OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 4,321
- 10,982
Ukiona mganga yeyote anakufuata akutatulie changamoto yako haijalishi kakufuata pm au ana kwa ana basi jua huyo ni tapeli.waswahili wanasema mwenye shida humfuata mganga. Kama yeye kakufuata basi wewe ndio mganga.
Mganga yeyote anayeweka bango kwenye nguzo ya umeme, kwenye magazeti, kwenye mtandao wa kijamii huyo ni tapeli.
SIFA ZA MGANGA KONKI
Ukifika stendi au kijiji cha mbali ukauliza naulizia kwa flani wakawa wanamjua na kumtambua na kukuelekeza anapoishi hata watoto wadogo wakawa wanamjua basi huyo ni dalili ya kwanza ya mganga konki.
Ukifika kwake ukakuta msululu wa watu au foleni kubwa sana na magali mengi yamepaki nje basi jua huyo ni mganga konki.
Ukienda kwake ukakuta kajenga nyumba nzuri ya kisasa hiyo ni dalili nyingine ya mganga konki.
Ukiwa unaongea nae hakubembelezi anakua kama vile hakuoni huku baadhi ya watu uliowakuta wakimnyenyekea na kujipendekeza kama watoto wadogo huku wengine wakisalimia kwa kupiga magoti tena ni wanaume kabisa basi jua huyo ni mganga konki.
Ukifika kwake ukakuta watu wapo bize na vibeseni huku wengine wakiwa wamevaa boksa tu basi jua huyo ni mganga konki.
Ukimkuta katulia simu yake inaita masaa 24 kwa kupigiwa sana basi jua huyo ni mganga konki.
Ukifika kwake hakuulizi shida yako yeye atapiga ndumba zake akakuambia kilichokuleta basi jua huyo ni mganga konki.
Ukifika kwake ukakuta anawasaidizi wengi basi jua huyo ni mganga konki.
Ongezeeni zingine wakuu mimi nimevhoka kuandika