NSSF Ianze kutoa gawio la faida kwa wanachama?

Mimi nafikiri hukutakiwa kumshambulia alietoa mjadala, nadhani kataja NSFF pengine kwa kuwa michango yake inakusanywa na NSFF.

Wakati mwingine muwe mnawasikiliza wateja na sio kuwashambulia kwa hoja nyingine, wewe jibu kwa hoja na sio kuleta mambo mengine.

Kwa ufupi ni kwamba mchangiaji alitakiwa kuwa na uhuru na anachochangia na sio kama inavyokuwa sasa.

Ukiniambia nichangie kwa ajili ya malipo ya uzeeni nani kakuambia anataka malipo uzeeni na sio sasa?

Pili, unawezaje kuzungusha fedha zangu utengeneze faida na mimi nisifaidike na faida?

Nafikiri kuna haja ya mifuko hii kufanya kama ambavyo tunafanya kwa katiba sasa. Fanyeni vipindi katika vyombo vya habari na mchukue mawazo ya wateja wenu kwa vile ambavyo wote mnaweza kufaidika na sio ninyi pekee.

Naomba kuwasilisha.
 
Usiwe na Roho ya kwa nini? Pension funds ziko ngapi mpaka unazungumzia NSSF Pekee? Kama unakiri bila kudhamiria kuwa NSSF inafanya vizuri lakini unakataa kutoa pongezi kwa kina Dau kwa sababu unazojua mwenyewe.

Pia tambua tofauti ya kampuni,Pension fund na shirika itakusaidia sana kujenga hoja, msingi wa pension fund sio kusaidia wafanyakazi pekee ni jamii nzima that is why inajukumu kwa upande mmoja kusaidia welfare of society na sio wafanyakazi pekee ndio sababu inajishughulisha kwenye ujenzikama UDOM, MADARAJA, NYUMBA ZA ASKARI N.K fAIDA IPATIKANAYO INAZUNGUSHWA SIO KUGAWANYWA kama unavyofikiri, Msingi mkuu ni kulea wastaafu kama una la kushauri ni kuishauri NSSF ibadili kanuni ya kulipa mafao iwe bora zaidi iwanufaishe wastaafu badal ya kutumia kanuni ya sasa inayotoa mafao kiduchu acha ukalulu kwenye fani za watu!

NSSF is a poorly managed fund in Tanzania. Ni bahati mbaya ndiyo yenye wanachama wengi kwani mfumo hapo awali ulikuwa unawabeba kabla ya PPF na mifuko mingine kuruhusiwa nao kuchukua wanachama kutoka sekta binafsi.

Leo hii kaulize rekodi ya mafao yako NSSF, hutapewa jibu. Rekodi zao ziko 6 months or more behind. PPF unapata last but one.

Issue sio Dr. Dau..issue ni mafao. Mwanakijiji anaweka kuwa na issue na Dau..hii sio hoja, hoja iliyopo mezani ni jinsi gani wanachama wanaweza kufaidika na michango yao. Sio wanachama wanakamuliwa wafanyakazi NSSF wanazidi kunawili.
 
sasa dau umemtaja taja hapo kama mungu mtu wa kazi gani??

Yan watu tuache kuzungumza na kuhoji mambo yetu ya msingi eti tumhofie dau?

Who the hell is he?

Haya mfikishie salam zake boss wako huyo

Mkuu inawezekana huyo mrnssf ndio Dau mwenyewe kaamua kupambana kwa mlango wa nyuma, hoja iko wazi kabisa yeye anataka kutuhamisha kwenye mada eti chuki binafsi.
 
mkuu inawezekana huyo mrnssf ndio dau mwenyewe kaamua kupambana kwa mlango wa nyuma, hoja iko wazi kabisa yeye anataka kutuhamisha kwenye mada eti chuki binafsi.

basi kama ni yeye hapa ataeleza tuh,,

kilichomtoa kanga manyoya
 
Hivi kuna uwezekano wa kuhifadhi jamii vizuri zaidi kuliko kutengeneza utajiri kwa watu? Kwanini tunafikiria pensheni inahifadhi jamii?
 
Shirika la Hifadhi ya Jamii limekuwa au niseme limegeuzwa kuwa Shirika la Uwekezaji la Hifadhi ya Jamii. Na kwa jinsi ambavyo linaendeshwa bila ya shaka linasukumwa na kutafuta faida na ni faida hii ambayo linapata imekuwa ikiwekezwa kwenye miradi mbalimbali. Hili si tatizo.

Hata hivyo kwenye mashirika ambayo yanafanya kazi kwa ajili ya faida (for profit companies) yanarudisha sehemu ya faida yake kwa wanahisa (shareholders) wake. Inaweza kurudishwa kama gawio (dividends) kila mwaka kufuatana na kanuni ambayo shirika limejiwekea.

NSSF inakadiriwa kuwa na wanachama karibu 600,000 hadi mwezi Juni mwaka huu likiwa na mali yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja ambayo inakadiriwa kukua kwa haraka hadi mwaka 2013. Kwa mujibu wa sera zao za uwekezaji NSSF hutenga asilimia 75 ya fedha zao kwenda kwenye uwekezaji na asilimia 25 kwenda kwenye mafao na gharama za uendeshaji. Ni wazi kuwa 2/3 ya fedha zinazoweza kuwekezwa zinawekezwa kwenye kile ambacho kinaonekana ni 'high yield' investments.

Je ipo haja ya kuligawa shirika hili na kuhakikisha upande unahusiana na hifadhi ya jamii (mafao kwa wanachama) unaendeshwa tofauti na upande unaohusika na uwekezaji? Je kuna uwezekano wa kuhakikisha kuwa huo upande wa uwekezaji unaendesha kama kampuni nyingine ya faida ambapo wanachama wa NSSF ndio wanakuwa wanahisa wa shirika hilo na ambao watalipewa gawio kila shirika linapotengeneza faida kabla halijaamua kuwekeza fedha kama faida?

Swali hili ni muhimu kwa sababu kwa mtu ambaye anachangia NSSF na bado hajaanza kupata mafao mbalimbali au hajatumia mafao yoyote kwa mwaka hapati faida yoyote ya kifedha kutokana mchango wake ambao unatumika kutengeneza faida kwa shirika. Na kama mtu atakuwa amechangia kwa miaka mitano au zaidi na labda amepata fao la msiba, n.k au aambiwe asubiri hadi kuretire kuanza kupewa shilingi themanini elfu kila mwezi baada ya kuchangia shirika kwa miaka thelathini au ishirini naona ni unyonyaji wa aina yake.

Ni muhimu kwa wanachama kufaidika kifedha (monetary benefit) na uwekezaji wa NSSF kila mwaka. Na namna pekee ya kuwafanya wanachama nao wanufaike ni kuhakikisha kuwa NSSF (bila ya shaka na mashirika mengine ya pensheni) inaweka utaratibu wa kuwagia wanachama wake ama kwa kutengeneza account au kuchangia kwenye akaunti ya mwanachama kiasi cha faida fedha ambazo mwanachama anaweza kuzitoa wakati wowote nje ya zile za pensheni.

Jambo la kwanza ambalo linahitaji kufanyika kwa haraka ni kubadili sheria ili NSSF isiwezeke fedha za wanachama kwenye miradi yenye kutarajia faida bila kuhakikisha kuwa sehemu ya faida inayopatikana inawarudia wanachama kama gawio siyo kama sehemu kiduchu ya mafao.

Swali la Ugomvi: Je CDM ina sera gani kuhusu NSSF na uwekezaji wa NSSF kwa sababu tayari tunajua sera ya CCM ni kutumia NSSF pale ambapo serikali imeshindwa au haina fedha au pale ambapo serikali inataka fedha ya haraka haraka kuikoa mbele ya wananchi.

hapo umenena..Pi umewahi jiuliza inakuweje wakunyime chukua hela yako na kujipatia mtaji, wanaamu akulazimisha kukopa hela yako kupitia saccos ili ukatwe riba ya saccos, na riba ya NSSF, huku siku unachukua hela hutopewa chochote ktk hiyo riba.

Wanafikiria kwa miguu. Hela yako ulazimishwe ikopa na kurudisha riba bila kuichukua.Yaani ni kama mctu achukue hela yako halafu akukopeshe.
 
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.


Threads ulizozianzisha kumshambulia Dr Dau ni hizi:




https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...erikali-na-hatima-ya-taasisi-ya-moyo-thi.html


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/16889-thi-yaibwaga-nssf-mahakamani.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19691-samahani-nssf-samahani-dr-dau-nyoni.html


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rof-kapuya-wawajibishwe;-nssf-ishitakiwe.html

https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/19593-cheche-mitaani-tume-yawanyoshea-kidole-nssf.html


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...inga-nssf-imekula-hasara-ya-bilioni-30-a.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kezaji-hayalipiki-ripoti-ya-cag-yafichua.html

https://www.jamiiforums.com/major-p...igamboni-bridge-ipp-road-construction-10.html



https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ra-uongozi-wa-nssf-makao-makuu-uwajibike.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/120673-ooh-poor-nssf-what-is-this-4.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ilia-mchakato-wa-ugawaji-viwanja-mafia-5.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...;-vitu-vyaibwa-vingine-vyarudishwa-kiana.html


Hebu nenda TRA,PPF na kwingine.

hata huna aibu NSSF ndo mfuko unaoongoza kula pesa za wafanyakazi na raia kwa ujumla badala ya kuja na majibu ya maana unakuja kusema tuwahoji na wengine we wa wapi,mada iliyopo ni NSSF shida nini kama kuna umuhimu wa kuwajadili wengine itaendelea siku nyingine.GIVE US A CRITIIQUE ANSWER mnajaza matumbo yenu tu huku wana hisa wanakondeana yaone.
 
hata huna aibu NSSF ndo mfuko unaoongoza kula pesa za wafanyakazi na raia kwa ujumla badala ya kuja na majibu ya maana unakuja kusema tuwahoji na wengine we wa wapi,mada iliyopo ni NSSF shida nini kama kuna umuhimu wa kuwajadili wengine itaendelea siku nyingine.GIVE US A CRITIIQUE ANSWER mnajaza matumbo yenu tu huku wana hisa wanakondeana yaone.
Tatizo ni little options ambazo wateja wanazo na pengine ujanja wa kujipanga mbeleni baada ya kustaafu (ambao hawana) au kuelewa what these cover entails. Wengine hatuwezi sema mengi kwakuwa hatujui sheria za mafao zinasemaje na wala mkataba wa NSSF na wachangiaji wake ukoje. Hila kinacho onekana NSSF wana advantage ya employers preference with little understandings and options from the contributors either way their business module is their business.

Lakini hawa jamaa inaonekana kwa upande mmoja wamekuwa wakipata michango mingi kutokana na government employees being directly reffered to them, sasa basi kwakuwa wanadirect monopoly and people have no options, hizo hela wanazopata lazima wazi-invest with social concioussness na si kutaka kuwaponda watu au kuwekeza kwa kutaka kuwaonea wengine. Mfano why do they have to forcefully remove people by paying them low and in the future make vast profits on those lands. Huo ndio ushe.zi wengine tunaouona hupo immoral.

By the way NSSF has no share holders to answer to, kwa hiyo habari ya Dividends ni kuropoka wewe utalipwa kutokana na mkataba wako, tatizo ni kwamba people are not given much options to invest elsewhere as employers tend to pick where to pay for their pensions funds.

Kuna mengi hapa ya kujadili.
 
Wiki iliyopita DG wa NSSF Ramadhani Dau, aliwapeleka wahariri Zanzibar na kuwapa Sh. Mil 1 kila mhariri. Ndoa ya mkurugenzi huyu na hao jamaa inatishia usalama wa michango ya wafanyakazi. Kuna kitu Dau anaficha na ameona namna bora ni kuwaweka wahariri mfukoni si anajua ni watu 'cheap'. Jukwaa la wahariri ni genge la wanafiki badala ya kusaidia jamii linaficha wezi
 
Wiki iliyopita DG wa NSSF Ramadhani Dau, aliwapeleka wahariri Zanzibar na kuwapa Sh. Mil 1 kila mhariri. Ndoa ya mkurugenzi huyu na hao jamaa inatishia usalama wa michango ya wafanyakazi. Kuna kitu Dau anaficha na ameona namna bora ni kuwaweka wahariri mfukoni si anajua ni watu 'cheap'. Jukwaa la wahariri ni genge la wanafiki badala ya kusaidia jamii linaficha wezi

Tafuta hicho kitu anachoficha ndio uje kamili huna haja ya kukurupuka, posho yako utaipata tu!!
 
Alhaj Ramadhan Dau ana UDINI SANA. Ana chuki binafsi na Wakristo. Anawapendelea sana Waislam katika ajira hapo NSSF. Bahati mbaya sana Alhaj Kikwete hawezi kumfuta kazi kwani ni Mwislam mwenzake na wote wana UDINI. Dr Dau ni mtu hatari sana katika Umoja wa Taifa letu.
 
Wajameni hizo milioni moja kila mhariri zimetoka mfukoni mwa Dr. Dau au offisi ya NSSF ndio imetoa??????

Tunaomba maelezo mtoa mada tafadhari. Inatishia amani hili jambo!!!!!



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Wiki iliyopita DG wa NSSF
Ramadhani Dau, aliwapeleka wahariri Zanzibar na kuwapa Sh. Mil 1 kila
mhariri. Ndoa ya mkurugenzi huyu na hao jamaa inatishia usalama wa
michango ya wafanyakazi. Kuna kitu Dau anaficha na ameona namna bora ni
kuwaweka wahariri mfukoni si anajua ni watu 'cheap'. Jukwaa la wahariri
ni genge la wanafiki badala ya kusaidia jamii linaficha wezi

na wewe ulipewa?
 
Alhaj Ramadhan Dau ana UDINI SANA. Ana chuki binafsi na Wakristo. Anawapendelea sana Waislam katika ajira hapo NSSF. Bahati mbaya sana Alhaj Kikwete hawezi kumfuta kazi kwani ni Mwislam mwenzake na wote wana UDINI. Dr Dau ni mtu hatari sana katika Umoja wa Taifa letu.

Jina na lenyewe linasadifu uwezo wa akili wa mtu,jadili hoja sio udini
 
hili kwa wahariri wa Tanzania sio geni na ndio unaona maendeleo yanavochelewa,kuna siku tulikwenda pale airpot kwa mwalimu nyerere na habari yetu ilikua na ushahidi kamili,ilikua ni taarifa ya kuibiwa kwa box za simu pale airpot na wezi ni wafanyakazi wa swisspot,alikamatwa na mzigo anauza mitaan tukaita vyombo habari tukahojiwa sana ni jinsi gani mali zetu zinavoteketea pale airpot mpaka leo tumepata ushahidi, tulipomaliza mahojiano sisi na waandishi mwisho ikawa zamu ya mkurugenzi wa swizzpot anaitwa GAUDENCE TEMU hapo boc alimwaga posho nzuri kwa waandishi ile habar iliyeyuka hapo ikawa ndio mwisho.
 
Back
Top Bottom