NSSF na Infrastructure Investment: Kigamboni Bridge, IPP, Road Construction.. ???

Mwanakijiji,
Inawezekana wana nia nzuri na inaweza kutuepusha na haya ma capacity charge ya kina dowans kwa kuwa hili ni shirika la umma na faida watakayopata itaingia hazina. Lakini kwa upande mwingine wenye fedha hizo wangekuwa na sauti kidogo kwenye fedha zao. Haiwezekani Sumaye ambaye si mwanachama wa mfuko huo kukopa wakati mimi mwenye akiba yangu huko nashindwa kukopeshwa hata nusu ya akiba yangu.
 
Kama Serikali imeshindwa, na NSSF wanaweza, basi ni bora atafutwe mwekezaji aichukue serikali ili aweze kufanya wanayoyashindwa
 
NImeanza kuangalia hapa (ndani ya siku hizi chache zilizopita) na ninaanza kuona tatizo mahali fulani; japo kwa juu inaonekana vizuri sana lakini naanza kuhofia na ninashindwa kuelewa kwanini NSSF inawekeza fedha za wafanyakazi wake kwenye miradi hii mikubwa ya Umeme, Ujenzi wa Madaraja na sasa Ujenzi wa Barabara. Kuna kitu hakiko sahihi; nia yaweza kuwa nzuri lakini kuna kitu hakiko sahihi... sijui ni kitu gani bado.. lakini something is very very wrong somewhere..
Mkuu hakuna tatizo lolote. NSSF inachofanya ni purely busines na tena yenye returns kubwa kuliko biashara halali unazozijua. Kinachofanyika ni kama kuikopesha serikali ambayo italipa kidogo2. Kwa upande wa Kiwira kuna faida nyngi zikiwemo za rasmali za nchi na faida zake zinabaki nchini. Inachokifanya NSSF ni kuwa reliable Financier wa GOT opportunity ambayo haijawa utilized na Taasisi za ndani.
 
1.Kwa nini tumeshindwa kuwawajibisha waliotuletea Dowans na Richmond?

2. Kwa nini mpaka teo tunashindwa kuiendesha Tanesco kiufanisi?

3. Kwa nini tumeshindwa kutokomeza rushwa?

4. Kwa nini tumeshindwa kundesha ATC?

5. As such Kwa nini hiyo mipango ya NSSF isishindwe?

Kwa hivyo inatakiwa tufanyaje? Tuache kujaribu kuleta maendeleo kwasababu tanroads, atc na tanesco vimekufa.. Tanroads wamekuwa na mafanikio makubwa katika miaka kadha kisha matatizo yakaanza, tanesco imekufa kwasababu ya mikataba yaajabu ya IPTL, Aggrecco sijui (chenge, Mary ndosi,etc). Kwamaana nyingine unataka nchi isimame kwasababu kuna rushwa? That makes no sense.
 
Naomba kuuliza;

Hivi NSSF pamoja na taasisi nyingine za fedha haidhibitiwi na sheria yoyote kuhusu wapi na vipi wanaruhusiwa kuwekeza fedha za wanachama? Ninavyofanamu mabenki yanadhibitiwa na kanuni za BOT kuhusu jinsi ya kuwekeza akiba za wateja wake, na pia ni asilimia fulani tu ya akiba ndio wanaruhusiwa kufanyia biashara.
-Vipi kuhusu NSSF, PPF, PSPF nk?
-Hawa wako huru kuwekeza popote wanapotaka?
-Wanadhibitiwa na sheria yoyote?
 
Naomba nimnukuu mwananchi mmoja "This is proof that our country has too many politicians and too few statesmen. While the statesmen are concerned with the next generation, the politicians are terribly concerned with the next elections.
Kikwete,dont wait for the coming election"

Kinachokosekana ni ule uthubutu wa kufanya mambo kwa ajili ya vizazi vijavyo wanasiasa wanaangalia uchaguzi ujao vyama vya siasa wanajipanga kwa ajili ya 2015. Yaani wapo busy kiasi kwamba hawakumbuki kufanya mambo muhimu ya kulisaidia taifa.

Nadhani si sawa kwa NSSF kufanya hiyo miradi yote lakini kwa upande mwingine tukiwazuia hakutakuwa na wakuifanya matokeo yake muda unaenda na sisi tutakuwa tunajikongoja kwenye maendeleo.

Ukicompare NSSF contributions wanazokatwa wafanyakazi na pesa zinazopatikana kwenye VAT collections nahisi VAT collections inazidi NSSF duductions japo hizi fugures za VAT huwezi kuambiwa wanapata ngapi! Kuna kodi ya "RoadToll" kodi hii kama ingetumika kwa ajili ya miundombinu tu nina hakika tusingekuwa na matatizo ya kinetiweki na ingesaisa kukuza uchumi kwani accessibility kati ya mashambani na kwenye masoko ingekuwa ni ya uhakika.

