hela zimeenda wapi?
atakuwa ni yeye maana hii kitu inachanganya sana, pata picha uliacha kazi miezi mitano iliyopita hivyo unahesabu siku tu upate chako leo unaambiwa hunachako mpaka ufikishe miaka 60 wakati huo wewe una miaka 30..unaweza usirudi nyumbani
Jamani tuache hata kufa tu, kampuni nyingi za private zinafanya kazi kwa muda fulani mfano kama miaka 15, 20 n.k. Kwa hiyo wanachosema mafisadi ni kwamba ukiachishwa kisa muda wa kampuni umeisha au umefukuzwa au umeacha kwa hiari basi uendelee kula nyasi weeeeeeeeeeee hadi 55-60. Nakwambia tutapigana, hili haliwezekani hata kidogo.
wadau,hivi kweli hii serikali inaendashwa na watu wenye akili?.wanapoamua mambo haya bila kuwashirikisha wadau ambao ni sisi wanatutendea haki kweli??
We fikiria mimi nilipata kibarua mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili tu,na makato ya nssf yalianza mara moja baada ya kusaini mkataba huo je nitasubiri hadi nifikishe miaka 50 ndo nikadai mafao yangu hayo??
Kazi nimefanya 2011/2012 na nina umri wa miaka 20 so nitalazimika kudai mafao yangu ya miaka miwili niliyofanya kazi ifikapo mwaka 2062???
Haileti picha wala haikubaliki,kama wamezitafuna pesa zetu wakidai ni mali yao sasa wanaumbuka mchana kweupe!!!
Mkuu sasa maandamano yetu yaanze lini maana hakuna tofauti na kuliwa 0713 huku unajiona na huwezi hata kujitetea.Pension hapewi mrithi mkuu, ukiondoka dunia hii na pension kwishney! Assuming ulikuwa umeanza kupewa that is!
Hivi hili swala wapinzani wa kweli chadema huko bungeni hawajalisikia?ili waombe muongozo kwa spika lijadiliwe jamani,maana walalahoi wengi ndo wanakotegemea maana ajira zenyewe za wahindi hizi mwaka uko kazini mwaka nje.Hapa sasa kwa hili natarajia wazee wa magwanda watusaidie otherwise sitawaelewa.