Njia za kujiepusha na mapenzi haramu

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Mapenzi haramu ni jambo baya kiafya na hata kiimani.

Tukifanya mapenzi kulingana na utaratibu uliowekwa wa kibinadamu basi kuna faida nyingi ikiwemo. Kupata watoto na kujenga familia jambo ambalo ni baraka.

Zipo baadhi ya njia za kujiepusha na mapenzi haramu/mapenzi yanayofanyika pasipo kutumia viungo sahihi vya uzazi
Mfano: kushiriki mapenzi na kitu au vitu, wanyama, kutumia viungo visivyohalalishwa katika mapenzi kama viungo vya uzazi, kwa maana pana kwenda kinyume na taratibu zilizowekwa tangu binadamu anaumbwa

• Pendelea kusoma vitabu vya dini mara kwa mara huu ni msingi imara wa kukuepusha na fikra haramu
• Mwanaume unapobalehe na kufikia umri wa kutungisha mimba basi oa kwa kufuata misingi ya ndoa hii itakuepusha na kujichua na kuchezea sehemu za siri halikadhalika kwa wanawake, na hii ni njia muhimu ya kuikumbusha jinsia kwamba ipo tofauti na mwenzake
• Epuka kutizama sinema za ngono hii inapelekea watu wengi kushiriki mapenzi haramu
• Jishughulishe mara kwa mara kwani itakusaidia kukuweka busy na majukumu vilevile utaweza kupata kipato cha kujikimu, wakati mwingine watu wanaingiliwa kinyume kwasababu za kujipatia kipato

images (15).jpeg

Unaweza ukabalehe mwili ila kiakili haujabalehe bdo..kuoa pnd tu umebalehe ni kama kufanya betting...sidhn kama ni wkt sahihi wa kuoa
 
Unaweza ukabalehe mwili ila kiakili haujabalehe bdo..kuoa pnd tu umebalehe ni kama kufanya betting...sidhn kama ni wkt sahihi wa kuoa
Ni vyema mwanaume kuoa kupitia misingi ya ndoa,
Misingi ya ndoa itamwelekeza namna gani ya kuishi katika ndoa sahihi
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanaume aliyeoa na asiyeoa
 
Ni vyema mwanaume kuoa kupitia misingi ya ndoa,
Misingi ya ndoa itamwelekeza namna gani ya kuishi katika ndoa sahihi
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanaume aliyeoa na asiyeoa
Nafikir hujanielewa...wanaume wanabaleh kweny umri kuanziq 15s..cdhan kwa ww muda huo uliweza kuoa kwan ndo kpnd wengi wetu tupo shulen..saaa cjajua unamaanisha balehe ipi ndugu yangu
 
Unaongelea vijana wa sayari ipi? Mtu anabalehe na miaka 13. Anamaliza form 4 ana miaka 18, form six miaka 21, chuo miaka 27. Huyo mtoto wa miaka 13 anaoa anaishi vipi?
 
Wengne tumebalehe tupo drs la 5, kweli tunaweza kuolewa kwa kipind kile🤔🤔................tuombe tu neema ya Mungu maana hakuna nmna,kuna vtu haviepukiki.
 
Nafikir hujanielewa...wanaume wanabaleh kweny umri kuanziq 15s..cdhan kwa ww muda huo uliweza kuoa kwan ndo kpnd wengi wetu tupo shulen..saaa cjajua unamaanisha balehe ipi ndugu yangu
Sawa, nilitanguliza misingi ya ndoa kwa maana kwamba wakati kijana anajifunza misingi hiyo basi ataweza kufahamu ni umri upi sahihi anapaswa kuchukua uamuzi wa kuoa,
Naweza kusema kuwa sikuambatanisha misingi ya ndoa hii ingefafanua kwa upana zaidi
 
Unaongelea vijana wa sayari ipi? Mtu anabalehe na miaka 13. Anamaliza form 4 ana miaka 18, form six miaka 21, chuo miaka 27. Huyo mtoto wa miaka 13 anaoa anaishi vipi?
Swali lako lina maana kubwa sana, katika swala la kuoa kuna misingi ya ndoa ambayo inatuelekeza umri gani sahihi wa kuoa
Hatuna jinsi ya kushauri vijana wa kiume kuacha kushiriki mapenzi zaidi ya kupendekeza ndoa yenye misingi bora
 
Wengne tumebalehe tupo drs la 5, kweli tunaweza kuolewa kwa kipind kile🤔🤔................tuombe tu neema ya Mungu maana hakuna nmna,kuna vtu haviepukiki.
Kubalehe ikiwa mhusika ana umri mdogo ni vyema kupatiwa semina juu ya madhara ya kushiriki mapenzi akiwa na umri mdogo, na kipindi cha kubalehe kwa vijana wa kike tunashauri wawe karibu na wazazi wa jinsia ya kike ili waweze kueleza changamoto zao kwani ndoa kwa watoto wa kike ni mzigo mkubwa unaoweza kuathiri akili na maisha yao kwa ujumla
 
Back
Top Bottom