NSSF Ianze kutoa gawio la faida kwa wanachama?

Mwanakijiji mimi namshangaa huyu DAU ambaye amejipa uwaziri binafsi ndani ya serikali hamisha pesa Uswisi. Kuna wanachama wa NSSF wanaishi maisha mabovu hasa hasa katika suala la upangaji wa nyumba. Pesa zao zimekuwa zinapigiwa chapuo na CCM kutekeleza ahadi za Kikwete ili hali maisha ya wanachama wa Taasisi hii iko duni sana. HAkuna mradi wa unafuu uliwahi elekezwa kwa wanachama wa mfuko huu.

Kuna wanaJF humu wanataka Mwanakijiji asemee mifuko mingine kama PPF na mingineyo sasa sijui wao ndo Mwanakijiji. Kwani wao hawapo kujadiri hata uzuri wa hiyo mifuko??
 
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.

Threads ulizozianzisha kumshambulia Dr Dau ni hizi:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...erikali-na-hatima-ya-taasisi-ya-moyo-thi.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/16889-thi-yaibwaga-nssf-mahakamani.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19691-samahani-nssf-samahani-dr-dau-nyoni.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rof-kapuya-wawajibishwe;-nssf-ishitakiwe.html

https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/19593-cheche-mitaani-tume-yawanyoshea-kidole-nssf.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...inga-nssf-imekula-hasara-ya-bilioni-30-a.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kezaji-hayalipiki-ripoti-ya-cag-yafichua.html

https://www.jamiiforums.com/major-p...igamboni-bridge-ipp-road-construction-10.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ra-uongozi-wa-nssf-makao-makuu-uwajibike.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/120673-ooh-poor-nssf-what-is-this-4.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ilia-mchakato-wa-ugawaji-viwanja-mafia-5.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...;-vitu-vyaibwa-vingine-vyarudishwa-kiana.html

Hebu nenda TRA,PPF na kwingine.
Hivi wewe una akili timamu? mimi nikiwa kama Member wa NSSF nasema wapuuzi kama wewe mnastahili kunyongwa kabisa, Mwanakijiji anahoji maswali ya msingi akiwa kama Mwanahabari na anashirikisha sauti za wasiosikika halafu wewe unambeza?

Labda nikuulize swali dogo tu, kati ya Yusuf Manji na sisi Wanachama wa NSSF ni nani anastahili kupewa mkopo wa pesa? na unaposema kwenye huo uwekezaji sisi Wanachama tumeridhia ni lini kulikuwa na kikao hicho cha sisi kuridhia pesa zetu kutapanywa kwenye uwekezaji wa kiwehu? au mnadhani sisi hatukjui kama NSSF inaelekea kufirirsika?
 
Kuna ubaya gani kwa NSSF kuanzisha kampuni yake ya uwekezaji nje ya NSSF ya pensheni na wanachama wakapewa hisa humo?

Mkuu huna haja ya kuzunguka sana,mwanachama wa NSSF anapolipwa mafao yake hulipwa kile alichochangia na ka interest flani uchwara hivi! La msingi hawa wanatumia fedha zetu kuwekeza na kupitia uwekezaji (which is business) wanapata faida sasa kwanini hiyo faida wasipate wanachama?

Si lazima faida wanachama wapewe kama dividend,hata hicho kiji interest wanachotoa kwenye mafao kingekuwa level flani acceptable walau tungeridhika.
 
Nimepita kwenye website Kama ulivyonishauri, hata hivyo bado maswali yangu hayajajibiwa kwa sababu zifuatazo:
1. Performance reports zote ni kabla SSRA hajatoa investment guidelines.
2. It is unfortunate that actuarial valuation reports zingesaidia sana kujadili mada Kama hii, lakini hakuna hata moja. Je sisi wanachama hatuna haki ya kusoma hizo actuarial reports?
3. I stand to be corrected;
- Sio mifuko yote TZ iko under Defined Pension Scheme
- Hata NSSF kitendo cha kulipa withdraw benefit mfano kwa last year 2011 mlilipa Tshs. 106,221,067,003.52 ambayo performance financially ni 78% ya total amount paid kwa benefit zote. Je
Huoni Bado mnaoperate kama provident (defined contribution) wakati nyie ni pension fund ( defined scheme?)
- kwanini mmeendelea kulipa withdraw benefit tena kwa percent kubwa kuliko mifuko mingine huku mnawaambia watu Hilo sio fao? Mkiamua ku act ki profession msimumunye mumumnye
Maneno. Pia practice what you preach.

Mwisho
It is an obligation of management of the scheme or a legislation body to adjust the contribution rates when the financial resources are either insufficient enough to meet funds obligations or is in excess (buffer reserve) so that it reduce burden to contributors.

Sasa wewe unaposema mwajiri ndio apunguze au kuongeza kiwango cha uchangiaji umeitoa wapi hiyo? Je mwajiri amepewa acturial report?

Bado SSRA anatakiwa atolee maelezo ya kina haya mambo ya uwekezaji kwenye hii mifuko maana jinsi tunavyoenda umuhimu wa ofisi Yake unazidi kupwaya.

Nawasilisha.

Queen Esther
Queen Esther am happy kuona analysis yako nzuri isiyo ya kishabiki kama ya MMM. Yaelekea hayo mambo ya Hifadhi za jamii unayafahamu sema tu hutaki kuelewa.

1. Nikianza na hoja yako ya kwanza, ni kweli performance reports zote ni kabla SSRA hajatoa investment guidelines. Hizi guidlines za SSRA zinaanza kutumika mwaka huu, so Financials za mwaka unaoishia June 2013 zitakupa mwelekeo mzuri. Kumbuka pia before that kila mfuko ulikuwa na Investment policy yake na ilikuwa inafuatwa.

2.Actuarial valuation reports zipo na ni haki ya kila mwanachama kuziona na most of mifuko inaonekana inafanya vibaya kama serikali haitailipa madeni inayodaiwa. Nashangaa hili la MMM la kutaka kupewa dividend wakati mifuko karibu yote tanzania haipo kwenye hali nzuri

3. Mifuko yote TZ iko ni Defined Benefit Scheme, GEPF tu ndio provident fund. Kuhusu fao la kujitoa, kumbuka hamna fao kama hili unacholipwa ni michango yako uliyochangia na ya mwajiri wako bila kuconsider time value of money meaning factors kama interest na inflation hazikuwa taken into consideration. Dr Dau alishawahi kuelezea kuwa hata hizi withdraw zisingetakiwa ziwepo cuz hamna mfuko wowote duniani unaozitoa, but nia nzuri ya SSRA imekwamishwa na viongozi wachache wa upinzani waliotaka kujichukulia umaarufu kwa kulivalia njuga hili suala.

Kuhusu contributions, kuna proposal inayofanyiwa kazi asilimia ziongezwe zifikie at least 22-25% tofauti na 20% ya sasa. So hilo suala lako la kupunguzwa kwa sasa lisahau.
 
Mi nadahani wakati sasa umefika kwa wanachama wa mifuko ya jamii kuwa na mamlaka ya kuhoji kuhusu michango yao.
Wakurugenzi wengi wa hii mifuko wamekuwa wakitumia fedha katika kujitafutia umaarufu wa kisiasa bila kujali maslahi ya wanachama wa hii mifuko.....Ukienda kudai mafao yako lugha za hawa jamaa ni mbaya as if unaenda kukopa.

Lazima wanachama wawe wanapewa fursa ya kuamua ni wapi haya mashirika yawekeze na ni wapi wasiwekeze coz sometimes hua nashangaa sijui kama huko NSSF kuna investment policy.....maana hua hata watu binafsi (vigogo) hua wanakopeshwa!!! THIS IS SHAME FOR GIANT FUND LIKE THIS.
 
NSSF limekuwa shamba la bibi kwa wanasiasa wa CCM. Nimewahi kueleza humu jinsi CCM inavyomtumia Dau kuchangisha pesa za uchaguzi kutoka kwa makandarasi mbalimbali. Kama Takukuru yetu ingekuwa inafanya kazi, Dau alitakiwa awe gerezani kwani ni kati ya wahujumu uchumi wa kutisha. Dau ni kati ya mabilionea wa ki tz kupitia ufisadi. Kila miradi mikubwa ya shirika yeye na watu waliomzunguka wana % zao. Kama watu aliowaweka humu watazidi kumtetea kishabiki tutaanza kuwaga humu yote tunayoyajua, na jinsi wapambe wake ndani ya shirika walivyotajirikia kufikia kiasi cha kujenga majengo makubwa ya kibiashara eneo la makumbusho nk
 
Baada ya miezi 6 kuanzia mwezi ujao nitachukua kilicho changu NSSF,na ndio utakuwa mwanzo wa kukipotezea hicho chanzo cha mapato cha serikali ya CCM
 
Shirika la Hifadhi ya Jamii limekuwa au niseme limegeuzwa kuwa Shirika la Uwekezaji la Hifadhi ya Jamii. Na kwa jinsi ambavyo linaendeshwa bila ya shaka linasukumwa na kutafuta faida na ni faida hii ambayo linapata imekuwa ikiwekezwa kwenye miradi mbalimbali. Hili si tatizo.

Hata hivyo kwenye mashirika ambayo yanafanya kazi kwa ajili ya faida (for profit companies) yanarudisha sehemu ya faida yake kwa wanahisa (shareholders) wake. Inaweza kurudishwa kama gawio (dividends) kila mwaka kufuatana na kanuni ambayo shirika limejiwekea.

NSSF inakadiriwa kuwa na wanachama karibu 600,000 hadi mwezi Juni mwaka huu likiwa na mali yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja ambayo inakadiriwa kukua kwa haraka hadi mwaka 2013. Kwa mujibu wa sera zao za uwekezaji NSSF hutenga asilimia 75 ya fedha zao kwenda kwenye uwekezaji na asilimia 25 kwenda kwenye mafao na gharama za uendeshaji. Ni wazi kuwa 2/3 ya fedha zinazoweza kuwekezwa zinawekezwa kwenye kile ambacho kinaonekana ni 'high yield' investments.

Je ipo haja ya kuligawa shirika hili na kuhakikisha upande unahusiana na hifadhi ya jamii (mafao kwa wanachama) unaendeshwa tofauti na upande unaohusika na uwekezaji? Je kuna uwezekano wa kuhakikisha kuwa huo upande wa uwekezaji unaendesha kama kampuni nyingine ya faida ambapo wanachama wa NSSF ndio wanakuwa wanahisa wa shirika hilo na ambao watalipewa gawio kila shirika linapotengeneza faida kabla halijaamua kuwekeza fedha kama faida?

Swali hili ni muhimu kwa sababu kwa mtu ambaye anachangia NSSF na bado hajaanza kupata mafao mbalimbali au hajatumia mafao yoyote kwa mwaka hapati faida yoyote ya kifedha kutokana mchango wake ambao unatumika kutengeneza faida kwa shirika. Na kama mtu atakuwa amechangia kwa miaka mitano au zaidi na labda amepata fao la msiba, n.k au aambiwe asubiri hadi kuretire kuanza kupewa shilingi themanini elfu kila mwezi baada ya kuchangia shirika kwa miaka thelathini au ishirini naona ni unyonyaji wa aina yake.

Ni muhimu kwa wanachama kufaidika kifedha (monetary benefit) na uwekezaji wa NSSF kila mwaka. Na namna pekee ya kuwafanya wanachama nao wanufaike ni kuhakikisha kuwa NSSF (bila ya shaka na mashirika mengine ya pensheni) inaweka utaratibu wa kuwagia wanachama wake ama kwa kutengeneza account au kuchangia kwenye akaunti ya mwanachama kiasi cha faida fedha ambazo mwanachama anaweza kuzitoa wakati wowote nje ya zile za pensheni.

Jambo la kwanza ambalo linahitaji kufanyika kwa haraka ni kubadili sheria ili NSSF isiwezeke fedha za wanachama kwenye miradi yenye kutarajia faida bila kuhakikisha kuwa sehemu ya faida inayopatikana inawarudia wanachama kama gawio siyo kama sehemu kiduchu ya mafao.

Swali la Ugomvi: Je CDM ina sera gani kuhusu NSSF na uwekezaji wa NSSF kwa sababu tayari tunajua sera ya CCM ni kutumia NSSF pale ambapo serikali imeshindwa au haina fedha au pale ambapo serikali inataka fedha ya haraka haraka kuikoa mbele ya wananchi.

Hoja yako in mashiko, ila hapo kwenye "red", ngoja nione comment naja hizi ndo mada za maan juu ya mstakabali wetu!! achana na vyama vya siasa
 
Queen Esther am happy kuona analysis yako nzuri isiyo ya kishabiki kama ya MMM. Yaelekea hayo mambo ya Hifadhi za jamii unayafahamu sema tu hutaki kuelewa.

1. Nikianza na hoja yako ya kwanza, ni kweli performance reports zote ni kabla SSRA hajatoa investment guidelines. Hizi guidlines za SSRA zinaanza kutumika mwaka huu, so Financials za mwaka unaoishia June 2013 zitakupa mwelekeo mzuri. Kumbuka pia before that kila mfuko ulikuwa na Investment policy yake na ilikuwa inafuatwa.

2.Actuarial valuation reports zipo na ni haki ya kila mwanachama kuziona na most of mifuko inaonekana inafanya vibaya kama serikali haitailipa madeni inayodaiwa. Nashangaa hili la MMM la kutaka kupewa dividend wakati mifuko karibu yote tanzania haipo kwenye hali nzuri

3. Mifuko yote TZ iko ni Defined Benefit Scheme, GEPF tu ndio provident fund. Kuhusu fao la kujitoa, kumbuka hamna fao kama hili unacholipwa ni michango yako uliyochangia na ya mwajiri wako bila kuconsider time value of money meaning factors kama interest na inflation hazikuwa taken into consideration. Dr Dau alishawahi kuelezea kuwa hata hizi withdraw zisingetakiwa ziwepo cuz hamna mfuko wowote duniani unaozitoa, but nia nzuri ya SSRA imekwamishwa na viongozi wachache wa upinzani waliotaka kujichukulia umaarufu kwa kulivalia njuga hili suala.

Kuhusu contributions, kuna proposal inayofanyiwa kazi asilimia ziongezwe zifikie at least 22-25% tofauti na 20% ya sasa. So hilo suala lako la kupunguzwa kwa sasa lisahau.

Hapo kwenye red ndo na mimi nataka kujua, hivi wanachama tuwakilishwa vipi kwenye maamuzi ya mfuko? na unadhani kuwa tunafikishiwa mawazo yetu vizuri?
Kuhusu hali mbaya ya mifuko, hilo lipo wazi. hofu yetu wengine ni kama serikali itashindwa/kuchelewa kulipa unadhani kwa investment ambazo mifuko yetu inafanya itaweza kujiendesha 10yrs?
kuna ulazima gani wa NSSSF kuwekeza zaidi kwenye public good, which mostly have to be done by Government? mfano, daraja la kigamboni? kwanini wasijikite kwenye real estates by which are valuable on members bnefits and low risks?
Mwisho uundaji wa bodi ya NSSF umekaaje? maana kuna board meeting moja, 80% ya board members were empty on investment analysis ( nani anachagua na kwa vigezo gani)
hiyo kuongezwa kwa contribution toka 20-22-25% kuna ashiria nini kiundeshaji? mimi nahisi ni kama kukuza mapato ya NSSF, on cost of members? hiyo imebalance na nini interms of members' benefits.

wakatabahu
Nganga
 
Queen Esther am happy kuona analysis yako nzuri isiyo ya kishabiki kama ya MMM. Yaelekea hayo mambo ya Hifadhi za jamii unayafahamu sema tu hutaki kuelewa.

1. Nikianza na hoja yako ya kwanza, ni kweli performance reports zote ni kabla SSRA hajatoa investment guidelines. Hizi guidlines za SSRA zinaanza kutumika mwaka huu, so Financials za mwaka unaoishia June 2013 zitakupa mwelekeo mzuri. Kumbuka pia before that kila mfuko ulikuwa na Investment policy yake na ilikuwa inafuatwa.

2.Actuarial valuation reports zipo na ni haki ya kila mwanachama kuziona na most of mifuko inaonekana inafanya vibaya kama serikali haitailipa madeni inayodaiwa. Nashangaa hili la MMM la kutaka kupewa dividend wakati mifuko karibu yote tanzania haipo kwenye hali nzuri

3. Mifuko yote TZ iko ni Defined Benefit Scheme, GEPF tu ndio provident fund. Kuhusu fao la kujitoa, kumbuka hamna fao kama hili unacholipwa ni michango yako uliyochangia na ya mwajiri wako bila kuconsider time value of money meaning factors kama interest na inflation hazikuwa taken into consideration. Dr Dau alishawahi kuelezea kuwa hata hizi withdraw zisingetakiwa ziwepo cuz hamna mfuko wowote duniani unaozitoa, but nia nzuri ya SSRA imekwamishwa na viongozi wachache wa upinzani waliotaka kujichukulia umaarufu kwa kulivalia njuga hili suala.

Kuhusu contributions, kuna proposal inayofanyiwa kazi asilimia ziongezwe zifikie at least 22-25% tofauti na 20% ya sasa. So hilo suala lako la kupunguzwa kwa sasa lisahau.

Rejao
Nashukuru kwa ufafanuzi mzuri, pia nashukuru jambo hili umelijibu bila kuweka mambo ya ki siasa.

Ila naamini na wanachama wengine umetuongeze pressure. Kuchangia 20% tu ni kubwa, sasa ukipeleka 22 - 25% itakuwaje?
Ngoja nikupe mfano
Mshahara Tshs. 1,000,000
PAYG = 300,000 (assumptions 30%)
NSSF = 125,000 (assumption 12.5% employee) as per new rate
Ukiacha makato mengine Kama NHIF, TUICO, SACCOS, House loan etc. mbona mshahara umeisha. Je hili halitachangia rushwa na kuongeza umasikini? Mbona ktk east Africa rate zetu ni kubwa kuliko wenzetu?

Mifuko ya hifadhi ya jamii inatakiwa kuwa front kupunguza umasikini (poverty reduction) sasa kwa PAYG 30% na mifuko 12.5% = 42.5% si tunaongeza umasikini na rushwa?

Kama mifuko ina hayo mareserve makubwa kwanini haimpunguzii mchangiaji mzigo? Bado hainiingii akilini.

Mwisho Kama mifuko haina hela sababu za kuikopesha serikali Kama unavyosema, mbona bado wanaendelea kupeleka hela zetu huko?

Hii mada ni nzito tuipe uzito unaostahili. Hii mifuko ikifilisika nani anajibu SSRA, mgt ya mifuko au serikali?

Queen Esther
 
Hivi ni lini nyinyi watu mtaondoaka na hizo INFERIORITY COMPLEX? Akisolewa Dr. Ramadhani Dau au anayefanana na jina halo mapovu yanawatoka utafikiri aliyekosolewa ni mtume Mohammed SAW, this is too low.

Mwanakijiji ameuliza valid question kama NSSF ina mapesa yote hayo ya ku-invest kwanini pasi isrudishe japo faida kidogo kwa wanachama wake? FYI mifuko ambayo inatoa mafao kidogo sana kwa wanachama wake ni PPF ikifuatiwa na hiyo NSSF inayojitapa kujenga RELI wakati serikali yenyewe haiwezi kuboresha hata zile reli ilizonazo.

Kumbuka anayetakiwa afaidi kwanza uwekezaji wa NSSF ni mwanachama mwenyewe sio jamii soma sheria za ILO.

Gazeti la leo limeandika kwamba nyumba za bei nafuu za NSSF zinauzwa TSH 200 Milioni. Mimi ninajua wewe unafanya kazi NSSF hebu niambie tangu mwaka huu uanze ni mwanachama gani mumewahi kumlipa mafao ya 200 milioni? Kama yupo I will chop my neck.

Ni na amekwambia wanachama wa NSSF tunaridhika na mambo yanayofanywa na NSSF? If you are a real a scholar do your research. Dont tell me hizo kangaroo bodi zilizoundwa na yule aliyemteua Dr. Dau, I want you to do your homework among NSSF members.

Simple challenge kwa Dr. Dau kama NSSF ina mapesa yote hayo tunataka kwanza NSSF ianze kutoa mafao mazuri ya pensheni kama PSPF. Haihitaji kuwa rocket scientist, formula ya PSPF ipo it is just a matter of copy and paste.
suala hapa si inferiority complex, hapa ni ukweli tu tunawapa. mkiona hayo majina sijui huwa mnachachawa nini? hivi ni nssf tu ndo mfuko wa hifadhi wa jamii? tunakumbuka sana wakati DR. Idris Rashid alipokuwa mkurugenzi tanesco mlivyokuwa mnamsakama, lakini alipokuja willium mhando ikawa ndo mwisho wa kusakamwa MD wa tanesco as if yeye ndo alikuwa muarobaini wa matatizo ya tanesco. nani asiyejua hata uteuzi wa General Abdrahaman Shimbo mlivyochonga, lakini JK alivyowateua akina Ndomba na mfano wake mambo kimya. kwa kifupi mifano ipo mingi kwa hiyo usitafute excuse hapa. hiyo ndo kasumba yenu. mnamatatizo sana kwenye vifuu vyenu vya nazi juu ya shingo zenu kwani siamini kama mna vichwa. Naamini na huo ndo ukweli kuwa leo hii ikitokea Dr.Dau kahamia shirika lingine kama hilo mtahamia hukohuko na mjadala yenu ya kipumbavu. Hebu jiulize we fa.la, pamoja na kuvuruga kote bandarini, tanapa, tra, na mashirika mengi ya umma mbona hamchongi? napata tabu sana na uelewa wa ubongo wenu. mnaongea as if chuo kama udom, hombolo nyinyi hamsomi na wala hamajiriwi, na madaraja kama la kigamboni hampiti na hamtapita. na chelea kuwaita ma.ch.izi.
suluhisho ni badilikeni tujenge nchi yetu sote.
 
Queen Esther am happy kuona analysis yako nzuri isiyo ya kishabiki kama ya MMM. Yaelekea hayo mambo ya Hifadhi za jamii unayafahamu sema tu hutaki kuelewa.

1. Nikianza na hoja yako ya kwanza, ni kweli performance reports zote ni kabla SSRA hajatoa investment guidelines. Hizi guidlines za SSRA zinaanza kutumika mwaka huu, so Financials za mwaka unaoishia June 2013 zitakupa mwelekeo mzuri. Kumbuka pia before that kila mfuko ulikuwa na Investment policy yake na ilikuwa inafuatwa.

2.Actuarial valuation reports zipo na ni haki ya kila mwanachama kuziona na most of mifuko inaonekana inafanya vibaya kama serikali haitailipa madeni inayodaiwa. Nashangaa hili la MMM la kutaka kupewa dividend wakati mifuko karibu yote tanzania haipo kwenye hali nzuri

3. Mifuko yote TZ iko ni Defined Benefit Scheme, GEPF tu ndio provident fund. Kuhusu fao la kujitoa, kumbuka hamna fao kama hili unacholipwa ni michango yako uliyochangia na ya mwajiri wako bila kuconsider time value of money meaning factors kama interest na inflation hazikuwa taken into consideration. Dr Dau alishawahi kuelezea kuwa hata hizi withdraw zisingetakiwa ziwepo cuz hamna mfuko wowote duniani unaozitoa, but nia nzuri ya SSRA imekwamishwa na viongozi wachache wa upinzani waliotaka kujichukulia umaarufu kwa kulivalia njuga hili suala.

Kuhusu contributions, kuna proposal inayofanyiwa kazi asilimia ziongezwe zifikie at least 22-25% tofauti na 20% ya sasa. So hilo suala lako la kupunguzwa kwa sasa lisahau.

Rejao, kama mifuko yote ya jamii including NSSF iko kwenye hali mbaya kifedha, hizo pesa ambazo Dr. Dau anataka kuzitumia kujenga RELI, Bandari kavu Kisarawe, anazipata wapi? Hapa ndiyo tunasema Dr. Dau anatumiwa kisiasa. Serikali ndiyo mdaiwa sugu wa NSSF na report ya CAG inaonesha hadi leo 2012 ameshindwa kuanza kurudisha madeni kwa NSSF. Sasa kwanini huyu Dr. Dau aendelee kum-finance huyu mdaiwa (serikali) sugu.

Ndiyo nchi zilizoendelea hazitoa fao la kujitoa, lakini ambacho Dr. Dau na SSSR hawataki kusema ni kwamba nchi hizo zinatoa fao la UN EMPLOYMENT BENEFIT. Kama NSSF wanataka kutoa fao la kujitoa fine, lakini wakubali kutoa fao UN EMPLOYMENT benefit.
 
suala hapa si inferiority complex, hapa ni ukweli tu tunawapa. mkiona hayo majina sijui huwa mnachachawa nini? hivi ni nssf tu ndo mfuko wa hifadhi wa jamii? tunakumbuka sana wakati DR. Idris Rashid alipokuwa mkurugenzi tanesco mlivyokuwa mnamsakama, lakini alipokuja willium mhando ikawa ndo mwisho wa kusakamwa MD wa tanesco as if yeye ndo alikuwa muarobaini wa matatizo ya tanesco. nani asiyejua hata uteuzi wa General Abdrahaman Shimbo mlivyochonga, lakini JK alivyowateua akina Ndomba na mfano wake mambo kimya. kwa kifupi mifano ipo mimi kwa hiyo usitafute excuse hapa. hiyo ndo kasumba yenu. mnamatatizo sana kwenye vifuu vyenu vya nazi juu ya shingo zenu kwani siamini kama mna vyichwa.

Ndugu hivi umetoka leo Mars, au hizo miwani ya mbao ya UDINI uliyovaa inakufanya ushindwe kuona.

Unamsema William Mhando aliyefukuzwa TANESCO au unamsema Mhando mwingine? Mhando huyo tumemshikia bango humu baada ya kujilikana kwamba amempatia mke wake tenda ya ku-supply stationaries TANESCO hadi akafukuzwa. Hivi nyinyi wenye majina hayo mna matatizo gani? Mkikosolewa mnasema mnakoselewa kwasababu ya majina yenu, POOR

Hivi wewe ni mgeni hapa JF? Mpaka sasa hivi kuna thread inahoji uteuzi wa Lut. General Ndimbo kuwa CoS wakati walikuwepo SENIOR akina Ryoba, Makalala na Kisampa. Kwahiyo Ndomba naye tunamkosoa kwasababu ya dini yake?. Sisi tutaendelea kukosoa whatever anayefanya madudu bila kujali DINI yake, kama hamtaki kukosolewa nendeni MKASWALISHE huko MISIKITINI bana.

Tumechoka na hizo inferiority complex zenu.
 
Mwanakijiji anasema kweli kabisa mfano mimi nafanya kazi hapa US na mwaka jana kwenye retirement account yangu kama ilivyo ya NSSF nimepata faida ya 6% kwenye account yangu maana ile pesa imewekezwa na wamefanya mahesabu na kila mmoja kapata 6% ya pesa ambayo ilikuwa imewekezwa. Hii ni muhimu kwani faida ni ya nani wakati capital ni ya wanachama?? Hayo majengo yote si ya serikali ni ya wanachama na kwenye NSSF ni lazima wasema return kwenye Investment ni kiasi gani.
 
Hivi wewe una akili timamu? mimi nikiwa kama Member wa NSSF nasema wapuuzi kama wewe mnastahili kunyongwa kabisa, Mwanakijiji anahoji maswali ya msingi akiwa kama Mwanahabari na anashirikisha sauti za wasiosikika halafu wewe unambeza?

Labda nikuulize swali dogo tu, kati ya Yusuf Manji na sisi Wanachama wa NSSF ni nani anastahili kupewa mkopo wa pesa? na unaposema kwenye huo uwekezaji sisi Wanachama tumeridhia ni lini kulikuwa na kikao hicho cha sisi kuridhia pesa zetu kutapanywa kwenye uwekezaji wa kiwehu? au mnadhani sisi hatukjui kama NSSF inaelekea kufirirsika?
Mkuu Matola, nimekuwa nikiuliza swali hilo mara kadhaa na majibu ninayopewa ni kuwa "Trade Unions zinawawakilisaha kwenye decision making za NSSF"
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Matola, nimekuwa nikiuliza swali hilo mara kadhaa na majibu ninayopewa ni kuwa "Trade Unions zinawawakilisaha kwenye decision making za NSSF"
Upuuzi mtupu, huu ni udhaifu wa kutokuwa na vyam imara vya wafanyakazi kama ilivyo South Afrika ambapo ili uwe Rais ni lazima uhakikishe vyama hivi vinakuunga mkono, otherwise hauwezi kushinda, lakini kutokana na udhaifu wa hapa kwetu ndio maana Kikwete alipata jeuri ya kuwaambia hazihitaji kura zao.
 
Hapa tunaibiana aisee.
Hela yetu inawekezwa, dividends hatupewi. Maamuzi wanafanya wao. Ifike mahali kuanzishwe mifuko binafsi, watu waruhusiwe kuchagua mfuko wanaoupenda!!

Dau akiamka tu anakuambia kua watabomoa Manzese na Mburahati yote waijenge upya, wenye hela zetu hatuulizwi.

