NSSF yaelekea kufilisika

Wanajamvi heshima mbele,

NSSF imeanza zoezi la kuwabembeleza/kulazimisha wateja wake wakubwa [waajiri] kutoa mchango yao ya kila mwezi kabla ya wakati.Ni kawaida waajiri kupeleka michango ya kila mwezi mmoja nyuma[mfano mshahara wa mwezi tano michango yake inatakiwa ipelekwe mwezi sita],sasa NSSF inawataka waajiri wakubwa [waajiri wenye idadi kubwa ya wafanyakazi] kupeleka michango ya wafanyakazi mwezi mmoja mbele au mwezi huu wa sita ili kukabiliana na hali mbaya ya fedha inayoliandama shirika hilo la wafanyakazi nchini.

Taarifa toka chanzo cha uhakika ndani ya shirika hilo zinadai serekali imechota fedha toka NSSF kwaajili ya kugharamia mishahara ya watumishi wake baada ya chanzo chake muhimu cha mapato TRA kushindwa kupata fedha za kutosha kulipa mishahara ya watumishi wa serekali pamoja na shughuli nyingine muhimu.

Zipo taarifa za uhakika serekali ina mkakati wa kuwalazimisha wanachama wote wa NSSF na mashirika mengine ya hifadhi ya jamii kutokulipwa mafao yao hadi wafikishe umri wa kustaafu.Mkakati utasaidia kukabilia na upungufu mkubwa wa fedha unaotarajiwa kutokea kwakuwa fedha zinazochotwa na serekali hazitarajiwi kurejeshwa.

Source:Ngongo@Arusha.
WAO WANAWAKOPESHA Matajiri wasiojua kurudisha wanategemea nini?tena hovyo hovyo tu wacha wafilisike ilmradi watu wachii wapate hela zao za hifadhi,MAGAMBA YAKISHAINGIA MAHALI NDIO FINAL REPORT HIZO SIKU ZOTE.ALAFU WATAWABANA WATU WENGINE WACHINI NAKUWAACHA WADENI WAO WAKUBWA.
 
Mkuu Crashwise,

Mkuu wangu hata mimi niko katika harakati za kujiari hii sheria ikipitishwa itakula kwangu vibaya sana kwasababu vijisent vya NSSF ni sehemu ya mtaji wa shughuli ninayotarajia kuendeleza.

Sijui niache kazi kabla hakijanuka maana mwaka huu ni wa mwisho nijiajiri sasa nikisubiri si itakula kwangu.....
 
Mkuu Froida,

Mkuu wangu hili zoezi lilianza wiki ilipita hapa Arusha maafisa NSSF wamezunguka kampuni zote zenye wafanyakazi zaidi ya 20 na kuendelea.Bahati nzuri maafisa wa NSSF walipokuja ofisini kwangu nilipata wasaa wa kuhojiana nao na wakanieleza ni zoezi la Tanzania nzima ingawa linafanywa kwa siri na kwa uangalifu mkubwa.

Fedha za NSSF ni kama shamba la Bibi hakuna uwazi wa kutosha,hakuna uangalizi wa kutosha,hakuna uadilifu.NSSF ni sehemu ambayo wanasiasa wanachota fedha hovyo kwa faida za kisiasa[miradi ya kisiasa eg daraja la kigamboni & UDom].Wafanyakazi [wadau au ukipenda wanahisa wakuu] hawana mwakilishi halisi ndani ya bodi ya shirika wajumbe wote wa bodi ni wateule wa waziri wa kazi na mwenyekiti ni mteule wa Rais.

Hakika tungewapata wanasiasa aina ya Mch Mtikila au wanasheria mahiri ningefungua kesi mahakama kuu kupinga fedha zangu kuchukuliwa kwa nguvu na kutokuwa na msimamizi mwenye uakilishi wa wafanyakazi.
Yeah-wamepita hata hapa kazini kwetu,...nikawauliza kwamba inakuwa vip watu wasubiri mpaka kustaafu(60 yrs),..wakati life expectancy ya mtanzani inagomba,...wakajiumauma.....then wakasema eti ni mpango wa serikali ili watu wake wasipate shida wanapositaafu.....eti hata ulaya wanafanya hivyo.

Pooor nssf
 
Shemeji mbona unanitisha hiyo NSSF naitegemea eti baada ya kuacha kazi karibuni sasa kama ni kimbembe kuipata unanifanya nichanganyikiwe na nizidi kuichukia zaidi serikali ya CCM....hivi chama cha wafanyakazi kiko wapi au wamesha katiwa chao..............

Yaani wala usiitegemee kihivyo,nilikanyagia mpaka nikachoka, pale kuna watu ambao sijui niwaeleze vipi, yaani wanavyozungusha utafikiri ile pesa ni ya kwao kwa hiyo wewe unaomba msaada, Jaribu siku moja kwenda, fanya kama umeenda kutembea utakayo yaona hapo we mwenyewe utashangaa.
 
Mkuu IGWE,

Hata ukibahatika kufikisha 60 years bado watakachokulipa hakifanani na thamani ya fedha zako ulizochangia wafanyakazi tunanyonywa sana hakuna TUCTA wala mjomba wa kutusemea bora kuacha kazi wakati bado una nguvu kuliko kusubiria kiinua mgongo kiduchu.

Yeah-wamepita hata hapa kazini kwetu,...nikawauliza kwamba inakuwa vip watu wasubiri mpaka kustaafu(60 yrs),..wakati life expectancy ya mtanzani inagomba,...wakajiumauma.....then wakasema eti ni mpango wa serikali ili watu wake wasipate shida wanapositaafu.....eti hata ulaya wanafanya hivyo.

Pooor nssf
 
Duh hapa nimemtambua Jafari Abrahamani aliyekaa katikati wengine siwakumbuki.

rd.jpg
 
Mkuu Froida,

Mkuu wangu hili zoezi lilianza wiki ilipita hapa Arusha maafisa NSSF wamezunguka kampuni zote zenye wafanyakazi zaidi ya 20 na kuendelea.Bahati nzuri maafisa wa NSSF walipokuja ofisini kwangu nilipata wasaa wa kuhojiana nao na wakanieleza ni zoezi la Tanzania nzima ingawa linafanywa kwa siri na kwa uangalifu mkubwa.

Fedha za NSSF ni kama shamba la Bibi hakuna uwazi wa kutosha,hakuna uangalizi wa kutosha,hakuna uadilifu.NSSF ni sehemu ambayo wanasiasa wanachota fedha hovyo kwa faida za kisiasa[miradi ya kisiasa eg daraja la kigamboni & UDom].Wafanyakazi [wadau au ukipenda wanahisa wakuu] hawana mwakilishi halisi ndani ya bodi ya shirika wajumbe wote wa bodi ni wateule wa waziri wa kazi na mwenyekiti ni mteule wa Rais.

Hakika tungewapata wanasiasa aina ya Mch Mtikila au wanasheria mahiri ningefungua kesi mahakama kuu kupinga fedha zangu kuchukuliwa kwa nguvu na kutokuwa na msimamizi mwenye uakilishi wa wafanyakazi.

Kwa kweli tukizungumzia kauli ya JJ Mnyika sisi wafanyakazi ni dhaifu,wazembe na wapuuzi,hivi kweli tangu enzi za kina Sumaye,,kikwete,Lowassa,Rostam,Dewji,Manji wote hao kwa uchache wao na wengine wengi wamechezea fedha zetu sisi tumekaa tuu , utafikiri miili yetu haipukutiki tunapooelekea kwenye miaka sitini,hivi ni kwa nini hatujitambui mpaka watu watoke waliko toka waachote mapesa wajineemeshe na familia zao kweli wafanyakazi wa nchi hii hatuna maana kabisa
 
Yeah-wamepita hata hapa kazini kwetu,...nikawauliza kwamba inakuwa vip watu wasubiri mpaka kustaafu(60 yrs),..wakati life expectancy ya mtanzani inagomba,...wakajiumauma.....then wakasema eti ni mpango wa serikali ili watu wake wasipate shida wanapositaafu.....eti hata ulaya wanafanya hivyo.

