No control over Religious radio stations over hate speeches

Sasa sijui intelejensia ya Mwema ipo wapi? JK unafanya nini?

nashangaa serikali huwa inatishia sana kufungia baadhi ya vyombo vya habari, sijui hivi vingine hawavioni kwamba ni vya kichochezi? Mi nadhani wawatishie kdg labda watajirekebisha na kurudi kwenye misheni na visheni yao ya kiimani.
 
Mkuu mbona ulipandisha chart sana hili gazeti, hiki kipeperushi hakistahili kupoteza muda wetu kama great thinkers, ni sawa na toilet paper fulani. Kule kwetu ambako tunajisaidia machakani hiki kingefaa sana kusambazwa huko

kinachonisikitisha mimi ni kitendo cha hili jarida kuacha msingi na maudhui ya kuanzishwa kwake kama gazeti la kiroho la kiislam na kuanza kukurupuka kwenye siasa za uchochezi wa kidini na kutunyima haki ya kujifunza mambo ya kiroho na mafundisho ya ziada tuliyoyatarajia.
 
Ni vema liendelee kuwepo, ili tujue kwa hakika ni viongozi gani wanaendeleza udini..
 
Pole sana ndugu yangu Mfalme Suleiman, mwenye busara.
Nchi inaelekea kubaya. Bila kuficha redio Imaan na Alnuur yamebadilika sana pindi hii. Mimi ni msomaji wa Al-nuur tangu 1999. Lakini kutokana na mwelekeo lilikuwa nao siku hizi nimeliacha kabisa. Maana haliongei hata chembe mawaidha ambayo yatamjenga Muislamu au hata jamii kwa ujumla. Ni hatari sana.
 
mtoto wa nyoka ni nyoka, mtoto wa shetani ni shetwani, dini ya shetani ni shetani tu hata ifanyeje, hata ikijifanya mpole au mnyenyekevu, mfuga majini ni mfuga majini tu habadiliki, kuanzia roho nafsi na mwili....kwa wale wenye uelewa sawa na wangu, kilichobaki ni KUPIGANA VITA VYA ROHO na si vya mwili, manake vya mwili wanaweza sana, ila vya roho hawawezi kabisa. wengi wameshashindwa vya rohoni ndo maana makucha ya mwilini yanachipua....mwenye sikio la kusikilia na asikie, mwenye akili na aelewa niyasemayo!
 

asante sana ndg yangu Eliakim, ni kweli hizi media zetu za dini zimebadilka sana, zamani tulikuwa tunaona makala za ndoa, familia, jamii na mambo mengi ya msingi.

roho inaniuma sana mkuu sijui ninani kachezea hizi media mpaka zimepoteza dira na kuwan nje ya reli, "
ee Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na neema wajalie watu hawa warudi kwenye mstali na kuacha upotoshaji na uchochezi."
 

hapana ndg Hute, sio sawa kuhukumu wenzako kwamba ni wa shetani, mimi nadhani kama umeona mapungufu waambie wajirekebishe na uwaombee wasikosee na sio kuwapa laana wala kuwaombea mabaya. Naamini sana katika upendo bila kujali itikadi zetu za imani ya dini,kabila wala chochote cha kututenga.
 
labda msingi wa dini ya hilo gazeti/waandishi wake ni uchochezi, kama sivyo wasingekuwa wachochezi.
 
Hakuna cha maana utakachokipata toka kwenye hiki kipeperushi zaidi ya majungu na kuwakandia wakristo, KIAMA KIMEFIKA MTAKAOBAKI MTAIFAIDI HII NCHI
 

Kwa taarifa yako Uislamu hautenganishwi na Siasa! ktk Uislamu hakuna falsafa ya KAISARI MPE KAISARI na YA MUNGU MPE MUNGU! Enzi za utawala wa kidikteta umepitwa na wakati huu ni wakati wa mtu au kutoa maoni yake bila uoga mradi asivunje sheria!

Gazeti la Annur ni gazeti halali kabisa limeandikishwa kisheria na hufuata maadili ya uandishi wa habari! Mhariri wake O. Msangi namfahamu binafsi ni msomi na muadilifu na uchambuzi wake wa habari ni wa kina na uliofanyiwa utafiti! haandiki kibubusa bali anachoandika huwa naushahidi!

Sasa kama wewe King Suleman unategemea Gazeti la Annur liwe linaandika habari za pepo na moto na ahera tu, ningekushauri ukanunue vitabu viko vingi vyenyekuelezea habari za Ahera! lakini Annur halitawacha kuandika makala yoyote muhimu zinazohusu uhusiano wa mtu na mola wake, na uhusiano wa mtu na jamii yake inayoizunguka!

Unataka kuturudisha ktk enzi za ukiritimba wa Awamu ya kwanza na kauli ya "USICHANGANYE DINI NA SIASA" kauli hii haina nafasi ktk dunia ya leo ya utandawazi, uwazi, uhuru wa vyombo vya habari, nk!

Ndugu yangu kama wewe umechoka kulisoma hili gazeti hakuna anaekulazimisha! magazeti yako mengi, kuna TANZANIA DAIMA; MWANANCHI; RAIA MWEMA, MWANAHALISI na hata ukitaka magazeti ya udaku na umbea pia utayapata! ukitaka kusoma habari za ngono salama au ngono hatari pia yako magazeti ya aina hiyo nk. nk.

Mwisho, nakushangaa kushambulia gazeti la Annur lakini umeshindwa kuona hayo magazeti mengine yanayochochea ufuska na kusababisha gonjwa baya la ukimwi lisiishe nchini mwetu kwasababu ndio yanayosomwa kwa wingi!
 
Mkuu mbona ulipandisha chart sana hili gazeti, hiki kipeperushi hakistahili kupoteza muda wetu kama great thinkers, ni sawa na toilet paper fulani. Kule kwetu ambako tunajisaidia machakani hiki kingefaa sana kusambazwa huko

shuka bwana shuka, shukaaa bwanaaa.......ila shukaa.
 
Ni kweli jamani. Sisi ni watanzania , nchi ni yetu wote. Itikadi zisitufanye nasi tuwe kama Darfur, dini ziwe kanisani na msikitini. mwaka 2005 JK alipata kura 80% alipigiwa na waislamu tu, je wakati huo JK alikuwa mkristo ndio akashinda? CCM na JK hazipingwi kwa ajili ya uislam wa JK, zinapingwa kwa utendaji mbovu. sasa hivi kuna sakata la dowans, umeme umekuwa juu, labda nyie wenzetu waislam mnanunua umeme bei rahisi kwa sababu rais wenu muislam, na je wakati wa miaka saba ya mwanzo ya mkapa kulipokuwa hakuna mfumuko wa bei , wenzetu mlikuwa mnapandishiwa bei? Je walimu wa shule za wazazi wanaocheleweshewa mishahara ni wakristo tu?
mafuta yalivyopanda sasa hivi, ni wakristo tu inawaathiri? jamani tuangalie, tusitetee ujinga, kwa madai ya kujenga mshikamano wa kidini, wakati kuumia tunaumia wote, waliogoma UDOM, Mkwawa, ARdhi kwa kukosa pesa za kujikimu ni wakristo TU? tusitumiwe na watu wachache tukachuma dhambi. Wakati wao wanaoa kila uchao na wana mabibi ulaya nzima, sie tunalala kiza na kulipa deni la dowans wakati wattoto wetu wanasoma kwa shida.
 

Jamani hapa tunazungumzia dini na siasa za udini za kuwagawa watanzania, Imani kila mtu ana yake, tuzungumzie jinsi dinik inavyotumiwa kuwaondoa watanzania kutoka kwenye kuangalia masuala ya msingi ya kimaendeleo na kutuelekeza kwenye ugomvi usio na msingi. Heshimu imani za wenzio.
Ubarikiwe sana.
 
Ni gazeti la kiislam linalotumiwa na jk kueneza udini
 
Kiongozi, tumaini letu, mkombozi,etc hujaziona zinavyoeneza chuki za kidini unakurupuka kwenda kwa annur ..nyani haoni kundule pole.
 
Mkuu mbona ulipandisha chart sana hili gazeti, hiki kipeperushi hakistahili kupoteza muda wetu kama great thinkers, ni sawa na toilet paper fulani. Kule kwetu ambako tunajisaidia machakani hiki kingefaa sana kusambazwa huko

great thinker huyo....wacha weee..!
 
 
upo sawa ndg yangu, mimi ndio msingi wangu kwamba vyombo vya habari visitugawe kwa misingi ya dini
 
i Hongera Suleiman umejitahidi kuji-disguise sana, ila hukuweza kuficha yaliyo moyoni mwako! Wakati siungi mkono An-nur au gazeti lolote la kidini kuwa la kisiasa, siamini kulaumu vijarida ndio njia sahihi. Ungeanza kuwalaumu maaskofu wanaoingilia siasa mpaka wanafikia kuchagua meya wa kumtambua ! Au maaskofu walio anzisha CHRISTIAN DEMOCRATIC MOVEMEMT (CDM) ambayo imeapa kuifanya Tanzania isitawalike kwa kushadidia vurugu! P.S Waislamu hawatumii sana neno (kiroho) kama ulivyotumia wewe kwenye heading yako! Hapo ume-reveal your true identity!
 
[/QUOTE]

Nashukuru kwa ushauri wako ndg yangu,lakini angalia msingi wa gazeti letu je upo sahihi kushabikia siasa za upande mmoj? je siku Chadema wakimuweka candidate wa kiislam kwenye post ya uraisi na CCM wakamuweka mkristo, gazeti letu liko tayari kulamba matapishi kwa kuwasifia chadema wanao waona mashetani na kukiponda ccm wanaowaona wako safi?

[/QUOTE]

Sikubaliani na hoja yako hii kwa sababu katiba yetu haikatazi gazeti kushabikia chama cha kisiasa na hata ktk nchi zenye demokrasia iliyokomaa kama Uingereza kuna magazeti yanayoshabikia vyama vya Labor na consevative! sasa ni kawaida Annur kushabikia CUF bila kujali anaeongoza chama hicho ni Muislamu au ni Mkristo ndio maana Marehemu Mzee Mageni Musobi(Mkristo alipokuwa Mwenyekiti wa CUF tangu 1992-95 gazeti la Annur lilikuwa upande wa CUF! Gazeti hili lilianzishwa rasmi mwaka 1991!

Sasa haiwezekani Annur wakamsapoti Muislamu anaegombea Urais kupitia CHADEMA hata kama atakuwa anasali mara 5 kwa siku! kwa sababu Annur wako upande wa CUF kutokana na Sera za CUF za haki sawa kwa wote na wala sio sababu za udini!

Annur huenda wamepunguza kidogo mashambulizi yao dhidi ya chama tawala kipindi hiki sio kwa kuwa Rais alieko madarakani ni Muislamu bali kumbuka CUF kwa sasa pia wako Serikalini!

Wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi Gazeti la Annur lilikuwa limchambua na kumshambulia sana Mzee huyu na kama utataka ushahidi nitapost baadae! sasa Mwinyi alikuwa Muislamu au Mkirsto?

Kumbuka pia gazeti la Annur liko huru wala halina ubia wowote na Misikiti au Waislamu kwa ujumla hivyo maoni yao kuhusu vyama vya kisiasa ni maoni binafsi toka kwa jopo la uhariri hivyo tusiwahukumu Waislamu wote kwa kuwa Annur linamuelekeo wa Kiislamu!

Magazeti ya Lengo, mkombozi, Msema Kweli ni baadhi ya magazeti yenye muelekeo wa Kikristo na tulishuhudia uchaguzi uliopita jinsi walivyokuwa wakipigia debe chama cha CDM na hasa mgombea wake! lakini hawakuvunja sheria!

Hata magazeti ya Tanzania daima, Mwanahalisi, na kidogo Raia mwema ingawaje ni magazeti yasio na uhusiano na dini yoyote lakini yanaonekana kushabikia sana Chadema! ni haki yao wala hawavunji sheria ya nchi!

Uhuru, Habari leo, Mtanzania, Daily News nk, nayo yana julikana yako upande gani! zamani kulikuwa na gazeti likiitwa Dimba na hili likiegemea sana upande wa NCCR_Mageuzi!

We kama unaweza kusoma magazeti yote yasome na chomoa lolote zuri na lenye maslahi kwa taifa letu na lililo baya waachie wenye magazeti! huu ndio ukomavu na uhuru wa kujieleza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…