Nnauye: Viongozi wengi Chadema wanaganga njaa...

Nnauye: Viongozi wengi Chadema wanaganga njaa...

Duh!ina maana Nape hajui km wauaji wa Wananchi hao wasio na hatia ni Policcm?
 
Huyo ni NAPE aliyesomea NSUMBA akapata English-F, Civics-F form IV leo anawaita CHADEMA Makanjanja? I don't BELIEVE!!!!!!!!!!! Nasikia siku hizi ana Masters, jamani hizi degree hizi zinakosa pa kwendaga?? Even if he becomes a Professor he will still be a KILAZA. Nsumba Boys aka NYATI BOYS were used to produce such products!! Mr Ezekiel Kibona, wherever he is, he is ashamed of such a NIKAPOOMP PRODUCT

Bi kisura,Wangere hyo ndyo product yenu
 
Madhara ya kutumia mkorogo haya. natamani kuona rangi ya masabuli ya Nape
 
Adai wanaganga njaa kwenye siasa.
> Asema wanalojua ni kung'oa kucha watu.
> Laana ya damu kwenye operesheni zao inawatafuna.
> Wanataka madaraka kwa gharama yeyote.
> Awataka wananchi kuwa macho nao.

Ameyasema hayo kweny mkutano mkubwa hadhara mjini Kilosa

Naona anatekeleza ahadi za ccm kwa wapiga kula,adui ya ccm ni ccm wenyewe!
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)
kimedai kazi ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) ni sawa na makanjanja
wa siasa ambao kazi yao ni kung'oa
kucha za watu na kuwatesa. Kauli
hiyo ilitolewa jana mjini hapa na
Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye,
alipohutubia mamia ya wananchi
wa Wilaya ya Kilosa.
Nape alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku
chache baada ya Chadema
kuituhumu CCM kuwa imekuwa
ikipanga njama za na mipango ya
uaidi kukimaliza katika siasa.
Aliifananisha Chadema kuwa ni
sawa na kikundi cha makanjanja wa
siasa ambao kazi yao ni ya kupanga
mipango nchi isitawalike.
Nape alisema kutokana na mipango
hiyo, CCM imekuwa mstari wa
mbele kuhakikisha nchi inakuwa na
utulivu na amani wakati wote.
"Ndugu zangu kuweni macho a na
chama hiki ambacho kazi yao
imekuwa ni kufanya maandamano
na kuvuruga amani ya nchi eti
isitawalike.
“Nitawahakikishia wananchi wa
Kilosa na taifa letu kwa ujumla
katu mipango yao hii haitafanikiwa
na nchi itaendelea kuwa salama.
“Kwa sasa siasa imeingiliwa na
makanjanja wa siasa ambao kazi
yao kubwa ni kutumia siasa
kuganga njaa zao na bila shaka
wananchi mnawafahamu hawa na
kuweni macho nao," alisema Nape.
Alidai Chadema ilianza kutoa
msimamo wake baada ya Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2010 kwa
kutamaka hadharani kuwa katika
kipindi cha miaka mitano nchi
haitatawalika.
Source. Mtanzania.

Nape ulikuwa kimya juu ya Lwakatare na Mwigulu leo umekuwa shahidi kuwa chadema inatoa watu kucha naona siasa sasa inawashinda.
 
Huwezi amini eti hii thread naiona ni ndefu sana kuisoma hivyo nimeamua kuiacha tu
 
na yeye anaganga nini? kwa hiyo wamewatranfer kina mwigulu, ritz, ighondu kuwa wanachama wa cdm? maana ndio wang'oa kucha na meno tuwajuao
 
Adai wanaganga njaa kwenye siasa.
> Asema wanalojua ni kung'oa kucha watu.
> Laana ya damu kwenye operesheni zao inawatafuna.
> Wanataka madaraka kwa gharama yeyote.
> Awataka wananchi kuwa macho nao.

Ameyasema hayo kweny mkutano mkubwa hadhara mjini Kilosa

Nafikiri Nape kaongea ukweli ila kasau tu kuwa hata CCM waganga njaa ni wengi zaidi. Naamini anajua , na wote tunajua hivyo!! napita tu..
 
Kuna viumbe/vitu visivyokuwa na faida yoyote ile hapa duniani, ni kuondoa tu uchafu kama huu.
 
Back
Top Bottom