Noah Cup 2023 Kuanza Kutimia Vumbi Uwanja wa Ilboru Arusha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

NOAH CUP 2023 KUANZA KUTIMUA VUMBI UWANJA WA ILBORU ARUSHA

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Jijini Arusha, Mhe. Noah Lemburis Saputu Tarehe 12 Agosti, 2023 katika Uwanja wa Michezo wa Ilboru Jijini Arusha amefanya Uzinduzi wa Mashindano ya Michezo yaitwayo NOAH CUP 2023

Michuano ya Mpira WA miguu iliyoandaliwa na Mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe. Noah Lemburis Saputu Mollel imezinduliwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ilboru.

Katika uzinduzi huo,mgeni Rasmi alikuwa ni Mbunge Mhe. Noah Lemburis ambapo amezitaka timu zote shiriki kucheza mpira Kwa nidhamu na Wala si Kwa kukamiana na kuumizana.

Akitoa neno la ufunguzi, Mbunge huo amezipongeza timu zote zinazoshiriki pamoja na wadau wote waliofanikisha kupatikana Kwa timu hizo ikiwemo kamati ya mafanikio ya michuano hiyo.

Katika mechi ya ufunguzi hii Leo imezikutanisha timu za Ilboru Sekondari na Olturoto ambapo hadi dakika tisini zinakamilika Olturoto waliibuka kidedea Kwa kuichapa Ilboru goli tatu Kwa moja

Awali imefanyika Michezo kadhaa ambapo kwenye mchezo wa kukimbiza kuku wanaume Charles Sikoi aliibuka Mshindi wakati Kwa wanawake bi.Wema Mtendaji wa ilboru pamoja na bi.Halima Ndesajo waliibuka kidedea

Kwenye mchezo wa kutembea na yai likiwa kwenye kijiko mdomoni, Mtendaji wa Kata ya Musa aliibuka kidedea

Michezo mingine iliyochezwa Leo ni pamoja na kunywa soda Kwa haraka nk.

Matukio mingine ilikuwa ni pamoja na kugawa jezi pamoja na mpira Kwa timu zote shiriki.

Michuano hiyo itaendelea Tena kesho Kwa mujibu wa ratiba
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-08-12 at 22.02.10.mp4
    45.5 MB
  • WhatsApp Image 2023-08-12 at 22.02.12.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-12 at 22.02.12.jpeg
    127.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom