Njaa mbaya sana; Ni jambo gani la hatari uliwahi fanya ulipokumbwa na njaa?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,397
2,000
Njaa inaweza kumfanya mtu afanye jambo la ajabu sana!

Tena usiombe upatwe na njaa ikiwa unga umeisha, mafuta yameisha, gesi imeisha, luku imekata n.k Hakika kuna uchizi huwa unaingia ghafla hata usijue cha kufanya.

Njaa huifanya akili ifanye kazi kwa speed kubwa halafu isipate majibu sahihi!

Njaa huutweza utu!

Njaa inaweza kuifanya akili ikachoka ghafla na kukata tamaa!

Nakumbuka Siku moja nilikuwa sina kitu kabisa, mishe ilikuwa imegoma, njaa ilikuwa inauma balaa, nikapanda daladala nikiwa na mawazo makali hadi nikasinzia kwenye daladala kiasi cha kupitilizwa kituo! Na sikuwa na nauli ya ziada! Nikaamua kuuza saa nikapata 5000 ya nauli na kula!..

Njaa huleta hasira na maamuzi magumu! Njaa huifanya akili Ione kila kitu kitamu hata ukipewa ming'oko utasema keki!

Naomba tuelezane hapa, nikituko gani au jambo gani la hatari uliwahifanya ulipopatwa na njaa wakati huna kitu mfukoni?
 
Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
7,735
2,000
Nilikua na njaa one day. Nikiwa chuo. Nishakopa sana. Nishaomba sana kwa washkaji, wapishi wa cafeteria (ukoko) na kwa wauzaji wa mtaani.

Aisee natembea zangu kwenye floor nikatupia jicho kwenye dustbin, nakuta mtu kala wali kidogo tu katupa upo kwenye vile vi container vya alminium. Bila hiyana nikauchukua hakuna alieniona.

Pia nishawahi msimamisha mtu nikaomba muhindi alikua anakula kwa fun wakati mimi alivonipa aliokoa maisha.

Nishawahi kua natembea jua la Dar nikamkuta baharia mmoja amekaa huku pembeni kuna Uhai maji lita 1. Nikamfuata nikampa Hi, nikasema bro nina kiu sio ya nchi hii. Naomba unisaidie haya maji. Akanipa na jero juu.

Aisee. Si wengine tunawasindikiza watu tu hapa mjini.
 
Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
7,735
2,000
Binafsi me nikiwa sina hela nakua na njaa hatari yani tumbo linatetemeka usipime, ila nipate hela tu hapo hapo njaa inakataa nakuwa sina hamu ya msosi kabisa.

Ila njaa ina sababisha mtu afanye jambo lolote lile imradi tu apate chochote.
We utakua unaongelea kuskip msosi mmoja. Hapa tunaongelea njaa juzi ulikula chai na maandazi mawili tu, jana uji tu, leo hadi sasa bila bila.

Tumbo lishaachana na kuunguruma wala nn. Sasa kinauma kichwa.
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,260
2,000
Sijawahi kumbwa na njaa ya kutisha. Hapa ghetto wenzangu huwa wanafuja mali hela zinaisha wanashindia mihogo wakitaka niwakopeshe nawajibu ovyo kama "kwani wakati unazitumia na mademu zako hukujua njaa ni ya kila siku". Unakuta mtu katumia 60k juzi alafu leo hana maisha.

Zamu yangu ikafika simu yangu ikapotea, ninajua namba ya mama tu nikapiga kwa simu nyingine hapatikani siku nzima. Asubuhi sijala mpaka usiku kilichofata nilienda hostel usiku kwa ex wangu aniokoe akanipa 20k nikarudi ghetto na fujo kwa wana walionibania. Hiyo njaa ya siku hiyo naipa tuzo
 
dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,397
2,000
Nilikua na njaa one day. Nikiwa chuo. Nishakopa sana. Nishaomba sana kwa washkaji, wapishi wa cafeteria (ukoko) na kwa wauzaji wa mtaani.

Aisee natembea zangu kwenye floor nikatupia jicho kwenye dustbin, nakuta mtu kala wali kidogo tu katupa upo kwenye vile vi container vya alminium. Bila hiyana nikauchukua hakuna alieniona.

Pia nishawahi msimamisha mtu nikaomba muhindi alikua anakula kwa fun wakati mimi alivonipa aliokoa maisha.

Nishawahi kua natembea jua la Dar nikamkuta baharia mmoja amekaa huku pembeni kuna Uhai maji lita 1. Nikamfuata nikampa Hi, nikasema bro nina kiu sio ya nchi hii. Naomba unisaidie haya maji. Akanipa na jero juu.

Aisee. Si wengine tunawasindikiza watu tu hapa mjini.
Hatari tupu
 
Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,581
2,000
Njaa inaweza kumfanya mtu afanye jambo la ajabu sana!

Tena usiombe upatwe na njaa ikiwa unga umeisha, mafuta yameisha, gesi imeisha, luku imekata n.k Hakika kuna uchizi huwa unaingia ghafla hata usijue cha kufanya.

Njaa huifanya akili ifanye kazi kwa speed kubwa halafu isipate majibu sahihi!

Njaa huutweza utu!

Njaa inaweza kuifanya akili ikachoka ghafla na kukata tamaa!

Nakumbuka Siku moja nilikuwa sina kitu kabisa, mishe ilikuwa imegoma, njaa ilikuwa inauma balaa, nikapanda daladala nikiwa na mawazo makali hadi nikasinzia kwenye daladala kiasi cha kupitilizwa kituo! Na sikuwa na nauli ya ziada! Nikaamua kuuza saa nikapata 5000 ya nauli na kula!..

Njaa huleta hasira na maamuzi magumu! Njaa huifanya akili Ione kila kitu kitamu hata ukipewa ming'oko utasema keki!

Naomba tuelezane hapa, nikituko gani au jambo gani la hatari uliwahifanya ulipopatwa na njaa wakati huna kitu mfukoni?
Dah! Acha tu! Niliota Nina njaa eti nikapewa. 30,000 niipigie kura ccm, ile nataka tu kutumbukiza kwenye sanduku la kura nikashtuka haraka Sana usingizini, nilikemea Sana ile ndoto
 
adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
6,169
2,000
Ndo yapi hayo mkuu
haya matunda hupatikana porini yanakuwa na miba miba sana hata lile tunda lake lina miba juu ila ndani ni matamu sana!!ila kwa njaa iliyotushika ilibidi tuyale tu huko porini ili tusife tukashushia na maji ya barabarani siku ikapita..shida ni haya matunda tuu sijui yana nini cha ziada ukila huku nyuma kunakuwa kwa bariidi km umekalia barafu!!hahaha
 
Yanapoza kama rejeta!!!! Ndiyo maana nyani weusi matakoni huenda sababu ni hayo matunda
 
Kimwakaleli

JF-Expert Member
Apr 16, 2018
1,502
2,000
Tulienda na jamaa yangu nchini Malawi kuuza viazi,vikadunda,njaa ilitukomesha balaa!,ilifika Jumamosi tukazama kanisa la wasabato hana lugha ya kwao kinyanza hatukijui,Mchungaji wao akatukaribisha chakula cha mchana,tuligonga msosi na kuzinzia hapohapo,duuh njaa mbaya sana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom