BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Asilimia 50 ya wakazi 1,200 wa kijiji cha Utiriri kilichopo kata ya Lupanga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wamedaiwa kuwa ni walevi hali ambayo inasababisha watoto wao kukosa lishe bora.
Afisa lishe halmashauri ya wilaya ya Ludewa John Kiusa ametoa taarifa hiyo kwenye kampeni ya lishe wilayani humo ambapo amesema kiwango cha udumavu kwa asilimia 46.2 katika wilaya hiyo na kushika nafasi ya pili kimkoa kunachagizwa na ulevi wa wazazi wengi katika maeneo mbalimbali wakiwemo wa kijiji cha Utiriri.
Mkuu wa mkoa wa Njombe,Anthony Mtaka amesema kutokana na jambo hilo ni lazima afike kwenye vijiji vyote vyenye walevi na kuzungumza nao ili kuwanusuru watoto na udumavu huku mganga mkuu wa mkoa huo Dkt. Juma Mfanga akionya tabia ya ulevi kwani inasababisha watoto wengi kukosa lishe bora.