Fitinamwiko
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 4,803
- 1,416
Mwananchi Jumatano Septemba 4, 2013 "Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni wa mwaka 2013 uliokuwa ujadiliwe katika mkutano wa 12 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma, umeondolewa na sasa utajadiliwa Bunge lijalo. Habari za uhakika zilizopatikana jana, zilisema kwamba kuahirishwa huko kumetokana na wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge wanaotoka Zanzibar kupinga vikali kura ya maoni kupigwa visiwani humo kwa kuwa tayari huko kuna sheria hiyo." Katika miungano ya kweli Federal law supersedes state law, lakini hili muungano wazanzibar wanahisi wao ni nchi. Kuna kero chungu mzima zinazotokana na utata wa hili limuungano. Kuna gharama kubwa sana kuendesha limuungano hili, Marais wawili, mmoja amekuwa kama TV, remote ipo magogoni. Jimbo la Zanzibar lina makamo wa Rais wawili, mmoja kazi yake ni kupakia mikaa/mihogo ndani ya ndege ya Rais. Hizi gharama zote zisingekuwepo kama tungekuwa na Rais mmoja na waziri wakuu wawili Tanganyika na Zanzibar.