NMB/VODA mnatuibia

NMB/VODA mnatuibia

Infopaedia

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
1,231
Reaction score
1,495
NMB/VODA huu wizi mtaacha lini?. Napiga *150*66# ili nipate huduma ya bank mkononi. Naambiwa huduma hii kwa sasa haipatikani, lakini nakuta kiasi cha Tsh 50 mmekata kwenye simu yangu wakati sijapata huduma.

Narudia tena *150*66#. Nafika hatua ya nne kuelekea huduma ninayohitaji, naambiwa 'huduma hii kwa sasa haipatikani'. Naangalia salio, mmekata Tsh 200 kutoka kwenye simu yangu. Huu ni wizi. Kulipia ni sawa, lakini ulipie ukiwa umepata huduma unayokusudia.

Hii ni aibu kwa kaliba yenu na mnaojitanabahisha kufuata sheria za nchi. Mnakera sana.

Naamini ipo siku mtakutana na mwizi mwenzenu, atawaburuza na mtalipa gharama kubwa, iwe ya pesa ama taswira ya kampuni.

Wakatabahu
INFOPAEDIA
 
lakini nakuta kiasi cha Tsh 50
Wengine tunakatwa TZS. 100 kila tukitumia bank USSD, Huwa natuumia hii *150*07#
=
1679207344931.png
 
Makampuni ya wezi hayo na hakuna serikali inachosimamia,si kwenye bando wala kwenye huduma uliyoitaja.

Mamlaka ya usimamizi ipo kimiya ina maana imebariki wizi huu.Hapo huenda kuna mazingira ya rushwa mamlaka inayosimamia inapewa na makampuni ya simu kutuibia wananchi.
 
Kuna hawa CRDB na voda kwa wizi ni balaa wao wanakata 200, ukitaka kufanya muamala upo kati inakuja sms huduma haipatikani kwa sasa hapo ujue umeshakatwa 200 na haijawahi kutokea muamala ukakamilika mara moja lazima ujaribu mara tatu au nne
 
Mkuu huko utaumia sana bila kuanzia mia 5 huwezi kufanikiwa,tumia app ni rahisi tu.

NB:Mitandao yote ya simu mfano mi natumia voda na tiGO Pesa,ukitumia app ni rahisi sana kufanya mambo yako
 
Mtu anayetumia laptop na kuweza kukua bundle kwenye moderm aunganishe kwenye Laptop, huyo anaweza kumiliki smart phone tena nzuri tu
Nafikiri tuwe na tabia ya kushukuru Mungu hata kwa kile kiasi alichotuwezesha
Sina uhakika kama nimekuelewa vizuri. Ila nimeelewa kwamba kwa mtazamo wako, kumiliki simu fulani pia kunaendana na uwezo wa kiuchumi wa muhusika.

Kama ni hivyo, dah!! pole sana. Nachelea kusema ni dhana potofu sana. Wengine hizi simu ni mtindo wa maisha tu. Hazina uhusiano na uchumi.

Mtu anashuka kwenye gari yake ya bei ya juu tu, lakini mkononi kashika tochi yenye simu. Na kuna mtu kula yake ya kuunga-unga lakini anatumia simu janja ya bei ya juu sana. Ndio maisha yetu.
 
Sidhani kama kuna excuse ya maana ya kuyokutumia smart phone kama uchumi unaruhusu,
 
NMB/VODA huu wizi mtaacha lini?. Napiga *150*66# ili nipate huduma ya bank mkononi. Naambiwa huduma hii kwa sasa haipatikani, lakini nakuta kiasi cha Tsh 50 mmekata kwenye simu yangu wakati sijapata huduma.

Narudia tena *150*66#. Nafika hatua ya nne kuelekea huduma ninayohitaji, naambiwa 'huduma hii kwa sasa haipatikani'. Naangalia salio, mmekata Tsh 200 kutoka kwenye simu yangu. Huu ni wizi. Kulipia ni sawa, lakini ulipie ukiwa umepata huduma unayokusudia.

Hii ni aibu kwa kaliba yenu na mnaojitanabahisha kufuata sheria za nchi. Mnakera sana.

Naamini ipo siku mtakutana na mwizi mwenzenu, atawaburuza na mtalipa gharama kubwa, iwe ya pesa ama taswira ya kampuni.

Wakatabahu
INFOPAEDIA
😂🙆
 
Back
Top Bottom