NSSF na Infrastructure Investment: Kigamboni Bridge, IPP, Road Construction.. ???

NSSF na Infrastructure Investment: Kigamboni Bridge, IPP, Road Construction.. ???

NImeanza kuangalia hapa (ndani ya siku hizi chache zilizopita) na ninaanza kuona tatizo mahali fulani; japo kwa juu inaonekana vizuri sana lakini naanza kuhofia na ninashindwa kuelewa kwanini NSSF inawekeza fedha za wafanyakazi wake kwenye miradi hii mikubwa ya Umeme, Ujenzi wa Madaraja na sasa Ujenzi wa Barabara.

Kuna kitu hakiko sahihi; nia yaweza kuwa nzuri lakini kuna kitu hakiko sahihi... sijui ni kitu gani bado.. lakini something is very very wrong somewhere..

Indeed, something is very wrong! The impression I get is that wamewalewesha wanaotakiwa kuwasimamia (the government/politicians) na sasa wanafanya wanachokitaka na serikali inawaona kama wakombozi wao! It is quite unimaginable kwa nchi yenye uncertain investment environment kama Tanzania kwa pension fund kutapanya hela za watu maskini kiasi hiki! I have always said hizi funds ziwe chini ya members wenyewe (na si regulatory authority) ili members wawe na uwezo wa moja kwa moja wa kuwahoji Boards & Management decisions kama ambavyo inafanyika kwenye limited liability companies! Nina shaka sana na liquidity ya investment za pension funds Tanzania, ukiachia mbali profitability (in real terms). Wanaoperate katika mazingira ambayo hakuna accuntability ya kweli kwa sababu: (1) Wasimamizi si competent - wamejaa siasa tu na hawana ujasiri (expertise wise) wa kuhoji investment decisions za pension funds - ukizingatia ni very appealing kwa wanasiasa wakubwa! (2) Tanzania hatuna comprehensive investment performance benchmarks - kwa hiyo kupima inefficiency ya investment managers si rahisi kwa mtu wa kawaida! Pamoja na hayo instincts bado zinatuambia something is very wrong somewhere! Ukisoma reports zao unabaki na maswali mengi sana - sijui hata hizo kamati za bunge kwa nini wameingia kwenye mtego wa kuwasifu tu hao wakubwa wa pension funds kwa kujiingiza kwenye investment in infrastructure nk. eti kwa sababu tu pension funds za Asia zinafanya hivyo! Wamesahau kuwa TZ is the poorest of the poorest!
 
Hafu wachangiaji wa mfuko huu hawanufaiki kabisa.
 
kwa upeo wangu mdogo hii hela ya NSSF ni nyingi na haina haraka, so ni vizuri kuwekeza but nina wasi wasi kuna loop holes wajanja wanazitafuna tu kwa taratibu taratibu.
 
Inawezekana pia ni strategy ya management kutaka kubaki madarakani - kwa sababu waliowateua wataona ni afadhali wawaache ili wamatekeleze miradi yao waliyoianzisha! Na wataendelea kubuni miradi kama hiyo mpaka sijui lini?
 
Nadhani wasiwasi wako ni sawa kwa kuwa nionavyo kuna njia mbili kuu za ku recover hiyo fedha ikiwa na faida :
1. Wao wenyewe nssf kukusanya mapato hayo kulingana na investment waliyofanya,hapa ina maana watakuwa wabia wa serikali.
Hii nadhani ina risk kidogo.
2. Kuikopesha serikali kwa kutegemea malipo badaye.
Hapa ndio kwenye kasheshe ukichukulia kila siku tunaomba kufutiwa madeni.
Risk ya ile ya kwanza ni harufu
ya ufisadi ndani yake tukikumbuka mashirika ya umma yaliyofariki.
Inawezekana zipo njia nyingine
Ila mimi nimefikiria hizo tu.
 
NImeanza kuangalia hapa (ndani ya siku hizi chache zilizopita) na ninaanza kuona tatizo mahali fulani; japo kwa juu inaonekana vizuri sana lakini naanza kuhofia na ninashindwa kuelewa kwanini NSSF inawekeza fedha za wafanyakazi wake kwenye miradi hii mikubwa ya Umeme, Ujenzi wa Madaraja na sasa Ujenzi wa Barabara.

Kuna kitu hakiko sahihi; nia yaweza kuwa nzuri lakini kuna kitu hakiko sahihi... sijui ni kitu gani bado.. lakini something is very very wrong somewhere..

MM,

Kwanza nikupongeze kwa kuanzisha Topic hii.

Ukweli ni kwamba hawa NSSF na mifuko mingine ya Pensheni kama PPF,PSPF,LAPF n.k na n.k kuna matatizo makubwa sana. Mimi ni mmoja wa wachangiaji katika mfuko mojawapo ya hiyo lakini nionavyo hawa JAMAA WANACHEZEA PESA YETU NA MWISHO WA SIKU HATUONI FAIDA YOYOTE!

Ni jambo zuri kuwekeza ili kupata faida na kuongeza mtaji wako. NSSF wamekuwa wanawekeza pesa za wadau(wafanyakazi) bila ya kuwauliza wala kushauliana.Huwa wanakurupuka tu bila ya kuwashirikisha stakeholders. Na hata wanapopata hiyo faida NONO kama ipo inaishia kweny matumbo yao tu na haimnufaishi mwenye pesa ambaye ni mfanyakazi anayechangia!

Bado hawa jamaa wana policy(sera) mbovu sana kuhusiana na malipo ya uzeeni baada ya mfanyakazi kustaafu. Kwanza ni KUCHELEWESHEWA MALIPO YA MFANYAKAZI ANAPOSTAAFU lakini la pili na baya kabisa ni malipo duni anayopokea mstaafu baada ya miaka 30 au 35 kazini. Tatu wanasema ukipunguzwa kazinileo(retrenchment) ukiwa na miaka 40 kwa mfano itabidi ukae miaka 15-20 kusubiri kuanza kupewa malipo yako ya uzeeni baada ya kutimiza miaka 55-60 ya kustaafu kwa hiari(55) na lazima(60) kwa mjibu wa sheria.


Nihitimishe kwa kusema kwamba lazima policies zinazo-govern mifuko hii zihuishwe/zirejewe ili kuwanufaisha stakeholders kwa kubadilisha baadhi ya vipengele kama ifuatavyo:
  1. Kwanza kabisa NSSF,PPF,LAPF,PSPF lazima wakae na stakeholders wajadili na kukubaliana kuwa fedha inaenda kuwekezwa wapi na faida 1,2,3 itakayopatikna na dividend(gawio) watakalopata stakeholders.
  2. Mfanyakazi anapopunguzwa kazini(retenchment) apewe chake ili kiwe ndiyo mtaji wake wa kuanzia maisha maana anakuwa hana kazi tena.
  3. Kuwe na mfumo mmoja wa kulipa mafao ya wafanyakazi kwa mifuko yote. Kwa sasa kuna policy tofauti toka mfuko mmoja kwenda mwingine. Kwa mfano; wakti PSPF wanamlipa mstaafu sh. 100 milioni baada ya kustaafu akiwa amefanya kazi miaka 30, PPF watamlipa mfanyakazi wa aina hiyo hiyo(elimu sawa,umri sawa,aina ya kazi sawa) sh. 30 milioni. TOFAUTI YA SH. 70 MILIONI!!!!!Huu ni upuuzi.
  4. Wafanyakazi wakopeshwe na mifuko hii maana ni fedha yao na wao(mifuko) wanahakika ya kuikusanya hii pesa kirahisi maana kila mwezi kuna makato yanapitia kule. Kwa Policy ya sasa wao(mifuko) watakudhamini tu ukakope kwenye benki yoyote wao wanasema hawakobarapeshi kwa sababu siyo benki lakini at the same time wanakopesha wafanyi biashara na makampuni ya ujenzi wa majengo/barabara. This is bullshit!
  5. PPF,NSSF,PSPF,LAPF na serikali lazima wajue kuwa ile pesa ni ya WAFANYAKAZI na wana haki ya kukopeshwa na kujua inavyotumika na wanastahili ya kupatiwa FAIDA INAYOPATIKANA.
 