Huu ni utapeli uliohalalishwa. Na waliohalalisha (serikali) wanafaidika na utapeli huu ndio maana hutoskia wakibadili.
 
Mwanakijiji anasema kweli kabisa mfano mimi nafanya kazi hapa US na mwaka jana kwenye retirement account yangu kama ilivyo ya NSSF nimepata faida ya 6% kwenye account yangu maana ile pesa imewekezwa na wamefanya mahesabu na kila mmoja kapata 6% ya pesa ambayo ilikuwa imewekezwa. Hii ni muhimu kwani faida ni ya nani wakati capital ni ya wanachama?? Hayo majengo yote si ya serikali ni ya wanachama na kwenye NSSF ni lazima wasema return kwenye Investment ni kiasi gani.

Kwa Defined Contribution Schemes kulipa gawio ni sawa kabisa kwani ata pale mambo yalivyoenda kombo kwa mfano wakati wa Global Financial Crisis wanachama walipata share yao ya hasara. Kwa hapa kwetu ambapo mifuko yetu ni Defined Benefits Schemes kinachoweza fanyika kama mambo ni mazuri ni kuongeza replacement rates (via retirement benefits) au kupunguza kiwango cha kuchangia (contribution rates).

Hata hivyo cha kushangaza kama fununu za mchangiaji mmoja zitakuwa sahihi (contribution rates zinatarajiwa kupanda) inamaana hii inakwenda tofauti na DBs zenye mafanikio.

Hivyo kwa nini SSRA hawaweki financial statements na acturial reports za mifuko ya hifadhi ya jamii? kwanini wasiongeze uwazi katika mambo ya msingi? Publishing actuarial reports and financial statements would assist to clear some doubts if they are not well founded.

Kuna swala moja pia linahitaji kuliangalia kwa jicho la tatu........ kama withdrawal benefits za mifuko ya hifadhi ni asilimia kubwa (eg. kama mchangiaji wa aliyotoa takwimu kwamba zilikuwa 78% of all benefits, NSSF) inamaana kuwa mafao mengine likiwemo ya old age ni madogo sana (so meager). In short old age benefits sounds to be so meaningless because the replacement rate is so low.

Ni vizuri SSRA na Benki Kuu kuwa makini sana na mifuko hii vinginevyo tutapata Msukosuko mukubwa sana ktk mfumo wa kifedha ikitokea imepata matatizo na mafao ya uzeeni yatakuwa janga lingine kwa serikali kama la wazee wa EAC linavyotusumbua.

TUILINDE MIFUKO YETU KWA KULINDA UCHUMI WETU NA WAZEE WETU! Mungu ibariki Tanzania!
 
Rejao
Nashukuru kwa ufafanuzi mzuri, pia nashukuru jambo hili umelijibu bila kuweka mambo ya ki siasa.

Ila naamini na wanachama wengine umetuongeze pressure. Kuchangia 20% tu ni kubwa, sasa ukipeleka 22 - 25% itakuwaje?
Ngoja nikupe mfano
Mshahara Tshs. 1,000,000
VAT = 300,000 (assumptions 30%)
NSSF = 125,000 (assumption 12.5% employee) as per new rate
Ukiacha makato mengine Kama NHIF, TUICO, SACCOS, House loan etc. mbona mshahara umeisha. Je hili halitachangia rushwa na kuongeza umasikini? Mbona ktk east Africa rate zetu ni kubwa kuliko wenzetu?

Mifuko ya hifadhi ya jamii inatakiwa kuwa front kupunguza umasikini (poverty reduction) sasa kwa PAYG 30% na mifuko 12.5% = 42.5% si tunaongeza umasikini na rushwa?

Kama mifuko ina hayo mareserve makubwa kwanini haimpunguzii mchangiaji mzigo? Bado hainiingii akilini.

Mwisho Kama mifuko haina hela sababu za kuikopesha serikali Kama unavyosema, mbona bado wanaendelea kupeleka hela zetu huko?

Hii mada ni nzito tuipe uzito unaostahili. Hii mifuko ikifilisika nani anajibu SSRA, mgt ya mifuko au serikali?

Queen Esther

Pay As You Earn (not VAT) = {[30%*(1,000,000-125,000)-720,000]+107,600} au ingiza jibu la [1,000,000 - 125,000] kwenye http://www.tra.go.tz/documents/Paye.htm
 
Back
Top Bottom