Ninachofurahia zaidi ni kitu ambacho nilikisema kwa miaka mingi kuwa timu za bongo, hasa kubwa zinataka kocha ambaye hababaikiii wafadhili, habembelezi players na kuwakumbatia wanaojiona mastaa, na ofcoz anaujua mpira na saikolojia ya mpira. Huyu jamaa logi ameonyesha wazi katika siku chache kuwa anaweza kuleta mafanikio makubwa sana kwa Simba na hata taifa zima. Kuweza kujenga saikolojia ile mechi ya mtani jembe wakati YY wanatamba na timu yao mastaa akiwemo kwi kwi sio jambo dogo
Ona sasa alivyousuka ukuta na nidhamu ya timu kwa ujumla !! Hata YY wameanza kuiga styles zake za kukata mishahara wavivu na wanaochelewa kurudi kutoka likizo, ofcoz tulijua messi mzuri lakini ona sasa hivi !!
Sasa tukipata viongozi wazuri, wanaoujua mpira na waliopo kwa maslahi ya timu tutafika mbali zaidi. Wakitulia vizuri simba, mwambieni Logi atutafutie kocha mzuri kwao afundishe na kusimamia simba B !! Wala hatutakuwa na haja ya ma pro uchwara wa rwanda, tutatengeneza players na kuwauza kama SamaGoal, then labda kununua ma pro 1, 2 kutoka magharibi sasa na/au nchi zilizo juu zaidi ktk soka !!
Mwenyekiti ana bastola lakini timu haina website :sad: