Uliiba niniItakua Mungu amenisamehe.
HapanaUliiba nini
Dah! Acha tu! Niliota Nina njaa eti nikapewa. 30,000 niipigie kura ccm, ile nataka tu kutumbukiza kwenye sanduku la kura nikashtuka haraka Sana usingizini, nilikemea Sana ile ndoto
haya matunda hupatikana porini yanakuwa na miba miba sana hata lile tunda lake lina miba juu ila ndani ni matamu sana!!ila kwa njaa iliyotushika ilibidi tuyale tu huko porini ili tusife tukashushia na maji ya barabarani siku ikapita..shida ni haya matunda tuu sijui yana nini cha ziada ukila huku nyuma kunakuwa kwa bariidi km umekalia barafu!!hahaha
Daah pole mkuu ni mapitoMimi muda huu ndio napitia kwenye hiyo hali..
Yaani leo asubuhi nimetoka kwenda kwenye kibarua fulani hv, asubuhi sijapata breakfast!
Nimerudi gheto hapa tangu saa 7 nimekuta jamaa ninaye-share nae gheto hayupo halafu kafungia unga ndani na simu yake haipatikani.
Mara ya mwisho kula ilikuwa jana saa 10 (huwa nakula muda huo tu basi endapo asubuhi nikipata breakfast).
Leo niliacha kupata breakfast kwa vile nilijua nitawahi kurudi kutoka kibaruani.
Maamuzi yaliyonijia ghafla ilikuwa nivunje kibubu changu nachowekaga buku buku zangu ili nipate kwenda kula lakini kwa bahati mbaya nacho kimefungiwa.
Najaribu kujisahaulisha hii njaa kwa kuperuz hapa JF lakn wap!
Bila kibubu leo kufungiwa ningekivunja, SHIKAMOO NJAA!
HahahahSiku moja nikiwa bado kijana wa makamo hivi,usiku ulipofika si nikanunua mihogo ya kukaanga.Bwana we kufika home nikasema nimeshiba,basi chakula wakala na kukimaliza chote kwa maksudi.Kimbembe katikati ya usiku tumbo likaanza kusoma empty empty we nikavumilia we lakini wapi.Nikaona nisije kufa kibudu si nikalia kwa sauti yes ,mom akaja kunigongea mlango na kuniuliza tatizo.Nikamwambia njaaa inauma,
Sasa si akawiata wengine wakaja kunicheka eti dume zima nalia njaa,nikapikiwa chai ya maziwa nikanywa ndo nikalala hivyo.
Kabisa!Aliyesema adui yako muombee njaa wala hakukosea akyanani....
AiseeeDa kuna mapito nilipita mwaka 2018 sitasaha hapo ndio najua rafiki wa kweli mi yupi na mpenzi wa kweli nilipata kesi kazini nikatumia hela yot kusolve kimbembe sasa ni mama yangu mzazi ni mgonjwa kapooza nusu upande ...ili bidi nijifunze kupika maandazi tulawa tunashindia hayo hadi nilipopata muujiza kuna mtu alikosa kutuma hela akatuma kwenye mpesa yangu 280 k faster nikaitoa nikanunua mhitaji ...nikamuahidi kumlipa mwiaho wamwezi mshahara ulivyotoka nikamlipa nusu
Ukaludisha mpira kwa kipaSijawahi kumbwa na njaa ya kutisha. Hapa ghetto wenzangu huwa wanafuja mali hela zinaisha wanashindia mihogo wakitaka niwakopeshe nawajibu ovyo kama "kwani wakati unazitumia na mademu zako hukujua njaa ni ya kila siku". Unakuta mtu katumia 60k juzi alafu leo hana maisha.
Zamu yangu ikafika simu yangu ikapotea, ninajua namba ya mama tu nikapiga kwa simu nyingine hapatikani siku nzima. Asubuhi sijala mpaka usiku kilichofata nilienda hostel usiku kwa ex wangu aniokoe akanipa 20k nikarudi ghetto na fujo kwa wana walionibania. Hiyo njaa ya siku hiyo naipa tuzo