Njama za kuimega Sudan

Njama za kuimega Sudan

What are you trying to say?
My God is Jehova!
:smile-big: Kwa kinywa wasema...
Imani bila matendo...? Simama katika kweli, nadhani Juma amekuelewesha vya kutosha ila kwa kuwa ulishaamini utakavyo ngumu sana kuukubali ukweli ndicho nilichokigundua kwako.:smile-big:
 
Umeshaanza na sentensi zako zisizoeleweka!
Hebu eleza hapo:
1. Imani bila matendo inaingiaje nawe hunijui?
2. Ukweli upi unaouzungumzia?
3. kipi Juma kanielewesha?
 
Mpendatz! uliyozungumza ni propaganda tu tena za kitoto.
Habari za Okech zipo nyingi na huwa zimekusanywa kwa malengo maalum kama hayo ya kuwachochea watu.Wewe mwenyewe hushangai kuwa habari zake zilirekodiwa kikamilifu na kuhifadhiwa hivyo.
Haya mashirikia ya Save the children,Mwezi na misalaba mwekudu moja ya kazi zao ni kuendeleza ukoloni na hayapo kuwasaidia watu.Zaidi ni kuwa mengi yanashiriki kuupiga vita uislamu.Kule afghanistan,Pakistan wanawachukulia kama maadui sawa na majeshi ya America ndio maana mara nyingi hutekwa na hata kuuliwa.
Mwanzoni mwa mchango wako hapo juu umesema
Mimi nadhani katika Afrika kati ya nchi zitakazokua na historia ndefu ya binadamu kumfanyia binadamu mwenzie unyama Sudan Kaskazini inaweza kuongoza. Hiyo hapo chini ni mifano michache tu. Halafu bofya "Lostboys". NATAKA WOTE MKUMBUKE MUNGU IBARIKI TANZANIA! .

Hakuna unyama mbaya wa kumfanyia mwanadamu mwenzako kuliko kumuwinda na hata kumla.Hivyo ndivyo eskimo wa Congo na sehemu nyengine za Afrika wanavyofanywa.Watekelezaji wa hayo ni wazungu na makabila mengine ya kiafrika.Hakuna mwarabu aliyeshiriki.Jee utakubali kuwa unyama haufanywi Sudan ya kaskazini kuliko kusini ya Afrika.
Angalia vipande hapo chini.
1. Besides a small number of so-called "wild" Khomani San Bushmen living their ancestral live as hunters-gatherers, a truly stone-age way of life, to which they have clinged for at least 20 thousand years, this traditional Bushman way of life is now very scarce, and becoming scarcer by the day. The Khomani San Bushmen have maintained their way of life against all odds, and yes, against many dedicated extermination campaigns! For many years the San or Bushmen were actually hunted as wild animals or "vermin"! Possibly by your forefathers or mine. White, Black and Coloured people, both together and separately, were involved in these exterminations, and there is ample historical evidence of this.

2.In South Africa, the Bushmen were hunted and killed by Nguni Tribes moving south in search of new grazing. The Nguni tribes like the Zulu and the Xhosa, originally came from central Africa and are not indigenous to South Africa. The poor Bushmen, used to living by hunting found the Nguni people's cattle very easy to 'hunt' and this obviously upset the Nguni people, and they retaliated by hunting the Bushmen. As the Bushmen fled the advancing Nguni tribes, they met the European trekkers and farmers moving north, also in search of grazing. The Bushmen hunted the European's cattle and oxen which they didn't take lightly either. Bushmen hunting parties were organised. Both the Nguni tribes and the Europeans, did not view the Bushmen as being human beings. They thought they were animals, something like the missing link. This forced the Bushmen to move into and adapt to the dry, more desert-like areas, of Southern Africa.
Ukipenda unaweza ukasoma zaidi hapa.

Mimi ninachotaka ni uweze kupanua wigo wako wa kufikiria kwa mapana zaidi. Hiyo historia ya bushmen mbona umeiamini na mimi unataka nisiamini kitu ambacho wamesimulia wahusika wenyewe? Nimeshasema nimekaa sana Sudan, naielewa sana haswa Darfur. Ninachoongelea nimekiona kwa macho. Nimekihisi ndani ya damu yangu.

Ukizungumzia Western countries kuwa na interests zao, that is true, it has always been like that, hata vita ya Afghanistan walishakaa upande wa Taliban wakiwapa silaha na mafunzo na leo ndiyo hao hao wanawachapa. Na amini usiamini hata huko Darfur wanazo interests kibao. Ile sehemu inasemekana ina Uranium deposits nyingi sana. Kuna mawili kuwa wanaogopa kuwa itatumika vibaya na zaidi kuwapiga, haswa kwa kuona mambo yanayotokea Iran nk. au wanaitaka pia.

Lakini ninachotaka ulelewe ni kuwa sisi tubishe tusibishe watu wa Kusini mwa Sudan wanahamu isiyoelezeka ya kujitenga na Kaskazini. Na katika maongezi yao yote nia yao ni kujiunga na nchi zetu za Afrika Mashariki. Hayo ndiyo maongezi yao halisi ya kila siku. Tatizo kubwa la mawaidha yako ni pale yanapoegemea zaidi mambo ya udini. Mtu ambaye amelewa dini huwa haelewi wala hafikirii mawazo ya mtu mwingine ambaye anawaza bila nia ya kutetea dini yake. Hili ndilo tatizo ninaloliona kwako. Wengi wamajaribu kuchangia kwa kuonyesha kujali zaidi maisha ya binadamu ili kukutoa kwenye hilo pazia au niuite 'ukungu' lakini umeshindwa kutuelewa.

Ninaikumbuka hotuba moja ya Mwalimu aliyosema aliwahi kualikwa kwenye sikukuu ya Wakristo akawaambia Serikali ya Tanzania haina dini, Maaskofu kwenye ile sherehe kusikia hivyo wakahamaki Yesu wangu! Halafu akaalikwa tena kwenye sherehe ya Waislamu nao akawaambia hivyo hivyo napo Mashehe wakaruka Astakafir lah!. Unafikiri alikuwa anafanya utafiti gani hapo? Hapo alikuwa anatuelewesha jinsi ambavyo dini inalewesha haswa pale ambapo haitumiki inavyopasa.

Ukisoma historia ya Elimu ya sayansi ilivyoanza utawaonea huruma wakina Galileo Galilei, walipotangaza kugundua mambo kisayansi walitengwa na kanisa. Waliitwa makafiri wakanyanyaswa sana na jamii yao ya Kikristo. Hilo lilitokea kwa kuwa wakati huo ilikuwa hakuna kingine zaidi ya dini. Watu walitakiwa kuzungumzia mambo ya dini tu kwenye maisha yao. Sasa na leo pia Ami ndiyo unatutaka tuwaze kama wakati wa kina Galileo? Haiwezekani hata chembe! Mtu anatakiwa aibebe Dini yake moyoni mwake, ifungashe ndani ya roho yako ndipo watu wataiona kwa matendo yako yatokanayo na ulicho nacho moyoni mwako. Kinyume chake ni kuuana tuu tukisingizia dini.
Hayo ndiyo mawazo yangu.
 
wewe
:smile-big: Kwa kinywa wasema...
Imani bila matendo...? Simama katika kweli, nadhani Juma amekuelewesha vya kutosha ila kwa kuwa ulishaamini utakavyo ngumu sana kuukubali ukweli ndicho nilichokigundua kwako.:smile-big:
na huyu mnaweza mkaendelea bila ya kumtaja 'Juma' mbona siku nzima mme elewana bana, kwenye mi thread yote mliojibizana acheni zenu.
Umeshaanza na sentensi zako zisizoeleweka!
Hebu eleza hapo:
1. Imani bila matendo inaingiaje nawe hunijui?
2. Ukweli upi unaouzungumzia?
3. kipi Juma kanielewesha?

mimi tena simo humu.
 
Sudan haijauwa watu kama inavyofanya Marekani na umoja wa mataifa ya Ulaya magharibi-NATO.Hawafanyi hivyo kwenye eneo moja tu bali nchi zote za waislamu.Wanavunja miundo mbinu na kuangamiza mazingira.Kwa vile wanaouliwa ni waislamu sijakusikia ukilaumu.

Kwamba raia wa Sudan Kusini wamekufa kwa mamilioni kutokana na vita vya wenye kwa wenyewe, huo ni ukweli ambao hauwezi kupingika. Mimi sijaandika popote wala sijatamka kuwaunga mkono Wamarekani wala watu wa Magharibi kwa ujumla. Katika hili Waafrika tumekuwa na sauti moja. Ndio maana waafrika kwa ujumla wetu tuliungana kupingana na udhalimu wa kikoloni na tukapata uhuru.

Sasa huwezi kuleta hoja kuwa kwa kuwa Marekani ni wababe, basi tusizungumzie udhalimu wa serikali ya Sudani dhidi ya raia wake.

Ukiwapongeza watu wanaojitetea hadhi zao za kibinadamu na kwamba hawawezi kutulia mpaka wahakikishe kuheshimika kwao naamini uko pamoja na mashujaa wa kiislamu wa Iraq,Taliban wa Afghanistan na Hamas wa Palestina.Ikiwa si hivyo basi hujui unachokisema umekuwa kama kasuku tu.Huwezi kuaminika hayo unayoyaeleza kuhusu Sudan.Ni ukasuku tu unaoukufanya uandike.

Mimi nimepost na kujibu kilicho kwenye thread hii uliyoianzisha wewe Ami. Na ya humu yanahusu Sudan. Ningeanza kuzungumzia kuzungumzia kuhusu Iraq, Afghanistan na Palestina ningekuwa nimetoka nje ya mada.

Msimamo wangu ni huu: Popote pale ambapo ubinadamu unadhalilishwa hatuna sababu ya kuunga mkono. Na udhalimu dhidi ya binadamu unafanywa na serikali ya Sudan pia, jambo ambalo ndilo linahusika na thread hii, na hatuwezi kukanusha tu eti kwa kuwa Iraq, Afghanistan na Palestina nao wanaua binadamu.

Naongeza pia kuwa siungi mkono kitendo chochote kinachopelekea kuua raia wasio na hatia wakiwemo akina mama na watoto kwa njia kama za kujilipua au kurusha mabomu sehemu za kiraia (makazi ya watu, shule, hospitali n.k.) kwa kisingizio chochote kile. Kwa hiyo vitendo vya majeshi ya Israel, Wafuasi wa Taliban, Hamas, Al qaeda, Al Shabab, Majeshi ya Marekani na Washirika wake, popote pale wanapoua raia wasio na hatia sikubaliani navyo. No excuse in this. Je Ami unafurahia kujilipua kwa Al qaeda na Al Shabab? Unanitaka niunge mkono hilo?

Katika posts zangu naomba unioneshe mahali popote nilipounga mkono Marekani au nchi za magharibi katika udhalimu wao please. Au kwako nikikosoa Serikali ya Sudani ndio nimeunga mkono Magharibi. Kama unamaanisha hivyo basi kutakuwa na udhaifu mkubwa kwenye logic yako.

Bwana Ami, unaonesha ushabiki wa wazi kwa waarabu. Nami naona kuwa huo ndio ukasuku. Kwamba waarabu hawafanyi udhalimu, hawajawahi kufanya udhalimu na hawawezi kufanya udhalimu. Umewakweza kama malaika vile. Lakini hili si kweli, na hapa ndio iko wazi kuwa uko brain washed. Waarabu nao ni binadamu na kama binadamu wengine wote, nao wana mapungufu yao kama binadamu mmoja mmoja na kama mataifa pia. Tena kuna walio na ukatili uliopea dhidi ya Binadamu, killing in the name of God. Historia pia imetuthibitishia hilo. Mbona hata hapa Kwetu tu Zanzibar ilibidi wazee wetu wachukue mapanga dhidi ya Serikali ya Sultani?

Waafrika tunapaswa kuungana kweli na kukumbatia haki za raia wote. Yeyote anayekiuka haki hizo hata kama ni Mwafrika mwenzetu lazima tumpinge. Vilevile hata kama ni mzungu au Mwarabu, kama ni Mwislamu au Mkristo au mpagani lazima tumpinge pia.

Sumu ya udini inabidi kuiangalia sana. Kutetea matendo ya mtu, kundi la watu au taifa kwa kigezo kuwa ni wa dini yako au kuwapinga kwa kuwa si wa dini yako bila kuangalia zaidi ni upofu mbaya sana. Waarabu na Wazungu wanachekelea wakiona Waafrika tunamezwa na hilo.

Serikali ya Sudan imeshindwa katika kuwathibitishia raia wake kuwa Binadamu wote ni sawa, na kuwa wote wana haki sawa. Sasa serikali hiyo kwa nguvu ya mashujaa wa Sudan Kusini imelazimika kuitisha kura hii ya maoni.

Waache Wasudan waamue mambo yao kwa ajili ya kunusuru heshima ya utu wa Wasudan Kusini.

Kwa heri Bwana Ami.
 
Mimi ninachotaka ni uweze kupanua wigo wako wa kufikiria kwa mapana zaidi. Hiyo historia ya bushmen mbona umeiamini na mimi unataka nisiamini kitu ambacho wamesimulia wahusika wenyewe? Nimeshasema nimekaa sana Sudan, naielewa sana haswa Darfur. Ninachoongelea nimekiona kwa macho. Nimekihisi ndani ya damu yangu.

Ukizungumzia Western countries kuwa na interests zao, that is true, it has always been like that, hata vita ya Afghanistan walishakaa upande wa Taliban wakiwapa silaha na mafunzo na leo ndiyo hao hao wanawachapa. Na amini usiamini hata huko Darfur wanazo interests kibao. Ile sehemu inasemekana ina Uranium deposits nyingi sana. Kuna mawili kuwa wanaogopa kuwa itatumika vibaya na zaidi kuwapiga, haswa kwa kuona mambo yanayotokea Iran nk. au wanaitaka pia.

Lakini ninachotaka ulelewe ni kuwa sisi tubishe tusibishe watu wa Kusini mwa Sudan wanahamu isiyoelezeka ya kujitenga na Kaskazini. Na katika maongezi yao yote nia yao ni kujiunga na nchi zetu za Afrika Mashariki. Hayo ndiyo maongezi yao halisi ya kila siku. Tatizo kubwa la mawaidha yako ni pale yanapoegemea zaidi mambo ya udini. Mtu ambaye amelewa dini huwa haelewi wala hafikirii mawazo ya mtu mwingine ambaye anawaza bila nia ya kutetea dini yake. Hili ndilo tatizo ninaloliona kwako. Wengi wamajaribu kuchangia kwa kuonyesha kujali zaidi maisha ya binadamu ili kukutoa kwenye hilo pazia au niuite 'ukungu' lakini umeshindwa kutuelewa.

Ninaikumbuka hotuba moja ya Mwalimu aliyosema aliwahi kualikwa kwenye sikukuu ya Wakristo akawaambia Serikali ya Tanzania haina dini, Maaskofu kwenye ile sherehe kusikia hivyo wakahamaki Yesu wangu! Halafu akaalikwa tena kwenye sherehe ya Waislamu nao akawaambia hivyo hivyo napo Mashehe wakaruka Astakafir lah!. Unafikiri alikuwa anafanya utafiti gani hapo? Hapo alikuwa anatuelewesha jinsi ambavyo dini inalewesha haswa pale ambapo haitumiki inavyopasa.

Ukisoma historia ya Elimu ya sayansi ilivyoanza utawaonea huruma wakina Galileo Galilei, walipotangaza kugundua mambo kisayansi walitengwa na kanisa. Waliitwa makafiri wakanyanyaswa sana na jamii yao ya Kikristo. Hilo lilitokea kwa kuwa wakati huo ilikuwa hakuna kingine zaidi ya dini. Watu walitakiwa kuzungumzia mambo ya dini tu kwenye maisha yao. Sasa na leo pia Ami ndiyo unatutaka tuwaze kama wakati wa kina Galileo? Haiwezekani hata chembe! Mtu anatakiwa aibebe Dini yake moyoni mwake, ifungashe ndani ya roho yako ndipo watu wataiona kwa matendo yako yatokanayo na ulicho nacho moyoni mwako. Kinyume chake ni kuuana tuu tukisingizia dini.
Hayo ndiyo mawazo yangu.

Ipo sababu ya kutokuiamini hadithi yako ya Ajak Dau Akech.
Sisi katika dini yetu hatuukubali ushahidi wa mtoto mwenye umri kama wa Ajak wa miaka 8.
Mimi binafsi kuna vitu ambavyo nakumbuka niliwahi kusimulia nikiamini ni kweli.Nilisema nimemuona jinamizi nilipokuwa na umri kama huo.Hii ni kwa vile daima tulikuwa tukitishana na wenzangu kuhusu mdudu huyo.Hivi sasa nikikumbuka najuwa sikumuona kweli.
Mtoto mdogo kama yeye anawezaje kutofautisha makabila ya watu kwamba huyu ni mwarabu na huyu ni kabila jengine.Kumbuka rangi za watu na mavazi Sudan haviwezi kutumika kama kigezo cha kumjua mtu kabila lake.Halafu katika hadithi yenyewe kuna ladha kamili ya maneno ya kutiliwa mdomoni mwake na mafisadi wa kizungu wakristo.

Unamkumbuka mwanamke huyo hapo chini?.Huyo ni Ayaan Hirsi Ali ,tapeli aliyewahadaa wazungu wenye kupenda matusi kwa uislamu na akaweza kupata vyeo vikubwa katika serikali ya Nertherlands.Yeye ni mwenye asili ya kisomali.Ili kujipatia faida ya kidunia aliamua kuutukana uislamu kadiri alivyoweza.Wazungu wakamuona mtu wa maana na kumkumbatia.Hatimaye ilipogunduliwa kwamba wamedanganywa bunge na serikali vikavunjika.
Kwa malengo yao na kupenda kuupiga vita uislamu hadithi za Akech huchaguliwa na kutumika muda ukifika kama huu wa kura ya maoni ambayo wao ndio waasisi wake.
Kuna taarifa kwamba shirika la msalaba mwekundu lilisaidia kufanikisha mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwakimbiza wazanzibari wenye asili ya kiarabu huku wenyewe wakidhani wameokolewa na shirika hilo.Hii ndio sababu inayofanya Kiswahili nchini Oman iwe ni lugha ambayo kila unapokwenda utaizungumza.

Kukaa kwako Sudan hakukufanyi ujue kila kitu kinachoendelea humo.
Jiulize CHADEMA ambao ni watu wa humu humu walivyotiwa mkenge na CCM katika uchaguzi uliopita.Kabla uchaguzi haujafanyika walikosa viti na kubaki kuduwaa tu.Wana jamii forums walijitia kujua sana na kutoa takwimu nyingi kumbe nyingi za kudanganyana wenyewe kwa wenyewe.
Maalim Seif ni makamo wa kwanza wa rais huko Zanzibar.Kuna mambo ya uchaguzi yaliyofanyika ndani ya jimbo analoishi na amebaki kushangaa tu,itakuwa wewe mgeni wa kupita huko Darfur?.
Nyerere kama Marekani hawapaswi kufanywa rejea ya jambo lolote la maana.Wameshindwa na kudanganya sana katika uongozi wao.
 
Mwisho wa yote tuwaache watu wa Sudani ya kusini wajichagulie wanachotaka!
Kwa taarifa tu Rais wa Sudani kusini amewasisitiza watu wake wajitokeze kwa wingi. Magari yamekuwa yakipita mitaani kusisitiza hilo
 
Ama kweli kaazi kweli kweli!

Ukiristo kaleta Mzungu, Uislamu kaleta Mwarabu! Wajapani, Thailand, China n.k wamebaki na Imani zao..mnaona walipo sasa?

Ni Africa tu tulikataa imani zetu za jadi..tukaambiwa za Kishenzi na tutakubali!!! Leo hii tunashabikia imani ambazo mara nyingi zimezeta vita na taabu kwa ubaguzi kwa watu badala ya kufanya dunia yetu pawe mahali bora zaidi!

Let us think kwa mapana zaidi Waafrika wenzangu!
 
Perhaps there is some truth kwa yule aliyesema kwamba "religion is the opium of the poor".

kuanzia mwaka 1956 mpaka leo, hakuna kiongozi wa Sudan ambaye amewatendea haki raia wa Sudan kusini..kuanzia kwa Gen. Abood, Nimeir, Al Mahd na Bashiri mwenyewe..wamewanyanyasa sana raia wenzao wa kusini. Jamani kwa kweli nitafurahi sana nikiona Sudan ya kusini inaondoka kivyake kutoka kwenye utawala wa Khartoum. Hapana, lazima tufike mahali tutetee utu wa binadamu mwenzetu especially mwafrika. Hizi dini zisituzibe nyuso na macho.

Huwezi kuwa mkatoliki bora zaidi ya Papa kiongozi wa Vatican.
 
Nadharia yako unayotuletea hapa inafanana kabisaa na huyo mama. Are you related?
 
Halafu waambie hao watu wanaoandamana huko nyumbani eti kupinga Israel ama US kuvamia nchi wa waislamu, waandamane pia Sudan/Janjaweed wanapowaua na kuwabaka wanawake wa kiislamu na wa kiafrika mchana kweupeee kule Darfur. Waache kufuta mkumbo, wanaokufa kule Darfur ni waislamu pia. Ama ndio waarabu wamewabrainwash watanzania na wafrika kiasi hicho?
Bakwata Mnatakiwa muandamane kila Janjaweed wanapowabaka akina mama wa kiislamu kule Darfur na Mauritania. Acheni kufuata mkumbo
 
Nadharia yako unayotuletea hapa inafanana kabisaa na huyo mama. Are you related?
Mimi sina uhusiano na huyu mama
unaposema tunafanana .Fafanua
Usipofanya hivyo nachukulia umeshindwa na hoja za kuendelea na huu mjadala.
 
southern sudan, ..hii inafanana sana na southern korea na northern korea..na historia inaonyesha kuwa, wale wa south ndo huwa wanaendelea kuliko wa north...Mungu bariki hawa watu wang'oke hata kesho....naisubiria hiyo siku.
 
Kwa kweli dini inawapelekea watu wengi kutoona ukweli. kwa dini ya Kiislamu ndio hasa.
Mwaka 2005 wakati wanakubaliana wasudan kusitisha vita na kuweka muda wa kutawala Sudan kusini kabla ya kura ya maoni niliongea na ndugu yangu mmoja kuhusu kujitenga kwa Sudan kusini. Kitu ambacho sikumwelewa ni pale alipotetea dikteta na muuaji Bashir eti anaonewa na nchi za magharibi. Yaani hakuwa na furaha yoyote kwamba waafrika wenzake wamepata uhuru ila alimlilia Bashir eti kwa vile ni Muislamu. Hapa unaweza kukubaliana na watu wengi na wanasaikolojia wanaosema kuwa uislamu is brain washing. Yaani mtu hawezi kuona reality. Wakristo wangekuwa na imani kama hizi za wenzetu hata huo uhuru tusingeupata make tungemwona Mzungu yuko sahihi tu hatakama anatutawala. Kwanini wanafurahia kwisha kwa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini? Hawa ni wanafiki make inamaana ingekuwa Mwarabu ndo alikuwa SA wangesema wanamwona mwarabu mwislamu mwenzetu bora wamwache azidi tu kuwabagua hao wenzetu waafrika. Hawa watu kwa kweli ni wa kuwahurumia sana. Kungekuwepo na hospitali ya kubadilisha ubongo na kuleta mawazo mapya hawa watu wangeombwa kama wanataka kujua ukweli wa mambo wakubali wabadilishiwe hizo bongo zilizochakachuliwa na dini hata kwa muda mfupi tu ili waone tofauti na ukweli ulipo. Utawaonea huruma kwa jinsi wanavojichoma mioyo kwa imani na siasa kali lakini huwezi kuwasaidia make sumu waliyowekewa na dini ni hatari na ni wabishi kuliko jua. Sisi tunabaki tunawaangalia na kuwaonea huruma na hapo ndipo wenyewe wanajisifia wana akili sana na ukweli wanaujua kumbe waungwana hatusemi tu kuwaambia mmekuwa MACHIZI.
 
Mimi sina uhusiano na huyu mama
unaposema tunafanana .Fafanua
Usipofanya hivyo nachukulia umeshindwa na hoja za kuendelea na huu mjadala.
Ami, nadhani hujafahamu maana ya uwepo wa JF ndiyo maana unashindwa kutuelewa. This is where we dare! Hiyo habari ya huyo mama ni yako umependa kuileta hapa japo haina mantiki kabisa kuja hapa, haitabadilisha mawazo ya watu waelewa hapa JF kwamba referendum ya Sudan ni makosa kuwepo. Na ningependa uelewe wazi kuwa ninapojadili jambo hapa sifanyi hivyo kwa ushindi, la hasha ni kutoa mchango wangu wa mawazo. Kama wewe upo kwa ushindi basi nakutangazia "UMESHINDA!!!".
 
Waislamu wanaonewa? Be real!! Huu ni usemi wa Waislamu na ni njia ya kupenetrate kirahisi katika mambo ni kama jinsi ambavyo ukiona mzungu anataka kukuzingua then unamwambia "ARE YOU DOING THIS BECAUSE I AM BLACK?" basi anatia akili ni kiini macho tu lakini issue ya Sudan is about being African, wasikaji hawakujali kama wewe siyo mwarabu hata ukiwa na dini gani.Katika historia ya uislamu, dini ya Kiislamu ni dini ya kwanza kumkubali mtu mweusi kujiunga na kwa kusema wazi (700 AD), So uislamu haubagui lakini "WAARABU WANABAGUA hata hapa BONGO". Ni kama uzushi wanaotuleta wa Ziwa Victoria "HAMURUHUSIWI KUTUMIA MAJI KWA SABABU WAARABU WATAKUFA NA KIU KHARTOUM" WANGUKUWA HUKU NA SISI TUPO KULE WANGESEMA MANENO HAYO? MASHAKA!
 
Ramani ya Sudan. Sehemu ya pink ndio ya Kiarabu. Hayo majina yaliyoandikwa kwa herufi kubwa ni majina ya makabila mbalimbali ya Sudan.
 
Attachments

  • Sudan3.jpg
    Sudan3.jpg
    34 KB · Views: 38
Ama kweli kaazi kweli kweli!

Ukiristo kaleta Mzungu, Uislamu kaleta Mwarabu! Wajapani, Thailand, China n.k wamebaki na Imani zao..mnaona walipo sasa?

Ni Africa tu tulikataa imani zetu za jadi..tukaambiwa za Kishenzi na tutakubali!!! Leo hii tunashabikia imani ambazo mara nyingi zimezeta vita na taabu kwa ubaguzi kwa watu badala ya kufanya dunia yetu pawe mahali bora zaidi!

Let us think kwa mapana zaidi Waafrika wenzangu!

Siyo Kweli. Hizi dini hazikuletwa na Wazungu au Waarabu. Kila taifa limeletewa mitume ktk vipindi tofauti. Wazee wetu Afrika walikuwa wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja kabla ya Waarabu au Wazungu kuja Africa. Wazungu, na Waarabu wenyewe wanasema walipokuja Africa, walikuta tayari watu Waafrika wanaamini Mungu, Heaven, na mitume.
 
Hii article ni moja ya mfano kwamba Wazungu wanataka Sudan igawanyike kwa sababu ya Resources. Hamna sababu kubwa ambayo inaifanya US kushabikia kugawanyika zaidi ya resources. Marekani ni nchi yenye ubaguzi mkubwa juu ya Black American, lakini hatuoni progress yoyote inayofanywa na Marekani ktk kupunguza umaskini wa black American.
Ktk Sudan, US wanataka Oil kutoka Sudan na wanajua China wana dili kubwa sana na hawa Wasudan. Kama mgawanyiko ukiweza kutokea, Marekani itakuwa na nafasi kubwa sana ya kukonctroll oil kutoka South Sudan.
Hivi ni vita vya resources kati ya Marekani na China. Kazi ipo..

Washington (CNN) -- The Obama administration has offered to speed up Sudan's removal from its list of state sponsors of terrorism if the Khartoum government fulfills its obligations under a 2005 peace accord, senior State Department officials confirmed Monday.
Sen. John Kerry, D-Massachusetts, presented the proposal to Sudanese officials during a weekend visit, the officials told reporters on background, meaning the information cannot be attributed to them by name.
The proposal has no impact on Sudanese President Omar al-Bashir's arrest warrant by the International Criminal Court for alleged war crimes and crimes against humanity, the officials said. It also is separate from U.S. sanctions against Sudan over the humanitarian crisis in the Darfur region, they said.
The U.S. proposal to the East African nation called for dropping Sudan from the terrorism sponsor's list in mid-2011 if Bashir's government recognizes the results of the upcoming secession referendum by south Sudan, the State Department officials said.
Sudan was included on the U.S. list in 1993 and has been pushing for years to be removed, the officials said. Prior to the new administration proposal, the earliest possible date for removing Sudan from the list was considered to be the end of 2011 or in 2012, they said.
The referendum, part of a 2005 peace agreement, would allow the autonomous southern region -- which holds a majority of the nation's oil -- to secede from the north. The two-decade conflict led to the deaths of 2 million people, many from starvation.
Kerry said in a statement that President Barack Obama "made clear in the proposal conveyed this weekend that if Sudan's leaders take concrete steps to implement the Comprehensive Peace Agreement, including recognizing the results of the referendum in January, he is prepared to immediately take significant steps to begin to transform the bilateral relationship."
The secession referendum is considered a possible make-or-break event for the peace accord. Observers fear all-out war between the Khartoum-controlled north and southern Sudan if the government is perceived to have undermined the voting or refuses to accept the result.
The Sudanese peace agreement also calls for a separate referendum for residents of Abyei, a border area that has oil reserves, to decide if they want to join the north or south.
According to the State Department officials, the U.S. proposal is intended to encourage Sudan to fulfill its obligations under the peace agreement and therefore has no direct connection to the Darfur sanctions.
"By doing this, we would also be decoupling the state sponsor of terrorism from Darfur and from the Darfur issue," one of the officials said. "But by doing this, we would in no way undermine the importance that we attach to having a resolution of the humanitarian and political problems that have plagued Darfur for the last decade."
Kerry also said the Darfur situation was part of the overall formula for improved relations with Washington.
"I made clear in every meeting that many steps on the road to improved relations could only be taken with real progress in achieving lasting peace and security in Darfur," Kerry's statement said. "The United States stands ready to help, but the choices necessary to move forward ultimately lie with the Sudanese leaders."
Darfur, in western Sudan, has been beset by conflict since 2003 after rebels began an uprising against the Sudanese government.
To counter the rebels, Arab militias with ties to the Sudanese government went from village to village in Darfur, killing, torturing and raping residents there, according to the United Nations, Western governments and human rights organizations. The militias targeted civilian members of tribes from which the rebels drew strength.
The United Nations estimates that 300,000 people have been killed in the conflict in Darfur, and 2.5 million have fled their homes. Sudan denies the death toll is that high.
CNN's Tom Cohen contributed to this story.
 
Back
Top Bottom