Pooor nssf
Kwa hiyo ni confirmed kwamba kama hujafikisha miaka ya kustafu hakuna mkwanja....
 
NSSF ni wezi waliohalalishwa kisheria. Ni bora mtu unapoanza kazi ukaelewa kabisa kwamba unaibiwa na huna jinsi ya kuzuia. Usifanye kosa la kutegemea NSSF itakufaa unapostaafu. Wengi walioitegemea wamekufa mapema kwa kushindwa kujikimu. Usivae viatu hivyo.
 
Mkuu Masuke kama sheria itabadilishwa maana yake itabidi usubiri hadi utakapofikisha miaka sitini.Hapo hapo lazima utie akili wastani wa umri wa mtanzania ni chini ya hiyo miaka sitini ?.Jiulize serekali ina mpango gani na wafanyakazi wa nchi hii.

Ngongo ukitoa chuki yako binafsi na Lema michango yako mingine naipa uzito mkubwa sana nikiamini katika uchangiaji wako ambao unakuwaaga na mashiko.

Lakini pamoja na hayo, nakukatalia kuwa serikali ina mpango wa kubadilisha sheria hiyo kwa kisingizio cha kukosa kuwalipa wastaafu ambao wanastaafu kabla ya miaka ya sitini.

Naamini kweli serikali yetu ipo ICU kimapato na hilo la kuchota pesa NSSF linawezekana lakini si la kufikia kumdhulumu mtu alistaafu kazi chini ya miaka 60 eti mpaka afike hapo!!!!!!
 
Miradi mingi waliyowekeza hailipi au italipa baada ya miaka mingi sana ndio maana hali yao mbaya ukijumlisha na serikali ndio imegeuza shamba la bibi kwishne.
 
Mkuu Mzee wa Rula.

Napenda kukanusha kwamba nina chuki na Lema.Hapana sina chuki ila Lema akipotoka namkosoa,Kikwete akikoseanamkosoa,Freeman akikosea namkosoa bila taabu yoyote.Pengine hii yawekuwa kuw atofauti yangu mimi na wewe.Najua wapo wanazi wa CDM ambao kumkosoa kiongozi wake ni dhambi kuu ni sawa na kuvunja amri kumi za Mungu ndiyo wapo wanachama wa CCM wenye mtazamo huo huo.

Kuhusu NSSF kuwalipa wafanyakazi mafao hadi watakapofikisha miaka 60 mkuu wangu hili si pendekezo la serekali bali ni hali halisi ya NSSF ambayo serekali wameisababisha kwa kiasi kikubwa.Serekali inajua kabisa wakipush hili suala bila maandalizi ya kutosha watakabiliana na maandamano makubwa kama yale Tahriri nchini Misri,wanajua fika watawapa wapinzani nguvu kubwa katika uchaguzi wa mwaka 2015,wanajua wafanyakazi tunajua wanachezea fedha zetu.

Mkuu kama unaamini serekali inachota fedha zetu NSSF na kwamba shirika liko hoi bin taabani fedha za kulipa mafao kwa wakati zitatoka wapi kama si kuweka mkakati wa kuchelewesha fedha za wafanyakazi [Angalizo sijasema NSSF itazulumu wafanyakazi nimesema wanamkakati wa kuchelewesha malipo ya mafao hadi mstaafu afikishe miaka 60].

Ngongo ukitoa chuki yako binafsi na Lema michango yako mingine naipa uzito mkubwa sana nikiamini katika uchangiaji wako ambao unakuwaaga na mashiko.

Lakini pamoja na hayo, nakukatalia kuwa serikali ina mpango wa kubadilisha sheria hiyo kwa kisingizio cha kukosa kuwalipa wastaafu ambao wanastaafu kabla ya miaka ya sitini.

Naamini kweli serikali yetu ipo ICU kimapato na hilo la kuchota pesa NSSF linawezekana lakini si la kufikia kumdhulumu mtu alistaafu kazi chini ya miaka 60 eti mpaka afike hapo!!!!!!
 
Ndio maana wazee wanapostaafu wanazungushwa mnoo hadi kupata fedha yao walioitolea
jasho. Mifuko hii wakati mwingine ni kero na wala sio tulizo la mfanyakazi kama wanavyohamasisha!
 
Wanajamvi heshima mbele,

NSSF imeanza zoezi la kuwabembeleza/kulazimisha wateja wake wakubwa [waajiri] kutoa mchango yao ya kila mwezi kabla ya wakati.Ni kawaida waajiri kupeleka michango ya kila mwezi mmoja nyuma[mfano mshahara wa mwezi tano michango yake inatakiwa ipelekwe mwezi sita],sasa NSSF inawataka waajiri wakubwa [waajiri wenye idadi kubwa ya wafanyakazi] kupeleka michango ya wafanyakazi mwezi mmoja mbele au mwezi huu wa sita ili kukabiliana na hali mbaya ya fedha inayoliandama shirika hilo la wafanyakazi nchini.

Taarifa toka chanzo cha uhakika ndani ya shirika hilo zinadai serekali imechota fedha toka NSSF kwaajili ya kugharamia mishahara ya watumishi wake baada ya chanzo chake muhimu cha mapato TRA kushindwa kupata fedha za kutosha kulipa mishahara ya watumishi wa serekali pamoja na shughuli nyingine muhimu.

Zipo taarifa za uhakika serekali ina mkakati wa kuwalazimisha wanachama wote wa NSSF na mashirika mengine ya hifadhi ya jamii kutokulipwa mafao yao hadi wafikishe umri wa kustaafu.Mkakati utasaidia kukabilia na upungufu mkubwa wa fedha unaotarajiwa kutokea kwakuwa fedha zinazochotwa na serekali hazitarajiwi kurejeshwa.

Source:Ngongo@Arusha.

Tatizo lipo hapo kwenye red!!!

Shemeji mbona unanitisha hiyo NSSF naitegemea eti baada ya kuacha kazi karibuni sasa kama ni kimbembe kuipata unanifanya nichanganyikiwe na nizidi kuichukia zaidi serikali ya CCM....hivi chama cha wafanyakazi kiko wapi au wamesha katiwa chao..............

Mkuu Crashwise kama unaitegemea hiyo hela na sasa tunaona giza mbele, kitu ambacho unaweza kufanya ni kuitumia hiyo kazi uliyonayo sasa kuchukua mkopo na kuwekeza kwenye biashara ambayo ulikuwa na mpango wa kuanzisha baada ya kuchukua NSSF huku ukiendelea na kazi na ukiona biashara break even na baadaye kuleta faida ndo muda wa kuachana na hiyo kazi baada ya hapo sasa unaweza subiri huu umri wa kustaafu huku ukizidi kuimarisha biashara zako.
 
hivi mulivyosikia marekani na nchi za magharibi zimeyumba kiuchumi mulikuwa ulimwengu upi???!!!
wakati umefika sasa kuzinyonya nchi za ulimwengu wa tatu,ili kufidia hasara mbili tatu na hali kama hii si kwa tanzania pekee!!
kaeni sawa ipo siku njaa itatupiganisha na hii siku kwa mtazamo wangu haipo mbali saaana,bora kina mama na watoto kuwapeleka hata hapo kenya!
 
Back
Top Bottom