Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 80
NSSF na Mahakama; mjibuni mtu huyu- amewadhalilisha. Rai, Majira, Channel Ten na SAU; amesema kweli huyu?
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU MKOPO WA NSSF KWA MBOWE HOTELS LTD
UTANGULIZI
Ndugu wananchi wenzangu wa Tanzania, siku ya Alhamisi ya tarehe 13 Machi mwaka huu gazeti la kila wiki la Rai toleo namba 753 lilichapisha habari katika ukurasa wake wa kwanza yenye kichwa cha habari Mbowe aifilisi NSSF. Pamoja na mambo mengine, habari hiyo ilidai kwamba mimi ninadaiwa Shilingi milioni 1200 kutokana na mkopo kutoka NSSF mwaka 1990 kwa ajili ya upanuzi wa Mbowe Hotel ya Dar es Salaam. Siku mbili baada ya taarifa ya Rai, gazeti la kila siku la Majira toleo namba 5183 la tarehe 15 Machi nalo lilichapisha taarifa kwenye ukurasa wa mbele yenye kichwa Mzimu wa Ufisadi waingia upinzani. Gazeti hili lilimkariri Mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) Bw. Paul Kyara akielezea kushangazwa na kitendo cha Jeshi la Polisi la kushindwa kunikamata kwa kutolipa deni la NSSF. Maneno yanayokaribiana na hayo yalitolewa pia na Bwana Kyara katika kituo cha luninga cha Channel Ten katika taarifa yake ya habari tarehe 14 Machi, 2008. Napenda kutumia nafasi hii kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizi na kwa nini zinatolewa katika kipindi hiki cha historia ya nchi yetu na zina maana gani kisiasa.
1. MKOPO ULIKUWA SH. MILIONI 15
Tarehe 10 Machi mwaka 1990 kampuni ya Mbowe Hotels Ltd. ilipewa mkopo wa Shilingi milioni 15 kwa ajili ya upanuzi na uboreshaji wa hoteli yake ya jijini Dar es Salaam. Mimi ni mmoja wa wakurugenzi na wanahisa wa kampuni hiyo ya Mbowe Hotels Ltd. Ninaamini kuwa Bodi ya Wadhamini ya NSSF (wakati huo ikiitwa NPF) iliridhika kwamba sheria ilikuwa inaruhusu shirika hilo kutoa mikopo kwa shughuli za kibiashara za makampuni binafsi.
Katika maisha ya biashara halali na ujasiriamali, kukopa ni jambo la kawaida. Utaratibu wa kupitia upya na kutathmini mikataba nalo ni jambo la kawaida kwa kila taasisi ya fedha inayojua wajibu wake na yenye nia njema. Mazingira ya biashara wakati wa michanganuo ya biashara hutofautiana kwa kiasi kikubwa na hali halisi hasa kutokana na udhaifu wa uchumi wetu hususan mfumuko wa bei.
Katika maisha yangu ya biashara na uwekezaji, kwa kupitia makampuni mbalimbali nimewahi kukopa kutoka kwenye mabenki kadhaa kwa miradi mbalimbali inayotoa ajira kwa Watanzania wengi. Mikopo yote hii imelipwa na rejea ya mikataba katika baadhi ya mikopo hiyo ilifanyika. Nitaendelea kukopa na kuwekeza kwani ni njia muafaka ya kujisaidia binafsi, kuisaidia familia yangu, kuisaidia jamii na hata kuisaidia nchi yangu.
Mkataba na NSSF ulioingiwa mwaka 1990, uligubikwa na mizengwe mwaka mmoja tu tangu kuingiwa, napo ni pale kampuni yetu ilipoomba kuongezewa mkopo ili kukamilisha mradi uliokusudiwa. Ilichukua takribani mwaka mmoja wa mawasiliano kabla ya NSSF kutoa jibu la kukataa pamoja na wao kukiri kuwa mradi kweli ulihitaji fedha na una sifa zote za kukopeshwa. Sababu pekee iliyotolewa ni kuwa kutoa fedha za ziada kwa miradi siyo sera ya mfuko na hapo hapo ikitushauri tukope kutoka kwenye taasisi nyingine za fedha.
Hali hii ya kushangaza si kwamba ilichelewesha tu mradi, bali ilipandisha kwa kiasi kikubwa gharama za mradi huu. Ililazimu kampuni yetu kuanza upya mchakato wa kukopa toka benki nyingine, tena kiwango kikubwa sana cha fedha ili kuweza kukamilisha mradi huu. Wakati hali hii ikiendelea, NSSF ilianza kudai mrejesho wa riba na hatimaye kwa mkopo waliotoa kwa mradi walioufadhili na kuutelekeza.
Ni dhahiri mradi huu uliathiriwa kwa kiasi kikubwa, na ninaamini umakini na utaalamu wa kibenki haukutumika katika maamuzi haya. Kadhalika, mazingira na mlolongo wa sakata hili na namna uongozi wa mfuko umekuwa ukilishughulikia jambo hili kwa utaratibu unaoweza kutafsirika kirahisi kuwa wa inda na dhamira mbaya, inanilazimu kuhoji uwezo wa kitaaluma wa mfuko kujishughulisha na biashara za ukopeshaji.
2. MBOWE HOTELS LTD. INA NIA YA KULIPA DENI SIKU ZOTE
Septemba 1996 (takribani mwaka mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi ambayo nilishiriki kama mgombea wa upinzani); Bodi ya Wadhamini ya NSSF ilifungua kesi ya madai namba 277 katika Mahakama Kuu ya Tanzania ikidai malipo ya Shilingi milioni 80.1 ikijumuisha salio la deni mama la Shilingi milioni 12 na riba ya Shilingi milioni 68.1. Mdaiwa katika kesi hiyo alikuwa ni Mbowe Hotels Ltd. Tarehe 31 Julai 2001 (miezi michache baada ya Uchaguzi Mkuu wa pili ambapo nilichaguliwa kuwa Mbunge wa upinzani); Mahakama Kuu ilitoa uamuzi bila Mbowe Hotels Ltd wala wakili wake kuwakilishwa katika mlolongo mzima wa kesi hiyo (ex parte judgement) kwamba kampuni ilipe wadai NSSF kama walivyoomba. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2007 kampuni imeshalipa jumla ya shilingi milioni 75.5 ambayo kimsingi ni takribani mara tano ya kiwango kilichokopwa.
Tokea mwaka 2003 kwa takribani mara nne Mbowe Hotels Ltd na wawakilishi wake wameandika barua NSSF za kuomba wakubali mapendekezo ya kumaliza deni hilo na barua zingine lukuki za ama kukumbusha au kutaka majadiliano ya kumaliza swala hili. Hatimaye tarehe 7 June 2007 NSSF waliiandikia Mbowe Hotels Ltd barua ya kuomba kukutana kwa majadiliano. Mnamo tarehe 5 Julai 2007 Mbowe Hotels Ltd ilikubali mwito wa majadiliano na kupendekeza mkokotoo na utaratibu wa malipo; hata hivyo pamoja na kufuatwa na kufuatiliwa kwa njia mbalimbali NSSF hawajajibu barua hiyo hadi leo, ikiwa ni miezi minane tangu tulipowaandikia. Kwa mujibu wa mchanganuo wa kitaalamu, deni la sasa la Mbowe Hotels Ltd pamoja na riba ni shilingi 43,169,727.
3. KESI BADO IPO MAHAKAMANI
Wakati mawasiliano yakiendelea; tarehe 27 Januari 2004 NSSF ilienda mahakamani kuomba wakurugenzi wa Mbowe Hotels wakamatwe. Tarehe 5 Disemba 2006 Mahakama Kuu iliridhia maombi ya NSSF kwamba Mbowe Hotels Ltd, Manase A. Mbowe, Freeman A. Mbowe na Dr. Lillian M. Mbowe wakamatwe na kupelekwa mbele ya mahakama ili wajieleze ni kwanini wasipelekwe jela ya madai (civil imprisonment) kwa kushindwa kuheshimu amri ya kulipa deni. Tarehe 8 Januari 2007 Dr Lillian Mbowe mmoja wa wakurugenzi (ambaye ni mke wangu) alikamatwa na tarehe 20 Februari 2007 alipelekwa mahakama kuu mbele ya Jaji Kiongozi Amiri Manento. Katika kipindi cha kukamatwa kwake, mimi nilikuwa masomoni Uingereza na Bwana Manase Mbowe alikuwa nje ya Dar es salaam. Ningependa kutumia fursa hii kufafanua kwamba anayetajwa kama Mkurugenzi mwingine, yaani Bwana Manase A. Mbowe, kimsingi si mkurugenzi na hajawahi kuwa mkurugenzi wa kampuni bali ni msimamizi wa mirathi ya mmojawapo wa wakurugenzi wa awali wa kampuni. Kujitokeza kwa mkurugenzi mmoja Mahakama Kuu kulitosheleza amri ya mahakama na kuanzia siku hiyo kesi iliendelea kusikilizwa. Pia, kampuni na wakurugenzi wameomba mahakama ya rufaa irejee uamuzi wa mahakama kuu wa kutaka kufungwa kwa ombi namba 152 la mwaka 2006. Sanjari na ombi hilo lilifanyika pia ombi namba 151 la mwaka 2006 la kutaka amri ya kukamatwa isitekelezwe na tarehe 12 Februari 2008 Mahakama ya Rufaa chini ya Mh. Rutakangwa (Jaji Rufaa) ilitoa amri ya kusitisha.
