NSSF yaelekea kufilisika

UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKOYA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU
 
Sasa wanataka na wakulima (wajasiriamali) wawe wanachama si ajabu wakasema hawa wanapaswa kustaafu wakiwa na miaka 80!

hahaha! hadi bongo muvi na bongo fleva sasa ndani! hawa wawawekee kustaafu miaka 100! nssf sasa ivi ni kama mtandao wa simu kila kitu wao sasa! miradi yao wenyewe ya kiboya tu! haina mashiko! yanii,
 
Inashangaza sana umeacha kazi na utakitena kuajiriwa unataka kufanya biashara zako mwenyewe wanakulazimisha mpaka miaka 60. umeacha kazi na miaka 35 ina maana subiri miaka 25 mbele sasa itakuwa inaongezeka hiyo hela au ndio unakuja kupewa zile zile ulizokuwa upewe wakati unaacha kazi na miaka 35?. hapa ni uonevu na serikali ya namna hii ni yauonevu sana
 
hii itakuwa sio haki kabisa, hela inakaa miaka mingi halafu wanakurudishia bila riba, hela ya TZ inashuka thamani kila ukicha, tukija kulipwa si itakuwa ya kununulia soda au soksi jamani, ?? tukikaa kimya na hili, watafanya hivyo bila shaka, na ninavyoona inawezekana wakafanya hivyo, wanaanza kuongea halafu wanatenda. poor tanzanians
 
Sijui niache kazi kabla hakijanuka maana mwaka huu ni wa mwisho nijiajiri sasa nikisubiri si itakula kwangu.....

Too late... a Plane has just left the Ground. Rais kesha saini Mswada huo na sasa ni sheria kamili. huwezi toa hela hadi ufikishe miaka 55. period.
 
UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKOYA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU

Kwa sababu kama hizo Huu ndio wakati wa wafanyakazi kugoma na kupinga ukandamizaji wa namna hii... Heri yetu wajasiria mali tunaishi na kuvuna na kutumia 100% ya nguvu zetu. kwa mimi mwenye miaka 25, milioni 50 nitakapokuwa na miaka 55 itakuwa sawa na milion 5 ya leo so = to nothing kwa wengi wetu walio ajiriwa. let wait and see
 
Mkuu Endeleaaa wastani wa kuishi hivi sasa ni chini ya miaka 55 sijui sheria hii itatufikisha wapi ?.milioni 10 ya leo na milioni 10 ya miaka 10 ijayo thamani yake itakuwa imeshuka sana.

Ni wakti muhimu wafanyakazi wa sekta zote tukaanzisha mgomo kushinikiza sheria mbaya na mbovu inatupiliwa mbali.

Kwa sababu kama hizo Huu ndio wakati wa wafanyakazi kugoma na kupinga ukandamizaji wa namna hii... Heri yetu wajasiria mali tunaishi na kuvuna na kutumia 100% ya nguvu zetu. kwa mimi mwenye miaka 25, milioni 50 nitakapokuwa na miaka 55 itakuwa sawa na milion 5 ya leo so = to nothing kwa wengi wetu walio ajiriwa. let wait and see
 
Mkuu Masuke kama sheria itabadilishwa maana yake itabidi usubiri hadi utakapofikisha miaka sitini.Hapo hapo lazima utie akili wastani wa umri wa mtanzania ni chini ya hiyo miaka sitini ?.Jiulize serekali ina mpango gani na wafanyakazi wa nchi hii.

Sheria ishasainiwa na Mkulu wa Ikulu na unaweza chukua mafao yako ukistaafu kwa hiari miaka 55 au kwa lazima miaka 60. Kazi ipo
 
Duh siasa za ccm kweli za ajabu, juzi kwenye mkutano wao kule jangwani wanasema Daraja litaanza kujengwa mwaka huu na NSSF ndo wamepewa hio kazi ya kutoa nusu ya gharama za mradi, kule Kiwira wanatakiwa wazalishe umeme 200 megawatt, kuondoa Mgao wa umeme na NSSF walipewa kazi hio, sijui UDOM kama NSSF wamemaliza kujenga na majengo yanavuja! Kweli ccm ni DHAIFU, "JJ Mnyika Ukweli ni Uhuru"
kaka daraja tu la kigamboni ni over 300 billions
 
hawa ccm na serikali yao sasa wamegusa sehemu mbaya sana.....si wanasema uchumi unapaa?....wasichezee maisha ya watu masikini km sisi kwani watajuta kuijua tz na watz
 
Mkuu una ushahidi au wewe ndo mdini?
Mbona wanapo patia hamsemi ni udini???
au udini upo kweneye makosa tuuu.
acha hizo, think big....

Subiri ushahidi!
Akimaliza usioge usije ukaupoteza huo ushahi eeh!!
Huu ni ushauri toka kwa kova. Usinilaum
 
Mkuu Mzee wa Rula

Natumaini umesikia sheria imeshasainiwa na Mheshimiwa Rais wa JMT kwa maana hiyo hii sasa ni sheria kamili hakuna tena ujanja kama uko ndani ya ajira tegemea kupata mafao yako baada ya kufikisha miaka 55 au 60 upo mkuu wangu.Jiulize miaka 60 utaifikisha lini ?,

Ngongo ukitoa chuki yako binafsi na Lema michango yako mingine naipa uzito mkubwa sana nikiamini katika uchangiaji wako ambao unakuwaaga na mashiko.

Lakini pamoja na hayo, nakukatalia kuwa serikali ina mpango wa kubadilisha sheria hiyo kwa kisingizio cha kukosa kuwalipa wastaafu ambao wanastaafu kabla ya miaka ya sitini.

Naamini kweli serikali yetu ipo ICU kimapato na hilo la kuchota pesa NSSF linawezekana lakini si la kufikia kumdhulumu mtu alistaafu kazi chini ya miaka 60 eti mpaka afike hapo!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Assume hii kiwewe itafanya 200 Top executive walio na umri wa miaka 53 na kuendelea wakasoma hii trend ya economy na speculate kuwa hii tactic ya kumask liquidity itafanya kuwa after two year isiwake na kufanya yrs to be 60 wakaamua kuchota pesa je ni kiasi gani wamejiandaa.
 
Silaha pekee tuliyonayo wafanyakazi Tanzania dhidi ya sheria hii kandamizi ni kufanya mambo yafuatayo.

[1] Kuandaa mgomo nchi nzima ili kushinikiza serekali kuifuta sheria hii mbaya.

[2] kuandaa maandamano ya amani mikoa na wilaya zote Tanzania.

[3] kutafuata wanasheria mahiri kwaajili ya kuipinga sheria hii mahakamani.
 
Wanajamvi heshima mbele,

NSSF imeanza zoezi la kuwabembeleza/kulazimisha wateja wake wakubwa [waajiri] kutoa mchango yao ya kila mwezi kabla ya wakati.Ni kawaida waajiri kupeleka michango ya kila mwezi mmoja nyuma[mfano mshahara wa mwezi tano michango yake inatakiwa ipelekwe mwezi sita],sasa NSSF inawataka waajiri wakubwa [waajiri wenye idadi kubwa ya wafanyakazi] kupeleka michango ya wafanyakazi mwezi mmoja mbele au mwezi huu wa sita ili kukabiliana na hali mbaya ya fedha inayoliandama shirika hilo la wafanyakazi nchini.

Taarifa toka chanzo cha uhakika ndani ya shirika hilo zinadai serekali imechota fedha toka NSSF kwaajili ya kugharamia mishahara ya watumishi wake baada ya chanzo chake muhimu cha mapato TRA kushindwa kupata fedha za kutosha kulipa mishahara ya watumishi wa serekali pamoja na shughuli nyingine muhimu.

Zipo taarifa za uhakika serekali ina mkakati wa kuwalazimisha wanachama wote wa NSSF na mashirika mengine ya hifadhi ya jamii kutokulipwa mafao yao hadi wafikishe umri wa kustaafu.Mkakati utasaidia kukabilia na upungufu mkubwa wa fedha unaotarajiwa kutokea kwakuwa fedha zinazochotwa na serekali hazitarajiwi kurejeshwa.

Source:Ngongo@Arusha.

Mi NAUHAKIKA....NSSF ina uozo mkubwa kuliko hata BOT....maana hapa hela zimesimama tu........panaitajika uchunguzi wa kina. Tunaeza kuona ambavyo hatujaona.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom