Niwaulize watu wa Arusha, mnataka mageuzi gani?

Niwaulize watu wa Arusha, mnataka mageuzi gani?

RingaRinga

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2015
Posts
1,052
Reaction score
529
Kwamba labda mnataka kwa kuwa Magufuli amekuwa raisi awashitaki na kuwafunga watu fulani wenye kutuhumiwa kwa makosa yaliyoyumbisha taifa, (watajeni)
-labda mnataka watu fulani wafukuzwe chamani (watajeni)
-labda seraikari ifanye abc.. (taja)
-labda chama kifanye abc... (taja)

Kisaidieni CCM kufahamu haja ya mioyo yenu ili kipate wachumba (wabunge na madiiwani) wawili/watatu kutoka Arusha na Kilimanjaro, nina imani mtakisaidia kuelewa mambo muhimu ya kufanya kwa faida ya mikoa hiyo na taifa kwa ujumla, pia kujenga umoja wa kitaifa na kuepuka utengano maana tunakoelekea ss kuna siku watu watataka kujitenga na kuunda taifa lao au jamii fulani ya watanzania kuonekana ya wanaojikweza kisha tukabaguana waziwazi.

Tukisaidie CCM kirudi kuwa chama chakitaifa hata kama kuna vyama vingine.

(Siku nyingine tutashauri vyama vingine niini cha kufanya ili vijenge sura ya kitaifa
 
Tuku bize kukifuta ccm, bahati mbaya kanda ya ziwa wamepiga kura kikabila, basi hata Arusha nao ni vema wakaichukia ccm. Acha nchi igawanyike halafu tuone nani watafanikiwa kimaisha, kati ya wale wapenda mabadiliko na wale waoga wa mabadiliko.
Ukianza kutumia akili zako za kichwa niambie...umeandika pumba tupu
 
Tuku bize kukifuta ccm, bahati mbaya kanda ya ziwa wamepiga kura kikabila, basi hata Arusha nao ni vema wakaichukia ccm. Acha nchi igawanyike halafu tuone nani watafanikiwa kimaisha, kati ya wale wapenda mabadiliko na wale waoga wa mabadiliko.


Injili ya ukanda na ukabila ni injili ya mpuuzi siku zote,mimba za aina hii huzaa chuki! Hufai kuwa mtanzania.
 
Tuku bize kukifuta ccm, bahati mbaya kanda ya ziwa wamepiga kura kikabila, basi hata Arusha nao ni vema wakaichukia ccm. Acha nchi igawanyike halafu tuone nani watafanikiwa kimaisha, kati ya wale wapenda mabadiliko na wale waoga wa mabadiliko.

Hivi na wewe umechangia nini?
 
Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro na hata dar es salaam wanajua kwamba ccm ni ile ile hivyo hawakutaka kudanganyika na ahadi kibao, wamefanya kile ambacho kizazi chao hakitawalaumu
 
CCM Imeoza kila upande, hakirekebishiki
Lakini kwa ushauri wakiona wanaelemewa kwenye uchaguzi wasitumie mbinu chafu za UDINI,UKANDA na siku hizi Ukabila
Waache kutumia ujinga wa wananchi kama mtaji wao
Waache kufru ya kufisidi Watanzania
Waache kutumia vilaza kama Nape kutukana hovyo nk
 
Nafurahi nikiona mabadiliko ya kweli huwa kama Arusha wanavyoifuta ccm maana ni ile ile kama kipindu pindu wameshindwa kikifuta sasa kipo kila mkoa
 
mabadiliko ya kutembea kichwa chini miguu juu.
 
Mimi ni mwarusha naishi Kisongo lakini kwa Arusha naona kabisa watu wengi hawajui hata maana ya uchaguzi, ndo maana nimeamua kupita kuleee.

Kwao Lema ndo mtu wa maana kuwaletea maendeleo wakati hana issue, kila siku ni maandamano, na wao ni kufuata mkumbo tuuu na kupigwa na police.

CHAGUA MONABAN BHANA ARUSHA TUPATE MAENDELEO.
 
Arusha ata mfanye nini ccm njooni na marais wote wabunge wote Wa ccm monabana hawezi pata ata robo kula
 
Ni rahisi ngamia kupita tundu la sindano kuliko ccm kushinda Arusha
 
Na mkifanya jaribio lolote la wizi wakura ndio mtajuwa wamasai zile sime zao zinakazi gani ccm haitapata kura 20%
 
Arusha wanachuki zao wazijuwazo wenyewe tangu zama za Nyerere na akina Mtei
 
Mleta Mada mie nikuulize swali, je unapenda tuwe na chama kimoja tu nchi nzima na kwamba ccm tu kishinde majimbo yote nji nzima?? kama sivyo basi nawe toa ushauri utakaokiwezesha CHADEMA kupata walao majimbo mawili matatu hapo kanda ya kati hususani kwetu hapa dodoma. hoja nyepesi sana kutaka eti kwakua kajitokeza magufuli anayetekeleza ilani ya CHADEMA basi tufute vyama vingine
 
Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro na hata dar es salaam wanajua kwamba ccm ni ile ile hivyo hawakutaka kudanganyika na ahadi kibao, wamefanya kile ambacho kizazi chao hakitawalaumu

Hata uchaguzi hukufuatilia...ccm wameshinda mkoa wa mbeya na morgoro.
Cdm mbeya, walishinda tukuyu na mbeya mjini
 
Mleta Mada mie nikuulize swali, je unapenda tuwe na chama kimoja tu nchi nzima na kwamba ccm tu kishinde majimbo yote nji nzima?? kama sivyo basi nawe toa ushauri utakaokiwezesha CHADEMA kupata walao majimbo mawili matatu hapo kanda ya kati hususani kwetu phapa dodoma. hoja nyepesi sana kutaka eti kwakua kajitokeza magufuli anayetekeleza ilani ya CHADEMA basi tufute vyama vingine

Rais Dr magufuli hatekelezi ilani ya Chadema anachofanya ni fiscal and leadership discipline ili kuleta ufanisi na kutelekeza ahadi za chama chake na ilani yao.

Kitu cha wazi na rahisi sana kwa wapinzani ni kukosoa makosa ya serikali na chama tawala kwa kua yapo wazi na yanaoenekana ndiyo maana wapinzani duniani kote uwa kwenye offensive wakati wa kampeni, kichekesho hapa Tanzania wapinzani ni wapuuzi wanaongozwa na mpuuzi mmoja maamuzi yake ya kutofikiri yaliwafanya wapinzani wakati wa uchaguzi wakawa defensive Yale yote waliyowananga ccm yakawa kwao wakawa hawana platform yeyote na ccm kitaalam ikicapitalize na rhetoric ya kipinzani kwa kukubali kujikosoa yenyewe, wananchi wakapiga kura ilivyotakiwa na sasa rais anaendeleza na kusimamia kile alichokisema na kujinadi muda wa kampeni.

CCM wamepata lease mpya ya maisha kwa upuuzi wa wapinzani.
 
Hivi na wewe umechangia nini?

Nimechangia kuwa tumeanzia kuifuta ccm kanda ya kasikazini, kadri elimu inavyoongezeka pande zingine za nchi, deleting ccm itaendelea, mbegu zingine zimeshamwagwa mkoa wa morogoro. Ccm have to die ili tz ipate kupona/kuokolewa.
 
Back
Top Bottom