KWELI Njaa husababisha hasira kwa baadhi ya watu

KWELI Njaa husababisha hasira kwa baadhi ya watu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kichwa kinajieleza nijuzeni hili kwa Mwenye
Kujua,

Kwa nini mtu akiwa na njaa anakua na hasira za karibu sana...?

Nawasilisha..!
1786543137999.jpeg
 
Tunachokijua
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia makala za kitabibu na tafiti za afya imebaini kuwa kuna watu wanaopata hasira kutokana na njaa. Yaani kuna uhusiano kati ya njaa na hasira kwa baadhi ya watu ama kwa wanyama wengine pia.

Dkt. Christine Lee kupitia makala iliyochapishwa na clever land anaeleza kuwa watu hupata hasira wakiwa na njaa kwa sababu, ukiwa katika hali hiyo damu hupungukiwa na sukari na hivyo kuzalisha baadhi ya homoni ili kuweka sawa kiwango cha sukari.

Homoni zinazozalishwa mtu akiwa na njaa na upungufu wa sukari kwenye damu, ni homoni ya coristol na adrenaline ambapo homoni hizi licha ya kuwa na jukumu la kuweka sawa kiwango cha sukari lakini pia zinaweza kuathiri hisia na kupelekea hasira kwa baadhi ya watu.

Similar Discussions

Back
Top Bottom