Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,970
- 10,462
Itapendeza sana ndugu. Vifaa vipo kibao tu madukani.elimu bila nyenzo bado haijakamilika... ngoja nitafute kwanza vifaa nikianzia na hizo receiver, lnb nk.
- Nunua dish la ft 6 au ft 8 kwa ajili ya C band, mengi yanauzwa kati ya 200,000 mpaka 300,000 kutegemea uimara wake. Lkn pia unaweza kupata kutoka kwa mafundi wenzako
- Nunua dish la ft 3 kwa ajili ya kujifunzia kufunga chanels za KU band
- Nunua satellite finder, aidha analog ama digital. Analog kwa Kariakoo zinauzwa kati ya 30,000 na 40,000 na digital zinaenda hadi 350,000 (MPEG 4)
- Nunua seti ya spana na bisibisi
- Nunua waya wa coaxial (75 Ohm).