kushiriki katika kumiliki uchumi wa nchi yao kwa kuwapa fursa zaidi na mafunzo bora na ya kisasa zaidi.
(e) Tutafuta misamaha ya kodi kwa wawekezaji wageni isipokuwa kwenye sekta ya kilimo na mifugo tu.
(f) Tutaimarisha benki ya rasilimali (Tanzania Investment Bank) ili itoe mikopo kwa Watanzania kwa masharti na gharama nafuu na hasa kuzingatia umuhimu wa mikopo kwa wanawake ili masharti yalingane na uwezo wa wanawake na vijana katika kulipa.
(g) Tutajenga miundo mbinu ya barabara ili kurahisisha kukua kwa uchumi kwa mikoa ya pembezoni. Barabara za kuunganisha mikoa ya Rukwa, Mbeya, Tabora, Shinyanga na Kigoma zitajengwa ili kuunganisha mikoa hii na nchi nzima.
(h) Tutaelekeza halmashauri za wilaya kuanzisha benki za jumuiya pamoja vikundi vya kuweka na kukopa.
(i) Mikopo ya nje itakuwa ni kwa ruhusa ya Bunge ili kuthibiti ukopaji usio wa lazima.
(j) Kuanzisha mfumo utakaomwezesha kila Mtanzania kumiliki mali bila mizengwe- ikiwamo mali za vipaji.
(k) Sheria zote za umiliki wa mali ikiwemo ardhi zitapitiwa kwa lengo la kuhakikisha haki ya kumiliki mali hasa kwa wanawake na vijana inalindwa kisheria na kufuta sheria au kanuni zote za ubaguzi katika kumiliki mali.
(l) Tutathamini mchango wa Wanawake katika kukuza uchumi kwa kutoa vipaumbele kwa wanawake katika elimu na nafasi za kazi kama ujira wa kazi wasiolipwa ya kulea Taifa.

XVIII. Ulinzi na Usalama
Majeshi yetu tumeyarithi kutoka kwa mkoloni na kwa bahati mbaya baadhi yao bado yana ule mfumo wa utiifu (blind obedience) aliyekuwa anatarajia mkoloni kutoka kwao! Hisia za wananchi kwa baadhi ya vyombo hivi hasa Polisi na Magereza zimebaki kama ilivyokuwa kabla ya uhuru kwamba vyombo hivyo ni adui wa raia! Wananchi wanashambuliwa na polisi kwa maagizo ya wakubwa wao wa kazi wanaopokea amri zenye mnuko wa kisiasa kuliko ule wa kisheria.

Sera ya CHADEMA inajaribu kubadilisha imani, mwelekeo na maadili ya vyombo hivi ili imani ya wananchi irudi kuwa vyombo hivi vipo kwa manufaa yao na siyo kwa sababu tu ya kuwasumbua, kuwaumiza na kuwaswaga kifungoni kila wapendapo au wanapoamriwa. Vilevile inakusudia kuboresha hali duni ya wafanyakazi wa vyomho hivi. Afisa mwenye njaa kali hataacha kutumia cheo na wadhifa wake kudai na kupata rushwa kutoka kwa mwananchi. Vipi basi mwananchi huyu ataamini kuwa Afisa huyo na jeshi lake ni RAFIKI WA RAIA?
1. Hali ikoje?
(a) Utamaduni wetu wa asili unadharauliwa na kuharibiwa na tamaduni za kigeni.
(b) Mapato yatokanayo na kazi za kisanii hayalindwi ipasavyo na sheria.
(c) Watanzania wengi hawajui kuzungumza kiswahili fasaha – Kiswahili kama lugha ya Taifa hakipewi mkazo unaostahili.
2. Serikali ya CHADEMA itafanyaje?
1. Sheria za hatimiliki zitaboreshwa - adhabu kali zitatolewa kwa wakiukaji na fidia kubwa kwa waliodhulumiwa.
2. Itaagiza kila halmashauri ya wilaya kuanzisha maeneo ya makumbusho ya mila na desturi zetu.
3. Itaagiza balozi zetu kuendesha shughuli za kukuza kiswahili na kuonyesha utamaduni wetu wa asili kama kivutio kwa watalii.
4. Baraza la Sanaa la Taifa litapatiwa majukumu na uwezo wa kuendesha mashindano ya ngoma zetu za jadi kitaifa kila mwaka.
5. Itaweka mkazo wa kipekee kwenye lugha ya Kiswahili - Uswahili ndiyo umoja wetu na ndiyo utambulisho ulio wazi wa Watanzania.
6. BAKITA itaimarishwa kwa kupewa nyenzo za kazi na wataalamu zaidi.
7. Tutafungua mjadala wa kuona jinsi ya kutumia kiswahili katika kutoa elimu kwa Watanzania.



XIX. Sera ya Utawala
1. Utawala wa Ukiritimba na Urasimu, ukoje?
(a) Serikali kuu inaingilia mamlaka ya Serikali za mitaa. Katiba haipo wazi juu ya mamlaka ya serikali za mitaa.
(b) Serikali ni kubwa mno na haina ufanisi.
(c) Halmashauri za Wilaya zimebanwa, hazina uhuru wa kutosha na zinaingiliwa na watawala kutoka Serikali kuu.
(d) Wakuu wa wilaya wanaingilia utendaji wa halmashauri za wilaya na kudhoofisha demokrasia.
(e) Mikoa ni mingi sana na haina ufanisi kiutawala na kiuchumi.
(f) Mfumo wa Muungano ni tata na hautoi nafasi kwa Muungano mkubwa zaidi wa shirikisho la Afrika Mashariki.
2. Serikali ya CHADEMA itaondoa ukiritimba na urasimu kwa kufanya yafuatayo.
1. Cheo cha Mkuu wa Wilaya kitafutwa na kazi zote za Ofisi ya Mkuu wa Wilaya zitajuimshwa na Kazi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji pamoja na Meya.
2. Halmashauri za Wilaya zitapewa mamlaka na uhuru zaidi kwa mujibu wa Katiba Mpya itakayotungwa kwa ushiriki wa wananchi.
3. Mfumo wa serikali za mitaa utaimarishwa kwa kuimarisha serikali ya Kijiji kama chombo cha msingi cha uongozi (governance).
4. Mameya watachaguliwa na wananchi moja kwa moja na watakuwa na majukumu ya utendaji pia.
5. Mikoa ya sasa itaunganishwa na kuwa na mikoa kumi tu ili kuwezesha ufanisi wa kazi na pia kuleta ushindani wa kiuchumi miongoni mwa mikoa ndani ya nchi.
6. Mikoa itakayoundwa itakuwa na mabunge yao na kuchagua viongozi wao kidemokrasia.
7. Tutarekebisha mfumo wa Muungano ili kuiweka nchi tayari kwa shirikisho la Afrika Mashariki bila kuathiri uhuru na dola ya Zanzibar na Tanganyika.
8. Mabadiliko yote ya mfumo wa Utawala wa nchi yatafanywa kufuatia zoezi la kutunga katiba mpya nchi kufuatia
9. Mkutano Mkubwa wa Katiba utakaoshirikisha wananchi wote.
10. Nafasi za uongozi wa serikali zitakuwa na mtazamo mkubwa wa kijinsia.
11. Serikali itakayoongozwa na CHADEMA itahakikisha nafasi za Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Makatibu Wakuu zinashikiliwa na idadi ya kutosha ya Wanawake ili kuweka uwiano wa kijinsia katika utawala wa nchi.
12. Serikali ya CHADEMA itahakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi katika Mahakama na
13. Bunge kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake wengi zaidi kusomea sheria na kuajiriwa kuwa mahakimu wa mwanzo, wa wilaya na mahakimu wakazi na baadae kuwa Majaji.

XX. Vijana
1. Masikini Vijana wa Tanzania, kwa nini lakini?
(a) Vijana, wasichana na wavulana ni sehemu kubwa ya Taifa – zaidi ya nusu ya Watanzania wote.
(b) Vijana bado wanaonekana ni Taifa la kesho.
(c) Vijana wanatumiwa kama washabiki katika siasa - ushiriki wao katika uongozi ni finyu.
(d) Ukosefu wa ajira kwa vijana unazidi kuongezeka – Hasa vijana wa kike hawana ajira na kujikuta wanajiingiza katika vitendo vya biashara ya ngono.
(e) Vijana wenye vipaji wametelekezwa – vipaji vya vijana haviendelezwi.
(f) Vijana wengi ni hohehahe – vijana wako duni zaidi kiuchumi.
(g) Vijana wanabugudhiwa – wanakamatwa kwa uzururaji, wafanyabiashara ndogondogo wanatimuliwa!
(h) Vijana wanateketea kwa UKIMWI na madawa ya kulevya.
(i) Michezo imepuuzwa na vijana hawana cha kufanya hivo kujiingiza katika uhalifu.
2. Serikali ya CHADEMA na sura mpya ya Vijana wa Tanzania
(a) Tunaamini kwa vitendo kuwa kijana ni Taifa la Leo.
(b) Tutatoa fursa na kuwezesha kizazi kipya kuwa mstari wa mbele katika siasa, uchumi na sekta nyingine.
(c) Tutaweka mazingira ya kuundwa kwa Baraza Huru la Vijana Tanzania.
(d) Tutawezesha vijana wa kike na wa kiume kumiliki ardhi na rasilimali nyingine kwa kutenga maeneo kadhaa ya biashara kwa vijana tu.
(e) Tutaweka kipaumbele katika kukuza ajira kwa vijana kupitia vipaji vyao katika nyanja mbalimbali – tutazielekeza halmashauri kuanzisha mifuko ya ukuzaji vipaji vya Vijana.
(f) Tutaweka mazingira ya kuboreshwa kwa malezi ya Vijana katika familia na mashuleni ili kukabiliana na UKIMWI na madawa ya kulevya.
(g) Tutatoa leseni za bure na likizo ya kodi kwa Vijana wafanyabiashara ndogondogo na Vijana wanayojishughulisha na uzalishaji mali.
(h) Muziki wa kizazi kipya utapewa kipaumbele ili soko la muziki huu litakuzwa nje ya Tanzania.
XXI. Viwanda

1. Hali mbaya sana, kwa nini?
(a) Viwanda vimeuwawa kufuatia utawala mbovu.
(b) Vichache vilivyobaki vimemilikishwa na wageni.
(c) Hakuna sera dhabiti ya maendeleo ya viwanda.
(d) Hakuna sera ya kulinda viwanda vya ndani.
(e) Viwanda vidogovidogo huko Vijijini havijalwi.
2. Serikali ya CHADEMA itatatua tatizo la Viwanda kwa kufanya yafuatayo
(a) Tutatoa kipaumbele kwenye viwanda vya bidhaa za kilimo.
(b) Tutaimarisha SIDO kuwawezesha wananchi kuanzisha viwanda vidogovidogo vya usindikaji katika maeneo ya vijijini.
(c) Tutaimarisha VETA kutao mafunzo ya ufundi kwa vijana wetu wa kike na wa kiume.
(d) Tutalinda viwanda vya ndani mpaka vikue ili viweze kushindana.
(e) Tutatunga sera dhabiti za maendeleo ya viwanda na hasa viwanda vidogovidogo vya wananchi.


Wakati umefika sasa ya wananchi kuzijadili hizi sera za CHADEMA zilizoandaliwa miaka ya nyuma, na kuziboresha zaidi. Naamini viongozi wangu watasikiliza sauti ya watu na kuandaa sera nzuri zaidi. Na kuzizindua na kuzieneza kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010. Tatizo la CCM ni kuwa hawana sera na hawakubali kujikosoa.

MWISHO TUNACHOHITAJI TANZANIA SIO UZURI WA SERA TU, TUNAHITAJI VIONGOZI WAZURI WATAOONGOZA TAIFA NA KWA MUJIBU WA MATAKWA YA UMMA-AMBAYO NI SERA ZA KWELI ZINAZOJALI WATU BADALA YA MAWAZO YAO BINAFSI WANAYOYAPA BARAKA KWA KUYAITA SERA ZA CHAMA

Asha
 
Asha asante sana.

Naona hapa kuna nini (what) na kwa nini (why) nyingi sana. Kivipi (How) ndio inakosekana.
 
hapo umegusa pale ninapopasema mimi-wasiungane kwa namna waliyojaribu kufanya. Kama wanaamua kuungana kwa namna ya kuua vyama vyao, wakaunda kimoja chenye nguvu inaweza kusaidia lakini inabidi wawe na msingi mzuri wanapoingia kwenywe hicho chama kimoja, si kutoka na sentiments za kwenye vyama vilivyouawa.
Wakiwa na mentality ya ummoja zaisdi kuliko ya ubinafsi, yote yanawezekana. Kwa maana hiyo wanatakiwa kuwa waangalifu zaidi kuwa wanajiunga pamoja wakiwa na msimamo gani wa pamoja na kila mmoja apimwe nafsi yake msimamo wake binafsi katika lengo hilo la pamoja ili kuwaondoa wale ambao wanaweza kuwadhani kwua muungano huo ni opportunity ya wao kuibuka

Kinachoniogopesha ni pale uchaguzi unakaribia,, swali nani awe mgombea wetu? Kila mtu anataka kuwa Rais wa Tanzania. Wakiacha tabia ya umimi wakaweka maslahi ya watanzania mbele tutafanikiwa. Lakini wakiendelea na hii tabia ya kupenda vyeo basi hatufiki popote asilani. na waelewe tutaendelee kusikia haka ka wimbo ka siku zote ka CCM,CCM. Vyama vya upinzani tuache kufikiri tutashinda ka nguvu zetu ndogo dhidi ya hili Jidudu. Wakati umefika wa kuungana na kufanya yale waliyofikiri hayawezekani kuwa sasa yanawezekana. La sivyo tutaingia makaburini bila kuona upinzani wa kweli.
 
Watanzania amkeni! Ukombozi wa pili wa Bara la Afrika umeanza.

Kama nchi yetu ilikua ni miongozi mwa nchi za mwanzo kupata uhuru itakua ni aibu kama tutabaki nyuma katika ukombozi huu wa pili unaojumuisha ukombozi wa kifikra, kimaisha, kivisheni na kimisheni.

Wenzetu Kenya tuliowatangulia kupata Uhuru wa kwanza tayari wametutangulia kupata nuru ya uhuru wa pili. Zimbabwa wamefika nusu ya uhuru kamili wa pili, Ethiopia moto unafukuta siku yoyote utalipuka, Zambia nao wametenda licha ya Bwana Rupia Banda kucheza rafu. Congo-DRC, Rwanda, Burundi walitangulia kitambo. Hata Uganda nao walishafanya kweli ila inasikitisha kwamba baada ya kuondoa kisiki wameweka gogo (MUSEVENI). South Afrika nako siku yoyote kutakucha.

CCM inaelekea kuwa dikteta. Na dalili ziko wazi. Kwanza wameanza kushindana na vyombo vya habari. Pili viongozi wake wameshindwa kupambana kihoja na hivi sasa wanakumbatia matusi (CHILIGATI). Viongozi wa CCM wamekiuka miiko ya viongozi. Wengi wachumia tumbo badala kutumikia wananchi. Haya ni machache ya mengi tunayoyajua.

Tuendelee kujadiliana.
 
Mkuu Masanja kalalama: Watanzania wenzangu tunaonekena punguani tunaposema eti "Chadema ni chama kizuri lakini hakina watu wengi wa maana kwa hiyo hata tukiwapa nchi itawashinda kuongoza" Sasa watu wazuri ni sisi tulio busy tuki-criticize Chadema..why not join them? au unafikiri watu wazuri wa kujiunga na Chadema watatoka sayari ya Mars? ni mimi na wewe! Ni sisi inaobidi tuingie kwenye mapambano. Its really unfair kudelagate wajibu wako wa kutafuta mabadiliko kwa Zitto! You cant delegate your right and duty to be at the battle front!

Chadema or CUF OR ANY OTHER POLITICAL PARTY with genuine interests to rid Tanzania of our current ENEMY who is CCM deserve our assistance!

Nadhani Masanja hatutendei haki akisema tunaonekana punguani sie tunaohoji kwa nini tuwape CHADEMA uongozi midhali tunaona kwamba CCM imekengeuka haifanyi vizuri katika kuliongoza Taifa.

Tukiacha ule ushabiki wa “Yanga na Simba” usio na mantiki, naamini kwamba wengi wetu tunachangia mawazo yetu kuhusu CHADEMA na mikakati yake kwa nia njema maana naamini lengo letu Watanzania wazalendo ni kuona kwamba nchi yetu inapiga hatua kimaendeleo na kudumisha amani na utulivu tulivyorithishwa na watu waliokuwa na uzalendo uliojaa hekima na upendo mkubwa kwa nchi yao kiasi cha kuamua kuishi na kufa maskini ili kutunza heshima ya Taifa letu.

Hivi sasa tuna vyama. Mimi nikiwa mwanachama wa CCM wa miaka nenda rudi, siwezi kukurupuka nikajiunga na CHADEMA kwa kuwa kinapinga maovu ya CCM bila kupata maelezo yatakayoniridhisha kwamba chama hicho kina dhamira ya kweli ya kutaka kuongoza nchi kwa manufaa ya wananchi wote.

Yametolewa maelezo mazuri ya sera, malengo, mikakati ya kutaka kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania na kwamba CHADEMA siasa yao ni ya ‘mrengo wa kati’.

Watanzania, ni wale walio mijini na vijijini, wapo wasomi wa ngazi mbali mbali wakiwemo na wanafunzi wanaowania kuwa wasomi siku ya siku. Lakini, asilimia kubwa katika kipindi hiki tulichonacho, ni watu wa kawaida wa vijijini na sie wa jikoni na vijiweni ambao hatujui mrengo wa kati ni kitu gani, hata tofauti kati ya soko huru na soko huria hatuijui. Tunahitaji maelezo kwa lugha nyepesi.

Kwa maana hiyo, bado nasema kwamba CHADEMA wana kazi kubwa ya kutuelimisha ili tukubali kujiunga nao, na turidhike kwamba tutakapowapa uongozi hatutakuja kusononeka huko mbele ya safari. Nia njema haitoshi tunahitaji uthibitisho wa nia hiyo njema.

Nimesoma haraka haraka na kuona orodha ya mambo ambayo CHADEMA wanasema wanadhamiria kuyafanyia kazi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi na bila shaka kwa mabadiliko hayo kuleta maendeleo kwa wananchi walio wengi na si wachache.

Pengine ‘ujikoni’ unanizidi lakini nadhani pamoja na maelezo mazuri ya sera, mikakati, n.k. kilicho muhimu ni kuondoa kwanza KERO zilizopo katika jamii zinazosababisha Serikali ya CCM ionekana haifai tena kuongoza. Kwa mfano:

UBADHILIFU
Leo katika kuzurura mitaani nilipita mtaa wa Jamhuri lilipo jengo la Wizara ya Elimu ya Juu, nilikuwa sijapita siku nyingi. Nilipata mstuko kuona nguzo na kuta za jengo hilo kwa nje zimepambwa kwa vigae vya marumaru. Mie wa mwaka 47 nikajiuliza, hivi kuta hizi zingelipakwa chokaa tu au rangi za makopo za siku hizi si jengo lingependeza tu, kulikuwa kweli na ulazima kutumia fedha nyingi kununua marumaru? Hiyo ni wizara moja, sijui Wizara zingine kuna marembesho ya aina gani yasiyo ya lazima. Gazetini au humu JF nilisoma kwamba siku hizi ni fasheni, ofisi za Serikali, Mashirika ya Umma, na za Binafsi huagiza ama hununua nchini fenicha kutoka Dubai na kwingineko nje ya nchi. Fenicha za Keko siku hizi hakuna ofisi ya Serikali inayonunua!

