Hapo ni Omduruman kaskazini ya Sudan.Wewe kumbe huijui Sudan.Inashangaza sasa unasema deal sio mwafrika na mwarabu.Hebu pitia huu mjadala tangu mwanzo uone.Au tuseme baada ya kuona ukweli ndio umebadili mawazo?.Deal sio nani mwafrika na nani mwarabu. The deal is Southern Sudan wanajitenga mwakani na kuwa nchi huru. Kwa wale wanaowafagilia waarabu inawauma sasa but that is the fact and there is nothing you. Labda mkachakachue kura za maoni. Na hiyo picha na kakudanganya imechukuliwa kaskazini mwa sudan? Usitake kutufanya ka vile sis wajinga.
Sielewi unazungumzia kipengele gani.Pamoja na hivyo naona huna hoja za maana.Hujui maana ya elimu na historia yake.Toa mfano wa elimu za kiumbea umbea ili tukupe facts.Kaka unataka kusema dini yetu ya kiislamu inaruhusu kuwa midlleman katika biashara haramu? Kwa hiyo kaka katika koruani tukufu imeturuhusu kufanya udalali hata wa kuua au hata ya kuuza nguruwe? Tafadhali acha kupakazia dini ya kiislamu.ninyi ndio mnaotuharibia dini yetu.kama huelewi kitu achana nacho, achana na hizo pumba.
Mbona waarabu walileta elimu....sasa wazungu waliwanyimaje elimu waislamu??? Na kama elimu ya kizungu ni ya kibaguzi salaam aleikum
sasa wewe kwa nini unaisoma na unadai umenyimwa..
Ndugu yangu hapa sio league, kitu kinachotfanya waislamu tudharaulike ni kutokuelewa na kutokujifunza na mara nyingi hatuna facts na tunaelimu ya kiumbeaumbea. Samahani kwa waislamu wenzangu ambao tunaangalia mwaswala kwa opande zote.
Tushukuru elimu ya kizungu ndio imetuleta hapa ktk internet.
Masalaamu
sielewi unazungumzia kipengele gani.pamoja na hivyo naona huna hoja za maana.hujui maana ya elimu na historia yake.toa mfano wa elimu za kiumbea umbea ili tukupe facts.
hujui kwamba wazungu unaowaabudu elimu wamepelekewa na waislamu kwa ukarimu na mafunzo yao ya kiislamu.
wazungu waharibifu walillipa fadhila kwa kuchoma moto tafiti za kiislamu.internet unayoiona sasa isingekuwepo kama si waislamu.
tanzania wazungu walipokuja miaka ya karibuni walikuta uislamu umeota mizizi.watu wa mwanzo waliowakuta wakijua kuandika na kusoma ni waislamu.fadhila waliyolipa ni kuwatungia hadithi za uongo na kuzitia midomoni mwa watu kama nyengo.
they did it in Iraq, now they want sudan? Oh hell no! I know there is no more oil in alaska that's why! Say no to Sudan being divided!!Yeah tusisahau historia, during colonialism walitumia method inayoitwa "DIVIDE AND RULE" na wanataka kufanya hivyo Sudan, daima wazungu wanahatarisha amani ya maeneo wenye interest nayo km viongozi husika hawapo upande wao.
" O YOU who have attained to faith! Do not take the Jews and the Christians for your allies: they are but allies of one another and whoever of you allies himself with them becomes, verily, one of them; behold, God does not guide people who are unjust. "
Tatizo ni mitizamo ya wanaJF tunapochangia hoja. Suala la kijamii wanaligeuza kuwa la kisiasa, kidini au vinginevyo ili kukidhi mitazamo yao.
Suala la Sudan kusini ni la kijamii zaidi kuliko la kisiasa na kidini. Pengine, ningeshawishika kama mtu angeliita la ki-ubaguzi wa rangi (apartheid) . Sasa, apartheid inabeba yote niliyoyataja hapo juu. Sudan kusini wanahukumiwa kwa rangi ya ngozi zao, zinawanyima haki ya maendeleo ya aina zote. Stahili yao inabaki kuwa ni mambo duni na pia kuletewa utamaduni (dini, lugha na aina ya maisha) mpya unaodhaniwa kuwa ni wa kistaarabu kupitia nguvu za kisiasa na mabavu (kijeshi). Hayo ndiyo yaliyopo Sudan kusini!
Kwa mtazamo wangu, ni wakati muafaka kwa Sudan kusini kujitawala kama taifa huru linalojitawala na kujiongoza.
Kuhusu kujitenga ikiwa itakuwa kwa hiyari sawa,lakini elewa kuwa watakaojitenga hatimae watajutia uamuzi wao.Fitna itawaandama na watakumbuka umoja wa Sudan.Nyinyi hapa JF udini ndio unaowatesa,munadhani kwamba Sudan ya kusini wengi ni wakristo,sio hivyo.Mlishakaa na wasudan kusini mkawauliza maoni yao? ukweli wanaujua wao na watajitenga! kusini Christians ndo majority, kama hiyo surat aimeida 51: inasema usikae na Yahudi au Mkristo mkamfanya mshirika wenu mnawalazimisha nini wasudani kusini?
Kama ikiwezakana kuigawa Sudan, basi na sisi TZ inabidi tugawane nchi. Waislam wachukue chao, Wakristo wachukue chao. Maanake Waislamu, wanaonewa TZ.
Inawezekana wewe ni mwanachama wa Alshabab wa Somalia, waislamu wepi walio onewa, Zanzibar ina waislamu almost 98% mbona hatuoni maendeleo ya maana huko? Somalia ina mujahidina kibao lakini hakuna cha maana, Comoro je? Ujinga na ufisadi hauna dini. waacheni wasudani kusini wawe na nchi huru wajiletee maendeleo yao.
Sisi waafrika hatuwezi kutawala nchi kubwa, angalia DRC nchi kuubwa mpaka nchi zingine zinaingia kugombania mali lakini rais hachukui hatua! Hata hapa Tanzania baadhi ya viongozi wachovu wanadai nchi kubwa hivyo wanashindwa kupeleka maendeleo kila sehemu! Huu ni ujinga na uchovu wa kujua hasa kipaumbele cha Taifa ni kipi ambacho kitachochea maendeleo katika maeneo mengine!
salaam aleikumsielewi unazungumzia kipengele gani.pamoja na hivyo naona huna hoja za maana.hujui maana ya elimu na historia yake.toa mfano wa elimu za kiumbea umbea ili tukupe facts.
hujui kwamba wazungu unaowaabudu elimu wamepelekewa na waislamu kwa ukarimu na mafunzo yao ya kiislamu.
wazungu waharibifu walillipa fadhila kwa kuchoma moto tafiti za kiislamu.internet unayoiona sasa isingekuwepo kama si waislamu.
tanzania wazungu walipokuja miaka ya karibuni walikuta uislamu umeota mizizi.watu wa mwanzo waliowakuta wakijua kuandika na kusoma ni waislamu.fadhila waliyolipa ni kuwatungia hadithi za uongo na kuzitia midomoni mwa watu kama nyengo.
salaam aleikum
wewe ianaonekana huishi hapa znz na huijui historia ya hawa waarabu jinsi walivyo dhalilisha utu wa mwafrika. Wewe inaonekana unatoka huko bara ambako impact ya waarabu huijui na huenda wewe ni mmoja wa waarabu ambao unatetea uozo ambao mmetunyanyasa mpaka tukapata uhuru wetu kwa njia ya kumwaga damu, kama karume na wengine wasingeweza kuleta uhuru nakwambia mngezidi kututesa. Nyie chama chenu si cuf nyie na tafadhali rudini kwenu uarabuni.
Kitu walichotuletea kizuri ni dini tu ya kiislamu na mengineyo ni takataka.kwanza ni wabaguzi sana hawa waarabu mpaka sasa hivi pamoja na kwamba wako ktk bara la mwafrika.mie sishangai mwarabu kama bashiri anavyowatesa wenzetu waislamu wa darfur na sisi waislamu kama wewe tunashindwa kuliona hilo na badala yake tunawalaaumu mataifa ya magharibi. Na chakushangaza zaidi mbona sisi waislamu hatuandamani kupinga anachofanya bashiri huko darfur? Au damu ya muislamu ikimwagwa na mwislamu ni poa.yaani dini imetufanya tushindwe kuona hata mabaya. Kwa kweli dini ni opium . Jamani tuache kuwa wanafiki tuwe objective.
Masalaam
Kwa sababu wanaosoma huu mjadala ni wengi najibu kupitia kwako lakini sikujibu wewe.Wewe nimeona dalili kuwa huelewi na hueleweki.
Wale waliovamia huu mjadala na kuonesha ujinga na chuki zao walidhani kuwa ikisemwa mwarabu ni mtu aliyevaa kilemba kama Osama au wafalme wa nchi kibaraka za mashariki ya kati.Na hata waislamu pia watu hao hao.Kwa upande mwengine mwafrika ambaye ndiye mkristo ni mtu mweusi mara nyingi huvaa shati suruali na tai na kuchomekea shati lake.
Ukiangalia vitu vilivyowasilishwa kwenye hii mada na ukiingia ndani ya Sudan yenyewe mambo yafuatayo ndivyo utakavyoyaona:
1.Katika jeshi waafrika wanawabaguwa waarabu.
2.Katika bunge waafrika wamewanyima waarabu na waislamu nafasi katika chombo hiki muhimu
3.Mitaa ya kaskazini ya Sudan hakuna waarabu,inakaliwa na waafrika kwa asilimia kubwa.
4.Waarabu na waislamu nchini Sudan ni maskini sana kwana hata mlo wao ni wa tabu kwani ukiingia sokoni hawaonekani.
5.Katika misikiti ya Sudan waarabu hawaendi sana,wanaoingia ni waafrika Zaidi.
Chuki za kidini na kikabila na ubaguzi wa rangi na ujinga kwa ujumla ndio uliomuongoza Nyerere kuongoza mapinduzi ya Zanzibar.Kwa hivyo huko Zanzibar uliko matatizo yaliyopo ujuwe kwamba hayakuletwa na waarabu wala waislamu ,bali ni waafrika na wakristo ndio waliyoyaleta na ndio wanaoyasimamia yaendelee.
Kweli sikio la kufa halisikii dawa...mara kama sio Uislam kusingekuwa na internet..mara Wazungu waliwaibia Waislam elimu yao....My friend try to be smart ishu unayoongelea ni Uislam au Sudan? Mbona haueleweki....au umefanya JF kijiwe cha kahawa?
Haya mambo huwa hayatenganishiki.Mwenye kushangaa kwamba yamechanganyika ni yule ambaye hana cha kuongeza tu, kama wewe.Wenye hoja wamefanya kama ninavyofanya mimi,angalia utaona.
Iwapo una jipya, Sema!.Kinyume cha hivyo kaa chini kama wenzako.
Hebu nieleweshe uhusiano wa kuanzishwa na internet na Uislam. Pia nieleweshe kivipi wazungu waliwaibia Waislam/Waarabu elimu na ilikuwaje Waislam/Waarabu kubaki nyuma kama tunavyoona leo.