Hasira hasara

Hasira hasara

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
5,058
Reaction score
11,926
Hasira. Kuna maana nyingi ya neno hasira na mojawapo ni Ile inayoeleza kuwa ni hali ya moyo wa mtu ulioumia au kujeruhiwa,hivyo huweza kusababisha hasira.

Inakuja pale mtu anapohisi amedhalilishwa, amedanganywa, amenyang’anywa haki, au mtu kavunja ahadi yake.

Ni kitu fulani kinacholeta utambuzi kuwa "hapa nimefanyiwa kitu kibaya".

Shida inaanza pale hasira ikikataa kutoka moyoni Wiki, Miezi, Hadi Miaka. Ndipo inapoacha kuwa hasira inageuka kuwa mzigo.

Hasara pia ni kila kitu unachopoteza ukiwa umebeba huo mzigo. Unapoteza amani yako, usingizi wako, afya yako, fursa zako, na hata watu wazuri walio kukaribu nawe leo.

Kwa lugha nyepesi Hasira ukiibeba muda mrefu, inageuka kuwa hasara.

Madhara ya Kuiweka moyoni Muda Mrefu

1. Unajiumiza Mwenyewe

Yule aliyekukosea anaweza kusahau. Wewe bado unachemka. Presha inapanda. Kichwa kinauma. Unafikiri unamlipiza, kumbe unajihukumu wewe mwenyewe kila siku.

2. Unajifungia Milango
Mtu mwenye hasira haamini mtu mpya. Fursa mpya ikipita, haioni. Kwa sababu moyo uko kwenye jeraha la zamani.
Unakuwa umeamua kuishi jana ndani ya leo. Unacheka kwa mdomo, lakini moyo haupo hapo. Hiyo ni hasara kubwa sana.

Ushauri: Acha hasira Kwa Ajili Yako.

1. Kubali halafu achilia.
Sema "Nimeumia. Ni kweli". Baada ya hapo jiulize: "Kubeba hii leo kunanisaidia nini?" Ukiona ni hasara tu, achana nayo

2. Zungumza.

Mweleze rafiki 1 unayemwamini. Au andika kwenye daftari. Hasira ukiitoa unasahau.

3. Samehe
Huwasamehe kwa sababu wanastahili. Unasamehe kwa sababu wewe unastahili usingizi mzuri. Unastahili kuishi bila mnyororo.

Neno la Mwisho
Hasira ni hasara kubwa.
 
Screenshot_20260630-231012.png
 
Lakini pia mwanadamu furaha yake ni kulipa kisasi, ukimkosea anaweza kuonyesha kukusamehe na kusema nimesamehe na kusahu ila moyo wake hautapata utulivu hadi ulipwe, hata kama hata kulipa yeye ila siku nawe ukipata maumivu ndio msahamaha wake unatimia kwako , hii ni asili na hamna asie kuwa hivi miongoni mwetu
 
Msamaha sio rahisi kama unavyo hubiriwa na watu wa dini ama motivational speaker.......... msamaha unahitaji aliyekosewa aone sasa inahitaji niachilie ama nilipe kisasi ama wacha KARMA ichukue mkondo wake,,

Mioyo imeumizwa, kujeruhiwa, kulia kukosa matumaini na hata kupoteza Uaminifu na kuona haina maana ya kuwa na ndugu, familia mahusiano, kazi na marafiki

NB IKUMBUKWE SINA CHUKI HASIRA WALA HASARA NA MTU ILA NITAISHI KWENYE KULIPA KISASI NI SUALA LA MUDA TUU SITOJIVIKA VAZI LA UNAFIKI WALA KUKUMBATIA MZINGA WA NYUKI HUKU NAUMWA NA NYUKI HAO

NIRUDIA NITAISHI KWENYE KULIPA KISASI CHA YALE YALIYOFANYWA NA KUTOKEA NI SUALA LA MUDA TUU

VITA WALIYOANZISHA ITAISHI NA KUENDELEA KUDUMU.........
 
Ukweli ni mzuri sana.
 
Back
Top Bottom