Msichana wa kishua alinifundisha haya kuhusu maisha

Chilojnr

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
302
1,306
KUNA LA KUJIFUNZA HAPA

Nakumbuka siku moja nilipigiwa simu kwenda kumuona jamaa fulani niliyekuwa nataka ashughulikie suala langu la N.G.O ninayotaka kuanzisha.

Jamaa akanipanga niende kuonana naye katika hoteli mpya pale karibu na TRA iliyoitwa Johari Rotana. Nilifika mapema tu, nikakaribishwa na kuanza kumsubiri jamaa huyo ambaye alifika baada ya dakika kadhaa.

Tulianza kuzungumza mambo yetu. Tukiwa katikati ya maongezi, kuna wadada wawili wakaingia. Walikuwa weupe fulani hivi, yaani kwa kuwaangalia tu, nikajiambia hawa kama hawakai Osterbay basi Mbezi Beach kule kwa washua.

Unajua hakuna watu wanaojua wanawake wa uswahilini kama vijana wa uswahili. Hata mwanamke avae mavazi ya Beyonce, bado ukimuona tu unajua yule kama hakai Tandale kwetu, basi Mwanyamala, ama Temeke, Mbagala na sehemu nyingine.

Sasa bwana nikawa napiga stori na mchizi lakini macho yangu hayakuwa yakitulia. Kwenye suala la akinadada huwa macho ya mwanaume hayatulii kabisa, kwanza yanaanzaje kutulia.

Nilimuona mmoja akienda mapokezi, akaongea na dada wa mapokezi na mwingine kubaki kwenye sofa moja kubwa na la kifahari, aliletewa na juisi kama sisi na kuanza kunywa.

Jamaa alikuwa akizungumza lakini aligundua kabisa umakini wangu haukuwa kwake, nilikuwa namwangalia yule aliyebaki kwenye kochi. Alipendeza, alivalia suruali ya jinzi, fulana fulani ya kubana na aliipindisha mikono yake kwa juu na kupiga na miwani.

Kwa chini alivalia raba fulani zilizokuwa na chata ta Nike, aliikunja jinzi yake kwa chini, alipiga na miwani, na nywele zake alizikata kidogo na kuzipaka dawa, yaani kwa muonekano wake tu, nilichanganyikiwa.

“Upo na mimi?” jamaa aliniuliza huku akiniangalia. Nikayarudisha macho kwake, nikaanza kucheka.

Wakati akiniuliza hivyo, yule aliyekwenda mapokezi akamuaga na kuifuata lifti na kumwambia angerudi, hivyo akabaki peke yake. Niliskuti kidogo, nikasema haiwezekani. Ngoja nimfuate nikachonge naye hata kidogo.

“Naomba dakika mbili!” nilimwambia jamaa, akaachia tabasamu na kuniambia okay!

Kuna maisha fulani huwa najifunza sana kupitia wasichana mbalimbali. Nilichojifunza sijui kama nitakuwa natukana lakini wanawake wengi wanaoishi maisha ya uswahilini wanakuwa wanafiki, huwa hawapendi kuzungumza ukweli, yaani unaweza kumfuata na kumwambia akupe namba ya simu, anachokwambia, “Sina simu” na wakati unamuona nayo ama namba “Namba yangu siijui” na wakati anaijua.

Msichana wa uswahilini yupo radhi kukudanganya jina, sijui anahisi unataka kwenda kumroga ama vipi. Sasa bwana kwa huyu manzi nilipomfikia, nikakaa karibu naye na kumwangalia.

Alishtuka, akaniangalia, kwa mbali akatoa tabasamu pana. Harufu ya manukato yake nilikuwa naisikia puani mwangu, ilikuwa ni nzuri na ya ajabu kabisa, naweza kusema sikuwahi kuisikia hapo kabla.

“Naitwa Nyemo!” nilimwambia huku nikimpa mkono.

Unajua kwa nini nilianza kujitambulisha? Nilishamsoma kabisa huyu hakuwa kama wasichana wa mitaani kwetu, halafu kingine kilichonifanya nifanye hivyo ni jinsi filamu zilivyoniharibu. Kwa Wazungu, huwa wanapenda sana kutanguliza jina kabla ya kuzungumza na wewe, unajua kwa nini? Kwa sababu wanahitaji sana kuwa huru kuzungumza na mtu wakati tayari mkifahamiana.

“Naitwa Eliza!” alinijibu na kunipa mkono.

Kuna matukio yakitokea unakuwa kama hujielewi hivi, unaweza kuhisi unaota kwani alionekana kuwa msichana fulani simpo sana, asiyekuwa na presha, hofu wala kujisikia aibu.

Sasa kazi ikabaki kwangu! Nilitakiwa kuzungumza nini hapo, yaani kama akili iliruka kabisa na kusahau kilichokuwa kimenipeleka mahali pale.

“Umependeza sana! Nakufananisha na msichana fulani aitwaye Melanie Shaw,” nilimwambia.

“Nashukuru! Melanie ndiye nani?”

“Humjui?”

“Yeah! Who is she?” (Ndiyo! Ni nani?) aliniuliza.

Kwanza nikaachia kitabasamu kidogo na kumwambia kwamba huyo alikuwa msichana mrembo aliyezungumzwa kwenye kitabu cha One Night With A Billionaire kilichoandikwa na Vicki Lewis Thompson.

Nilimwambia jinsi msichana huyo alivyokuwa na muonekano mzuri, alifanana na yeye na ndiyo maana nilipomuona, sikusita, nikainuka na kumfuata pale na kuanza kuzungumza naye.

“Unasoma sana vitabu?” aliniuliza.

Nilitegemea swali hilo. Wasichana wengi wa maisha fulani wanapenda sana kusoma vitabu vya simulizi vya Kiingereza na si ajabu akakuuliza “Unampenda character wa kitabu gani?” Niliyajua hayo yote na ndiyo maana nikaamua kusoma sana vitabu ili kuepuka maswali kama hayo, ila pia nilijifunza kwa ajili ya kujua mengi.

“Yeah! Huwa nasoma!”

“Okay!”

Alikaa kimya kidogo. Nilimtolea macho, nikaanza kujiuliza nilitakiwa kuzungumza kitu gani. Yaani mapigo ya moyo yalikuwa yakidunda kwa nguvu, wakati mwingine nilihisi kabisa nikiishiwa maneno.

Lakini kumbuka yule mwenzake aliyekuja naye hapo hakuwepo, aliondoka na ilikuwa ni lazima nijue kwamba angerudi muda wowote ule, hivyo kama nilitaka kufanya yangu, nilitakiwa nifanya fasta.

“Nina mengi ya kuzungumza nawe,” nilimwambia, akaniangalia.

“Kama yapi?”

“Mengi yasiyokuwa na idadi, nahisi kama nitafurahi zaidi nikiwa na namba yako!” nilimwambia.

Nilishajua ni msichana wa aina gani. Kule kwetu Tandale ili kupata namba ya msichana wa huko unatakiwa kutumia nguvu kubwa ya kumsifia, kumdanganya sana, saundi nyingi, ila kwa kuwa nilijua nazungumza na msichana wa aina gani, nilitakiwa kupunguza uongo, nisiwe na maneno mengi.

“Namba yangu?”

“Yeah! Nataka niwe nakutafuta, tuwe tunapiga stori, nikiishiwa salio nakutumia meseji unitumie...” nilimwambia.

“Hahaha!” Akaanza kucheka.

Sikutaka kumfanya muda wote awe kauzu tu, ilikuwa ni lazima nimfurahishe kidogo, atabasamu na kucheka kama alivyofanya. Yaani sikuamini, hapohapo akatoa simu yake na kunipa niandike namba yangu.

“Ningependa niwe na yako pia!” nilimwambia.

Unajua kwa nini? Ubongo wangu ushaathiriwa na wasichana wa maeneo yetu, anakupa simu uandike namba yake, halafu hakutafuti, sasa kwa sababu nilikutana na huyu, nikajisahau na kuhisi naye alikuwa kama wale, kumbe haikuwa hivyo.

Nikaiandika, akachukua simu yake na kunibip! Alipomaliza, mara nikamuona mwenzake akitoka kwenye lifti na kumfuata mwenzake pale tulipokuwa, nikasimama na kumsalimia, tukaongea kwa sekunde kadhaa kisha kuaga, hao wakaondoka zao.

“Opsssss....mzee baba si mchezo!” nilimwambia jamaa baada ya kurudi kwenye kiti.

“Mzee umeniacha kabisa hapa!”

“Kaka! Hebu tuendelee kwanza manake daah! Unajua msichana unavyomuona si kama alivyo! Nishazoea wa nyumbani, mambo mengi, kuzungushana sana lakini kwa yule mtoto...daah! Mzee baba ni hatari!” nilimwambia.

Jamaa akacheka na kuendelea. Tulipomaliza, tukaagana na kurudi nyumbani. Sikutaka kuchelewa, nilipokuwa ndani ya daladala tu nikaanza kumchombeza kwa meseji za salamu na mambo mengine.

Ngoja nikatishe nisikuchoshe sana!

Sasa tukazoeana sana, tukawa tunapiga sana stori. Tulikutana, yeye alipenda kusoma vitabu na kuangalia muvi, ni kama mimi tu, tukawa tunakwenda sawa sana.

Aliniambia alikuwa akiishi huko Goba na wazazi wake na alikuwa amemaliza kidato cha sita na alitaka kwenda kujiunga chuo kipindi hicho.

Nilifurahi sana kusikia hivyo! Tukapiga stori na nilipomuuliza kuhusu mitandao ya kijamii, alikuwa na akaunti Twitter tu na si sehemu nyingine. Hukohuko nikamfuata na kumfollow.

Nikaanza kupekua akaunti yake, wakati mwingine watu unaowafollow wanaonyesha wewe ni mtu wa namna gani. Kama umewafollow akina Aisha Msambwanda....Beka Maumbeya...tayari mtu anajua wewe ni mtu wa aina gani.

Yeye aliwafollow watu smart, Obama, Opray Winfrey na watu wengine ambao walinionyesha yeye ni mtu wa namna gani, basi ikawa hivyo.

Sasa nakumbuka baada ya wiki kama mbili hivi akaniambia kulikuwa na sherehe huko kwao na alitamani sana kuniona nikienda huko.

Nilimuuliza watu ambao wangekuwa humo, akanitajia, daah! Watu wote aliowataja walikuwa smart sana, matajiri, watu waliokuwa na nyadhifa fulani, nikasema ningekwenda huko.

“Nivae vipi?” nilimuuliza.

“Simpo tu!”

Daah! Hiyo simpo alimaanisha nini? Anaijua simpo ya Tandale kweli? Nikaona haiwezekani! Nikasema nitanyuka suti moja matata sana.

Unajua kama wanawake wanapicha moja hivi matata, kila mwanaume akiomba basi lazima atatumiwa hiyo, inaitwa The Killing Picture, yaani hiyo ukitumiwa, hutoki.

Sasa hata kwa wanaume ipo hivyo! Atakuwa na nguo hata hamsini lakini atakuwa na moja hiyo, yaani ni hatari, akiambiwa kwenda kwenye sherehe tu, basi ana hiyo. Sasa mimi nilikuwa na suti yangu fulani hivi...nikiivaa hiyo, sharti la kwanza lazima nichukue Uber...huwa sipandi bodaboda.

Sasa siku hiyo nikainyuka, fasta nikaita Uber, ikanichukua na kuanza kwenda huko. Sikuchukua muda mwingi nikafika na kunipokea.

Ilikuwa sherehe ya kumpongeza mzee fulani hivi baada ya kumaliza masomo yake huko Marekani, sasa kulikuwa na watu wachache, kama ishirini na wengine walikuwa vijana wadogo.

Nikwambie kitu kimoja tu! Mahali pale ni mimi peke yangu ndiye niliyevalia suti. Wengine walikuwa simpo sana, vijana wao kama mimi walivalia fulana, majinzi, yaani walionekana kuwa simpo sana.

“Najua hii ni pati kubwa, ya kishua, sasa kwa nini hakuna mtu aliyevalia suti?” nilimuuliza Elizabeth.

“Samahani sikukwambia kwamba watu waliofanikiwa wamekwishavaa kila aina ya mavazi, thamani yao wameitoa kwenye mavazi kwa kipindi kirefu sana. Unaona ile fulana aliyovaa yule jamaa pale pembeni, inauzwa dola hamsini!” aliniambia huku akinionyesha jamaa aliyevalia fulana niliyoiona ya kawaida sana, na kiasi cha pesa alichoniambia kwa sasa ni sawa na shilingi laki na elfu kumi na tano hivi.

“Mh!” niliguna.

“Nyemo!” akaniita, nikamwangalia.

“Mtu asiyefanikiwa anatamani kuwadanganya watu kupitia mavazi yake, anatamani kila mmoja ajue kwamba amefanikiwa kumbe kwenye akaunti yake benki hakuna kitu. Watu wasiokuwa na pesa wanajitahidi kumiliki iPhone, wanahitaji kuwatisha watu kwamba wamefanikiwa lakini si kweli.

“Kuna watu wanahisi kuwa na simu ya bei ni kufanikiwa, mwingine anahisi kuvaa sana ni mafanikio. Hapana! Mafanikio ni kiasi ulichokuwanacho benki. Leo Bill Gates tunasema amefanikiwa kwa kuwa ana pesa nyingi. Kuwa na pesa ni mafanikio makubwa japokuwa pesa hainunui kila kitu!” aliniambia. Akanifikisha sehemu yangu sasa, nikajiweka vizuri.

“Unahisi mafanikio ni pesa tu?” nilimuuliza.

“Naweza kusema ndiyo! Unapokuwa huna pesa, unahisi kudharauliwa, unahisi kutosikilizwa, unahisi kutengwa, unakuwa na moyo wa kuhisi kila mmoja anakudharau tu. Unapokuwa huna pesa unajisikia mnyonge, kutokuwa na pesa kunakufanya ushindwe kujiamini! Unapokuwa huna pesa hata ukiandika vitu vyako mtandaoni, utapenda sana kuwazungumzia watu kwa mabaya tu, ila huwezi kuona mtu mwenye pesa akamzungumzia mwingine kwa mabaya,” aliniambia. Na mimi nikaanza kuvuta picha za masela zangu na watu wengine, kweli bwana! Ukiona mtu ana wivu wa kijinga, anachukia mafanikio ya mwenzake, kiukweli huyo hana pesa, akiwa nazo, kila kitu kinabadilika.

“Matajiri wengi wanakuwa na nguo za aina moja nyingi. Mwangalie kama Mark Zuckerberg, ana fulana fulani anapenda sana kuivaa ya rangi ya kijivu, unahisi anayo hiyo tu? Anazo nyingi za aina hiyo, ila anabadilisha lakini wewe unahisi ameivaa ile ya jana. Au unahisi kwa nini Manji alipokuwa akienda mahakamani alikuwa na nguo ya aina moja? Unahisi ilikuwa ni ileile? Unahisi hakuwa akibadilisha? Alikuwa anabadilisha, ila alibadilisha na kuvaa nguo kama ile ya jana!” aliniambia.

“Mh! Kwa sababu gani?”

“Siku ukiwa na mafanikio utajua kwa sababu gani. Siwezi kukwambia sasa hivi, ukitaka kujua kwa sababu gani, anza kutafuta mafanikio na utajipa jibu hapo baadaye,” alisema huku akiachia tabasamu, akachukua glasi na kupiga cheers.

“Swali la kizushi Eliza!”

“Na nitalijibunkizushi!” alisema...tukacheka.

“Kwa nini haupo Facebook ama Instagram?”

“Hahaha! Kweli la kizushi!”

“Aya lijibu kizushi sasa!”

“Naomba na mimi nikuulize swali?”

“Ila hujajibu langu ujue!”

“Ni kwa sababu jibu la swali langu linaweza kuwa jibu la swali lako!” aliniambia.

“Aya uliza!”

“Kwa nini ibada za Kiswahili zinakuwa ndefu kuliko za Kiingereza?” aliniuliza.

Kwanza nikacheka, swali lake nalo lilikuwa la kizushi, nilichomjibu ni kwa sababu kunakuwa na mambo mengi sana kwenye ibada ya Kiswahili! Yaani matangazo kama yote na mpaka muda wa ibada unakwisha watu hawajamaliza.

“Hivyo ni kama mitandao hii ilivyo! Unapojiunga Facebook ama Instagram unataka kuandika mambo mengi sana. Nyemo, watu waliofanikiwa hawana muda wa kuandika vitu vingi, muda huo unapata wapi? Mtu unaandika kitu kifupi, kinachoeleweka na ndiyo maana watu wengi maarufu hawapo huko, wapo Twitter inayokupa uwanja mdogo wa kuandika maneno yako,” aliniambia.

“Lakini mbona Mo Dewji yupo Instagram?” na mimi niliuliza.

“Alianzia wapi?”

“Twitter!”

“Kumbuka yule ni mfanyabiashara! Ana vitu ambavyo inambidi akutane na maoni ya wateja wake, anamiliki klabu, hiyo klabu ina watu mitaani, ni lazima awe huko kwa lengo la kubadilishana nao mawazo au hata kusikia maoni yao. Wengi wanasema Twitter ngumu kuitumia, ila kwa nini watu wengi waliofanikiwa wanapenda kuitumia kuliko hiyo mingine?” aliniuliza, kidogo nikakaa kimya.

“Labda kwa sababu ya usalama!”

“Yeah! Twitter ni salama zaidi na ndiyo maana inapendwa mno!” aliniambia.

Siku hiyo Elizabeth alinifundisha mambo mengi kuhusu maisha. Nilichogundua sisi masikini huwa tunaishi maisha magumu kwa lengo la kuwafurahisha watu wengine.

Mwingine yupo radhi awe na maumivu moyoni mwake lakini watu wafurahie anavyoishi. Mtu anataka kuonekana kwamba ana pesa kwa kuvaa nguo za gharama na wakati akaunti yake haina hata laki tano.

Tunatumia nguvu nyingi mno kuwafurahisha watu wengine bila kujua ni kwa namna gani tunaumia mioyoni mwetu. Mwingine ananunua viatu vya laki mbili, baada ya siku mbili anakwambia hana pesa yoyote ile, yaani anataka kuwafurahisha watu wengine na wakati muda huohuo nafsi yake inasononeka mno.

Mwingine anakwenda kwenye hoteli kubwa, anapiga picha na kuuonyesha ulimwengu kwamba anaishi maisha fulani kumbe si uhalisia wake, cha ajabu wale wenye pesa wanaishi maisha ya kawaida kabisa.

Inawezekana kwenye ile sherehe watu walikuwa wakinishangaa! Nilitaka kuwaonyesha watu nina maisha fulani kumbe sipo kama nilivyo. Nilikuwa radhi dunia inione nimefanikiwa lakini ukweli ni kwamba sikufanikiwa hata kidogo.

Hayo ni makosa tunayoyafanya sisi masikini. Tunaishi maisha ya watu wengine, ndiyo maana leo unamuona mtu kwenye mitandao, ukikutana naye, unajiuliza mbona yupo hivi? Kwa nini? Yule msichana anayepiga mapicha kwenye mahoteli, mbona analala mahali pale? Ni kwa sababu anaishi maisha ya watu wengine ili kuuonyesha ulimwengu kwamba amefanikiwa lakini si maisha yake halisi.

Elizabeth aliendelea kunifundisha mambo mengi mno. Mpaka siku hiyo narudi nyumbani, nilijifunza mengi kutoka kwake.

Kwa sababu nililipata somo hilo, nikaona si kazi kama na mimi nitaweza kuwaambia wenzangu, tujifunze, somo la Elizabeth liendelee kuishi.

Kamwe usiishi maisha ya watu wengine.

ISHI MAISHA YAKO. DON’T FAKE LIFE.

NYEMO CHILONGANI.
5e1fda130c903d271302a66428e29579.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NYEMO CHILONGANI.View attachment 1364794

Sent using Jamii Forums mobile app

Super. Sana. Danke mkuuu.
 
Kuna demu nilimwomba namba ya simu, akaniomba simu aandike, nikampa kitochi, eti akaghairi kunipa, nilimshangaa sana.
 
Imenigusa hii,Enx Sana nimejifnza kitu pia kutoka kwko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom