Njoo uone huyu jamaa anavyomzodoa shetani hadharani

Njoo uone huyu jamaa anavyomzodoa shetani hadharani

Kitu kilichoweza kupambana na Mungu na Malaika zake bila kushindwa ndio mkiweze kwa maneno tu?
Acha uongo, ni nani aliyekuambia kiumbe hicho cha hovyo kilipambana na Mungu bila kushindwa?? Kitu kimetupwa chini na sasa kinangojea kutupwa motoni milele, wewe unasema hakikushindwa??
Halafu kumbuka, tunapomkemea shetani tunatumia Jina la Yesu, sio maneno tu. Jina la Yesu ni Jina la Mungu, linalopita majina yote.
 
Mtafute psychiatrist kabla hujaanza kutembea uchi..
Utasubiri sana. Leo shetani na wafuasi wake wamekanyaga mbigili. Hakuna jinsi, lazima tuitangaze kweli nayo kweli itawaweka huru
 
Acha uongo, ni nani aliyekuambia kiumbe hicho cha hovyo kilipambana na Mungu bila kushindwa?? Kitu kimetupwa chini na sasa kinangojea kutupwa motoni milele, wewe unasema hakikushindwa??
Halafu kumbuka, tunapomkemea shetani tunatumia Jina la Yesu, sio maneno tu. Jina la Yesu ni Jina la Mungu, linalopita majina yote.
Imeandikwa alimshinda au alitupwa?
Kitu kinachoweza kupambana Mungu kinakuwaje Cha hovyo?

Yesu sio Mungu na Mungu sio Yesu, ndio maana alisema Mungu wangu Mungu mbona unaniacha Ina maana yupo.
 
Yesu sio Mungu na Mungu sio Yesu, ndio maana alisema Mungu wangu Mungu mbona unaniacha Ina maana yupo.
Hiyo ni mada nyingine nje ya mada hii. Soma kwa makini uzi huu
 
"We shetani, nakuambia bila kupepesa macho, na kila mtu asikie. Wewe ulikuwa malaika mbinguni; uliumbwa ukiwa mzuri na mwenye utukufu. Ukaanza kujiona bora zaidi ya Muumba wako. Ukadhani unaweza kukaa kwenye kiti cha Mungu. Ona kilichokupata. Ulitupwa chini kama takataka! Kiburi chako kilikuangusha, upumbavu wako ulikufanya kuwa wa hovyo.

Wewe ni wa ajabu sana. Una umri mkubwa, lakini huna hekima. Yote unayofanya ni marudio tu ya hila za zamani. Huna jipya!

Yesu alipokuja duniani, ulijiona umeshinda ulipompeleka msalabani, kumbe ulikuwa unajimaliza mwenyewe. Kwa kifo chake na kufufuka kwake, Yesu alikupiga "knock out" na kuzivunja kazi zako zote. Kuanzia siku ile, ikajulikana wazi kuwa wewe si chochote, si lolote.

Unajivuna eti wewe ni simba angurumaye. Lakini ukweli ni kwamba wewe ni simba mwenye meno ya karatasi! Unajua kuunguruma sana, lakini huna meno ya kung’ata. Umejaa kelele tupu. Unawatisha tu wasiomjua Mungu: walevi, wazinzi, waongo na wenye dhambi kama wewe. Lakini sisi tuliookoka tunakutazama na kukucheka.

Kila siku unazunguka huku na kule ukitafuta mtu wa kummeza. Kumbuka siku ile, uliwatuma majambazi wanimalize barabarani. Walikuja kwa njia moja, nikawapiga "fire" kwa Jina la Yesu, wakatawanyika kwa njia saba.

Ukatuma tena wachawi usiku, eti waniangamize. Kwa Jina la Yesu niliwapiga kipigo cha mbwa koko! Wakachoropoka mbio kama paka aliyefukuzwa jikoni kwa kutaka kuiba nyama.

Aibu yako shetani! Hata mtoto mdogo akitaja jina la Yesu, unatetemeka!

Na sasa nakukumbusha hatima yako, kila mtu asikie. Your days are numbered. Mwisho wako tayari umeandikwa: ni kutupwa katika ziwa la moto. Utakaa humo daima na kupata mateso yasiyoisha.

I dare to talk openly: sikuogopi shetani. Yesu alinipa mamlaka ya kuzikanyaga nguvu zako za giza. Kwa Jina la Yesu, nakupinga sasa, nakukemea, natangaza mbele ya kila mmoja kuwa umeshindwa. Wewe ni wa hovyo, nimekuaibisha leo. Nimekuzodoa!

Kwa jina la Yesu Kristo, toka hapa, ondoka!"
Amezodolewa.jpg
 
Hiyo ni mada nyingine nje ya mada hii. Soma kwa makini uzi huu
Kuitwa anaweza kuitwa, je ni kweli?
Jibu ni hapana
 
Ni cha hovyo ndio sababu kinangoja kuchomwa motoni
Dunia Ina miaka 4.5 billion na maisha yana miaka 3.5 billion, modern human ana miaka 200,000.

Huo moto nao ni hadithi za kusadikika tu.
 
Huo ndio uongo wa shetani. Anawachinja watu halafu anawadanganya kwa kuwaambia: "jirani yako ndio mchawi" Matokeo yake watu badala ya kupambana na shetani wanapambana na majirani zao.
Shetani leo nimekuumbua; ukome kuwadanganya watu.
Usiogope hawezi kukufwata wala kukutesa, umemkosea nini mpaka akufanyie hayo yote
Ni Wachawi wanakutesa

Bado upo kwenye tatizo la kushindwa kutofautisha
Lakini pia unasumbuliwa na changamoto ya kutokutumia madaraja/rank/classification unapokuwa ukilinganisha vitu

Tunapokuwa tunazungumzia vitu tunatumia ranks
Kama ni Tembo basi waweke kwenye kundi lao la Tembo

Kama ni Paka weka kundi la Paka
Unachofanya wewe ni kuweka Paka kundi la Tembo ndio maana classification inakataa

Na hiki ndicho tunachoshindwana hapa sio kingine
Wewe unanieleza kuwa mjusi anaweza kumnyonga Simba ndio maana tunabishana

Waone Mashehe wenye elimu ya Majini wakusaidie kutofautisha kati ya Wachawi, Mizimu, Vibwengo na Majini na hawa ndio wanaokusumbua

Fanya hivyo itakusaidia sana
Huna cha kumshawishi Shetani apoteze muda wake kuja kwako kwasababu wewe sio Malaika wala haupo daraja la Malaika ambalo ndio rank yake
Wewe huwezi kukaa daraja la Malaika bali daraja lako ni la binadamu

Angalao ungekuwa Malaika ndipo angekukumbuka au kukuona lakini wewe ni binadamu, daraja lako ni la binadamu na mara nyingi utapambananishwa na binadamu wenzako pamoja na Wanyama
Hakuna atakae kuandalia shindano la mapigano na Malaika kwasababu utashindwa
Lakini ukiandaliwa shindano na binadamu mwenzako unaweza kushinda

Shikilia kanuni yangu ya Ukuu
Siku zote raisi ataweka miadi na raisi mwenzake
Dollar ya Marekani itakaa kwenye kundi la dollar
Euro itakaa kundi la Euro, Tshillings hali kadhalika

Huwezi kuwambia watu kuwa Tshillings au Kshillings ipo kwenye kundi la Dollar au Euro

Nikieleza watu kuwa raisi wa Marekani alifunga safari kuja mtaani kwangu kuzungumza na mimi kwanza kabisa nitatengeneza taswira ya uenda wazimu mbele za watu, watu watasadiki kuwa nasumbuliwa na matumizi ya mihadarati au kichaa
Kwanini watasema hivi ni kwasababu watatumia formula ya Ukuu

Formula ya Ukuu inasema kuwa Tembo atakaa kundi la Tembo wenzake kwasababu wanaendana lakini Tembo hataweza kukaa kundi la Paka kwasababu ya kupishana kwa madaraja

Nazungumza kwa kutumia Ukuu na Madaraja, sizungumzi kama Chiriku mwenye lengo la kusifia

Nakuacha na swali hili naomba unijibu tafadhali

Swali: Je yupo mbuzi aliyewahi kumnyonga Tembo?

Kama yupo basi thibitisha
Kama hayupo toa sababu kwanini haijawezekana mbuzi kumnyonga tembo!

Setfree
 
Ni cha hovyo ndio sababu kinangoja kuchomwa motoni
Setfree kumbuka moto umeandaliwa wewe binadamu kwa lengo la kukuadhibu
Usipende sana kuzungumzia habari za moto kwasababu zinakuhusu
Atakayechomwa moto ni binadamu
Nakushauri habari ya moto uachane nayo kwanzia leo sio nzuri sana lazima utafakari aliyekuandalia moto alichukizwaje na binadamu mpaka akaamua kuandaa adhabu

Huna uhakika wa kusema hutachomwa ndugu yangu moto huo huo unaweza kukurudia wewe kwasababu tayari ni wetu binadamu
Punguza panic za kuwaza Shetani anakutesa, hao ni Wachawi tena hapo mtaani kwenu na mnaonana sana na mnafahamiana wameamua kukuwangia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom