Ontario: Mahakama Kuu ya Canada Yatupilia Mbali Shauri la Wanaharakati Walioshitaki Barrick Kukiuka Haki za Binadamu Kwa kutumia Polisi North Mara.

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
9,436
10,946
Mwenyekiti wa Makampuni ya Barrick amesema amefurahishwa na maamuzi ya Mahakamani ya kutupilia mbali Shauri lilopelekwa na Wanaharakati wa Tanzania ambao Walioshitaki kampuni hiyo Kwa kile kinachodaiwa Kukiuka Haki za binadamu kwenye mgodi wa North Mara Kwa kutumia Polisi.

1732813688578.png

Kampuni ya Dhahabu ya Barrick (NYSE:GOLD)(TSX:ABX) imepokea kwa furaha uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Ontario wa kutupilia mbali madai yaliyotolewa na wakazi wa Tanzania waliokuwa wakilalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania jirani na mgodi wa dhahabu wa kampuni hiyo wa North Mara.

Mahakama hiyo iliamua kwamba Ontario haikuwa jukwaa mwafaka la kusikiliza madai hayo.

Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, alisema kampuni hiyo imekanusha mara kwa mara kile inachokiona kama madai yasiyo na msingi yanayotolewa asasi chache zisizo za serikali zenye mrengo wa kianaharakati zinaodai kuwapo kwa ukiukwaji wa kihistoria wa haki za binadamu katika maeneo yanayozunguka mgodi wake wa North Mara.

“Tunajivunia mafanikio tuliyoyapata nchini Tanzania kutokana na ushirikiano wetu na Serikali ya nchi hiyo kupitia ubia wa Twiga. Mchango wa mapato ya migodi yetu umeleta mageuzi katika uchumi wa nchi hiyo wakati uwekezaji wetu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya jamii za wenyeji, ukiambatana na mkakati wetu wa kuleta maendelea ya jumla, umeboresha hali ya maisha yao," alisema.

My Take
Tatizo la Mara ni la kijamii na mihemko ya Kisiasa sio mgodi.
 
Mwenyekiti wa Makampuni ya Barrick amesema amefurahishwa na maamuzi ya Mahakamani ya kutupilia mbali Shauri lilopelekwa na Wanaharakati wa Tanzania ambao Walioshitaki kampuni hiyo Kwa kile kinachodaiwa Kukiuka Haki za binadamu kwenye mgodi wa North Mara Kwa kutumia Polisi.

View: https://x.com/Mwanahalisitz/status/1862164168838709339?t=pmpXa5GiKXKN3fNaONsPSw&s=19

My Take
Tatizo la Mara ni la kijamii na mihemko ya Kisiasa sio mgodi.

..wameshindwa sio kwasababu madai yao ni ya uongo, bali kwasababu mahakama za Canada hazina mamlaka ya kuamua kesi ya aina hiyo.

..wanaharakati / wananchi wamejaribu kuifungamanisha barrick na uonevu uliofanywa na jeshi la Polisi la Tanzania.

..kesi hiyo ingehusu jambo lililofanywa moja kwa moja na kampuni ya Barrick upo uwezekano kwamba wanaharakati / wananchi wangeshinda.

..binafsi nawapongeza wanaharakati / wananchi walioamua kupeleka shauri hilo mahakamani pamoja na kwamba hawakufanikiwa.

NB:

..najiuliza kampuni ingekuwa ya Kichina, au ya Kituruki, sijui hata tungeanzia wapi kuishtaki.
 
Mwenyekiti wa Makampuni ya Barrick amesema amefurahishwa na maamuzi ya Mahakamani ya kutupilia mbali Shauri lilopelekwa na Wanaharakati wa Tanzania ambao Walioshitaki kampuni hiyo Kwa kile kinachodaiwa Kukiuka Haki za binadamu kwenye mgodi wa North Mara Kwa kutumia Polisi.

View: https://x.com/Mwanahalisitz/status/1862164168838709339?t=pmpXa5GiKXKN3fNaONsPSw&s=19

My Take
Tatizo la Mara ni la kijamii na mihemko ya Kisiasa sio mgodi.

We mjinga unashangilia ujinga naona,
 
Polisi wanalinda usalama ulitaka wawaache hao wavuta Bangi zenu ?

..hii ni kesi ya wananchi wa maeneo ya North Mara.

..tunafanya makosa sana kuingiza mambo ya vyama vya siasa.

..Na kwa taarifa zilizoko mitandaoni hii ni kesi ya tatu dhidi ya Barrick.

..kesi mbili za awali ilibidi ilibidi Barrick na wadai wasuluhishane nje ya mahakama.

..Nasisitiza kwamba hawa ni Watanzania wenzetu wanadai haki zao.

..Mawakili wanaokwenda kusimamia kesi huko Canada, si mawakili wa Tanzania, bali mawakili wenye usajili na leseni za kutetea kesi Canada.
 
Back
Top Bottom