Mambo ya aina hii yanaweza kuonekana ni madogo lakini ni kero kubwa. Ubadhilifu huo na mwingine wa aina hiyo, ndiyo mambo yanayorudisha nyuma kupatikana kwa ‘maisha bora kwa kila Mtanzania’. Kabla ya kujiunga na CHADEMA tunataka tuelewe kuna mikakati gani na mbinu gani zilizoandaliwa ama zitakazotumika kutoondolea kero ya Ubadhilifu?

RUSHWA
Siku hizi ukienda sehemu yoyote ile ya huduma inabidi utoe ‘kitu kiduchu’ ili upate huduma. Ma-secretary wa mwaka 47 walikuwa wakiruhusu wageni kuona ma-boss bila mikwala yoyote lakini wenzetu wa leo mpaka utoe ‘chai’ ndio ufikiriwe kupata appointment! Jijini Dar es Salaam pamoja na Kamanda Kova kuja na ‘moto’ alioingia nao jijini, hadi jana ‘Wazee wa Feza’ bado wanapokea buku tatu ama mbili kila wanaposimamisha daladala barabarani! Rushwa kubwa siwezi nikazielezea maana sie wajikoni hatuna uzoefu nazo. CHADEMA watudokezee kidogo tu watakapoingia madarakani watajipanga vipi ama watatumia mbinu gani kupunguza ama kukomesha RUSHWA iliyokithiri nchini.

UKABILA/UDINI
Wapo wanaojidanganya na kusema kwamba kudai kuwa nchi imeshaanza kurudi kwenye ukabila na udini ni uzushi. Maaskofu na Masheikh wakishaanza kulumbana kuhusu jambo lolote lile, kama huo si udini ni nini? Wanachama wa chama fulani, wafanyakazi wa ofisi, hata waumini wa kanisa wakiishaanza kulalama kwamba kuna ukabila katika maeneo yao, ni wazi suala la ukabila linarejea nchini. CHADEMA kuna mikakati gani kuhusu kero hii? Yataanzisha makongamano ama yatatumika majukwaa kuhubiri?

MUUNGANO
Tukiwapa uongozi CHADEMA mwaka 2010, kama muafaka haujafikiwa kati ya CCM na CUF, Serikali mpya itafanya nini kuhusu kero hii? MUUNGANO wenyewe je? Tunataka tujue mtauvunja turudi Tanganyika, ama mtafanya kila juhudi kuuimarisha ili hatimaye tuwe na Serikali moja, ama mtakuwa na Sera ya Serikali Tatu?

ITIKADI YA CHAMA
Hao asilimia 70 au 80 na ushei walio vijijini na akina sie wa jikoni na vijiweni, mara kwa mara tunalinganisha masuala na itikadi tuliyoizoea ya Ujamaa na Kujitegemea. Nimesoma CHADEMA mna itikadi ama siasa ya ‘Mrengo wa Kati’. Kazi ipo ya kutuelimisha akina sisi tuelewe maana ya huo mrengo wa kati. Tuone huo Mrengo wa Kati utatuondoleaje matatizo ya barabara za mashimo mijini na vijijini, mrengo utazibuaje mitaro ya maji machafu nayayotiririka kutokana na tatizo la watu kujenga nyumba kiholela bila kufuata utaratibu. Mrengo utatusaidiaje kupata maji ya safi na salama wakati wote. Naweza nikaorodhesha kero na nisimalize.

UFISADI
Naamini suala la ufisadi ni pana kwa sababu linahusiana na vipengele vyote vya kero. Hata kama tutafuata Mrengo wa Kati katika harakati za kiuchumi bado Ufisadi unaweza ukajitumbukiza na kuwepo humo humo!

Kama nilivyosema awali, nia si kuwakatisha tamaa CHADEMA wasipate wafuasi ama watu wasijiunge na Chama hicho. Haya ni mawazo ya mwananchi wa kawaida kama walivyo wananchi wengi wa Tanzania. Hayana hata chembe ya usomi ndani yake, lakini ni mawazo ambayo yanaweza kuwemo katika vichwa vya asilimia kubwa ya wapiga kura wanaotaka kujiridhisha kwamba hawafanya makosa mapya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom