Njoo tujuzane ujuzi wa kutafuta sattelite za chaneli bila kubahatisha

Dola Iddy Wa Chelsea

JF-Expert Member
Sep 26, 2014
2,114
1,485
Habari zenu wakuu ?
Matumaini yangu mpo salama na afya njema!,
Dhumuni la kuanzisha uzi huu ni kushare ujuzi tulio nao ili kuweza kufaidi chaneli za FTA kupitia sattelite mbalimbali,
Tuanze na namna ya kuitafuta sattelite kwa uhakika bila kubahatisha pasipo kutumia satelite finder na makolo kolo kibao,
Ili kufaidi vizuri kazi au jaribio lako unatakiwa uwe na MPEG 4 DIGITAL RECEIVER ,LNB ZA C BAND NA KU BAND , PAMOJA NA DISH KUANZIA CM 60 NA KUENDELEA KWA LNB YA KU NA DISH KUANZIA FUTI 6 ,8 , 10 na kuendelea KWA LNB YA C BAND.
Hakikisha kila kitu kipo sawa na umejiandaa na majaribio bila kukata tamaa,
Tukianza na namna ya kujua ni wapi satelite inapatikana unatakiwa ujiulize ikiwa IS 906 ni nyuzi 64 Mashariki , (EUTELSAT 36 A ) Dstv ni nyuzi 36 mashariki, Nile sat (ZUKU NA STARTIMES) 7 Mashariki na IS 22 ni nyuzi 72.1 mashariki....
Tutaendeleaaa......
 
Hapo ukiwa mtafiti utagundua kuwa kumebe kadiri unapozungusha dishi kulia (ukiwa nyuma ya dishi) ndivyo nyuzi zinavyozidi kupanda na kadri unaporudisha dish kushoto (ukiwa nyuma ya dishi) ndivyo nyuzi zinavyozidi kupungua ,
Ila cha muhimu unapotafuta signal ya satelite yoyote usitegemee uone mafanikio kwa haraka haraka inakubidi usome level ya msitari mwekundu ndo upate uhakika kuwa unachokitafuta utakipata muda sio mrefu ,
Kwa mfano unatafuta satelite ya Intelsat 10 unatakiwa kuvizia mida ya jioni jua linapotaka kuzama lengesha lnb ya kwenye dish iangaliane sambamba na jua halafu anza kuzungusha kurudi kushoto itafika sehemu mritari wa level au strength utakataa kupanda zaidi ya 80% au 81% uzilazimishe anza kupandisha na kushusha im sure lazima msitari wa quality utaonekana tu ,

ANGALIZO.
=>HAKIKISHA LNB UMEIFUNGA IMELENGA KATIKATI YA DISH ,
=>MAHALA ULIPOPWEKA DISH KWA MBELE KUSIWE NA VIZUIZI VINAVYOPUNGUZA AU KUKATA SIGNAL (MITI, UKUTA )
=>HAKIKISHA SEHEMU YA ARDHI UNAYOTAKA KUWEKA DISH IPO SAWIA ,

Bahati njema!
 
kama unataka kusearch satelite bila kubahatisha unatakiwa uwe na satelite finder, unaweza kuhunt satelite bila hata kuliangalia hilo dishi. na kama mfuko wako upo vizuri zipo hadi zenye built in tv na receiver ukienda site unabeba tu satelite finder yako yenye ukubwa kama simu huna haja kuhangaika na tv na decoder.
06%E4%BA%A7%E5%93%81%E4%BB%8B%E7%BB%8D1.jpg
 
bongo zinauzwaje?
 
Mkuu ni vizuri usemavyo ila mimi tatizo langu ni receiver ya strong srt 4922 unaweza ukawa nayo ? Na je inasuport power vu channels.
 
kama unataka kusearch satelite bila kubahatisha unatakiwa uwe na satelite finder, unaweza kuhunt satelite bila hata kuliangalia hilo dishi. na kama mfuko wako upo vizuri zipo hadi zenye built in tv na receiver ukienda site unabeba tu satelite finder yako yenye ukubwa kama simu huna haja kuhangaika na tv na decoder.
06%E4%BA%A7%E5%93%81%E4%BB%8B%E7%BB%8D1.jpg
Kuna app fulani ya android nilionaga some where inadilisha simu yako kuwa kama satellite finder app hii ni nzuri sana nitawapa link hapa mkaijaribu na nitawapa some shots pia ngojeni niwaangalizieni uku
 
hizo app zipo platform zote ila sio nzuri kama satelite finder yenyewe

1. sio accuracy 100%
2. hazina receiver
3. hazina tv
4. hazikuongozi ukizungusha dish etc

mfano angalia hii picha
211840-1318293447352_opt.jpg

hio ni app ya satelite finder ikikuonyesha satelite, itakuchorea tu dot satelite ilipo halafu kazi kwako wewe kulengesha dish kwenye hio satelite. so haijapunguza kazi yote itabidi tu uwe na tv na receiver kuhakiki kama umelengesha vizuri.

angalia tena na picha hii
Digital Satlink WS-9603 Satellite Finder Meter-1-800x600_0.jpg

nimekuekea tena satelite finder simple, hio kila ukizungusha dish inakwambia hapo dish limeelekea wapi, hivyo hupat shida sana, ndio maana nikasema unaweza hunt satelite bila hata kuangalia dish lenyewe. pia signal zinakuwa nzuri ukitumia satelite finder sababu unapata exactly muelekeo wa satelite
 
Asante kwa elimu nzuri naomba kama kuna group la WhatsApp la mambo haya au mambo ya ufundi plz add me 0784815017
 
hizo app zipo platform zote ila sio nzuri kama satelite finder yenyewe

1. sio accuracy 100%
2. hazina receiver
3. hazina tv
4. hazikuongozi ukizungusha dish etc

mfano angalia hii picha
211840-1318293447352_opt.jpg

hio ni app ya satelite finder ikikuonyesha satelite, itakuchorea tu dot satelite ilipo halafu kazi kwako wewe kulengesha dish kwenye hio satelite. so haijapunguza kazi yote itabidi tu uwe na tv na receiver kuhakiki kama umelengesha vizuri.

angalia tena na picha hii
Digital Satlink WS-9603 Satellite Finder Meter-1-800x600_0.jpg

nimekuekea tena satelite finder simple, hio kila ukizungusha dish inakwambia hapo dish limeelekea wapi, hivyo hupat shida sana, ndio maana nikasema unaweza hunt satelite bila hata kuangalia dish lenyewe. pia signal zinakuwa nzuri ukitumia satelite finder sababu unapata exactly muelekeo wa satelite
Ni kweli mkuu hizi apps zinachora kama hapo ulivoonyesha ila satellite finder ndo yenyewe kwa hapo
 
Ki ukweli Mimi finder huwa situmii kabisaaaa,kuliko kutumia finder nafuu nitumie manual tu,ila kifaa ninachokiamini kwa 100% ni spectrum analyzer
 
Kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kuelekeza dish kwenye satellite, ukiyafuata dakika 10 nyingi unakua umemaliza, mafundi wetu wengi wanafanya kubahatisha kuzungusha dish hadi kuipata satellite. Ngoja nieleze kwa uzoefu wangu nilionao, unaweza tafuta satellite yoyote ile na kwa muda mfupu kama ukifuata taratibu hizi
  1. Pata footprint(Eneo lote ambalo mawimbi ya satellite husika yanafika) ya satellite. Kuna Website nyingi na tools zinazowezesha hili kwa mfano kwa kutumia Satbeams - World Of Satellites at your fingertips chagua satellite unayoitaka na utaona footprint yake na taarifa zaidi kama inavyoonekata kenye hii picha
    satellite-png.387957
Hapo ni kwa dar es salaam satellite ya Eutelsat 36B ipo nyuzi 36 mashariki (DSTV wanaporusha matangazo). Pia utaona ukubwa wa dishi linalotakiwa ili kupata signal, mfano hapo ni kuanzia 80cm unaipata vizuri tu. mkono wa kushoto kuna taarifa zaidi muhimu. hizi ni elevation angle 80.8 (hii ni kiasi gani dishi linatakiwa linyanyuke), True azimuth 334.2 (ni uelekeo wa dish) na lnb skew 25.6 (Uelekeo wa lnb). Hivyo vitu vi 4 nilivyobold ndiyo muhimu uvijue ukitaka kutafuta satellite yoyote ile.

2. Hatua inayofuata ni kufunga dish pole (ule mlingoti wa kuwekea dishi lenyewe). Hakikisha ile mlingoti umesima wima kwa nyuzi 90 (Ni muhimu sana hili) unaweza pima kwa kutumia kipima pembe au pima maji. Angalia hii picha
hqdefault-jpg.387977

3. Baada ya hapo ni kuweka dish lako sasa kwa kufuata vipimo ulivyopata hapo juu (Elevation, azimuth na lnb skew). Kuweka elevation angle 80.8 tumia alama zilizowekwa kwenye dishi mfano angalia picha hii hapo kuna kuanzia 0 hadi 90. elevation angle hutofautiana kutokana na satellite unayouitafuta, kwa mfano kwa hiyo ya dstv ni 80.8 na Eutelsat 7 (azam wanaporusha matangazo) ni 51.6 hivyo utakweka hapo kwenya hizo alama za dishi. kama dishi lako halina alama hizo unaweza kutumia kipima pembe kama hicho kenye picha hapo juu.
images-png.387978

adjustment-jpg.387981

4. Hatua inayofuata ni kuweka azmuth angle (uelekeo wa dishi kwa kuzungusha kulia au kushoto ukiwa nyuma ya dishi). Kifaa ninachotumika ni compass (dira), hichi kipo hata kwenye smartphone na uelekeze kwenye nyuzi 334.2

5. Katika hatua hii ni kuweka uelekeo wa lnb (Lnb skew angle) ukiangalia pale unapoweka lnb kuna alma pia za kuweka, angalia mfano kwenye picha hii
lnbf-skewing-angle-check-jpg.387986

Ukifuata hatua hizi 5 unapata satellite yoyote unayouitaka ndani ya muda mfupi sana dakika 10 nyingi siyo kubahatisha tu vitu vinaenda kwa vipimo kila kitu kipo kutokana na satellite unayoitaka. satellite zingine signal yake ni weak mfano Nilesat ukisema utafute kwa kuzungusha tu dish kwa kubahatisha unaweza kumaliza siku nzima hujaipata ila ukifuata vipimo vyake unaipata haraka sana.

Unaweza uelewa zaidi kwa kuangalia video hii youtube

satellite.PNG
hqdefault.jpg
images.png
adjustment.jpg
lnbf-skewing-angle-check.jpg
 
hizo app zipo platform zote ila sio nzuri kama satelite finder yenyewe

1. sio accuracy 100%
2. hazina receiver
3. hazina tv
4. hazikuongozi ukizungusha dish etc

mfano angalia hii picha
211840-1318293447352_opt.jpg

hio ni app ya satelite finder ikikuonyesha satelite, itakuchorea tu dot satelite ilipo halafu kazi kwako wewe kulengesha dish kwenye hio satelite. so haijapunguza kazi yote itabidi tu uwe na tv na receiver kuhakiki kama umelengesha vizuri.

angalia tena na picha hii
Digital Satlink WS-9603 Satellite Finder Meter-1-800x600_0.jpg

nimekuekea tena satelite finder simple, hio kila ukizungusha dish inakwambia hapo dish limeelekea wapi, hivyo hupat shida sana, ndio maana nikasema unaweza hunt satelite bila hata kuangalia dish lenyewe. pia signal zinakuwa nzuri ukitumia satelite finder sababu unapata exactly muelekeo wa satelite
Zinasaidia kwa kiasi fulani ukiangalia hapo kwenye picha kuan taarifa zaidi za elevation, azimuth na lnb skew ambazo ndiyo muhimu sana wakati wa kuelekeza dishi kwenye satellite husika, satfinder hukumika ku fine tune signal to the maximum ila hata bila sat finder ukifuata vipimo unapata faster tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom