Noandoka Tanzania

Noandoka Tanzania

Mkuu nenda kacheki ustaarabu ......mambo yakiwa poa bs naomba unistue na mm......mi ntakuja kuoa huko huko....damu ya bongo tyr inanuksi bhana
 
Naondoka Tanzania,

Hivi sasa naelekea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwa ajili ya safari yangu hii. Nimeacha mke na watoto pamoja na wazazi ambao natarajia watanifuata baada ya mwezi mmoja kwani naenda kuwaweka sehemu salama zaidi na ambayo wanangu watakuwa na haki ya kuota ndoto.

Nirudi kwenye sababu za kuondoka;

Kwanza niseme sababu ya kwanza ya kuondoka na kwasababu ninao uwezo wa kuondoka, pili kwa kweli uzalendo unanishinda na naona kabisa kuwa kadiri siku zinavyoendaelea nazidi kuichukia nchi yangu, kuwachukia viongozi wangu, kuwachukia aia wenzangu na hata kujichukia mwenyewe.

Najisikia vibaya kwani sasa nina mashaka na wasi wasi wakati wote, naona aibu kuwa Mtanzania.

Ubaya mkubwa ni ukweli kwamba tayari nchi yetu imeshapiga magoti, wananchi wamekata tamaa, taifa limepoteza mwelekeo na hata sasa ukimuuliza hata Rais wetu ni wapi anakopeleka nchi yetu hana hata jibu dogo analoweza kukupa bila kujiuma uma na kuchanganya mambo.

Sijui tulikosea wapi, sijui turekebisheje ila kwa wale ambao tunaweza kuondoka basi tuondoka, nyumba na mali zangu zote nimeweka kwa madalali waziuze ili pesa hiyo itusaidie kwenda kuanza maisha mapya mimi na familia yangu.

Ee Mungu utusaidie
eeeh Mungu akusaidie tuu kamanda maana.biashara za madili na makontena hewa na ukwepaji kodi hauna.nafasi tena nchini mwetu..tunajenga nchi mpya..maisha yako ya ujanja ujanja ni bora ukaanza mbele kuliko kusubiri uumbuliwe..pole sana..nenda kajaribu maisha nchi nyingine masikini kama ilivyokuwa nchi yetu kipindi cha nyuma ili upate nafasi ya kupiga hela vizuri kabla hawaja kustukia...nenda salama
 
Naedna kuanza maisha mapya at any cost,N itabakiza nyumba ya urithi kwa sababu za kiutamaduni ila nilivochuma kwa hela yangu vyote nauza niende nikabebe maboksi na kusafisha choo ng'ambo nikiwa na amani moyoni sio kukaa kwenye nchi ambayo inatia kichefuchefu na kuhara wakati wote
We nendra ila kumbuka huku ukiwa na genge la kuuza nyanya unathaminika ila huko mpaka utusue ujùe umebahatika kuwa na talent.
 
Sijaona sababu ya kuandama kwenye nchi ambayo haina maana sana sana wataniudhi halafu nitaharibu maisha yangu na watoto wangu wakati dunia ina nafasi sehemu zingine.Waandamane wale ambao hawana pa kwenda ili wahakikishe nchi inaenda sawa.Wasipoandamana wataandamanishwa
Nenda syria kwa sasa kazi zipo nyingi mno
 
Nlikuwa nawaza kitu kama hiki dakika 30 zilizopita.
Nikajikuta naangalia bei za nyumba hispania.
Huu mwaka ukiisha sijaondoka Tanzania basi siondoki tena.

Naichukia hii nchi kuliko maelezo.
yani mimi ndio kila baada ya dakika tatu ninapata hili liwazo, kila mara akili yangu inaniambia niko mahala nisipo stahili. silipendi hili nchi hata kidogo.

niajiapizia mwaka huu ndio mwisho wa kuishi kwenye hili jehanamu mnaloiita tanzania. nikiondoka nafanya na sherehe kabisa huko ntakapoenda,
 
Naondoka Tanzania,

Hivi sasa naelekea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwa ajili ya safari yangu hii. Nimeacha mke na watoto pamoja na wazazi ambao natarajia watanifuata baada ya mwezi mmoja kwani naenda kuwaweka sehemu salama zaidi na ambayo wanangu watakuwa na haki ya kuota ndoto.

Nirudi kwenye sababu za kuondoka;

Kwanza niseme sababu ya kwanza ya kuondoka na kwasababu ninao uwezo wa kuondoka, pili kwa kweli uzalendo unanishinda na naona kabisa kuwa kadiri siku zinavyoendaelea nazidi kuichukia nchi yangu, kuwachukia viongozi wangu, kuwachukia aia wenzangu na hata kujichukia mwenyewe.

Najisikia vibaya kwani sasa nina mashaka na wasi wasi wakati wote, naona aibu kuwa Mtanzania.

Ubaya mkubwa ni ukweli kwamba tayari nchi yetu imeshapiga magoti, wananchi wamekata tamaa, taifa limepoteza mwelekeo na hata sasa ukimuuliza hata Rais wetu ni wapi anakopeleka nchi yetu hana hata jibu dogo analoweza kukupa bila kujiuma uma na kuchanganya mambo.

Sijui tulikosea wapi, sijui turekebisheje ila kwa wale ambao tunaweza kuondoka basi tuondoka, nyumba na mali zangu zote nimeweka kwa madalali waziuze ili pesa hiyo itusaidie kwenda kuanza maisha mapya mimi na familia yangu.

Ee Mungu utusaidie
Unaenda kujifunza kuishi, ongera uko magharibi ndo utamwelewa vizuri pombe John , uko si sehemu nzuri kabisa kuishi, rudi nyumbani na usiuze asset zako.
 
Kila la kheri! Maisha nu popote, cha muhimu nafsi iwe na Amani.
 
Tanzania ni nchi nzuri saana tuipende tuithamini wote bila kusubiri wanaotuongoza wafanye hivyo.

Kila mmoja ana maamuzi binafsi ila nakuhakikishia ukiwa nje unaweza kuipenda Tanzania na ukabadili mawazo.
Sure.napenda sana watu mnaojielewa

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Ni mtazamo wako ila hakuna Sababu ya kuandika mtandani kwani mtazamo wako sio wa mwingine pia jihadhari unaweza kujikuta unatenda makosa ya kimtandao na Sijui unaaminije kuwa uwendako ndiko utapapenda?
 
makosa yametendwa sana kiasi kwamba tunajua kuwa sio makosa tena
 
Back
Top Bottom