Njoo uone huyu jamaa anavyomzodoa shetani hadharani

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,699
Reaction score
7,418
"We shetani, nakuambia bila kupepesa macho, na kila mtu asikie. Wewe ulikuwa malaika mbinguni; uliumbwa ukiwa mzuri na mwenye utukufu. Ukaanza kujiona bora zaidi ya Muumba wako. Ukadhani unaweza kukaa kwenye kiti cha Mungu. Ona kilichokupata. Ulitupwa chini kama takataka! Kiburi chako kilikuangusha, upumbavu wako ulikufanya kuwa wa hovyo.

Wewe ni wa ajabu sana. Una umri mkubwa, lakini huna hekima. Yote unayofanya ni marudio tu ya hila za zamani. Huna jipya!

Yesu alipokuja duniani, ulijiona umeshinda ulipompeleka msalabani, kumbe ulikuwa unajimaliza mwenyewe. Kwa kifo chake na kufufuka kwake, Yesu alikupiga "knock out" na kuzivunja kazi zako zote. Kuanzia siku ile, ikajulikana wazi kuwa wewe si chochote, si lolote.

Unajivuna eti wewe ni simba angurumaye. Lakini ukweli ni kwamba wewe ni simba mwenye meno ya karatasi! Unajua kuunguruma sana, lakini huna meno ya kung’ata. Umejaa kelele tupu. Unawatisha tu wasiomjua Mungu: walevi, wazinzi, waongo na wenye dhambi kama wewe. Lakini sisi tuliookoka tunakutazama na kukucheka.

Kila siku unazunguka huku na kule ukitafuta mtu wa kummeza. Kumbuka siku ile, uliwatuma majambazi wanimalize barabarani. Walikuja kwa njia moja, nikawapiga "fire" kwa Jina la Yesu, wakatawanyika kwa njia saba.

Ukatuma tena wachawi usiku, eti waniangamize. Kwa Jina la Yesu niliwapiga kipigo cha mbwa koko! Wakachoropoka mbio kama paka aliyefukuzwa jikoni kwa kutaka kuiba nyama.

Aibu yako shetani! Hata mtoto mdogo akitaja jina la Yesu, unatetemeka!

Na sasa nakukumbusha hatima yako, kila mtu asikie. Your days are numbered. Mwisho wako tayari umeandikwa: ni kutupwa katika ziwa la moto. Utakaa humo daima na kupata mateso yasiyoisha.

I dare to talk openly: sikuogopi shetani. Yesu alinipa mamlaka ya kuzikanyaga nguvu zako za giza. Nakukemea, kwa Jina la Yesu Kristo, toka hapa. Natangaza mbele ya kila mmoja kuwa umeshindwa. Wewe ni wa hovyo, nimekuaibisha leo. Nimekuzodoa!"
Amezodolewa.jpg
 
Shetani ameaibika, amezodolewa

Lyrics
Verse 1

Yo devil, you fake, you plastic-teeth pretender
Thought you were tough but the cross was your surrender
You roar like a lion but you just a house cat
Jesus crushed your head, now where you at?
Chorus
Shetani ameaibika, amezodolewa

Jesus is the King, the Lion of Judah yuko juu forever

Verse 2
You tried to tempt the Son but failed miserably
Cross left you broken, defeated completely
I got authority, power in His name
Devil you're finished, put to shame
 
Tafadhali, usipite hapa bila kuacha comment ya kumzodoa shetani.
 
"We shetani, nakuambia bila kupepesa macho, na kila mtu asikie. Wewe ulikuwa malaika mbinguni; uliumbwa ukiwa mzuri na mwenye utukufu. Ukaanza kujiona bora zaidi ya Muumba wako. Ukadhani unaweza kukaa kwenye kiti cha Mungu. Ona kilichokupata. Ulitupwa chini kama takataka! Kiburi chako kilikuangusha, upumbavu wako ulikufanya kuwa wa hovyo.

Wewe ni wa ajabu sana. Una umri mkubwa, lakini huna hekima. Yote unayofanya ni marudio tu ya hila za zamani. Huna jipya!

Yesu alipokuja duniani, ulijiona umeshinda ulipompeleka msalabani, kumbe ulikuwa unajimaliza mwenyewe. Kwa kifo chake na kufufuka kwake, Yesu alikupiga "knock out" na kuzivunja kazi zako zote. Kuanzia siku ile, ikajulikana wazi kuwa wewe si chochote, si lolote.

Unajivuna eti wewe ni simba angurumaye. Lakini ukweli ni kwamba wewe ni simba mwenye meno ya karatasi! Unajua kuunguruma sana, lakini huna meno ya kung’ata. Umejaa kelele tupu. Unawatisha tu wasiomjua Mungu: walevi, wazinzi, waongo na wenye dhambi kama wewe. Lakini sisi tuliookoka tunakutazama na kukucheka.

Kila siku unazunguka huku na kule ukitafuta mtu wa kummeza. Kumbuka siku ile, uliwatuma majambazi wanimalize barabarani. Walikuja kwa njia moja, nikawapiga "fire" kwa Jina la Yesu, wakatawanyika kwa njia saba.

Ukatuma tena wachawi usiku, eti waniangamize. Kwa Jina la Yesu niliwapiga kipigo cha mbwa koko! Wakachoropoka mbio kama paka aliyefukuzwa jikoni kwa kutaka kuiba nyama.

Aibu yako shetani! Hata mtoto mdogo akitaja jina la Yesu, unatetemeka!

Na sasa nakukumbusha hatima yako, kila mtu asikie. Your days are numbered. Mwisho wako tayari umeandikwa: ni kutupwa katika ziwa la moto. Utakaa humo daima na kupata mateso yasiyoisha.

I dare to talk openly: sikuogopi shetani. Yesu alinipa mamlaka ya kuzikanyaga nguvu zako za giza. Kwa Jina la Yesu, nakupinga sasa, nakukemea, natangaza mbele ya kila mmoja kuwa umeshindwa. Wewe ni wa hovyo, nimekuaibisha leo. Nimekuzodoa!

Kwa jina la Yesu Kristo, toka hapa, ondoka!"
Mnatuchanganya 😳
Kuna baadhi ya binadamu huwa wanamzungumzia Shetani kana kwamba wanawazungumzia baba zao vizee vilivyojichokea

Binadamu wote kuanzia wa kwanza mbele za Shetani ni sawa na kuku au mende na ana uwezo wa kufanya lolote na hatuna chakufanya

Kwanza kabisa kabla ya kumzungumzia Shetani tizama

Umri
Uzao
Nguvu
Cheo
Akili
Kifo

Umri
Binadamu wote kwanzia wa kwanza hakuna mwenye umri wake au anayekaribia umri wake
Katika swala la umri inatupasa tuogope kabisa kwasababu ni vigumu kushindana na Mwanajeshi aliyekuzidi umri anayofahamu yeye ni sawa na trillions za siri, sisi hatuna tunachokijua

Uzao
Binadamu wote tunatoka kwenye matumbo ya mama zetu yeye hakuzaliwa
Tuliotoka kwenye tumbo za mama zetu tunathubutu kunyooshea jua kidole lazima litatuchoma

Nguvu
Hakuna binadamu mwenye nguvu yeyote ya kumfanya Shetani angalao tu amtazame, anachokiona yeye mbele zake ni sawa na nzi
Ana uwezo wa kugeuza dunia ikageukia chini bahari ikakaa juu
Wewe binadamu unaweza kufanya hivyo?

Akili
Kamwe hatuwezi kuzungumzia akili za Shetani kwasababu ni za kiwango kisichopimika
Binadamu ndiye mshenzi ana akili za kipuuzi ndiyo maana anaua wenzake kwasababu amejaa mavi akilini
Wajinga kama hawa ndio wanaothubutu kunyooshea Shetani kidole

Cheo
Hakuna mdudu binadamu mwenye Cheo cha Shetani
Yeye anakaa na Mungu meza moja wanazungumza mambo mengi, wewe uliwahi kukaa na Mungu meza moja mkazungumza??

Kifo
Binadamu wote tunazaliwa na kufa huo ndio utaratibu
Yeye alizaliwa wapi na ulishawahi kumsikia amekufa??
Watu ndio wanakufa wanamwacha

Wamekuja mitume wengi, ukianza na Yesu ameondoka kwa kifo, amekuja Mtume Muhammad vivyo hivyo

Kwa haya machache niliyo orodhesha hapa tunapaswa kukimbia na kuogopa kabisa kufanya masihara na Shetani
Yeye ni Tembo siku zote itakayokanyagwa ni nyasi

Unapata wapi kiburi cha kupambana na kitu ambacho wewe ndiye utakayekufa na kubaki mifupa atakayebaki ni yeye???
 
Nipo sina mengi zaidi ya kuwaomba tusipambane na vitu vilivyotuzidi umri tutaumia sisi

Nipo tayari kupigana ngumi na rafiki zangu tuliosoma wote lakini sio kupigana na bahari, nitakayemezwa na maji ni mimi na sio Bahari kumezwa na tumbo langu

Sikuanzisha mada yangu kwa lengo la kusifia lakini nilitizama daraja kwamba tumepishanaje na haya tunayopambana nayo

Umri na mamlaka ni vigezo vya muhimu sana
Setfree
 
"We shetani, nakuambia bila kupepesa macho, na kila mtu asikie. Wewe ulikuwa malaika mbinguni; uliumbwa ukiwa mzuri na mwenye utukufu. Ukaanza kujiona bora zaidi ya Muumba wako. Ukadhani unaweza kukaa kwenye kiti cha Mungu. Ona kilichokupata. Ulitupwa chini kama takataka! Kiburi chako kilikuangusha, upumbavu wako ulikufanya kuwa wa hovyo.

Wewe ni wa ajabu sana. Una umri mkubwa, lakini huna hekima. Yote unayofanya ni marudio tu ya hila za zamani. Huna jipya!

Yesu alipokuja duniani, ulijiona umeshinda ulipompeleka msalabani, kumbe ulikuwa unajimaliza mwenyewe. Kwa kifo chake na kufufuka kwake, Yesu alikupiga "knock out" na kuzivunja kazi zako zote. Kuanzia siku ile, ikajulikana wazi kuwa wewe si chochote, si lolote.

Unajivuna eti wewe ni simba angurumaye. Lakini ukweli ni kwamba wewe ni simba mwenye meno ya karatasi! Unajua kuunguruma sana, lakini huna meno ya kung’ata. Umejaa kelele tupu. Unawatisha tu wasiomjua Mungu: walevi, wazinzi, waongo na wenye dhambi kama wewe. Lakini sisi tuliookoka tunakutazama na kukucheka.

Kila siku unazunguka huku na kule ukitafuta mtu wa kummeza. Kumbuka siku ile, uliwatuma majambazi wanimalize barabarani. Walikuja kwa njia moja, nikawapiga "fire" kwa Jina la Yesu, wakatawanyika kwa njia saba.

Ukatuma tena wachawi usiku, eti waniangamize. Kwa Jina la Yesu niliwapiga kipigo cha mbwa koko! Wakachoropoka mbio kama paka aliyefukuzwa jikoni kwa kutaka kuiba nyama.

Aibu yako shetani! Hata mtoto mdogo akitaja jina la Yesu, unatetemeka!

Na sasa nakukumbusha hatima yako, kila mtu asikie. Your days are numbered. Mwisho wako tayari umeandikwa: ni kutupwa katika ziwa la moto. Utakaa humo daima na kupata mateso yasiyoisha.

I dare to talk openly: sikuogopi shetani. Yesu alinipa mamlaka ya kuzikanyaga nguvu zako za giza. Kwa Jina la Yesu, nakupinga sasa, nakukemea, natangaza mbele ya kila mmoja kuwa umeshindwa. Wewe ni wa hovyo, nimekuaibisha leo. Nimekuzodoa!

Kwa jina la Yesu Kristo, toka hapa, ondoka!"
Ndugu yangu tema mate ukimbie na usigeuke nyuma, hiki unachokidhihaki kikikugeukia utajuta kuzaliwa

Usifanye masihana na haya mambo, ni mazito sana, yamegharimu mabilioni ya watu

Hahaa, nimemeza mate badala ya kutema!
Ndugu yangu Mr Why mbona nimekupa mifano hai jinsi nilivyomsambaratisha shetani na mapepo yake na wachawi wake. Tafadhali soma nyuzi hizi:
Shetani ni mbwa koko. Labda anakutisha wewe kwakuwa hujaokoka. Ukishaokoka, shetani ni kama mende tu. Ukimkemea kwa Jina la Yesu, anaanguka chini, chali
 
Au ulipigana na vibwengo ndugu yangu kwasababu kuna mambo mengi
Kuna mizimu na vibwengo na majini hapa watu wanachanganya sana
Setfree
 
Wachawi, vibwengo, majini na mizimu sio yeye
Hao ni wasaidizi wa shetani. Wanafanya uovu wao kwa nguvu za shetani. Hivyo ukiwashinda wao, umemshinda shetani. By the way, wewe husomi Biblia? Kama unaisoma, hili andiko unalielewaje?
Yak 4:7-10
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.

Wewe unataka mimi nimkimbie shetani wakati yeye ndiye anayepaswa kunikimbia mimi.
 
Safi sana. Naona idadi ya wanaomcheka shetani inazidi kuongezeka. Acha azidi kuaibika
Kuna Wachawi, vibwengo, Mizimu na majini hawa ndio watu wanapambana nao kila siku
Huwa watu wanadhani ni Shetani
Shetani hafuati binadamu
Anaongea na watu wakubwa tu mfano mitume kwasababu ya daraja lake ni kubwa sana hawezi kufwata watu labda mitume
Setfree
 
Hao ni wasaidizi wa shetani. Wanafanya uovu wao kwa nguvu za shetani. Hivyo ukiwashinda wao, umemshinda shetani. By the way, wewe husomi Biblia? Kama unaisoma, hili andiko unalielewaje?
Yak 4:7-10
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.

Wewe unataka mimi nimkimbie shetani wakati yeye ndiye anayepaswa kunikimbia mimi.
Iko hivi sio kwamba ni wasaidizi au labda anawatuma
Hawa mizimu na majini nao wana uroho wa madaraka wanafanya hivyo ili nao waheshimike
Na mara nhingi wanatumia jina lake kuwahadaa watu kwamba wao ndio Shetani lengo lao wapate heshima
Ni sawa na Wachungaji matapeli watakudanganya Mungu amewatuma kwako ila lengo lao wanataka uwaheshimu na uwape fedha zako
Kwahiyo hawa majini na mizimu watakudanganya wao ni Shetani kwasababu wanataka uwaogope Setfree
 
Kuna Wachawi, vibwengo, Mizimu na majini hawa ndio watu wanapambana nao kila siku
Huwa watu wanadhani ni Shetani
Shetani hafuati binadamu
Anaongea na watu wakubwa tu mfano mitume kwasababu ya daraja lake ni kubwa sana hawezi kufwata watu labda mitume
Setfree
Kila mtu awe mdogo awe mkubwa, awe mtume awe layman, maadam amekokoka, amepewa mamlaka ya kumkanyaga shetani (Luka 10:19). Shetani ni muongo, anajimwambafy tu lakini Jina la Yesu likitajwa anatetemeka. Unafikiri hii mada haioni? Anaiona sana tu lakini hana nguvu ya kunizuia kumzodoa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom