Jumong S
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 7,427
- 10,749
Nilitembelea maonesho ya Nane nane last year Arusha. Watu walikuwa wengi kiasi. Nilipofika karibu na banda la Veta walikuja mbele yangu wadada watatu. Walivalia kawaida kidogo. Suruali za wawili hazikuvutia sana kuwaangalia na mmoja alivaa suti kama za mke wa mchungaji.
Yule mwenye suti aliniomba nimuelekeze lilipo banda la Mosanto. Sikua napajua ila nikamwambia akamuulize mlinzi aliyekuwa jirani. Wakati namuelekeza mlinzi alipo na akaridhika nilianza kuondoka. Nilichogundua wale wenzake wawili walikuwa washaondoka. Nikarudia kumwangalia niliyekuwa namuelekeza naye alikuwa keshapotea. Sikujali. Niliendelea na mizunguko. Nikahisi nywele zinanisisimka. Nilipogusa mfuko wangu wa suruali niligundua Samsung yangu haipo na kisimu changu kidogo cha Nokia pia. Nilianza kurudi kuwatafuta sikuwaona. Nikawa nimelizwa tena na wadada!!
Nitarudi kueleza nilivyolizwa PC yangu ya 950E.
Je, wewe uliibiwaje? Tutumie njia gani kujilinda na kuibiwa vifaa hivi vidogo ila ghali sana?
Karibu!