NSSF na Mahakama-muumbuueni huyu

Dada Asha,

Mbona hicho ni kitu cha kawaida kwenye sheria? Wao wamekata rufaa na jaji kaamua wasikamatwe mpaka rufaa yao isikilizwe.

Pili kama jaji alisema NSSF hawana case asingelisema waende wakakubaliane nje ya mahakama. Mara nyingi cases za biashara wahusika wanapewa nafasi ya kukaa pamoja na kukubaliana nje ya mahakama mpaka pale wanaposhindwa kukubaliana.

Mtanzania,

kwa msingi huu, basi inabidi mahakama zitoe uamuzi ili ijulikane kama kuna case au hakuna. Inaonekana kuna watu huko NSSF hawataki hii case iishe na walikuwa wanataka kutumia hii case ili kuzuia presha dhidi ya serikali ili kukamata wote walioiba pesa BoT. Kumbuka how many days zimepita hapa JF ambako watu walitaka story za wizi BoT zisahauliwe.

Sasa wameumbuka na for another time, Kikwete anashauriwa na JF ili atoe majina ya waliokwiba pesa BoT. Hapa halali mtu na hawamishwi mtu mawazo mpaka kieleweke BoT!
 
Kama anaona habari "imemchafua" aende mahakamani

Kila kitu mahakamani? :confused:
Mahakama zenyewe zimejaa kesi za tangu mwaka 47 ambazo bado zinakokotwa tu ama kwa kutokuwa na mahakimu wa kutosha ama "bado tunaendelea na uchunguzi"

Alichokisema kinajitosheleza kabisa hahitaji kuongeza lolote, labda kama kuna ngumbaro ambao wataka kutafsiri kauli yake tofauti na alivyoitoa basi ni hiyari yao kufanya hivyo.
 
Umeniwahi kumpasha huyu sijui hasomi au ana lake jambo?

Asha

Asha,

Mimi sio mwanasheria na wala sijitii kujua sheria, ila kwa ueleo wangu kama layman, anachopinga Mbowe mahakamani ni tofauti na mnachosema.

Kwa kusoma maelezo yake ni kama anajaribu kuvuta muda tu ili amri za mahakama zisitekelezwe.

Kuhusu SWAP, alichofanya Mbowe ni tofauti. Yeye alienda bank zingine na kupata mkopo wa kumalizia majengo yake, huku deni la NSSF likiwa bado liko pale pale. Yeye alichotakiwa ilikuwa ni kuiambia hiyo bank nyingine kwamba
ana deni na NSSF lakini halina maslahi, badala yake anataka hilo deni alihamishie kwao na kupata pesa ya ziada ya kumalizia hoteli yake. Hiyo bank nyingine wangempa pesa yote ya kuwalipa NSSF na pesa ya ziada ya kumalizia jengo lake. Angebakiwa na deni la hiyo bank nyingine tu.

Lakini yeye aliamua kuchukua loan ya pili na akawa analipa loans zote mbili, hapo akawa analiwa interest kubwa ya NSSF bila sababu ya maana.
 
Nadhani hii case ikitolewa uamuzi itatufungua mengi. Asante Mtanzania kwa shule nzuri hapa. GOing back to the whole case hapa, Je ccm wako tayari kuunda kamati huru ya kuchunguza pesa zote za NSSF kuanzia mwaka 1990?
 
Mtanzania,

kwa msingi huu, basi inabidi mahakama zitoe uamuzi ili ijulikane kama kuna case au hakuna. Inaonekana kuna watu huko NSSF hawataki hii case iishe na walikuwa wanataka kutumia hii case ili kuzuia presha dhidi ya serikali ili kukamata wote walioiba pesa BoT. Kumbuka how many days zimepita hapa JF ambako watu walitaka story za wizi BoT zisahauliwe.

Sasa wameumbuka na for another time, Kikwete anashauriwa na JF ili atoe majina ya waliokwiba pesa BoT. Hapa halali mtu na hawamishwi mtu mawazo mpaka kieleweke BoT!

Mwafrika wa Kike,

Nafikiri unajua msimamo wangu kuhusu BOT. Labda anayefurahi hapa ni Mwanakijiji kwasababu rafiki yake Balali hatajwi tena kwi kwi kwi!!!

Inabidi kupambana na ouvu wa aina zote Tanzania kama tunataka huko mbele angalau tuje tupate viongozi wa maana.

Kwa wengine principles ni za maana zaidi kuliko kujuana. Mwafrika wa kike Ukikosea nitakulima tu bila kujali uliwahi kuniletea majani kwi kwi kwi!!
 
Nadhani hii case ikitolewa uamuzi itatufungua mengi. Asante Mtanzania kwa shule nzuri hapa. GOing back to the whole case hapa, Je ccm wako tayari kuunda kamati huru ya kuchunguza pesa zote za NSSF kuanzia mwaka 1990?

Mwafrika wa Kike,

Toka lini uliona mimi nawatetea CCM? Wao ndio wezi namba moja, hata hawa wajanja wajanja tunaowajadili sasa wamejifunza huko huko CCM.

Inatakiwa tuachane na ufisadi wa CCM lakini pia hawa wengine nao wabadilke na kuwa whiter than white.
 
Mtz, am back pal. Hawa wanasiasa wanatakiwa kuwa wasafi bila kujalisha wako chama gani. Lakini kwa ninachokiona kwa sasa ni kuwa CCM are playing games now. Wameamua kututumia 'sisi' wenye raha zetu kuhakikisha tunawasahaulisha 'ninyi' wenye njaa zenu. Shutuuuu, mbona kazi ipo mwaka huu?
 
Asha,

Mimi sio mwanasheria na wala sijitii kujua sheria, ila kwa ueleo wangu kama layman, anachopinga Mbowe mahakamani ni tofauti na mnachosema.

Kwa kusoma maelezo yake ni kama anajaribu kuvuta muda tu ili amri za mahakama zisitekelezwe.

Kuhusu SWAP, alichofanya Mbowe ni tofauti. Yeye alienda bank zingine na kupata mkopo wa kumalizia majengo yake, huku deni la NSSF likiwa bado liko pale pale. Yeye alichotakiwa ilikuwa ni kuiambia hiyo bank nyingine kwamba
ana deni na NSSF lakini halina maslahi, badala yake anataka hilo deni alihamishie kwao na kupata pesa ya ziada ya kumalizia hoteli yake. Hiyo bank nyingine wangempa pesa yote ya kuwalipa NSSF na pesa ya ziada ya kumalizia jengo lake. Angebakiwa na deni la hiyo bank nyingine tu.

Lakini yeye aliamua kuchukua loan ya pili na akawa analipa loans zote mbili, hapo akawa analiwa interest kubwa ya NSSF bila sababu ya maana.

Mi siyajui hayo ya SWAP wala ya SWAT ili uhamishaji wa madeni wataka ushauri wa pande mbili ati. Katika hili NPF chini ya Mkulo inasemekana baada ya kunyimwa cha juu wakaweka kauzibe. Sakata zima laelekea kuwa 'mkomoeni'.

Ya kesi yako bayana,tatizo lako wewe ni kuwa hujazisoma hukumu zenyewe wala hati ya mashatka.

Alichoenda kuuliza Mbowe mahakamani ni je, alipe bei gani? Kwa kuwa kuna hukumu mbili, ya 1999 na ya 2001.

Labda nikuulize wewe mtaalamu wa mafedha? Mbowe alipe bei gani wakati NSSF wenyewe hawajui anadaiwa bei gani?

Na kwanini hawaikamati mali iliyowekwa dhamana na kuipiga mnada badala yake wanatafuta kumkata Mbowe mwenyewe?

Hapa kuna siasa zaidi ya biashara.

Nungwi,

2005 wakati wa kampeni Rostam kwa kushirikiana na Salva, kwa baraka za Kikwete mwenyewe waliitoa hili sakata kwa wahariri wote baada ya NSSF kuwapatia nyaraka zote. Wahariri wakaweka kauzibe, ikaandikwa na gazeti la Mzalendo pekee

Leo linaibuka tena baada ya MBowe kumsema Kikwete na mafisadi wa EPA.

Rostam kazi kwako, umegundua Balile anakupotosha? Ona sasa amekuchonanganisha na Mengi.

Na wiki ijayo akiandika lile suala lingine alilokushauri mlitoe kuhusu mke wa upanga wa Kikwete hakika mtagombana na mkuu wa nyumba.

Na hiyo ndio itakuwa mwisho wako.

Waweke kitomoto Balille na Muhingo kwanza wakupe ushahidi kabla ya kuandika. Wanakuingiza mkenge.

Asha
 
Mtanzania wakati nakubaliana na wewe on principle, natofautiana na wewe kihali halisi, we have to get the best leaders ambao wamekuwa vetted na ambao kwa hakika hata tukiangalia nyuma ya maisha yao tunaweza kuona madoa ambayo tunaweza kuishi nayo. Kutarajia kuwa atakuja kutoka kiongozi asiye na baka hata moja au doa ni kusubiri Malaika, na vizazi vingine vimepita mtu wa namna hiyo hajatokea bado.

Watakaotuongoza ni viongozi ambao waliweza kusahihisha makosa yao, kujitengeneza upya, na kujilinda kuwa hawataanguka tena. Akili zangu zinaniambia nikitarajia kuwa kiongozi hatokuwa na deni hata moja, hatakuwa na mgogoro hata mmoja, hatakuwa amemuudhi mtu hata mmoja, au hatakowa na tatizo fulani la kitabia au kimaamuzi, nitakuwa niko kwenye nchi ya kufikirika.

Hata hivyo nadhani la maana ni kuhakikisha kuwa viongozi wetu siyo tu wananaonekana wasafi, lakini hata waliochafuka tujue kwamba waliweza kujisafisha kweli kweli. Nadhani hapa mimi na wewe tunatofautiana, wewe kiongozi akikosea au mwenye makosa hastahili hata uongozi (ndivyo ninavyokuelewa); wakati mimi naamini kiongozi hata Lowassa akijirudi, na kutengeneza alichoharibu, na kuonesha kuwa amejifunza toka huko nyuma anastahili nafasi nyingine isipokuwa mtu kama Dito!
 
Kwa kweli hizi siasa za Tanzania zinachosha. Mhe Mbowe alipaswa kuwa makini zaidi. Yeye amekopa deni mwaka 1990 nafikiri alikuwa hajafikiria hata kugombea urais. Sasa alipoamua kugombea urais alipaswa kujiweka sawa. Kisheria mpaka hapo hana tatizo, lakini kisiasa ameshachemsha tayari. Hapa ni kwamba wananchi wanaona eehe kumbe huyu naye ni kama haohao tu. Hayo mambo ya 75million hayaingii akilini kwa wananchi. Kwa wananchi ni kwamba Mbowe anadaiwa, tena na shirika la serikali. Sasa katika kiwingu hiki cha ufisadi sasa hivi, naye anaonekana kuwa ni fisadi tu mbele ya macho ya wananchi. Hana wa kumlaumu hapa zaidi ya kujilaumu mwenyewe. Kwenye siasa ukimpa mwenzake mwanya anautumia, na hapa CCM wana haki ya kuutumia huo mwanya. Tena mimi ningewashangaa sana kama CCM wasingeutumia huo mwanya. Sasa mambo ya kulinganisha na Sumaye ni kosa lingine kubwa wanalofanya baadhi ya watu hapa. Two wrongs will never make a right. Tena ni kosa zaidi kujilinganisha na watu ambao wewe unawakosoa kila siku na unataka kubadilisha. Jamani hivi hakuna sehemu ya kusomea haya mambo ya mbinu za kisiasa. Hapa lazima CHADEMA wakubali kwamba Mbowe kawatia mchanga machoni na itabdi mjisafishe. Mtajitetea wee, lakini sisi tusio na haya mavyama yeni ndivyo tunavyoona. Haya nami niiteni mtetezi wa mafisadi, maana hapa inaonekana lazima utete CHADEMA hata kama wamechemsha.
 
I give up!
 
Nadhani hapa mimi na wewe tunatofautiana, wewe kiongozi akikosea au mwenye makosa hastahili hata uongozi (ndivyo ninavyokuelewa); wakati mimi naamini kiongozi hata Lowassa akijirudi, na kutengeneza alichoharibu, na kuonesha kuwa amejifunza toka huko nyuma anastahili nafasi nyingine isipokuwa mtu kama Dito!

Mwanakijiji,

Mimi sisemi kuwa kama kiongozi aliwahi kukosea basi ndio hukumu imepita, hapana, mimi mwenyewe nina makosa mengi sana ambayo nisingetaka watu wanihukumu kwa hayo. Ila ni muhimu mtu kuwa mkweli na kukubali makosa kama yalikuwepo badala ya kukimbilia kulaumu watu wengine.

Kama alivyosema binti Maria hapo juu, Mbowe angetoka clean na kuhakikisha
suluhu inapatikana ya huo mkopo wake. Ni miaka mingi sana imepita, naamini angelikuwa na nia njema hili suala lingelikuwa limeisha zamani.
 
nimekupata barabara, ndio maana Obama yamemkuta yaliyomkuta!!
 
Ni miaka mingi sana imepita, naamini angelikuwa na nia njema hili suala lingelikuwa limeisha zamani.

I know your concern Mtz, am with you pal. Inapendeza sana kuwa clean, lakini si jadi ya wanasiasa wetu. Lakini huyu si nimesikia kajitetea pal? Labda nadanganywa mie
 
Wakuu,

Mimi nitoke nje ya mada, naona kwenye haya mambo ya Mbowe, Ballile ametajwa mara nyingi. Hivi huyu ni nani?

Nakumbuka kuna mjadala huko nyuma walisema kuna vijana wawili wa CHADEMA walipelekwa Hull university. Ninaweza kuwa na makosa hapo, huenda walikuwa vijana wawili wa Mbowe na wala sio CHADEMA.

Ilikuwaje akaishia kwa Rostam?

Hapa natafuta Umbeya tu, kwa wale wenye habari kamili.

Ni vizuri kuwajua wasaliti mapema ili ukikutana nao basi uangalie upande mwingine.
 
Wakuu,

Mimi nitoke nje ya maada, naona kwenye haya mambo ya Mbowe, Ballile ametajwa mara nyingi. Hivi huyu ni nani?

Nakumbuka kuna mjadala huko nyuma walisema kuna vijana wawili wa CHADEMA walipelekwa Hull university. Ninaweza kuwa na makosa hapo, huenda walikuwa vijana wawili wa Mbowe na wala sio CHADEMA.

Ilikuwaje akaishia kwa Rostam?

Hapa natafuta Umbeya tu, kwa wale wenye habari kamili.

Ni vizuri kuwajua wasaliti mapema ili ukikutana nao basi uangalie upande mwingine.
Balile namfahamu ni mdogo wangu mmoja ambaye anatumiwa na wenye pesa chafu. Ni jamaa ambaye kila anayemtetea huwa namtilia shaka. Mtz, naanza kupata akili kuwa umefumbuka kiwango flani kujua wanaopika mambo kama haya ni kina nani.

Kosa la Mbowe ni moja, kumwamini mtu kama huyu bila kumjua kwa undani kwanza. Lakini wengine ndio hivo babu. Balile ni mchafu ananuka uchafu wa kutumiwa. Waulize walio Habari Corruption watakwambia. Kishasababisha mambo ya ajabu pale. Wadogo zangu wanaoandika habari pale wamenithibitishia yeye alitumwa kule kwa Lowassa kuandika 'story' kama wapendavyo wao kusema na Rostam akawalazimisha wahariri wake waiweka 'as is' na endapo wangeleta nyodo wangekiona.

Waliojaribu kujitoa walikutana na joto ya jiwe. Believe me or not. Mmoja kati ya waandishi wachafu Tanzania ni Balile. Labda tuanzishe mada kabisa ya kujadili waandishi WANAOTUMIWA ndipo mtawajua wanaotumiwa kumaliza vyombo vya habari na wanaofanya unafiki kama Balile. Mungu aepushe mbali
 
Huko tuendako tutajikuta waandishi wetu wa habari ni hatari kuliko hao mafisadi. Ukifuatilia kwa ukaribu ni waandishi wa habari waliowaporosha watu wote Tanzania waliokuwa na nia ya dhati ya kulisaidia taifa letu, lakini ni waandishi wa habari hao hao waliowapamba, kuwapaka mafuta na kuwabeba na kuwafikisha watu mahala ambapo hawakustahili kuwepo na sasa wanahangaika wasijue cha kufanya maana samaki kawekwa nchi kavu. Baadhi ya waandishi wetu wa habari wametenda na wanaendelea kutenda dhambi kubwa kuliko zile zilizoandikwa kwenye vitabu vya dini! Mungu anisamehe tu kwa kuhukumu maana nami nitahukumiwa, lakini this is how I feel about our "journalists".
 
Balille hajawahi kuwa kijana wa CHADEMA. Alisomeshwa chuo cha diplomasia na mafisadi. Akamgeuka mwajiri wake Mbowe na kulitumia tanzania daima katika vita vya makundi vya mafisadi. Kama zawadi akaenda kusomeshwa na fisadi mwingine Hull. Kama ilivyo ada ya mkuki, amerejea na kurudi msituni. Kwa sasa ni mwandishi mwandamizi wa Habari Corruption. Na ndiye aliyeandika ile habari ya mwajiri wake wa zamani Mbowe kwenye gazeti la Rostam Aziz International(RAI). Lakini ameanza mzozo na Mengi, tusubiri tutaona mengi ndani ya mwezi mmoja. Ilikuwa amepewe uhariri mkuu ama uafisa mtendaji mkuu. Amewachimba wakina Mwakitangwe na Atilio Tagalile, amefanikiwa kiasi. Lakini hili la wiki hii(Sio la Mbowe) kuna lingine halijatoka hadharani bado. Limemfanya aonekane kauzu kabisa. Wallah mwanaume huyu anajua kuziuza, hata ajuza ana afadhali. Mwana ajizi, shabiki wa mijizi

Bado nasubiria kuona huu ugomvi wa Rostam na Mengi ambao Balile anataka kuanzisha. Tatizo lake anadhani kuwa "mafanikio" aliyopata dhidi ya kina Tagalile yatadumu. Kinachoonekana Balile amepania kuwa na total control kwenye media za mwizi na mkoloni Rostam Azizi.

Kitakachomwangusha ni wana mtandao ambao wanamuunga Kikwete na ambao wanajua mpango wa siri unaopangwa na Lowasa na Rostam ili kulipa kisasi dhidi ya kile alichofanya Kikwete (kumtosa Lowasa).

kazi kweli kweli, sijui Balile atapambana na wangapi, ameanza na Mbowe, akaja Mengi, alianza kumpamba Lowasa akachemsha, na sasa anataka pia kupambana na Kikwete na wenzake! yangu macho
 
Baada ya kupata pia upande wa pili wa bwana Mbowe kuhusu sakata hili nimeelewa sasa kuwa huu ulikuwa mkopo katika jitihada zake za kujiendeleza kibiashara. Kuna tofauti kubwa sana na mafisadi ambao huchota (kuiba) hela, yeye kakopa, tena kwa riba kubwa sana, ni deni na si wizi. Na hajakataa deni hilo. Kinachoonekana ni mgogoro kati ya mkopaji na mkopeshaji kuhusu ulipaji, hasa taratibu za kukokotoa kiasi cha deni lililobaki. Wakikubaliana (au mahakama ikiwaamulia), basi watalazimika kutekeleza makubaliano au hukumu hiyo. Nadhani si haki hata kidogo kufananisha hili na ufisadi, yaani hii kuiweka kundi moja na Richmond, Kagoda etc ni kumuonea sana Mbowe kama si kumtukana. Kwa sasa tuiachie mahakama iwapatie suluhisho.
 
Back
Top Bottom