NSSF Ianze kutoa gawio la faida kwa wanachama?

sasa dau umemtaja taja hapo kama mungu mtu wa kazi gani??

Yan watu tuache kuzungumza na kuhoji mambo yetu ya msingi eti tumhofie dau?

Who the hell is he?

Haya mfikishie salam zake boss wako huyo

Wimbi la nyuma.....
 
MM naona sasa unaanza kutupeleka sipo, najua story yako inanoga kwa washabiki wenzako wa chama chenu, mnapenda kubeza kila kitu hata ambavyo amvielewi vizuri,

Lazima kujua majukumu makubwa ya mifuko hii ya kijamii, moja kubwa ni ku-invest pesa za wanachama ili zizae na wakati wa uzeeni mtu apate pension yake vizuri. Kumbuka mwanachama anapostaafu bila kujali hali ya mfuko kisheria ni lazima aendelee kupata pension yake (the risk of investment remain with the fund and not the pensioner). Kwa mazingira hayo NSSF si kampuni igawe dividend, wanachoweza kufanya ni kuongeza huduma kwa wanachama kama mikopo, matibabu na mambo kama hayo.
NSSF wana haki ya kuwekeza popote wanakoona italeta faida na ndiyo kazi ya mifuko (institutional investors).
Wewe sijawahi kuona ukisifia mazuri yoyote wanayofanya zaidi ya kuponda tu.
 
Mzee Mwanakijiji, nashangaa hata wewe unashindwa kuelewa tofauti ya mifuko ya hifadhi za jamii na kampuni za kibiashara.
Nafikiri ungeishauri NSSF iwe na supplementary schemes ambazo itakuwa ni uamuzi wa mtu kujiunga kwa ajili ya unachokilenga-gawio/dividend kutokana na faida watakayoipata.

Kilichotolewa hapo juu ni swali; sijasema iwe hivyo nimeuliza swali kwa kujenga hoja. Inaweza kuulizwa pia kwa jinsi NSSF inaendesha uwekezaji wake je inajitambua kuwa ni shirika la hifadhi ya jamii na siyo kampuni ya kibiashara? Maana kama siyo ya kibiashara kwanini inaonekana iko obsessed sana na uwekeaji na kupata faida? Faida ambayo hairudi kwa wanachama bali inaingizwa kwenye uwekezaji mwingine?
 
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.

Threads ulizozianzisha kumshambulia Dr Dau ni hizi:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...erikali-na-hatima-ya-taasisi-ya-moyo-thi.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/16889-thi-yaibwaga-nssf-mahakamani.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19691-samahani-nssf-samahani-dr-dau-nyoni.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rof-kapuya-wawajibishwe;-nssf-ishitakiwe.html

https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/19593-cheche-mitaani-tume-yawanyoshea-kidole-nssf.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...inga-nssf-imekula-hasara-ya-bilioni-30-a.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kezaji-hayalipiki-ripoti-ya-cag-yafichua.html

https://www.jamiiforums.com/major-p...igamboni-bridge-ipp-road-construction-10.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ra-uongozi-wa-nssf-makao-makuu-uwajibike.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/120673-ooh-poor-nssf-what-is-this-4.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ilia-mchakato-wa-ugawaji-viwanja-mafia-5.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...;-vitu-vyaibwa-vingine-vyarudishwa-kiana.html

Hebu nenda TRA,PPF na kwingine.

Mbona hujibu hoja kwa hoja? afu unaonekana kuweweseka, kutoa hoja namna hiyo nikutaka kumziba mdomo Mzee mwanakijiji, anachosema yeye ni kuhusu NSSF kugawa gawio la faida kwa wadau wake period! kwani nani asiyejua kwamba NSSF inaingiza faida kubwa kwa kuwekeza fedha za wanachama? au kuliongea hili ni chuki binafsi? kwani mbona tunawaona mtaani mnavyoishi maisha ya anasa kwa fedha zetu? au ulitaka tujadili nini sasa,nani asiyejua udini uliopo hapo NSSF, unataka tujadili hayo? hayo mambo mengine ya ufisadi wa TRA au taasisi zingine kama ulivyozitaja PPF N.K hata wewe ni mtanzania hukatazwi kujadili, Jibuni hoja tafadhali acha kubwabwaja!
 
MrNSSF, kabla sijasema uwekekaji huo ni mzuri au ni mbaya,naomba msaada wa elimu,

1. hivi hii miradi imepitiwa na Bodi ya SSRA kama sheria inavyotaka? Tafadhali rejea pia investment guidelines za social security funds. Jibu lako litasaidia wadau waelewe namna ya uwekezaji ktk mifuko na ndipo wapime kama ni sahihi au la, tena bila kuhusisha chama.

2. Pia kwenye mifuko hakuna dividents ila mfuko unapokuwa na reserve kubwa inatakiwa kuboresha mafao au kupungura contribution rate (asilimia ya uchangiaji) au yote mawili.

3. Mods wekeni (attach) ile doc ya SSRA ya investment guidelines for SSF's kuutendea haki mjadala.

Queen Esther
 
Kilichotolewa hapo juu ni swali; sijasema iwe hivyo nimeuliza swali kwa kujenga hoja. Inaweza kuulizwa pia kwa jinsi NSSF inaendesha uwekezaji wake je inajitambua kuwa ni shirika la hifadhi ya jamii na siyo kampuni ya kibiashara? Maana kama siyo ya kibiashara kwanini inaonekana iko obsessed sana na uwekeaji na kupata faida? Faida ambayo hairudi kwa wanachama bali inaingizwa kwenye uwekezaji mwingine?
Kazi za mifuko ya hifadhi ya jamii ni kuchuchuka michango, kuiwekeza na kulipa mafao pale wanachama wake wanapostaafu. Ukiangalia budget za hii mifuko, ni kweli unakuta kuna proportional kidogo ya kiasi kilichotengwa kwa mafao, na kiasi kikubwa huwa kunawekezwa. Kumbuka nia ya mifuko ni kutoa long term benefits, ndio maana wanatakiwa wainvest kwa long term tena kwenye miradi yenye faida kubwa.
Asilimia zinazotengwa kulipa mafao ni kidogo, hii inatokana na projection zao kwa financial year hiyo wanastaafu wanachama wangapi. Siyo kwamba miaka yote itakuwa hivi, kuna miaka ambayo watakuwa wanalipa mafao zaidi kuliko watakachokuwa wanakiwekeza.
So cha muhimu ni kuhakikisha wanawekeza in a prudent manner ili tutakapokuja kustaafu tusikose mafao yetu.
 
Kuna ubaya gani kwa NSSF kuanzisha kampuni yake ya uwekezaji nje ya NSSF ya pensheni na wanachama wakapewa hisa humo?
 
Mzee Mwanakijiji, nashangaa hata wewe unashindwa kuelewa tofauti ya mifuko ya hifadhi za jamii na kampuni za kibiashara.
Nafikiri ungeishauri NSSF iwe na supplementary schemes ambazo itakuwa ni uamuzi wa mtu kujiunga kwa ajili ya unachokilenga-gawio/dividend kutokana na faida watakayoipata.

:nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono:
 
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.

Hebu nenda TRA,PPF na kwingine.

Hivi ni lini nyinyi watu mtaondoaka na hizo INFERIORITY COMPLEX? Akisolewa Dr. Ramadhani Dau au anayefanana na jina halo mapovu yanawatoka utafikiri aliyekosolewa ni mtume Mohammed SAW, this is too low.

Mwanakijiji ameuliza valid question kama NSSF ina mapesa yote hayo ya ku-invest kwanini pasi isrudishe japo faida kidogo kwa wanachama wake? FYI mifuko ambayo inatoa mafao kidogo sana kwa wanachama wake ni PPF ikifuatiwa na hiyo NSSF inayojitapa kujenga RELI wakati serikali yenyewe haiwezi kuboresha hata zile reli ilizonazo.

Kumbuka anayetakiwa afaidi kwanza uwekezaji wa NSSF ni mwanachama mwenyewe sio jamii soma sheria za ILO.

Gazeti la leo limeandika kwamba nyumba za bei nafuu za NSSF zinauzwa TSH 200 Milioni. Mimi ninajua wewe unafanya kazi NSSF hebu niambie tangu mwaka huu uanze ni mwanachama gani mumewahi kumlipa mafao ya 200 milioni? Kama yupo I will chop my neck.

Ni na amekwambia wanachama wa NSSF tunaridhika na mambo yanayofanywa na NSSF? If you are a real a scholar do your research. Dont tell me hizo kangaroo bodi zilizoundwa na yule aliyemteua Dr. Dau, I want you to do your homework among NSSF members.

Simple challenge kwa Dr. Dau kama NSSF ina mapesa yote hayo tunataka kwanza NSSF ianze kutoa mafao mazuri ya pensheni kama PSPF. Haihitaji kuwa rocket scientist, formula ya PSPF ipo it is just a matter of copy and paste.
 
Kazi za mifuko ya hifadhi ya jamii ni kuchuchuka michango, kuiwekeza na kulipa mafao pale wanachama wake wanapostaafu. Ukiangalia budget za hii mifuko, ni kweli unakuta kuna proportional kidogo ya kiasi kilichotengwa kwa mafao, na kiasi kikubwa huwa kunawekezwa. Kumbuka nia ya mifuko ni kutoa long term benefits, ndio maana wanatakiwa wainvest kwa long term tena kwenye miradi yenye faida kubwa.
Asilimia zinazotengwa kulipa mafao ni kidogo, hii inatokana na projection zao kwa financial year hiyo wanastaafu wanachama wangapi. Siyo kwamba miaka yote itakuwa hivi, kuna miaka ambayo watakuwa wanalipa mafao zaidi kuliko watakachokuwa wanakiwekeza.
So cha muhimu ni kuhakikisha wanawekeza in a prudent manner ili tutakapokuja kustaafu tusikose mafao yetu.

Tafadhali Rejao, tuwekee investment portfolio ya NSSF tuilinganishe na guidelines zilizotolewa na SSRA. Baada ya hapo ndio mjadala utaendelea kitaalamu zaidi.

Pia Kama reserve iko vizuri hivyo kwanini hakuna adjustment ya contribution rate kumpunguzia mzigo mchangiaji au kuboresha mafao, au yote mawili.

Queen Esther
 
Social security ni bima.Kama unavyokata bima ya gari yako sasa mbona mwisho wa mwaka huwa hamuendi ku claim mrudishiwe kilichobakia?

Nadhani issue hapa ni kuwa sisi wenye pesa kule tuwe tunashirikishwa japo kidogo kuepuka miradi ya kijinga kama hii MACHINGA COMPLEX sehemu ni prime area wangeweza kuweka mjengo wa maana wangeuza apartments zote wangepata some billions za chap chap lakini jengo sasa hivi linalala popo!
 
MrNSSF, kabla sijasema uwekekaji huo ni mzuri au ni mbaya,naomba msaada wa elimu,

1. hivi hii miradi imepitiwa na Bodi ya SSRA kama sheria inavyotaka? Tafadhali rejea pia investment guidelines za social security funds. Jibu lako litasaidia wadau waelewe namna ya uwekezaji ktk mifuko na ndipo wapime kama ni sahihi au la, tena bila kuhusisha chama.

2. Pia kwenye mifuko hakuna dividents ila mfuko unapokuwa na reserve kubwa inatakiwa kuboresha mafao au kupungura contribution rate (asilimia ya uchangiaji) au yote mawili.

3. Mods wekeni (attach) ile doc ya SSRA ya investment guidelines for SSF's kuutendea haki mjadala.

Queen Esther

http://www.ssra.go.tz/wp-content/up...IAL-SECURITY-SCHEMES-INVESTMENT-GUIDLINES.pdf
Nafikiri ungeifuatilia hapa
 
Tafadhali Rejao, tuwekee investment portfolio ya NSSF tuilinganishe na guidelines zilizotolewa na SSRA. Baada ya hapo ndio mjadala utaendelea kitaalamu zaidi.

Pia Kama reserve iko vizuri hivyo kwanini hakuna adjustment ya contribution rate kumpunguzia mzigo mchangiaji au kuboresha mafao, au yote mawili.

Queen Esther
Visit web site ya NSSF kuna financial statements za miaka yote. unaweza kuanalyze ujue preformance yao na kama wapo in line na hiyo guideline ya SSRA niliyokupa link yake hapo juu.

Kuhusu kuadjust contributions, kumbuka mifuko yote ya Tanzania ni Defined Benefit Scheme na main sponsor ni employer. So ni jukumu ya waajiri kudetermine rates
 
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.

Threads ulizozianzisha kumshambulia Dr Dau ni hizi:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...erikali-na-hatima-ya-taasisi-ya-moyo-thi.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/16889-thi-yaibwaga-nssf-mahakamani.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19691-samahani-nssf-samahani-dr-dau-nyoni.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rof-kapuya-wawajibishwe;-nssf-ishitakiwe.html

https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogo/19593-cheche-mitaani-tume-yawanyoshea-kidole-nssf.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...inga-nssf-imekula-hasara-ya-bilioni-30-a.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kezaji-hayalipiki-ripoti-ya-cag-yafichua.html

https://www.jamiiforums.com/major-p...igamboni-bridge-ipp-road-construction-10.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ra-uongozi-wa-nssf-makao-makuu-uwajibike.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/120673-ooh-poor-nssf-what-is-this-4.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ilia-mchakato-wa-ugawaji-viwanja-mafia-5.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...;-vitu-vyaibwa-vingine-vyarudishwa-kiana.html

Hebu nenda TRA,PPF na kwingine.

Kwani hoja ni NSSF au Dr. Dau? Kama wanatengeneza faida, basi si haba wakawa wanachangia kidogo watoa michango...na sio NSSF tu bali pension funds zote.
 
Mbona uko kimya juu ya uwekezaji na uendeshaji wa mifuko mingine ya pensheni Tanzania ambayo inaendeshwa vibaya zaidi?

Hii yote ni ugomvi wako na Dau toka suala la Dr Masau na lile la magodown aliyokosa Reginald Mengi?

Let it go, wawakilishi wa wanachama na bodi wameridhia sera zao sasa kwa nini hutaki kukubali kuwa NSSF wanafanya ambayo wanachama wao wameridhia?

Kwa nini husemi kitu kuhusu ufisadi ulio tukuka TRA? Tatizo lako ni Dr RAMADHANI Dau na saa zingine hata kama una hoja lakini chuki yako binafsi kwa Dr ina negate chochote kile utakachokisema.....
Ingekuwa vema, na ningekuelewa zaidi kama ungejikita kwenye hoja. Sioni ni kwa nini tujadili mifuko mingine wakati mleta hoja ametaka tujadili NSSF? Nadhani jambno ni jema ni kuwa kama wewe una hoja kuhusu uendeshaji wa hiyo mifuko mingine, ilete ijadiliwe.

Pia, hiyo unayosema ridhaa ya wanachama kuhusiana na uendeshaji wa NSSF, hivi unaweza kutufafanulia ni kwa jinsi gani wananchaiam wanavyoshirikishwa katika kufikia maamuzi hayo? (NOTE: Mimi ni mwanachama wa NSSF na wala sijawahi kuulizwa chochote au kuombwa ushauri na NSSF kuhusiana na suala la uendeshaji wake)
 
Shirika la Hifadhi ya Jamii limekuwa au niseme limegeuzwa kuwa Shirika la Uwekezaji la Hifadhi ya Jamii. Na kwa jinsi ambavyo linaendeshwa bila ya shaka linasukumwa na kutafuta faida na ni faida hii ambayo linapata imekuwa ikiwekezwa kwenye miradi mbalimbali. Hili si tatizo.

Hata hivyo kwenye mashirika ambayo yanafanya kazi kwa ajili ya faida (for profit companies) yanarudisha sehemu ya faida yake kwa wanahisa (shareholders) wake. Inaweza kurudishwa kama gawio (dividends) kila mwaka kufuatana na kanuni ambayo shirika limejiwekea.

NSSF inakadiriwa kuwa na wanachama karibu 600,000 hadi mwezi Juni mwaka huu likiwa na mali yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja ambayo inakadiriwa kukua kwa haraka hadi mwaka 2013. Kwa mujibu wa sera zao za uwekezaji NSSF hutenga asilimia 75 ya fedha zao kwenda kwenye uwekezaji na asilimia 25 kwenda kwenye mafao na gharama za uendeshaji. Ni wazi kuwa 2/3 ya fedha zinazoweza kuwekezwa zinawekezwa kwenye kile ambacho kinaonekana ni 'high yield' investments.

Je ipo haja ya kuligawa shirika hili na kuhakikisha upande unahusiana na hifadhi ya jamii (mafao kwa wanachama) unaendeshwa tofauti na upande unaohusika na uwekezaji? Je kuna uwezekano wa kuhakikisha kuwa huo upande wa uwekezaji unaendesha kama kampuni nyingine ya faida ambapo wanachama wa NSSF ndio wanakuwa wanahisa wa shirika hilo na ambao watalipewa gawio kila shirika linapotengeneza faida kabla halijaamua kuwekeza fedha kama faida?

Swali hili ni muhimu kwa sababu kwa mtu ambaye anachangia NSSF na bado hajaanza kupata mafao mbalimbali au hajatumia mafao yoyote kwa mwaka hapati faida yoyote ya kifedha kutokana mchango wake ambao unatumika kutengeneza faida kwa shirika. Na kama mtu atakuwa amechangia kwa miaka mitano au zaidi na labda amepata fao la msiba, n.k au aambiwe asubiri hadi kuretire kuanza kupewa shilingi themanini elfu kila mwezi baada ya kuchangia shirika kwa miaka thelathini au ishirini naona ni unyonyaji wa aina yake.

Ni muhimu kwa wanachama kufaidika kifedha (monetary benefit) na uwekezaji wa NSSF kila mwaka. Na namna pekee ya kuwafanya wanachama nao wanufaike ni kuhakikisha kuwa NSSF (bila ya shaka na mashirika mengine ya pensheni) inaweka utaratibu wa kuwagia wanachama wake ama kwa kutengeneza account au kuchangia kwenye akaunti ya mwanachama kiasi cha faida fedha ambazo mwanachama anaweza kuzitoa wakati wowote nje ya zile za pensheni.

Jambo la kwanza ambalo linahitaji kufanyika kwa haraka ni kubadili sheria ili NSSF isiwezeke fedha za wanachama kwenye miradi yenye kutarajia faida bila kuhakikisha kuwa sehemu ya faida inayopatikana inawarudia wanachama kama gawio siyo kama sehemu kiduchu ya mafao.

Swali la Ugomvi: Je CDM ina sera gani kuhusu NSSF na uwekezaji wa NSSF kwa sababu tayari tunajua sera ya CCM ni kutumia NSSF pale ambapo serikali imeshindwa au haina fedha au pale ambapo serikali inataka fedha ya haraka haraka kuikoa mbele ya wananchi.
hayo ni mawazo yako. we are late mwanakijiji, na kama sikosei wewe si mwanachama wa nssf labda huko merikani, sioni kinachokuwasha au ndo kufurahisha jukwaa? miradi inayofanywa na nssf ni zaidi ya gawiwo unalolitaka. biinafsi ni mwanachama tofauti na wewe lakini kwa yanayofanya na nssf kwa kweli kuwepo kwa vitu kama udom, mabibo hostels na mengine mengi yafanywayo, sioni ni gawiwo gani tena unataka. kwa kifupi ninachoona hapa ni majungu tu na kutaka kuwaridhisha hao mabwana zako wa chadema (kumbuka walivyokushambulia ulivyoonyesha kwenda kinyume nao). kwakweli lazima tuwe wazalendo if we want to move, we are behind in almost all aspect except majungu kama haya uliyoyaleta hapa labda ndo tunaongoza. better you shut up you mouth.
 
Visit web site ya NSSF kuna financial statements za miaka yote. unaweza kuanalyze ujue preformance yao na kama wapo in line na hiyo guideline ya SSRA niliyokupa link yake hapo juu.

Kuhusu kuadjust contributions, kumbuka mifuko yote ya Tanzania ni Defined Benefit Scheme na main sponsor ni employer. So ni jukumu ya waajiri kudetermine rates

Nimepita kwenye website Kama ulivyonishauri, hata hivyo bado maswali yangu hayajajibiwa kwa sababu zifuatazo:
1. Performance reports zote ni kabla SSRA hajatoa investment guidelines.
2. It is unfortunate that actuarial valuation reports zingesaidia sana kujadili mada Kama hii, lakini hakuna hata moja. Je sisi wanachama hatuna haki ya kusoma hizo actuarial reports?
3. I stand to be corrected;
- Sio mifuko yote TZ iko under Defined Pension Scheme
- Hata NSSF kitendo cha kulipa withdraw benefit mfano kwa last year 2011 mlilipa Tshs. 106,221,067,003.52 ambayo performance financially ni 78% ya total amount paid kwa benefit zote. Je
Huoni Bado mnaoperate kama provident (defined contribution) wakati nyie ni pension fund ( defined scheme?)
- kwanini mmeendelea kulipa withdraw benefit tena kwa percent kubwa kuliko mifuko mingine huku mnawaambia watu Hilo sio fao? Mkiamua ku act ki profession msimumunye mumumnye
Maneno. Pia practice what you preach.

Mwisho
It is an obligation of management of the scheme or a legislation body to adjust the contribution rates when the financial resources are either insufficient enough to meet funds obligations or is in excess (buffer reserve) so that it reduce burden to contributors.

Sasa wewe unaposema mwajiri ndio apunguze au kuongeza kiwango cha uchangiaji umeitoa wapi hiyo? Je mwajiri amepewa acturial report?

Bado SSRA anatakiwa atolee maelezo ya kina haya mambo ya uwekezaji kwenye hii mifuko maana jinsi tunavyoenda umuhimu wa ofisi Yake unazidi kupwaya.

Nawasilisha.

Queen Esther
 
Back
Top Bottom