NSSF Ianze kutoa gawio la faida kwa wanachama?

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,933
2,000
Shirika la Hifadhi ya Jamii limekuwa au niseme limegeuzwa kuwa Shirika la Uwekezaji la Hifadhi ya Jamii. Na kwa jinsi ambavyo linaendeshwa bila ya shaka linasukumwa na kutafuta faida na ni faida hii ambayo linapata imekuwa ikiwekezwa kwenye miradi mbalimbali. Hili si tatizo.

Hata hivyo kwenye mashirika ambayo yanafanya kazi kwa ajili ya faida (for profit companies) yanarudisha sehemu ya faida yake kwa wanahisa (shareholders) wake. Inaweza kurudishwa kama gawio (dividends) kila mwaka kufuatana na kanuni ambayo shirika limejiwekea.

NSSF inakadiriwa kuwa na wanachama karibu 600,000 hadi mwezi Juni mwaka huu likiwa na mali yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja ambayo inakadiriwa kukua kwa haraka hadi mwaka 2013. Kwa mujibu wa sera zao za uwekezaji NSSF hutenga asilimia 75 ya fedha zao kwenda kwenye uwekezaji na asilimia 25 kwenda kwenye mafao na gharama za uendeshaji. Ni wazi kuwa 2/3 ya fedha zinazoweza kuwekezwa zinawekezwa kwenye kile ambacho kinaonekana ni 'high yield' investments.

Je ipo haja ya kuligawa shirika hili na kuhakikisha upande unahusiana na hifadhi ya jamii (mafao kwa wanachama) unaendeshwa tofauti na upande unaohusika na uwekezaji? Je kuna uwezekano wa kuhakikisha kuwa huo upande wa uwekezaji unaendesha kama kampuni nyingine ya faida ambapo wanachama wa NSSF ndio wanakuwa wanahisa wa shirika hilo na ambao watalipewa gawio kila shirika linapotengeneza faida kabla halijaamua kuwekeza fedha kama faida?

Swali hili ni muhimu kwa sababu kwa mtu ambaye anachangia NSSF na bado hajaanza kupata mafao mbalimbali au hajatumia mafao yoyote kwa mwaka hapati faida yoyote ya kifedha kutokana mchango wake ambao unatumika kutengeneza faida kwa shirika. Na kama mtu atakuwa amechangia kwa miaka mitano au zaidi na labda amepata fao la msiba, n.k au aambiwe asubiri hadi kuretire kuanza kupewa shilingi themanini elfu kila mwezi baada ya kuchangia shirika kwa miaka thelathini au ishirini naona ni unyonyaji wa aina yake.

Ni muhimu kwa wanachama kufaidika kifedha (monetary benefit) na uwekezaji wa NSSF kila mwaka. Na namna pekee ya kuwafanya wanachama nao wanufaike ni kuhakikisha kuwa NSSF (bila ya shaka na mashirika mengine ya pensheni) inaweka utaratibu wa kuwagia wanachama wake ama kwa kutengeneza account au kuchangia kwenye akaunti ya mwanachama kiasi cha faida fedha ambazo mwanachama anaweza kuzitoa wakati wowote nje ya zile za pensheni.

Jambo la kwanza ambalo linahitaji kufanyika kwa haraka ni kubadili sheria ili NSSF isiwezeke fedha za wanachama kwenye miradi yenye kutarajia faida bila kuhakikisha kuwa sehemu ya faida inayopatikana inawarudia wanachama kama gawio siyo kama sehemu kiduchu ya mafao.

Swali la Ugomvi: Je CDM ina sera gani kuhusu NSSF na uwekezaji wa NSSF kwa sababu tayari tunajua sera ya CCM ni kutumia NSSF pale ambapo serikali imeshindwa au haina fedha au pale ambapo serikali inataka fedha ya haraka haraka kuikoa mbele ya wananchi.
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,457
2,000
Katiba Mpya inahusika sana hapa! Ngoja Tuone CDM sera zake ni zipi kwenye Hii issue!! Kweli maana sie ni kama tumeweka hisa(share) zetu so lazima tupate Dividend kila mwisho wa mwaka!
 
MrNSSF

MrNSSF

Senior Member
Mar 17, 2011
136
0
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.

Threads ulizozianzisha kumshambulia Dr Dau ni hizi:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...erikali-na-hatima-ya-taasisi-ya-moyo-thi.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/16889-thi-yaibwaga-nssf-mahakamani.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19691-samahani-nssf-samahani-dr-dau-nyoni.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rof-kapuya-wawajibishwe;-nssf-ishitakiwe.html

https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/19593-cheche-mitaani-tume-yawanyoshea-kidole-nssf.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...inga-nssf-imekula-hasara-ya-bilioni-30-a.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kezaji-hayalipiki-ripoti-ya-cag-yafichua.html

https://www.jamiiforums.com/major-p...igamboni-bridge-ipp-road-construction-10.htmlhttps://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ra-uongozi-wa-nssf-makao-makuu-uwajibike.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/120673-ooh-poor-nssf-what-is-this-4.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ilia-mchakato-wa-ugawaji-viwanja-mafia-5.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...;-vitu-vyaibwa-vingine-vyarudishwa-kiana.html

Hebu nenda TRA,PPF na kwingine.
 
mangikule

mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
3,857
2,000
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.

Hebu nenda PPF na kwingine na mpumzishe Dau.
This is too personal!! Give us a chance to air out our views!!! We are members and we demand our rights and even our rights of expression!! Mwanakijiji has opened the floor for us!!
Tunahitaji migao yetu kila mwaka!! Ninaumia sana ninapokuja hata kwa dai la haki mnajifungia na kuwa wakali kana kwamba hizo ni fedha zenu na serikali! Na hii tabia umeionyesha hapa ukitaka kumfunga mtoa uzi mdomo! spare us please!!
 
Songoro

Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,127
0
Usiwe na Roho ya kwa nini? Pension funds ziko ngapi mpaka unazungumzia NSSF Pekee? Kama unakiri bila kudhamiria kuwa NSSF inafanya vizuri lakini unakataa kutoa pongezi kwa kina Dau kwa sababu unazojua mwenyewe.

Pia tambua tofauti ya kampuni,Pension fund na shirika itakusaidia sana kujenga hoja, msingi wa pension fund sio kusaidia wafanyakazi pekee ni jamii nzima that is why inajukumu kwa upande mmoja kusaidia welfare of society na sio wafanyakazi pekee ndio sababu inajishughulisha kwenye ujenzikama UDOM, MADARAJA, NYUMBA ZA ASKARI N.K fAIDA IPATIKANAYO INAZUNGUSHWA SIO KUGAWANYWA kama unavyofikiri, Msingi mkuu ni kulea wastaafu kama una la kushauri ni kuishauri NSSF ibadili kanuni ya kulipa mafao iwe bora zaidi iwanufaishe wastaafu badal ya kutumia kanuni ya sasa inayotoa mafao kiduchu acha ukalulu kwenye fani za watu!
 
Elli Mshana

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
37,514
2,000
Hahahhaaaa ngoja waje wakuwekee mahesabi kibao na wataishia kusema wanapata hasara, hakuna faida...........
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,540
2,000
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.Mkuu kwanini tusijifunze kujibu hoja? hoja ni gawio la faida kwa wanachama wewe unaleta mtizamo wa chuki!
 
omujubi

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,153
2,000
Katiba Mpya inahusika sana hapa! Ngoja Tuone CDM sera zake ni zipi kwenye Hii issue!! Kweli maana sie ni kama tumeweka hisa(share) zetu so lazima tupate Dividend kila mwisho wa mwaka!
na hawa jamaa wa ccm ndio maana wanatumia kila njia iwezekanayo kubakia madarakani maana kuna neema nyingi zinazoweza kuwaijia wananchi kwa kubadilisha tu sheria kidogo.
Tangia lini haya yote yanafanyika mchana kweupe; nssf inawekeza pesa za wanachama bila kuwauliza na faida wanachukua wengine wasiochangia!
 
W

wikolo

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
801
195
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.

Hebu nenda PPF na kwingine na mpumzishe Dau.
Mkuu, mbona kama umemshambulia Mwanakijiji sana kwa hoja yake aliyoileta? Nimesoma uzi wake na sijaona sehemu yoyote ambayo amemtaja Dr. Dau, kwa nini basi umshambulie kiasi hicho?

Kama umekerwa na jina la NSSF kutumika ungeweza tu kupanua mjadala kwa kuongeza na majina ya mashirika mengine. Mimi binafsi nakubaliana na hoja ya Mwanakijiji manake kinachofanywa na NSSF na mashirika mengine ya pensheni ni wizi tu uliopitiliza.

Si kweli kwamba wanachama wamekubaliana na hayo yanayofanywa na NSSF, shirika lisitumie udhaifu wa wanachama kutohoji kama tiketi ya kufanya kile litakacho hata kama mwisho wa siku hakuna faida ambayo mwanachama anaipata.

Hizo mnazowekeza ni fedha za wanachama na ni lazima wafaidi matunda yanayopatikana kutokana na kazi inayofanywa na fedha zao. Huo ndo ukweli mchungu.
 
E

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
15,782
2,000

...Sera ya CCM ni kutumia NSSF pale ambapo serikali imeshindwa au haina fedha au pale ambapo serikali inataka fedha ya haraka haraka kuikoa mbele ya wananchi.
 
Elli Mshana

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
37,514
2,000
Kama wameshindwa kunipatia kadi yangu ya Uanchama tangu Juni had Desemba hii, huoni kwamba hio ya kugawana mapato itakua ndoto?
 
MrNSSF

MrNSSF

Senior Member
Mar 17, 2011
136
0
This is too personal!! Give us a chance to air out our views!!! We are members and we demand our rights and even our rights of expression!! Mwanakijiji has opened the floor for us!!
Tunahitaji migao yetu kila mwaka!! Ninaumia sana ninapokuja hata kwa dai la haki mnajifungia na kuwa wakali kana kwamba hizo ni fedha zenu na serikali! Na hii tabia umeionyesha hapa ukitaka kumfunga mtoa uzi mdomo! spare us please!!
Mkuu, mbona kama umemshambulia Mwanakijiji sana kwa hoja yake aliyoileta? Nimesoma uzi wake na sijaona sehemu yoyote ambayo amemtaja Dr. Dau, kwa nini basi umshambulie kiasi hicho? Kama umekerwa na jina la NSSF kutumika ungeweza tu kupanua mjadala kwa kuongeza na majina ya mashirika mengine. Mimi binafsi nakubaliana na hoja ya Mwanakijiji manake kinachofanywa na NSSF na mashirika mengine ya pensheni ni wizi tu uliopitiliza. Si kweli kwamba wanachama wamekubaliana na hayo yanayofanywa na NSSF, shirika lisitumie udhaifu wa wanachama kutohoji kama tiketi ya kufanya kile litakacho hata kama mwisho wa siku hakuna faida ambayo mwanachama anaipata. Hizo mnazowekeza ni fedha za wanachama na ni lazima wafaidi matunda yanayopatikana kutokana na kazi inayofanywa na fedha zao. Huo ndo ukweli mchungu.

Mwanakijiji allianzisha threads hizi hapa na zote hazina cha zaidi ya mashambulizi binafsi dhidi ya Dr Dau.

Lakini waswahili wanasema Wimbi la Nyuma............
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...erikali-na-hatima-ya-taasisi-ya-moyo-thi.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/16889-thi-yaibwaga-nssf-mahakamani.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19691-samahani-nssf-samahani-dr-dau-nyoni.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rof-kapuya-wawajibishwe;-nssf-ishitakiwe.html

https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/19593-cheche-mitaani-tume-yawanyoshea-kidole-nssf.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...inga-nssf-imekula-hasara-ya-bilioni-30-a.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kezaji-hayalipiki-ripoti-ya-cag-yafichua.html

https://www.jamiiforums.com/major-p...igamboni-bridge-ipp-road-construction-10.htmlhttps://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ra-uongozi-wa-nssf-makao-makuu-uwajibike.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/120673-ooh-poor-nssf-what-is-this-4.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ilia-mchakato-wa-ugawaji-viwanja-mafia-5.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/58874-nyumba-ya-dr-dau-yavamiwa%3B-vitu-vyaibwa-vingine-vyarudishwa-kiana.html
 
mika kati

mika kati

Senior Member
Dec 2, 2012
135
0
Dau hana lolote ni urafiki tu na JK,ndio unaomlinda.Alipokua mmoja wa wakurugenzi THA ambayo kwa sasa ni TPA hakuleta tija yoyote.Kuhusu mifuko ya jamii kwa nini isingetoa mikopo ya nyumba za bei nafuu kwa wanachama wake ambao ndio wadau wa uhakika kuliko kung'ang'ania kuwakopesha mabilioni akina Yusuph Manji
 
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
13,999
2,000
mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na dau toka suala la dr masau na lile la magodown aliyokosa reginald mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa nssf wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka tra? Tatizo lako ni dr ramadhani dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa dr ina negate chochote kile utakachokisema...

jibu hoja hiyo ya gawio la faida kwetu sisi wanachama,,umeshupalia dau dau,,dau nani??

Au dau ndiye anaekuweka mjini??
 
mangikule

mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
3,857
2,000
jibu hoja hiyo ya gawio la faida kwetu sisi wanachama,,umeshupalia dau dau,,dau nani??

Au dau ndiye anaekuweka mjini??
Kweli mkuu huyu mbona anayeyusha hoja? Aseme pochi yetu tutapataje faida? au bado anataka kutetea kukopesha wasio wanachama na majambazi ya chama tawala; Hivi alilipa I mean waziri wa zamani Sumaye aliyedai wamemkopesha?
 
MrNSSF

MrNSSF

Senior Member
Mar 17, 2011
136
0
jibu hoja hiyo ya gawio la faida kwetu sisi wanachama,,umeshupalia dau dau,,dau nani??

Au dau ndiye anaekuweka mjini??
Hakuna hoja ya kujibu

Kila kitu kuhusus NSSF kilishasemwa humu

tumia search utapata tuu majibu yako na kama hujaridhika andika barua rasmi na utajibiwa
 
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
13,999
2,000
hakuna hoja ya kujibu

kila kitu kuhusus nssf kilishasemwa humu

tumia search utapata tuu majibu yako na kama hujaridhika andika barua rasmi na utajibiwa

sasa dau umemtaja taja hapo kama mungu mtu wa kazi gani??

Yan watu tuache kuzungumza na kuhoji mambo yetu ya msingi eti tumhofie dau?

Who the hell is he?

Haya mfikishie salam zake boss wako huyo
 
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
13,999
2,000
kweli mkuu huyu mbona anayeyusha hoja? Aseme pochi yetu tutapataje faida? Au bado anataka kutetea kukopesha wasio wanachama na majambazi ya chama tawala; hivi alilipa i mean waziri wa zamani sumaye aliyedai wamemkopesha?

hawa si watu wa longo longo??

Wanataka kulandana tuh na watu wa desi,,na ole wao...!!

Ama zetu ama zao
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,933
2,000
Inawezekana kwa kuanzisha mada za Bodi ya mikopo, ATC, CCM nina ugomvi na kila kiongozi mkuu wa taasisi hiyo. Kwenye hili sijamtaja Dau si kwa sababu namuogopa au namheshimu kivile ni kwa sababu nazungumzia taasisi ya NSSF. Dau is irrelevant kwenye hili. Hata akija kiongozi mwengine akiendelea na sera hizi hizi za NSSF ya sasa bado swali langu litasimama.
 
Rejao

Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,238
2,000
Mzee Mwanakijiji, nashangaa hata wewe unashindwa kuelewa tofauti ya mifuko ya hifadhi za jamii na kampuni za kibiashara.
Nafikiri ungeishauri NSSF iwe na supplementary schemes ambazo itakuwa ni uamuzi wa mtu kujiunga kwa ajili ya unachokilenga-gawio/dividend kutokana na faida watakayoipata.
 
Top Bottom