Nukuu ya hotuba Shaka Hamdu Shaka katika uwekaji jiwe la msingi ofisi ya CCM wilaya Musoma Vijijini - 02 Februari 2022

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
NUKUU YA HOTUBA YA KATIBU MWENEZI SHAKA HAMDU SHAKA KATIKA UWEKAJI JIWE LA MSINGI OFISI YA CCM WILAYA MUSOMA VIJIJINI 02 FEBRUARI 2022

"Uamuzi wa kuanza kuyaunganisha Mataifa ya Tanganyika na Zanzibar baadae vikaungana TANU na ASP Februari 5 Mwaka 1977 laiti hatua hizo zisingefanyika kwa haraka wakati ule utulivu wa ndani huenda ungebaki mashakani" Shaka Mwenezi Taifa

"Kitendo cha kuviunganisha vyama, tija yake kumekiongezea CCM nguvu za kisiasa na kiuchumi, kuimarika utulivu wa ndani, kuongezeka mitaji, rasilimali watu na vyanzo vya mapato" Shaka Mwenezi Taifa

"Bila uamuzi huo wa kihistoria kuamuliwa maadui wa ndani na nje wangepata mwanya na wepesi wa kulivuruga Taifa" Shaka Mwenezi Taifa

"Hatua ya kuunganisha vyama si kwamba ilikuwa ni ya kizalendo, pia ilifanikiwa kuzima ndoto batili za wasaka madaraka na kudhibitiwa wanasiasa wakorofi ambao walishindwa kutekeleza mbinu chafu za uchochezi na usaliti" Shaka Mwenezi Taifa

"Waasisi wa Taifa walipima kwa darubini kali za kisiasa hatua iliokifanya ccm kijikite na kushiriki moja kwa moja katika harakati za mapambano ya ukombozi Kusini mwa Afrika na kufanikiwa kujiweka kando ya vita baridi ambayo iliigawa dunia Mashariki na Magharibi" Shaka Mwenezi Taifa

"Tunawapa heko wasisi wetu kwa uamuzi wa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar baadae TANU na ASP kuungana mwaka 1977, Kwakweli lilikuwa pigo takatifu dhidi ya maadui wa kisiasa. Waasisi wetu kimsingi walitafakari kwa kina hadi kupitisha misimamo thabit kwa maslahi ya Taifa " Shaka Mwenezi Taifa

" Kadri unaposoma vitabu vya historia na nakala za mapitio ya mapambano ya kisiasa, utayaona mataifa ya Afrika yalivyoendelea kusakamwa kwa mbinu chafu huku maadui wa ndani wakitumiwa kama vibaraka ili kuvuruga ustawi wa amani na utulivu" Shaka Mwenezi Taifa

"Hatua ya kupiga marufuku mfumo wa vyama vingi kwa wakati ule kulizifunga njia za panya na milango ya vichochoroni . Sehemu kubwa ya mataifa ya Afrika baada ya kujitawala yalikubali chama kimoja yakihofia kuundiwa mizengwe na utapitapi wa kisiasa"
Shaka Mwenezi Taifa

"Wakati CCM kikifikisha miaka 45 toka kuzaliwa kwake, kimefanikiwa kuwaunganisha wananchi, kusimamisha umoja na kuunda mtandao wa uendeshaji wa siasa zake kwa uwazi kwa uhakika na utendaji wa pamoja" Shaka Mwenezi Taifa

"Ni jambo la kujivunia kuwa na taasisi yenye mizizi mirefu ya kisiasa, kinachojiendesha kimfumo, kimaadili, kinidhamu na hata kutoa maamuzi mazito kwa mujibu wa katiba yake kanuni , miiko na taratibu zake " Shaka Mwenezi Taifa

"Wakati huu Tanzania ikiwa na vyama vingi vya siasa ni fahari ilioje kuwa na taasisi imara ya kisiasa iliyoimarika, kuheshimika mbele ya uso wa dunia huku baadhi ya vyama vikishindwa kujiendesha kwa uwazi, vikikosa demokrasia ya ndani na viongozi wake wakifukuzana kibabe" Shaka Mwenezi Taifa

"CCM hakimfukuzi kiongozi au mwanachama wake bila kumkusanyia ushahidi wa makosa yake kinyume yanayokiuka katiba , kanuni na taratibu. Pia kiko tayari kuwapokea wanachama waliofukuzwa au wenyewe kujiondoa baada ya kukidhi matakwa yaliowekwa kwa mujibu wa katiba ya CCM "
Shaka Mwenezi Taifa

End

IMG-20220202-WA0093.jpg
 
Wakati huu Tanzania ikiwa na vyama vingi vya siasa ni fahari ilioje kuwa na taasisi imara ya kisiasa iliyoimarika, kuheshimika mbele ya uso wa dunia huku baadhi ya vyama vikishindwa kujiendesha kwa uwazi, vikikosa demokrasia ya ndani na viongozi wake wakifukuzana kibabe"

Shaka Mwenezi Taifa

Kwa maneno haya nadhani wao hawana utamaduni wa kufukuzana kibabe, ndo maana mdogo wake na mkwere atakuwa alijiondokea kurudi kusini. Na sidhani kama wanamakundi ndani ya chama chao. Najaribu kujiuliza kama huyu ni team group ya chifu hangaya ndo maana kasema hivi au la sina hakika sana. Ila bado Nina maswali mengi kuhusu hii hotuba ngoja nieendelee kutafari huenda ..........
 
NUKUU YA HOTUBA YA KATIBU MWENEZI SHAKA HAMDU SHAKA KATIKA UWEKAJI JIWE LA MSINGI OFISI YA CCM WILAYA MUSOMA VIJIJINI 02 FEBRUARI 2022

"Uamuzi wa kuanza kuyaunganisha Mataifa ya Tanganyika na Zanzibar baadae vikaungana TANU na ASP Februari 5 Mwaka 1977 laiti hatua hizo zisingefanyika kwa haraka wakati ule utulivu wa ndani huenda ungebaki mashakani" Shaka Mwenezi Taifa

"Kitendo cha kuviunganisha vyama, tija yake kumekiongezea CCM nguvu za kisiasa na kiuchumi, kuimarika utulivu wa ndani, kuongezeka mitaji, rasilimali watu na vyanzo vya mapato" Shaka Mwenezi Taifa

"Bila uamuzi huo wa kihistoria kuamuliwa maadui wa ndani na nje wangepata mwanya na wepesi wa kulivuruga Taifa" Shaka Mwenezi Taifa

"Hatua ya kuunganisha vyama si kwamba ilikuwa ni ya kizalendo, pia ilifanikiwa kuzima ndoto batili za wasaka madaraka na kudhibitiwa wanasiasa wakorofi ambao walishindwa kutekeleza mbinu chafu za uchochezi na usaliti" Shaka Mwenezi Taifa

"Waasisi wa Taifa walipima kwa darubini kali za kisiasa hatua iliokifanya ccm kijikite na kushiriki moja kwa moja katika harakati za mapambano ya ukombozi Kusini mwa Afrika na kufanikiwa kujiweka kando ya vita baridi ambayo iliigawa dunia Mashariki na Magharibi" Shaka Mwenezi Taifa

"Tunawapa heko wasisi wetu kwa uamuzi wa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar baadae TANU na ASP kuungana mwaka 1977, Kwakweli lilikuwa pigo takatifu dhidi ya maadui wa kisiasa. Waasisi wetu kimsingi walitafakari kwa kina hadi kupitisha misimamo thabit kwa maslahi ya Taifa " Shaka Mwenezi Taifa

" Kadri unaposoma vitabu vya historia na nakala za mapitio ya mapambano ya kisiasa, utayaona mataifa ya Afrika yalivyoendelea kusakamwa kwa mbinu chafu huku maadui wa ndani wakitumiwa kama vibaraka ili kuvuruga ustawi wa amani na utulivu" Shaka Mwenezi Taifa

"Hatua ya kupiga marufuku mfumo wa vyama vingi kwa wakati ule kulizifunga njia za panya na milango ya vichochoroni . Sehemu kubwa ya mataifa ya Afrika baada ya kujitawala yalikubali chama kimoja yakihofia kuundiwa mizengwe na utapitapi wa kisiasa"
Shaka Mwenezi Taifa

"Wakati CCM kikifikisha miaka 45 toka kuzaliwa kwake, kimefanikiwa kuwaunganisha wananchi, kusimamisha umoja na kuunda mtandao wa uendeshaji wa siasa zake kwa uwazi kwa uhakika na utendaji wa pamoja" Shaka Mwenezi Taifa

"Ni jambo la kujivunia kuwa na taasisi yenye mizizi mirefu ya kisiasa, kinachojiendesha kimfumo, kimaadili, kinidhamu na hata kutoa maamuzi mazito kwa mujibu wa katiba yake kanuni , miiko na taratibu zake " Shaka Mwenezi Taifa

"Wakati huu Tanzania ikiwa na vyama vingi vya siasa ni fahari ilioje kuwa na taasisi imara ya kisiasa iliyoimarika, kuheshimika mbele ya uso wa dunia huku baadhi ya vyama vikishindwa kujiendesha kwa uwazi, vikikosa demokrasia ya ndani na viongozi wake wakifukuzana kibabe" Shaka Mwenezi Taifa

"CCM hakimfukuzi kiongozi au mwanachama wake bila kumkusanyia ushahidi wa makosa yake kinyume yanayokiuka katiba , kanuni na taratibu. Pia kiko tayari kuwapokea wanachama waliofukuzwa au wenyewe kujiondoa baada ya kukidhi matakwa yaliowekwa kwa mujibu wa katiba ya CCM "
Shaka Mwenezi Taifa

End

Kazi nzuri sana Ndg Shaka
 
Back
Top Bottom