North Korea has the Lowest IQ in the World

North Korea has the Lowest IQ in the World

Korea kasikazini wapo juu kimaendeleo licha ya vikwazo vya Wazungu na Fitna za Jirani yake Korea kusini hizo tabia za kuwazushia kuwa wana IQ ndogo ni tabia za Wazungu wenye nia mbaya wakidhani watu hawajui kuwa Korea ipo mbali kimaendeleo.

...Wapo juu kimaendeleo? Ndio maana watoto wana utapia mlo tena kwenye vituo vya serikali?

...Kuna nchi iliwekewa vikwazo na kupigwa fitna kama Iran? Sasa, unaweza fananisha maendeleo ya Iran na Korea Kaskazini?
 
Korea kasikazini licha ya kubanwa na vikwazo vya America na ulaya wapo mbali kimaendeleo huwezi kuwalinganisha na Tanzania kuwaitwa eti wana IQ ndogo ni uzushi wa hao Wazungu.

Ni kweli mkuu.

Juzikati vijana wa IT wa Korea Kaskazini walihack mtandao mzima wa SONY na kukomba nyeti zao zote kwa sababu tu ya SONY kutoa sinema inayomdhalilisha kiongozi wao.

Hawa ndio watu wenye IQ ndigo kweli? Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi mkuu.
 
...Kifyatu, nimejiuliza swali hili nilipoitia machoni hii post. Yawezekana, tatizo liko kwenye upimaji wa hiyo IQ, kwa maana ya vipimo au vigezo vilivyotumika. Maana, hao jamaa maisha yao ni duni, ukichanganya na ufinyu wa elimu ya mambo, waweza onekana wana IQ ndogo.

Pengine tatizo lipo kwenye upimaji wa IQ. Unapopima IQ lazima mtihaniwa aulizwe maswali yanayotokana na mazingira yake. Kama walikuwa wanawauliza maswali ya sinema za Holywood wakati wao wametengwa na wa-west kwa zaidi ya miaka 60 sasa hilo ni tatizo la wapimaji. IQ mara zote ni genetically linked. Kama ndugu zao wa damu wa Korea Kusini wana IQ kubwa halafu wao wanaambiwa wana IQ ndogo - Pleeeeease, give me a break.

...Mataifa ya magharibi yanahujumu vipi kitu ambacho hakipo? Wana uchumi gani hao, zaidi ya kutengeneza silaha na kutegemea utalii finyu na SEZ za makampuni ya Korea Kusini?

Hawa watu wanatengeneza silaha za nyuklia. Unataka kuniambia hawawezi kutengeneza magari, electronics, na consumer goods nyingine?

Ukishabanwa na mfumo wa kifedha wa mataifa ya magharibi kama ilivyo Cuba na Iran, na sasa wanafanya hivyo hivyo kwa Urusi basi unakosa uwezo wa kupata credit ambayo ni muhimu kujiendeleza. Sijui kama unafahamu uwepo wa umoja wa nchi zijulikanazo kama BRICS (Brazil, Russia, India, China, South-Africa). Huu umoja unataka kujinasua na mfumo wa dola za kiMarekani ili kukwepa huu uhujumu. Umeona Cuba na Iran zilivyokuwa zimebanwa - kama unafuatilia haya mambo.

Kujibu swali lako kwa kifupi ni kuwa Korea Kaskazini haiwezi kujiinua kiuchumi kwa sababu imetiwa kabari vibaya sana na mfumo wa kifedha wa mataifa ya magharibi.
 
makubwa! ikiwa wana IQ ndogo hivyo halafu wanapigana cyber war na marekani pamoja na korea kaskazini je wangekuwa na IQ kubwa sijui ndo ingekuwaje?.... IQ ndogo hivyo inatengeneza bomu la nuclea ingekuwa kubwa je? wangetusumbua sana hawa asee...propaganda hizi!!
 
Ni upumbavu mtupu hili suala la IQ,yani watu wanapenda kuongea mambo hayana uhalisia kabisa,hebu angalia mnavyojichanganya kwenye hivyo vigezo vya wenye IQ mara ndogo
 
Mwaaa!
Sura ya mtoto inaongea Yote.
Teh teh teh.

Unaona sasa....nilijua tu huwezi kukawia kutoka ndani ya closet.

Mwanaume alonyooka kamwe hawezi kumchumu mwanaume mwenzake.

Ni walopinda tu ndo wawezao.

Kujitekenya wewe....kujichekesha wewe....kuchumu wewe......what's next Shamira?
 
Hii kipimo cha IQ ni very debatable. Kuna ranking inawapanga watu kutoka na maeneo husika na Waafika kuwa wa mwisho. Wengine huenda na kuconclude kuwa imekuwa ni dhana ya racism. Ndio maana ukifuata literature za IQ kutokea miaka ya 70 mpaka sasa tone zimebadilika na appreciation kwa weusi inaonekana. Lakini pia zipo literature nyingine zina-question kama IQ ni inborn au ni matokeo ya mazingira.
Kwenye mada, si kweli kwamba N.Korea wapo hivyo. Haiwezekana ule mpaka uliochorwa miongo kadhaa iliyopita ndio uwe mpaka wa IQ pia.
 
That would be crime,though unlawful but not as preposterous or abominable as RACISM.
The reason being you can choose not to steal but you cannot choose your race/color before-hand.
Concerning crime,Laws vary from place to place,marijuana maybe illegal where you are but legal somewhere else.
What you call crime in the US e.g polygamy is perfectly legal and normal in the whole African/Middle Eastern and Asian continents.
Yet RACISM is totally abhorrent in the entire galaxy.
 
Back
Top Bottom