Njia ipi ya Mpango wa uzazi ni bora kwa wanandoa?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Kumekuwa na dhana mbalimbali nyingine potofu juu ya njia bora za uzazi. Wengine wanaogopa kutumia kondomu kwa sababu tu zinatumika na vijana wazinifu.

Wengine wanaogopa kutumia vidonge eti vinaongeza makalio au cancer.

Sasa ebu tuambiene kwa wanandoa ipi ni njia bora ambayo haina madhara kiafya wala kimaadili.

1. Kondom
2. Sindano
3. Vidonge
4. Vijiti

Hizo ndio ninazo zifahamu kwa sasa kwa kujisomea kwenye vijitabu.

 
Kalenda ikiwa siku hazivurugiki ni the best sio ya kuiamini pia

Za hospital nyingi kama sio zote zina madhara na zina mtu na mtu

Kuna sa asili kama majivu, mbegu za mnyonyo na kufungia kitambaa

Ukweli hizi zote pia zinasaliti wengi tu

Muhimu na cha msingi tumia unayoona inaendana na wewe wala usifate mkumbo sababu fulani anatumia ngoja na mimi nitumie huwezi jua itareact vipi na mwili wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