NSSF Kimewaka

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,268
17,097
Ni baada ya kubandika tangazo rasmi la kusitisha malipo ya ''mafao''.

Wanachama waliokuwa hawana taarifa na wamekuja kuchukua malipo yao wamekuwa mbogo ile mbaya.

Nilikuwa napita na hamsini zangu nikakutana na hizi mia!!
 
Mkuu Safari
Mbona leo unaonekana kuwa na mawazo mengi?
Ni wapi unapoongelea? ...habari yako iko kimkatokmato!
 
Last edited by a moderator:
duh aisee ningekuwa mie ni liwalo na liwe ningeingia na rocket launcher, pesa ni ya kwangu kwa nini niwekewe masharti, tena sababu ya ujinga wa CCM, liwalo na liwe
 
Ni baada ya kubandika tangazo rasmi la kusitisha malipo ya ''mafao''.

Wanachama waliokuwa hawana taarifa na wamekuja kuchukua malipo yao wamekuwa mbogo ile mbaya.

Nilikuwa napita na hamsini zangu nikakutana na hizi mia!!

Heeeeeeee!!!!!

Hivi ina maana ni kwamba imeanza mara moja!!!!!!

mimi nilifikiri wametoa muda kuwa hawapokei maombi mapya tena bali wanamalizia na yale waliyopokea!!!!!!

Hawatutendei haki kabisa!!! huu niwizi na dhurumati kubwa!!!!!

Ni heri waseme pia siyo lazima mfanyakazi kukatwa hayo makato ya mifuko ya jamii, mtu ajiamuamulie kama kujiunga au la!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mkuu Safari
Mbona leo unaonekana kuwa na mawazo mengi?
Ni wapi unapoongelea? ...habari yako iko kimkatokmato!

atakuwa ni yeye maana hii kitu inachanganya sana, pata picha uliacha kazi miezi mitano iliyopita hivyo unahesabu siku tu upate chako leo unaambiwa hunachako mpaka ufikishe miaka 60 wakati huo wewe una miaka 30..unaweza usirudi nyumbani
 
Kweli hili swala litaumiza yaani nifanye kazi halafu ninapo jitoa kwenye ajira naambiwa sitopewa hela zangu hadi nifike miaka 55 ama 60 halafu hiyo pesa wala hupewi kwa intrest unapewa kama ulivyo iacha.

thamani ya pesa itakuwa imeshuka baada ya miaka 15.

tunazidi kunyonywa tu hela zetu na hawa mafisadi zile walizokopa nssf bado hawajazirudisha bado tena wanataka kuendelea kutugandamiza.
 
atakuwa ni yeye maana hii kitu inachanganya sana, pata picha uliacha kazi miezi mitano iliyopita hivyo unahesabu siku tu upate chako leo unaambiwa hunachako mpaka ufikishe miaka 60 wakati huo wewe una miaka 30..unaweza usirudi nyumbani

Mjumbe hauwawi jamani.....sijachanganyikiwa hata!
 
atakuwa ni yeye maana hii kitu inachanganya sana, pata picha uliacha kazi miezi mitano iliyopita hivyo unahesabu siku tu upate chako leo unaambiwa hunachako mpaka ufikishe miaka 60 wakati huo wewe una miaka 30..unaweza usirudi nyumbani
hawa jamaa ni wapuuzi sana, mi nadhani sasa serikali ituambie sisi wenyewe tuamue kukatwa kwenye mifuko ya jamii au tuweke hela zetu wenyewe kwenye VIBUBU, huu ni wizi kutuibia hela zetu kwenda kujengea magorofa.
 
hili binafsi sikulipenda kabisa mbaya sana naelewa jinsi linavyo sumbua kibaya zaidi mtu anapokosa kazi hili ndilo fao pekee analolitegemea nimsogeze wakati akijipanga sasa nini hiki wanafanya?
tatizo hawa jamaa hawajawahi kukaa bench ndo mana wanafanya huu upumbafu
fikiria watu wanadaiwa mtaani na taasisi mbalimbali za fedha je wao wanaweza kuyakabili madeni yao? inauma sana serikali inakopa na kufadhili miradi mikubwa bila hata kuwaeleza wanachama na wanachama wanaangalia.
limekuwa kimbilio kwa serikali kwa shida zake zisizo za lazima kwa uzembe wa kutokukusanya mapato
hili linauma sana.
lakini wafanya kazi wanatakiwa kujifunza kitu kipya
 
Nasikia ni mpango wa magamba wa kukusanya pesa kwa ajili ya kampeni ya 2015. CDM mtutetee na hila hizi. Pesa ni zetu, hawajafanya makataba na Mungu kuwa kila mfanyakazi ataishi miaka 55 au 60. Ukimwi njenje siku hizi na unaruhusu walau kuishi kwa miaka 20. Nonsense.
 
nafikiri kuna aja ya kuanzisha mifuko yetu ya fedha katika ofisi zetu ambayo tunaweza kuianzisha kwa kivuli cha saccos na tukafaidika nayo kwa muda wote kwa kukopeshana na kugawana faida vilevile kuwekeza kwa vitege uchumi tunavyo fikiria vinaweza kutulipa nikirudi nitarudi na mfano wa miaka mitatu wa heasbu za maana kuliko za serikali na fedha za watu huu ni upuuzi.
 
walijifanya kutekeleza sera za ccm ambazo hazitekelezeki matokeo yake wametumia hela za wanachama. kwani nisipochangia itakuaje? wanipe hela yangu nikawekeze vikoba. na daraja la kigamboni sijui kama litajengwa.
 
Hii si sawa kwa kweli, hivi na hizi ajali za boti, mabasi, treni si tutakufa kabla ya kufika maika 55, hapo itakuwaje hata warithi wetu inamaana watasubiri mpaka tufike miaka hiyo tukiwa kaburini?
 
Tuambie ni wapi huko maana wengine jana tumehudumiwa kama kawaida hapa twali la NSSF Geita, na wanatuambia kuwa hawana taarifa yoyote wanasikia tu na wao magazetini.
 
Tuambie ni wapi huko maana wengine jana tumehudumiwa kama kawaida hapa twali la NSSF Geita, na wanatuambia kuwa hawana taarifa yoyote wanasikia tu na wao magazetini.

Hebu nenda na leo....mimi nilifika pale Ubungo
 
Hii si sawa kwa kweli, hivi na hizi ajali za boti, mabasi, treni si tutakufa kabla ya kufika maika 55, hapo itakuwaje hata warithi wetu inamaana watasubiri mpaka tufike miaka hiyo tukiwa kaburini?

Pension hapewi mrithi mkuu, ukiondoka dunia hii na pension kwishney! Assuming ulikuwa umeanza kupewa that is!
 
Jamani tuache hata kufa tu, kampuni nyingi za private zinafanya kazi kwa muda fulani mfano kama miaka 15, 20 n.k. Kwa hiyo wanachosema mafisadi ni kwamba ukiachishwa kisa muda wa kampuni umeisha au umefukuzwa au umeacha kwa hiari basi uendelee kula nyasi weeeeeeeeeeee hadi 55-60. Nakwambia tutapigana, hili haliwezekani hata kidogo.
 
Back
Top Bottom