Nnauye: Viongozi wengi Chadema wanaganga njaa...

Nnauye: Viongozi wengi Chadema wanaganga njaa...

atatoa hayo majina wakati wenzake wanatekeleza ilani na ahadi walizoahidi....nadhani alichaguliwa kwenda kuwapa watu majina

we ushapokea posho yako tayari???
 
Nape jina jipya ndio maanalizomewa kilosa wewe na kinana aka muuaji wa tembo.ccm haina kazi zaidi ya chadema...mtoe watu kucha na meno msingizie chadema.nyie 2015 hakuna pakutokea..nape siasa huziwezi wewe ni vuvuzela.wananchi tumeamka@
 
Adai wanaganga njaa kwenye siasa.
>. Asema wanalojua ni kung'oa kucha watu.
>. Laana ya damu kwenye operesheni zao inawatafuna.
>. -Wanataka madaraka kwa gharama yeyote.
>.Awataka wananchi kuwa macho nao.

Ameyasema hayo kweny mkutano mkubwa hadhara mjini Kilosa. Hata hivyo nashauri watu wajaribu kumvumilia nape, alifeli sana huyo, 'reasoning capacity is very low, approximately to zero' tunamkuza tunapojadili hoja zake, binafsi siamini kama nape anaweza kuwakilisha nchi kimataifa, huyo ni 'local figures in gutter politics'
 
Kanjanja wasiasa ni wewe nape, pamoja na ccm yako...wewe ni mpuuzi na mbakaji wa siasa...ndio maana mnazomewa na wananchi..kigoma mlizomewa, kilosa. Mkazomewa mapumbavu hayoooo majangili hayooo....mafisadi hayooo.....hamtakaa mumsahau dr wetu slaa alivyowasambaratisha mpaka leo ccm haina wapenzi.pumbavu maccm nyie
 
Huyo ni NAPE aliyesomea NSUMBA akapata English-F, Civics-F form IV leo anawaita CHADEMA Makanjanja? I don't BELIEVE!!!!!!!!!!! Nasikia siku hizi ana Masters, jamani hizi degree hizi zinakosa pa kwendaga?? Even if he becomes a Professor he will still be a KILAZA. Nsumba Boys aka NYATI BOYS were used to produce such products!! Mr Ezekiel Kibona, wherever he is, he is ashamed of such a NIKAPOOMP PRODUCT
 
Pia kusema hivyo ni sawa kwa maana ndiyo ajira yake inayomuweka mjini. Ulitaka aseme CDM inachukua nchi 2015 akose mshahara?

Yeye kama siyo KANJANJA Kwa matokeo yake ya Civics-F, English-F anaweza kufanya kazi gani??????? Inabidi apige domo ili maisha yaende
 
uwe na aibu jukwaani hapa..video ni ya lwakatare ile au hujaiona? Nenda youtube andika lwakatare au bukoba boy

Imekuumae!! Nyie mnatumia ubabe lkn wenzenu tunaongozwa na Mungu alie hai
 
Na Raymond Kaminyoge, Mwananchi | Jumatano, Aprili 17 2013

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye amesema Chadema ni chama kilichovamiwa na watu wanaotumia siasa kuganga njaa.

Nape alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana


"Ndugu zangu kuweni macho kwa sasa, siasa imeingiliwa na watu wasiokuwa na sifa za uongozi na kazi yao kubwa ni kutumia siasa kuganga njaa zao," alisema.

Alisema wananchi wanapaswa kuwa macho na wanasiasa hao ambao malengo yao ni kuwaangamiza wananchi.


Akitaja baadhi ya sifa za wanasiasa aliowaita makanjanja, Nape alisema wengi wao ndiyo wanaotaka madaraka kwa gharama yoyote.

"Moja ya sifa kubwa ya wanasiasa hawa ni pamoja na kutaka madaraka kwa gharama zozote hata ikiwa ni pamoja na kuondoa uhai wa mtu," alisema.


Alisema Chadema wanachojua kwa sasa ni kuwahujumu wale wote wenye mawazo tofauti na yao kwa kuwatesa na hata kupoteza maisha ya wanaowapinga.

"Badala ya kushindana kwa hoja na sera, wanachokijua wao ni kung'oa kucha za wanaowapinga, kuwatesa na wakati mwingine hata kumwaga damu kwenye operesheni zao," alisema.


Alisema kwa kuwa wamekusudia kwa gharama yoyote kushika dola, hawajali damu za Watanzania zinazomwagika ili mradi wanafanikisha wanalolitaka.

Akikumbushia operesheni mbalimbali zilizofanywa na Chadema nchini tangu uchaguzi uishe mwaka 2010, Nape alitoa mifano ya operesheni ya mjini Arusha, Morogoro, Iringa, Singida na kwingine ambako maisha ya baadhi ya Watanzania yalipotea lakini hawakushtuka wala kuwajibika.


"Tunamwamini Mungu hataruhusu damu hizi ziendelee kumwagika kisa wanasiasa makanjanja, pia laana ya damu hizi zilizomwagika zitaviua vyama hivi na nchi yetu itabaki salama," alisema.

Nape alitoa wito kwa wananchi kuwa macho dhidi ya wanasiasa wa namna hiyo.

"Hewa wanayovuta wanasiasa makanjanja ni ya watu wanaowaunga mkono, tunaweza kuamua leo kuwanyima hewa hiyo na huo ndiyo utakuwa mwisho wao," alisema Nape.

 
Nape " Alisema Chadema wanachojua kwa sasa ni kuwahujumu wale wote wenye mawazo tofauti na yao kwa kuwatesa na hata kupoteza maisha ya wanaowapinga"

Kweli anapoongelea hayo... Kwanini Serikali ya CCM haisemi Matokeo ya Mauaji ya Mwandishi wa Habari - MWANGOSI? kama ni CHADEMA? Tupewa Taarifa sio kuelezea kwenye MIKUTANO ya HADHARA; Nadhani hiyo kisheria Haitakiwi

Nape kama angefuata ELIMU yakr tu Sasa hivi angekuwa Sasa hivi ni MGANGA NJAA TU; Ashukuru CCM kumpeleka INDIA na kufeli kwake... ELIMU ya INDIA ni TAKATAKA?
 
Nape kuwa sasa embu itendee haki hiyo nafasi yako...historia itakuhumu vibaya mno..!
 
Adai wanaganga njaa kwenye siasa.
>. Asema wanalojua ni kung'oa kucha watu.
>. Laana ya damu kwenye operesheni zao inawatafuna.
>. -Wanataka madaraka kwa gharama yeyote.
>.Awataka wananchi kuwa macho nao.

Ameyasema hayo kweny mkutano mkubwa hadhara mjini Kilosa
nape bwana, anashirikiana na usalama wa taifa kung'oa kucha watu, halafu anawasingizia chadema! Kweli ccm ni janga kwa taifa letu!
 
QUOTE=Honey K;6152881]Adai wanaganga njaa kwenye siasa.
>. Asema wanalojua ni kung'oa kucha watu.
>. Laana ya damu kwenye operesheni zao inawatafuna.
>. -Wanataka madaraka kwa gharama yeyote.
>.Awataka wananchi kuwa macho nao.

Ameyasema hayo kweny mkutano mkubwa hadhara mjini Kilosa[/QUOTE]

Baada ya kumaliza kutoa hiyo gesi iliyomjaa tumboni, naamini hao wananchi wakayaona maisha bora waliyowaahidi 2010. Ndio aina ya viongozi wanaoitawala hii nchi. Halafu Ziro eti hajui ni kwanini hii nchi ni masikini! Duh!
 
Wewe baba yako ni nani?
Hebu rudi kijijini kwenu kamuangalie unaemuita baba kama mnafanana
Usitake kumuudhi mama yako mzazi bure manake yeye ndio anajua
We unadhani tabia za Mamako ndo tabia za kila Mama wa watu?Mhehe gani bogus hivyo...?U mnyalukwale
 
Kamba ambavyo waungwana hupenda kutumia msemo "kama ni chuzi basi limepata mjambaji", ndivyo ambavyo naweza kushabihisha na msemo wangu wa "kama ni siasa, basi za Tanzania zimepata wabwatukaji"...
Leo hii CCM ni wa kuwanyooshea wapinzani vidole kwa nia ya kuhukumu?
Hivi huyu ndugu Nape kweli anajua Kolimba alichofanywa? Vipi kuhusu Kombe, Kambona n.k?
 
Hivi Napa anapata wapi ujasiri wa kuongea mbele za watu baada ya siku 90 kuisha na hakuna lolote lililofanyika?

Lakini pia, Nape ana maoni gani kuhusu 'matamshi ya Peter Serukamba?
 
Kama yeye alivyokuwa anaganga kipindi kile cha lile jengo pale vijana!!!
 
Back
Top Bottom