Wakati huo huo imegundulika kwamba shauri la msingi lina hukumu mbili ambazo zimetolewa na Mheshimiwa Jaji Mstaafu Buxton Chipeta. Hukumu ya kwanza ilitolewa tarehe 9 June 1999 na ya pili ilitolewa tarehe 31 Julai 2001 kwa kile kilichoelezwa na jaji kuwa in view of the ensuing confusion. Baada ya kuona kwamba kuna hukumu mbili ambazo si kitu cha kawaida kisheria, kampuni ya Mbowe Hotels imewajibika kwenda mahakama kuu kuomba kuongezewa muda wa kwenda mahakama ya rufaa kutafuta usahihi wa kuwepo kwa hukumu mbili katika kesi moja. Ombi hili limepangwa kusikilizwa tarehe 29 Aprili 2008 mbele ya Mahakama Kuu.
HITIMISHO
Ndugu Watanzania, ninyi ni mashahidi wazuri kwamba, habari hizi zinazojaribu kunipaka matope leo hii zikigeuza kesi ya Mbowe Hotels ambayo kimsingi ni ya kibiashara ili ichukue sura ya kisiasa na kifisadi, zinaandikwa wakati mimi binafsi na chama changu tukiwa mstari wa mbele kutaka kuona mafisadi walioiba mabilioni ya shilingi kupitia Benki Kuu wakichukuliwa hatua za kisheria, zikiwamo za kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Habari ya Rai kwamba Mbowe aifilisi NSSF ni dhahiri kwamba ililenga kuniharibia heshima yangu katika jamii na kunichonganisha na wanachama wa mfuko huo. Lakini ukweli uliodhahiri ni kwamba mkopo wa milioni 15 wa kampuni ya Mbowe Hotels Limited hauwezi kuwa umeifilisi NSSF. Na kama NSSF itafilisika basi ni kutokana na mabilioni ya shilingi yaliyokopwa na wakopaji wengine wanaotajwa na ripoti mbalimbali za kampuni hiyo ya umma ambao hawajawahi kutajwa, kushtakiwa wala kukamatwa.
Ninaamini kwamba, habari hizi zinakuja leo hii si kwa bahati mbaya au kwa sababu ni habari muhimu na za kulisaidia taifa hili. Kwa hakika habari hizi zinalenga kuzima moto tuliowasha dhidi ya mafisadi wa EPA, Richmond, Buzwagi na wale wote wanaotafuna rasilimali za taifa hili. Ni wazi kwamba taarifa hizi zinakusudia kupotosha mwenendo mzima wa namna wapinzani na hususan Chadema tunavyotaka serikali iwashughulikie wezi wa EPA na wale wa Richmond.
Watu hawa wenye nia mbaya na taifa hili kwa makusudi mazima wameamua kuvitumia vyombo vya habari kutimiza malengo yao maovu ya kuzima uzalendo wetu juu ya rasilimali za Tanzania na mapambano yetu dhidi ya ufisadi.
Ndugu Watanzania, mwisho kabisa napenda kusema yafuatayo. Kama kuna watu wanafikiri au wanaota kwamba kwa kutumia njia hizi za kifedhuli wanaweza wakazima dhamira na ari yangu binafsi na ya chama ninachokiongoza ya kutetea haki za Watanzania, watu hao wanapaswa kutambua kuwa wamepotea njia. Bila woga wala ajizi, nitaendelea kupigania haki zangu binafsi, za familia yangu, za chama changu, na za taifa langu Tanzania. Hakuna kulala mpaka kieleweke!
Wenu katika demokrasia na maendeleo,
Freeman Mbowe
17 Machi 2008