Njia za kupokea mzigo wako ulionunua kwenye mtandao(ebay,alibaba,amazon)

Mkuu unaagizia wapi naomba kujuzwa pia niko mbeya nmejarbu kuagiza amazon nmeshindwa pia sina visa naomba kujua kuhusu mpesa mastercard

Nenda bank pale ya exim katengeneze card kisha uta ilink kwa amazon ila kwa amazon ili mzigo wako ufike kwetu jisajili na myus
 
Amazon na eBay wanazingua na zile restrictions zao.
Eti hawaship Tz!!!
Ukiona wanaship basi ni zile bidhaa zisizo na gharama au zinazotokea china
Nilijaribu kuwabana sellers wanadai kwamba walipata hasara siku za nyuma Kwa upotevu wa parcel walizotuma Tz, so hata ubembeleze vipi jibu ni kwamba hawaship.
Over

Inawezekana ukiwatumia hawa myus mzigo unakufikia
 
Mizigo yangu miwili ilingia yote DSM tarehe 29/09 na nikapokea mzigo mmoja huku wilayani nilipo tarehe 08/10. Mzigo mwingine mpaka leo sijaupata..
Je ntaulizia wapi taarifa za huu mzigo tofauti na hii posta ya wilayani..? au ni endelee kusubiria kimya kimya tu..
 
Mizigo yangu miwili ilingia yote DSM tarehe 29/09 na nikapokea mzigo mmoja huku wilayani nilipo tarehe 08/10. Mzigo mwingine mpaka leo sijaupata..
Je ntaulizia wapi taarifa za huu mzigo tofauti na hii posta ya wilayani..? au ni endelee kusubiria kimya kimya tu..
Mkuu subiria kimyakimya inanukia kuletwa dah kazi kwelikweli. Mimi nakumbuka kuna mizigo niliagiza toka mwezi wa tatu jana nimepata michache mingine bado,nami nasubiria kimyakimya tu. Ila ninachoshangaa mizigo yote niliyoiagiza mwezi wa nne,tano au sita nimepata. Hii ya mwezi wa tatu ilishaletwa toka mwezi wa nne kwa mujibu wa tracking. Tuendelee kusubiri tu
 
Kuna jamaa wapo pale dar free market wanaitwa “e-shop” wale ni rahisi sana kukuagizia na kukupokelea mzigo wako wanakutumia popote ulipo tz,chochote utakachoagiza uko ebay wanaleta
 
Back
Top Bottom