Nnauye: Viongozi wengi Chadema wanaganga njaa...

Nnauye: Viongozi wengi Chadema wanaganga njaa...

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Posts
629
Reaction score
72
Adai wanaganga njaa kwenye siasa.
> Asema wanalojua ni kung'oa kucha watu.
> Laana ya damu kwenye operesheni zao inawatafuna.
> Wanataka madaraka kwa gharama yeyote.
> Awataka wananchi kuwa macho nao.

Ameyasema hayo kweny mkutano mkubwa hadhara mjini Kilosa
Na Raymond Kaminyoge, Mwananchi | Jumatano, Aprili 17 2013

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye amesema Chadema ni chama kilichovamiwa na watu wanaotumia siasa kuganga njaa.

Nape alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

"Ndugu zangu kuweni macho kwa sasa, siasa imeingiliwa na watu wasiokuwa na sifa za uongozi na kazi yao kubwa ni kutumia siasa kuganga njaa zao," alisema.

Alisema wananchi wanapaswa kuwa macho na wanasiasa hao ambao malengo yao ni kuwaangamiza wananchi.

Akitaja baadhi ya sifa za wanasiasa aliowaita makanjanja, Nape alisema wengi wao ndiyo wanaotaka madaraka kwa gharama yoyote.

"Moja ya sifa kubwa ya wanasiasa hawa ni pamoja na kutaka madaraka kwa gharama zozote hata ikiwa ni pamoja na kuondoa uhai wa mtu," alisema.

Alisema Chadema wanachojua kwa sasa ni kuwahujumu wale wote wenye mawazo tofauti na yao kwa kuwatesa na hata kupoteza maisha ya wanaowapinga.

"Badala ya kushindana kwa hoja na sera, wanachokijua wao ni kung'oa kucha za wanaowapinga, kuwatesa na wakati mwingine hata kumwaga damu kwenye operesheni zao," alisema.

Alisema kwa kuwa wamekusudia kwa gharama yoyote kushika dola, hawajali damu za Watanzania zinazomwagika ili mradi wanafanikisha wanalolitaka.

Akikumbushia operesheni mbalimbali zilizofanywa na Chadema nchini tangu uchaguzi uishe mwaka 2010, Nape alitoa mifano ya operesheni ya mjini Arusha, Morogoro, Iringa, Singida na kwingine ambako maisha ya baadhi ya Watanzania yalipotea lakini hawakushtuka wala kuwajibika.

"Tunamwamini Mungu hataruhusu damu hizi ziendelee kumwagika kisa wanasiasa makanjanja, pia laana ya damu hizi zilizomwagika zitaviua vyama hivi na nchi yetu itabaki salama," alisema.

Nape alitoa wito kwa wananchi kuwa macho dhidi ya wanasiasa wa namna hiyo.

"Hewa wanayovuta wanasiasa makanjanja ni ya watu wanaowaunga mkono, tunaweza kuamua leo kuwanyima hewa hiyo na huo ndiyo utakuwa mwisho wao," alisema Nape.

Hahahahaha honey umeua...maana hapo umepiga ikulunoabisa

Adai wanaganga njaa kwenye siasa.
>. Asema wanalojua ni kung'oa kucha watu.
>. Laana ya damu kwenye operesheni zao inawatafuna.
>. -Wanataka madaraka kwa gharama yeyote.
>.Awataka wananchi kuwa macho nao.

Ameyasema hayo kweny mkutano mkubwa hadhara mjini Kilosa
 
Hiyo ni kazi yake kuleta uzushi na udaku na maneno ya taarab, kisha Kinana anafyagia kwa kuweka sawa
 
Alikuwa anawaambiea watu gani maana nasikia mkutano wake ulijaa watoto tu.
 
Na serikali ilivyo daifu imeshindwa kufuta chama na kukamata watuhumiwa wa hayo maasi.
 
Pia kusema hivyo ni sawa kwa maana ndiyo ajira yake inayomuweka mjini. Ulitaka aseme CDM inachukua nchi 2015 akose mshahara?
 
Sasa mbona watoa kucha na meno watu tumewajua ni Ramadhani Abeid Ighondu na Mwigulu Lameck Nchemba,,, Mbona wazee wa matusi ya nguoni ni Peter SeruTHREAD na Juma Nkamia!! Wote hao ni CCM...

Labda kama huko alikoenda hawaangalii bunge lakini JF itaendelea kuwaumbua maCCM. Ukweli kwa sasa uko wazi kwa hiyo wananchi tunawaangalia tu na kuwazodoa
 
Nape tafuta baba yako kwanza.pili mhamishe shemeji bagamoyo watu wanamgalagaza tu kwenye mitaro
 
Adai wanaganga njaa kwenye siasa.
>. Asema wanalojua ni kung'oa kucha watu.
>. Laana ya damu kwenye operesheni zao inawatafuna.
>. -Wanataka madaraka kwa gharama yeyote.
>.Awataka wananchi kuwa macho nao.

Ameyasema hayo kweny mkutano mkubwa hadhara mjini Kilosa

Je, ameshapata dodoso baba yake ni nani na yupo wapi? Au mama alikuwa anagawa tu sasa hajui mtoto ni wa nani au amsingizie nani....
 
Nape tafuta baba yako kwanza.pili mhamishe shemeji bagamoyo watu wanamgalagaza tu kwenye mitaro
Wewe baba yako ni nani?
Hebu rudi kijijini kwenu kamuangalie unaemuita baba kama mnafanana
Usitake kumuudhi mama yako mzazi bure manake yeye ndio anajua
 
Mi nilizani atawapa majibu ya maisha bora waliyoahidi na nauli za daladala zilivyopanda. Kwa Hali Hiyo yeye Ndio kanjanja
 
me nashindwa mwelewa nape yani chadema ndo wamegeuka wang'oa kucha baada ya wao kutuhadaa kwa video ya mwigulu wanataka uaminisha uma kuwa chadema ndo wang'oa kucha kwel mfa maji haachi kutapa tapa
R.I.P Nape na ccm yako
 
Adai wanaganga njaa kwenye siasa.
>. Asema wanalojua ni kung'oa kucha watu.
>. Laana ya damu kwenye operesheni zao inawatafuna.
>. -Wanataka madaraka kwa gharama yeyote.
>.Awataka wananchi kuwa macho nao.

Ameyasema hayo kweny mkutano mkubwa hadhara mjini Kilosa

Atachezea viwanja vya vumbi mnyika anapiga ktk red carpet na anampa dhaifu kila jina linalofaa.
 
me nashindwa mwelewa nape yani chadema ndo wamegeuka wang'oa kucha baada ya wao kutuhadaa kwa video ya mwigulu wanataka uaminisha uma kuwa chadema ndo wang'oa kucha kwel mfa maji haachi kutapa tapa
R.I.P Nape na ccm yako

uwe na aibu jukwaani hapa..video ni ya lwakatare ile au hujaiona? Nenda youtube andika lwakatare au bukoba boy
 
Atachezea viwanja vya vumbi mnyika anapiga ktk red carpet na anampa dhaifu kila jina linalofaa.

atatoa hayo majina wakati wenzake wanatekeleza ilani na ahadi walizoahidi....nadhani alichaguliwa kwenda kuwapa watu majina
 
Back
Top Bottom