Always mimi sielewi kabisa hizi vision na mision za haya mashirika ya FFFF.


  • Hakuwezi kuwa na mipango miji na wala miji yetu haiwezi kuwa ya kuvutia kwa kuacha kila mtu ajenge nyumba. Kwa mshahara gani?

  • Dar, mwanza mbeya na mikoa mingine haiwezi kuwa ya kisasa kwa kuwa na matower sita au 10 au madaraja tu . wakazi wanahitaji nyumba za kuishi. wawaachie wenye majukumu ya madaraja wajenge madaraja.

  • Wanasema wanawekeza kwenye miaradi yenye faida lakini ni faida gani hiyo anayopata mstaaafu ate the end. Asset kubwa anayoweza kupata msataafu yeyote ni nyumba.Mtanzania wa awaida anaweza kutumia miaka mingapi kukamilisha nyumba. Je hawajafanya utchambuzi huu na kuongea na serikali iwe gurantee kuwauzia watu nyumba kama vile vile serikali inavyokuwa guranteekwenye miradi yao mingine

  • Kuna shirika moja lilijenga nyumba za viongozi. ni viongozi wangapi ni wateja na mafao yao yanawekwa kwenye haya shirika. mafao ya wabunge yanawekwa kwenye shirika gani.

  • Haya mashirikia focus yao ni maendeleo ya shirika binafsi na sio maendeleo ya wateja wao kitu ambacho ni kosa. Maisha ya pensioner yanakuwa sacrificed kwa sababu ya shirika. Huko ulaya na USA ni mashirika yanapata hasara sababu ya Mikopo kwa pensioners. sio vice versa.
Hizi "FFF" zinapokuwa too much profit orinted kama ilivyo CRDB , EXIM etc basi kuna shida kubwa
 
Mkuu hakuna tatizo lolote. NSSF inachofanya ni purely busines na tena yenye returns kubwa kuliko biashara halali unazozijua. Kinachofanyika ni kama kuikopesha serikali ambayo italipa kidogo2. Kwa upande wa Kiwira kuna faida nyngi zikiwemo za rasmali za nchi na faida zake zinabaki nchini. Inachokifanya NSSF ni kuwa reliable Financier wa GOT opportunity ambayo haijawa utilized na Taasisi za ndani.

Kuna injinia wa masuala ya umeme hapo juu ametoa tahadhari kuwa aliposoma proposala zao, amepatwa na hofu na kinachofanywa na NSSF ambao kimsingi hawana utyalaamu katika eneo hilo la umeme. Na mwanakijiji ameshasema kwua tatizo si NSSF kuwekeza...
 
What is social security?

"Social security may be defined as any programme of social protection established by legislation, or any other mandatory arrangement, that provides individuals with a degree of income security when faced with the contingencies of old age, survivorship, incapacity, disability, unemployment or rearing children. It may also offer access to curative or preventive medical care. As defined by the International Social Security Association, social security can include social insurance programmes, social assistance programmes, universal programmes, mutual benefit schemes, national provident funds, and other arrangements including market-oriented approaches that, in accordance with national law or practice, form part of a country's social security system."

Cha kushangaza hapa Tanzania tunatumia Social Security zetu kwenye miradi mikubwa ya Umeme, Ujenzi wa Madaraja na Ujenzi wa Barabara. Hivi sisi tunaakili kweli???

Nimefuatilia hoja za mjadala huu tokea ulipoanzia nimegundua yafuatayo

1- Wengi wanakubali kua NSSF inachotakiwa kufanya ni biashara zenye faida kwa shirika na watu wake, ispokua wana wasiwasi na hiyo faida kupatikana kitu ambacho kipo ktk biashara ya aina yoyote

2-Wengi hawayafahamu vizuri malengo ya NSSF

3- Wanaopinga wengi hawatoi plan mbadala

4-Wengi hawafahamu elimu ya biashara (business)

5- Wengi hawafahamu kanuni za uongozi bora

6- Wengi wanafikiri nchi au shirika linaweza kuendelea kwa kua na pesa nyingi bila pesa hizo kuzitafutia miradi ya kuziongeza.

7- Wengi wanakataa kukubali kua biashara inafaida na hasara na wanataka faida tu, kituambacho hakiingii akilini hata kwa mfanya biashara wa njugu. Na mengine mengi.

Sio umeme tu au barabara tu, kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kupewa watu binafsi kama ikionekana serikali inashindwa kuyafanya kwa ufanisi. Hivi ni miaka mingapi Tanzania tunazungumzia tatizo la umeme, ni aibu kubwa kwa taifa kutaja hata neno maendeleo wakati huduma ambayo inauzwa sio kama inatolewa bure pia bado inatushinda. Watu wengi wanaofuatilia tatizo la umeme inawafanya kujiuliza kua je huu umeme unatolewa bure? Kuna unyonge kiasi gani kama kua mwananchi amepigana na maisha mpaka amepata pesa anataka kununua umeme lakin umeme hakuna.

Wacha shirika, mtu binafsi au yoyote aneona biashara ya umeme itamlipa afanye. Wasiwasi wa wengi ktk swala hili sio wa msingi na unaweza ukaonekana uko ktk theory sana kuliko practical. Kwa mfano mtu anaweza kuuliza je wanachama wa NSSF wameshauriwa ktk hili? Aangalia policy ya shirika inasemaje ktk kulifanya hilo na sio utoe tu conclusion bila ya information za kutosha. Lolote lifanyike tumalize matatizo yetu sio ya umeme tu na mengineyo.
 
Mwanakijiji kwa hilo nakuunga mkono inakuwaje shirika liwe na fedha kuliko serikali??na itafika kipindi serikali itaenda kukopa huko na hatimaye kuliua kabisa!!!!nchi hiii management ni mbovu sana hv kweli vichwa vyote vyenye akili vya watanzania vinashindwa kabisa kuwa creative na innovative kwaajili ya maendeleo ya taifa maana ukiangalia barabara tunatumia za mkoloni,mitambo ya kuzalisha umeme ni ya mkoloni,majengo mengi ya mahospitali na shule na shumba za shirika la nyumba la taifa ni za mkoloni tatizo ni nini hasa hata mimi huwa naona kwamba kidogo kipindi cha mkapa kulikua na unafuu sana wa maisha!!!ila sasa tunazidi kwenda minuzz!
 
Mi naona hapa kuja haja ya watu kuelewa madhumuni na maana ya mifuko ya hifadhi ya jamii. Kwenye mifuko ya pension kama NSSF/PPF/LAPF hakuna kitu kinachoitwa pesa/account yangu, bali kuna stahili ya mafao yangu(defined benefits scheme),... Hii mifuko sio benki, ila ina wajibu wa kulipa mafao baada ya kukusanya michango. Halafu wanachama wanawakilishwa kwenye board na vyama vya wafanyakazi ambao wanapewa theluthi moja ya viti vya board kwa hii mifuko yote. Kwahiyo upo uwakilishi wa wanachama kwenye maamuzi ya uwekezaji. Lakini cha muhimu lazima tufahamu kwamba kazi kuu za mifuko ya pension ni tatu.

  • Kukusanya michango
  • Kuwekeza/kuinvest
  • kulipa mafao yaliyoainishwa kisheria
Tukichukulia suala la kuwekeza, kama hii mifuko itakaa tu na hizi pesa inazokusanya leo benki bila kuziwekeza, itashindwa kulipa pensions wenyewe watakapostaafu say 2030 huko...ili kuadd value kwenye michango, ni lazima iwekezwe. Swali ni je iwekezwe wapi?
20years BoT Bonds zinakupa return ya 10%, whereas kuikopesha Serikali inakupa return ya 13-15%(hii imetamkwa kwenye mkutano wa wadau wa NSSF last week),...kwahiyo hapo utaona returns nzuri iko wapi.

Lakini vilevile katika wakopaji, hakuna mlipaji aliye mzuri kuliko serikali(nalo tuliambiwa pale).

Wakuu haya mambo yalifafanuliwa vizuri sana kwenye mkutano wa wadau wote wa NSSF uliofanyika Arusha last week. Wengi tulikua hatufahamu na kuelewa sababu za maswali hayahaya, lakini majibu yalikua wazi pale. Aidha wakalie hela za madafu washindwe kulipa mafao stahili baadae au wawekeze kuziongezea thamani. Na kwenye kuwekeza, serikali ndio inayolipa the best returns na kwa wakati, kwenye miradi yote NSSF waliyowahi kufanya na serikali.

Kwa vile umeme, madaraja, na mabarabara bado ni kero(hapa nilipo nasweat na battery inakata anytime hakuna umeme), mi nawaunga mkono kwa kuingia kwenye miradi ya infrastructure. Ni bora wajenge hiyo mitambo ya umeme, na madaraja atleast wanananchi tutanufaika nayo. Jamaa walichallenge mtu aoneshe mradi mmoja tu wa infrastrure ambao wameumismanage au haujalipwa vizuri, jibu likawa hakuna.

Kunaweza kukawa na swala la transparency, lakini hiyo isitufanye tukawa na inertia ya kufanya mambo makubwa kama watanzania kwa kuogopa eti Tanesco alishindwa, au sijui Tanroad alishindwa. Jibu tuwabane watupe transparency itakayo tureassure.

Kama wanaweza kutupunguzia matatizo waungwe mkono na akina PPF, LAPF, PSPF wote tusaidiane kujenga nchi provided serikali inawalipa kwa wakati...nyumba mtu utajibana utajijengea mwenyewe,... madaraja makubwa na mitambo ya umeme je? mnataka tumsubiri Ngeleja asiyekuwa na majibu na ahadi zisizo na ukweli au kila atayeweza a play their part kutatua tatizo?... NAWAUNGA MKONO 100%

My 2 cents
 
Kwa mbali napata harufu ....

Wasingewekeza pesa hii ingekuwa benk siyo?

Halafu unailaje??

There you are!!! The whole thing is nothing but a scam bag!!! Hao wanatafuta jinsi ya kula fedha zetu tu! Katika nchi kama yetu iliyojaa rushwa, nepotism.... you name them.... a proposal like that can never go without strings atouched!!
 
Being a specialist in electricity sector...I will speak only of their move to generate as IPP...

they initially engaged non engineers to design project just because they sawa power generation deficit...
After I had a chance to see the proposal...oh! Salale!

U just don't do that..the best I can independently adviced them to do, was to procure and install and not whatever they wanted earlier because its not inlinewith PSMP however;

Any private investor should seek first the original n approved POwer System Master plan before venturing..am speaking of power utility investors

Also by committing pensioner's money on a project they have little expertise with..is gamblin...

Mhandisi, mifumo na njia kuu za umeme

Every business will always have some gambling (risks) but still we have to do business to go forward.

If the investments involves nothing fishy, atmost important is to hire expertise (if it lacks) through contractors etc and run the investments in open - shareholders (members) should be informed risks aforehand. I don't know if members knows the true accounts of NSSF, otherwise politicians (under CCM everything is politics & ufisadi) could steal the money through those projects like it was no ones business. In TZ we should draw laws and have law firms which protects small shareholders in big companies like NSSF otherwise in near future NSSF may file for bankruptcy and get a free ride without any accountability.

Sifahamu NSSF ikifirisika boss ama board yao iko accountable vipi kwa wenye hizo pesa.
 
Inawezekana kweli NSSF wana pesa nyingi zimekaa tu. Na wenyewe kujiingiza katika miradi mikubwa ndani ya nchi ni nzurisana, ila wasiwasi unatokea pale ambapo tunajiuliza hivi wakurugenzi wa hii NSSF wanateuliwa na nani?
Kama ni mkuu wa serikali ya ccm basi itakuwa ni yale yale kwamba baada ya kuikomba tanesco, atcl, reli, nk ambao kimsingi wakurugenzi ni makada wake sasa wanaimezea mate Nssf.
Hapa itakuwa ni ccm wanaifuata nyuki ili wale asali na kwa upande wa pili ni Nccf wanaifuata asali ili waliwe na nyuki.
.
 
There you are!!! The whole thing is nothing but a scam bag!!! Hao wanatafuta jinsi ya kula fedha zetu tu! Katika nchi kama yetu iliyojaa rushwa, nepotism.... you name them.... a proposal like that can never go without strings atouched!!

Kwahiyo mzee tukae hivihivi bila kufanya chochote kwa sababu ya kuogopa kuibiwa? Idea kubwa ya biashara yoyote ni upatikanaji wa faida. Bank wanaibiwa, serikali wanaibiwa, mashirika binafsi wanaibiwa lakin at the end of the day if you are making profit that is the whole idea of business. Kama kuna faida ifanyike
 
NImeanza kuangalia hapa (ndani ya siku hizi chache zilizopita) na ninaanza kuona tatizo mahali fulani; japo kwa juu inaonekana vizuri sana lakini naanza kuhofia na ninashindwa kuelewa kwanini NSSF inawekeza fedha za wafanyakazi wake kwenye miradi hii mikubwa ya Umeme, Ujenzi wa Madaraja na sasa Ujenzi wa Barabara.

Kuna kitu hakiko sahihi; nia yaweza kuwa nzuri lakini kuna kitu hakiko sahihi... sijui ni kitu gani bado.. lakini something is very very wrong somewhere..

Na Kiwira Coal Mine nayo wanataka kuwekeza
 
in 2009 investment kwenye govt bonds ilikuwa 48% of total investment, sasa hivi itakuwa above 60%. this is serious regulator wanaachiaje NSSF invest hela yote hii mahali pamoja. je yakitokea yale yaliyotokea dubai au argentina inamaanisha na wafanyakazi wote wa sekta binafsi tumekwisha TBL wanauza bond ya 60bn tunataka kuona NSSF ina invest kwenye kampuni kama hizopia tunataka kuona nssf ikijenga nyumba za kukaa watu na kuziuza ili kupata quick return ya investment na siyo kung'ang'ana na hizi non-performing office blockskuhusiana na IPP, nssf ina sera ya kukopesha local business depending na reputation of the company, the management na reputation ya owner, IPP and mengi fits the criteria
 
Kilichowashinda kwenye daraja la kigamboni ni nini siku zote hizo! Hawana jipya. wanatumika kisiasa tu. Ni waajiriwa wao!
 
Mwanakijiji hata mimi nilikuwa na wasiwasi lakini nilipata kukutana na hawa ma Director wa NSSF kwenye Diaspora ya MN mwaka jana na ukweli ni kwamba wana tumia pesa ya faida tu!!. NSSF haitumii pesa za mwanzo bali faidi waliopata kwa miaka mingi na ndiyo maana wana 1.5B dollars. Hawa jamaa wana Invest vizuri hata kama kuna ufisadi wameleta faida kubwa sana kwa wananchi wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom