dreamchaser94
Member
- Jul 26, 2016
- 32
- 4
Kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kuelekeza dish kwenye satellite, ukiyafuata dakika 10 nyingi unakua umemaliza, mafundi wetu wengi wanafanya kubahatisha kuzungusha dish hadi kuipata satellite. Ngoja nieleze kwa uzoefu wangu nilionao, unaweza tafuta satellite yoyote ile na kwa muda mfupu kama ukifuata taratibu hizi
Hapo ni kwa dar es salaam satellite ya Eutelsat 36B ipo nyuzi 36 mashariki (DSTV wanaporusha matangazo). Pia utaona ukubwa wa dishi linalotakiwa ili kupata signal, mfano hapo ni kuanzia 80cm unaipata vizuri tu. mkono wa kushoto kuna taarifa zaidi muhimu. hizi ni elevation angle 80.8 (hii ni kiasi gani dishi linatakiwa linyanyuke), True azimuth 334.2 (ni uelekeo wa dish) na lnb skew 25.6 (Uelekeo wa lnb). Hivyo vitu vi 4 nilivyobold ndiyo muhimu uvijue ukitaka kutafuta satellite yoyote ile.
- Pata footprint(Eneo lote ambalo mawimbi ya satellite husika yanafika) ya satellite. Kuna Website nyingi na tools zinazowezesha hili kwa mfano kwa kutumia Satbeams - World Of Satellites at your fingertips chagua satellite unayoitaka na utaona footprint yake na taarifa zaidi kama inavyoonekata kenye hii picha
2. Hatua inayofuata ni kufunga dish pole (ule mlingoti wa kuwekea dishi lenyewe). Hakikisha ile mlingoti umesima wima kwa nyuzi 90 (Ni muhimu sana hili) unaweza pima kwa kutumia kipima pembe au pima maji. Angalia hii picha
3. Baada ya hapo ni kuweka dish lako sasa kwa kufuata vipimo ulivyopata hapo juu (Elevation, azimuth na lnb skew). Kuweka elevation angle 80.8 tumia alama zilizowekwa kwenye dishi mfano angalia picha hii hapo kuna kuanzia 0 hadi 90. elevation angle hutofautiana kutokana na satellite unayouitafuta, kwa mfano kwa hiyo ya dstv ni 80.8 na Eutelsat 7 (azam wanaporusha matangazo) ni 51.6 hivyo utakweka hapo kwenya hizo alama za dishi. kama dishi lako halina alama hizo unaweza kutumia kipima pembe kama hicho kenye picha hapo juu.
4. Hatua inayofuata ni kuweka azmuth angle (uelekeo wa dishi kwa kuzungusha kulia au kushoto ukiwa nyuma ya dishi). Kifaa ninachotumika ni compass (dira), hichi kipo hata kwenye smartphone na uelekeze kwenye nyuzi 334.2
5. Katika hatua hii ni kuweka uelekeo wa lnb (Lnb skew angle) ukiangalia pale unapoweka lnb kuna alma pia za kuweka, angalia mfano kwenye picha hii
Ukifuata hatua hizi 5 unapata satellite yoyote unayouitaka ndani ya muda mfupi sana dakika 10 nyingi siyo kubahatisha tu vitu vinaenda kwa vipimo kila kitu kipo kutokana na satellite unayoitaka. satellite zingine signal yake ni weak mfano Nilesat ukisema utafute kwa kuzungusha tu dish kwa kubahatisha unaweza kumaliza siku nzima hujaipata ila ukifuata vipimo vyake unaipata haraka sana.
Unaweza uelewa zaidi kwa kuangalia video hii youtube
View attachment 387957 View attachment 387977 View attachment 387978 View attachment 387981 View attachment 387986
safi xana mkuu