No offence, ila tunaoishi na wanawake form four na la saba, tunakula maisha sana

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Mwaka wa tano huu sasa, hakuna mba mba mba wala nye nye nye! Namshukuru Mungu.

Sijui ni kwanini ipo hivi, no offence pia kwa wanawake wenye degree zenu. Ila mimi nazungumzia sisi tuliooa form four na la saba, yaani kwa kweli, hata kama huyu mwanamke ana makando kando, ila life lipo poa sana, sio la kuforge.

Sielewi uhusiano wa mwanamke kusoma sana na kuwapeleka waume zao mzobe mzobe mwendo wa Ngiri

Ila kwa mifano hai niliyonayo, waliooa wanawake wenye degree na hawa career women hawa, kwa kweli wanaipata. Wale wanaume ambao walikuwa hawana emotional intelligence, ndoa zao nyingi tayari tumeshazizika.

Mahali nafanya kazi, ndoa tatu naziona na zimezikwa naziona kwa macho yangu.. Wanawake wote walikuwa ni so called educated na wenye career zao.

Kuna siri Mungu aliiweka hapa, ila nasisitiza tu, mwanaume kama huna emotional intelligence, mziki wa wanawake wasomi na wenye career zao, hautaweza kuucheza. Wewe kimbilia chap kwa wanawake la saba na form four.

Kwanza la saba na form four, ndani ya nyumba huwa hawaleti kujua, na hiyo sisi ndo wanaume hupenda... tunataka kuulizwa mambo...

Sasa wewe shawishika na hawa hawa career ladies and educated, kwanza mwanzoni wanakujaga kama malaika, kwa gia ya kutaka ndoa... Mwanzoni wapole sana!... miezi mitatu baada ya ndoa.. ndo sebene huwa linaanza .... alooooo
 
Ukiwa mwanaume kamili na ukaijua nafasi yako kwenye jamii hakuna mwanamke ataleta shida kwenye maisha yako tatizo vijana wa sasa hamna misimamo ya kiuanaume kwahyo mnatafuta wanawake mnaoweza kuwakandamiza ni ujinga na mtarithisha watotowenu uoga wa mbwa koko wanaume kama ww nawaona mafakeni tu hamna jipya kwenye ulimwengu huu
 
Mwaka wa tano huu sasa, hakuna mba mba mba wala nye nye nye! Namshukuru Mungu.

Sijui ni kwanini ipo hivi, no offence pia kwa wanawake wenye degree zenu. Ila mimi nazungumzia sisi tuliooa form four na la saba, yaani kwa kweli, hata kama huyu mwanamke ana makando kando, ila life lipo poa sana, sio la kuforge.

Sielewi uhusiano wa mwanamke kusoma sana na kuwapeleka mzobe mzobe waume zao.

Ila kwa mifano hai niliyonayo, waliooa wanawake wenye degree na hawa career women hawa, kwa kweli wanaipata. Wale wanaume ambao walikuwa hawana emotional intelligence, ndoa zao nyingi tayari tumeshazizika.

Mahali nafanya kazi, ndoa tatu naziona na zimezikwa naziona kwa macho yangu.. Wanawake wote walikuwa ni so called educated na wenye career zao.

Kuna siri Mungu aliiweka hapa, ila nasisitiza tu, mwanaume kama huna emotional intelligence, mziki wa wanawake wasomi na wenye career zao, hautaweza kuucheza. Wewe kimbilia chap kwa wanawake la saba na form four.

Kwanza la saba na form four, ndani ya nyumba huwa hawaleti kujua, na hiyo sisi ndo wanaume hupenda... tunataka kuulizwa mambo...
Shida ya wasomi ni kujifanya feminists uchwara. Anaona kumheshimu mumewe ni udhaifu...na ni nadra kwake kujishusha.
Screenshot_20221226-172125_Instagram.jpg

Ni wanaume wachache sana wanaoweza kukaa na mwanamke mwenye dharau, ego, maneno mengi na uanaharakati. Na zote hizi ni sifa za hawa wasomi.

Screenshot_20221227-133527_Instagram.jpg

Halafu kumbuka hawa wasomi wanakuwa wameolewa huko vyuoni na vianaume vyao uchwara kwa miaka miwili mpaka mitatu. Yaani wameishi kinyumba kabisa vijamaa vikila na kupakua for 2yrs+ na baadaye kutemwa na vijamaa vyao. Wengi wao tayari wana makovu na maumivu makali ya kisaikolojia ya kuchezewa miili yao kwa miaka yote hiyo halafu wakatemwa. Ndo hawa utawasikia eti wanaume wote mambwa. Mwanamke wa aina hii (mke wa mtu aliyetemwa kibabe) atakuwaje mke mwema?

Labda ubahatishe sana!
 
Back
Top Bottom