I ADMIRE YOUR FIRST PARAGRAPH!!
I want to ask you one question that;
"Have you ever heard a Tanzania Leader/politician apart from Nyerere who stood on the platform and on his speech he/she say this sentence: we are doing this for the future generation:? Siku ukimsikia mwanasiasa yeyote amesema hiyo sentensi jukwaani nakuomba usifiri mara mbili kumuunga mkono.
OTHERWISE; hao NSSF, PPF, PSPF,LAPF na wengine unaowafahamu ni genge la mawakala wa wezi waliojibatiza u- peace keeper kwa kusema wao ndo walinda amani ya nchi hii kwa hivo tuwasikilize na kufuata chochote wanachosema!! Genge hili linatumia hizo taasisi kuwanyonya wa-TZ!!!
 
NImeanza kuangalia hapa (ndani ya siku hizi chache zilizopita) na ninaanza kuona tatizo mahali fulani; japo kwa juu inaonekana vizuri sana lakini naanza kuhofia na ninashindwa kuelewa kwanini NSSF inawekeza fedha za wafanyakazi wake kwenye miradi hii mikubwa ya Umeme, Ujenzi wa Madaraja na sasa Ujenzi wa Barabara.

Kuna kitu hakiko sahihi; nia yaweza kuwa nzuri lakini kuna kitu hakiko sahihi... sijui ni kitu gani bado.. lakini something is very very wrong somewhere..
Kweli Mzee Mwanakijiji , tutashuhudia wastaafu wakibadilishiwa masharti muda si mrefu kwa ukosefu wa fedha za kuwalipa, mf.kuongeza umri wa kustaafu ili kuupa mfuko pumzi kidogo , pia kubadilisha formula ya mafao ili kumnyonga mchangiaji na mengine mengi .
 
mimi nilidhani...NSSF ingekuwa ni shirika la umma la kwanza na kubwa kwa ajili ya utoaji mikopo kwa wanachama wake ambao wengi huenda kuchukua mikopo kwenye mabenki binafsi kwa riba kubwa na mikopo hiyo hupatikana kwa nyodo kubwa sana

hivi hii sector ya social security ni monopolized na serikali tu...au private sector wnaweza kufanya... mimi nashauri kuwe na policy ya ku involve private sector kuingia kwenye social security ili kuwe na competition

Tatizo mkuu sisi watanzania hatuna utamaduni wa kulipa tunapokopa, watu wakubwa kama kina Mengi na Mbowe wanadaiwa mamilioni na NSSF na sio kama hawawezi kufanya marejesho ila wanazungushia kwenye biasha zao nyingine huku NSSF wakisubiri marejesho. Kwa kusema wawakopeshe wanachama mie nakukatalia NSSF labda useme wajenge nyumba za bei nafuu "low cost housing project" ambazo zitawanufaisha wanachama wake na waweke policy ya mtu kulipia nyumba hizo kwa muda mrefu "housing finance" itakayochukua mpaka miaka 20! Kwa hakika hapo watakuwa wamewasaidia wanachama na watarudisha gharama zao lakini suala la kukopeshana siliafiki!
 
I ADMIRE YOUR FIRST PARAGRAPH!!
I want to ask you one question that;
"Have you ever heard a Tanzania Leader/politician apart from Nyerere who stood on the platform and on his speech he/she say this sentence: we are doing this for the future generation:? Siku ukimsikia mwanasiasa yeyote amesema hiyo sentensi jukwaani nakuomba usifiri mara mbili kumuunga mkono.
OTHERWISE; hao NSSF, PPF, PSPF,LAPF na wengine unaowafahamu ni genge la mawakala wa wezi waliojibatiza u- peace keeper kwa kusema wao ndo walinda amani ya nchi hii kwa hivo tuwasikilize na kufuata chochote wanachosema!! Genge hili linatumia hizo taasisi kuwanyonya wa-TZ!!!

Mkuu ifike sisi wenyewe tujitambue tumeshafanya chaguzi nne mpaka sasa za vyama vingi kuna vyama vilitikisa nchi na hivi sasa vimezinduka kutoka ICU, hivi vyama vitavuma vitakufa vitafufuka lakini Tanzania itabaki palepale tuijenge Tanzania yetu na sio vyama tunavyoshabikia, lazima tukubaliane kuwa hawa wanasiasa wote ni baba mmoja mama mmoja sisi wanatuambia hatushirikiani nao na kutujaza maneno ya chuki! Wao wakikutana wanaenda kula nyamachoma pamoja mnadani dodoma wanagonga glasi sisi huku tunateseka na mgao wa umeme wananchi wanaambiwa mtakula nyasi kwa kitu kisicho na tija kwa Taifa!

Tunahitaji statesmen hatuhitaji mwansiasa, tunahitaji watakao ijenga Tanzania ya kesho hatuhitaji wanaoweka mazingira ya uchaguzi ujao.... ndio maana nikasema "our country has too many politicians and too few statesmen. While the statesmen are concerned with the next generation, the politicians are terribly concerned with the next elections".
 
Tatizo mkuu sisi watanzania hatuna utamaduni wa kulipa tunapokopa, watu wakubwa kama kina Mengi na Mbowe wanadaiwa mamilioni na NSSF na sio kama hawawezi kufanya marejesho ila wanazungushia kwenye biasha zao nyingine huku NSSF wakisubiri marejesho. Kwa kusema wawakopeshe wanachama mie nakukatalia NSSF labda useme wajenge nyumba za bei nafuu "low cost housing project" ambazo zitawanufaisha wanachama wake na waweke policy ya mtu kulipia nyumba hizo kwa muda mrefu "housing finance" itakayochukua mpaka miaka 20! Kwa hakika hapo watakuwa wamewasaidia wanachama na watarudisha gharama zao lakini suala la kukopeshana siliafiki!

kwani hakuna mahakama za kwenda? Ina maana NSSF nayo imesaini mikataba mibovu na hao wafanya biashara? Mbona pesa inarudishwa kama wanataka? Si unaenda kuuza hizo assets zao. By the way...tofautisha mtu Mengi au Mbowe kukopa na kampuni yao kukopa. Hivyo ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Nimependa hii topic. kuna wakati niliuliza kuhusu hili shirika la nssf na mishahara ya viongozi wao. Ni kweli wanaweza kuwa na pesa nyingi, lakini lazima tuhakikishe kuwa hizi pesa zetu zinarudi. Kuendesha shirika kama NSSF sio kitu kidogo. Lazima ugawe watu katika makundi mengi, na uta-target investment zilizo na return zinazoendana na hayo ma-group ya wawekezaji. Kwa mfano...mtu mwenye miaka hamsini huwezi kuwekeza hela zake katika biashara yenye risk kubwa. Lakini kijana wa miaka 25 ni rahisi kumweka katika kundi la risky investors.
Tunachohitaji ni kupata data zaidi kutoka kwao, kwa ajili ya kujua wana-expect return ya kiasi gani kutoka kwenye hizi investments. Ama sivyo siku tuna-retire utasikia pesa zimeisha! Wapi naweza kupata data zao hawa?
 
What is social security?

"Social security may be defined as any programme of social protection established by legislation, or any other mandatory arrangement, that provides individuals with a degree of income security when faced with the contingencies of old age, survivorship, incapacity, disability, unemployment or rearing children. It may also offer access to curative or preventive medical care. As defined by the International Social Security Association, social security can include social insurance programmes, social assistance programmes, universal programmes, mutual benefit schemes, national provident funds, and other arrangements including market-oriented approaches that, in accordance with national law or practice, form part of a country's social security system."

Cha kushangaza hapa Tanzania tunatumia Social Security zetu kwenye miradi mikubwa ya Umeme, Ujenzi wa Madaraja na Ujenzi wa Barabara. Hivi sisi tunaakili kweli???
 
mkuu...kusoma bandiko lako inahitaji uwe na binocular au theodolite
 
Mimi sidhani kama Nina tatizo na hili. Ni bora kuliko kuziacha hizo pesa zinafujwa na wanasiasa. Afterall, ukistaafu watakunyanyasa tuu hata kama hawakuinvest hizo pesa. Pia bora kwamba ni taasisi ya home kuliko Richmond ambao pesa zetu wamehamishia nchini kwao
 
Tatizo mkuu sisi watanzania hatuna utamaduni wa kulipa tunapokopa, watu wakubwa kama kina Mengi na Mbowe wanadaiwa mamilioni na NSSF na sio kama hawawezi kufanya marejesho ila wanazungushia kwenye biasha zao nyingine huku NSSF wakisubiri marejesho. Kwa kusema wawakopeshe wanachama mie nakukatalia NSSF labda useme wajenge nyumba za bei nafuu "low cost housing project" ambazo zitawanufaisha wanachama wake na waweke policy ya mtu kulipia nyumba hizo kwa muda mrefu "housing finance" itakayochukua mpaka miaka 20! Kwa hakika hapo watakuwa wamewasaidia wanachama na watarudisha gharama zao lakini suala la kukopeshana siliafiki!

MS: Kwenye kukopesha wanachama nadhani mtazamo wako sio sawa.
1. Usi-generalize kwamba sisi watanzania hatuna utaratibu wa kulipa tunapokopa. Ni kweli wewe haukopesheki??? Ukikopa huwa haurejeshi??
2. Haya mabenki mbona yameweza kutukopesha tena kwa barua ya mwajiri tu na kasalare slip kako. Hizi foleni unazoziona zinazidi kila siku ni kwa sababu leo hii mtanzania anaweza kupata mkopo wa 10m ndani ya 24hrs.

Hofu yangu kama ilivyo ya wengi ni juu ya ajenda iliyo nyuma ya hii miradi maana hakuna wa kumwamini (siasa kila mahali).
Kama ni swala la miradi Shirika la Maendeleo (NDC) kazi yake nini???
NSSF kama wanahela kibao watukopeshe wanachama kwanza, mfuko ni wa wanachama ambao ni sehemu ndogo sana ya watanzania. Mwenye wajibu wa kujenga hiyo miundo mbinu ni serikali maana pesa wanayo tatizo hakuna wenye kuwaza kizazi cha kesho.
 
Back
Top Bottom