Nuclear physicist recalling his knowhow..............after years of intellectual hibernation | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nuclear physicist recalling his knowhow..............after years of intellectual hibernation

Discussion in 'Jamii Photos' started by Rutashubanyuma, Mar 30, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,254
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwauliza maswali ya masomo ya Fizikia na Kemia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Edward Lowassa Wilayani Monduli, alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea majengo ya shule hiyo pamoja na kuangalia maendeleo ya wanafunzi hao. Makamu wa Rais yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya siku nne ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. (Picha na Amour Nassor)
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,254
  Trophy Points: 280
  Hivi mtanzania anapokwenda ng'ambo kusomea nuclear physics kwenye miaka ya sitni au ya sabini wakati sisi hatuna uwezo wa kutumia utaalamu wake.................................hivi kweli huyo msomi ni kiongozi wa kutumainiwa????????????????????
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Ama kweli, ikiwa wa Tanzania tunafikra na kuhoji maswali kama yako ndio maana tupo hapa tulipo. Kwa nini kusomea Nuclear Physics iwe haina faida? Au wewe unafikiri nuclear physics hutumika kwenye kutengeneza mabomu tu?

  Kama fikra zako ni hizo, basi umekosea tena sana. Nuclear Physician ana manufaa makubwa katika nchi na huweza kutumika ama kufundisha wengine ili muwe na wataalam wengi wa kutosha kwa maendeleo. Kumbuka, nchi haiwezi hata kupewa ruhusa ya kuwekeza katika nuclear energy (umeme) kama haina wataalam wake wenyewe.

  Kuna kitu inaitwa "nuclear medicine" sijui kama umeisikia? Kama ndio, unahitaji wataalam, jee kama hauna wasomi utakuwa na uwezo wa kuwekeza huko? Namjuwa mTanzania mwingine bingwa wa nuclear medicine anaitwa Dr. Mohamed Tuli, na Mwingine Bin Daar, wote watoto wa Kariakoo (kwenye vibaraghashia) na tunawahitaji sana.

  Leo Tanzania tuna uranium, bila kuwa na hawa watu japo kutushauri tu namna ya kuiuza na "grading" si tutapakwa vumbi la macho tu?

  Elimu haina mwisho na hata kama hauitumii hapa, ukiajiriwa tu nje na kutuma vijisenti nyumbani unakuwa umeisaidia sana nchi yako.
   
 4. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145  Tatizo letu kubwa ni kuwa mara nyingi huwa "tunaua mbu kwa kutumia Atomic bombs",naomba utafakari kauli hii.
   
 5. BongoLogik

  BongoLogik JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nuclear Physician ndo nani? au unamaanisha Nuclear Physicist!
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Inawezekana, physicist na physician pia (anaetibu kwa kutumia nuclear medicine ni nuclear physician).
   
 7. G

  Gathii Senior Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu!
  Umefanya kitu kimoja sahihi;kujaribu kumueleza aliyehoji umuhimu wa wataalam wa Nuclear physics na wapi wanaweza kutumika (ingawa sina hakika kama kweli wametumika ipasavyo),ni kitu chema kumpa elimu mtu mwingine ambaye hakuwa na ufahamu ulio nao..Lakini sioni sababu ya msingi ya kuwapamba na "wote watoto wa Kariakoo (kwenye vibaraghashia) " sioni inamsaidiaje mtu mwingine kuelewa umuhimu wa hao wataalamu wa Nuclear Physics.
  Ni kweli kuwa na wataalamu wa hiyo "Nuclear medicine" ni kitu chema,lakini kupata manufaa na wataalamu hao kunahitajika zaidi ya kuwa na hao wataalamu-mifano michache tu,tuna Professors in Geology lakini embu tuone yanayotokea kwenye sekta ya madini leo hii,nini tunafaidika?na wataalamu tunao?embu angalia Tanzanite inavyohujumiwa...Tuna madaktari bingwa wengi tu wako Amerika na Ulaya achilia mbali nchi kama South Afrika na Botswana,nini mwananchi wa kawaida anafaidika na hao wataalamu??
  Ni mtazamo tu!!
   
Loading...