baba yako sio mjinga
anajua anachofanya ni wrong ndo maana alifanya kwa siri
muache atalisahihisha mwenyewe...........
hupaswi kumkasrikia huyo housegirl......unamuonea....
na hupaswi kujifanya wewe ndo mlinzi wa 'heshima ya mama yako'...... utajipa stress za bure
nakushauri utafute boyfriend kama huna......the world is not perfect......soon you will realize that...
angekuwa mwanamke mwingine wa nje kweli ungechukia kiasi hicho?
whats the difference now with the house maid?
watch yourself, utazidi kudharaulika kwa HG ukiendekeza hako karoho kako ka kwanini,
mwisho wa siku wewe utakuwa house maid, na house maid atakuwa mama yako!!!!
GO SLOWLY GIRL! JIFANYE HUONI.. WAKIYAKOROGA, JIFANYE HAUPO!
Kuna mentality moja umeweka kuwa house maid ni mtu duni. Sio sahihi. She is a woman, she deserves to love and to be loved, sawa na wewe sawa na baba yako.
Tukirudi kwenye mada, ni kweli inaweza kukuuma kugundua hilo. Lakini the way ulivyolihandle is totally wrong. Kama mtu mzima hukutakiwa kuparamia jambo emotional kama hilo kwa pupa. Ulipaswa utulie, ujifanye hujui kinachoendelea, with time may be in several days or even weeks akili yako ingetulia alafu ukaamua kwa busara zaidi. May be una mashangazi, bibi au jamaa wengine ambao ungewaeleza kiutaratibu mkashauriana mfanye nini...
Umemkosea baba yako heshima, kama una busara natarajia kesho umuombe msamaha...
Pole sana. Ngoja nikuambie, hata kama mama yako angekuwa hai huwezi kuwa mlinzi wa ndoa yake. Jifunze hilo.
halafu nitakupa ushauri wa wazi. Mwanaume yeyote anahitaji mlinzi mwanamke. Mama yangu alifariki 10 yrs ago na tunatamani hata kumlengesha mshua kwa mwanamke ili aoe na atunzwe. Its a headache kula yake, usafi wa nyumba, afya yake na hata control ya vitu vya nyumbani. Mama yako ameshaondoka, huyo maid hajachukua nafasi ya mama. Na angeweza kuwa mwanamke mwingine asiwe maid. Hata nguo za marehemu zinarithiwa, hicho chumba as long as mama yako hatarudi hapo achana nacho.
sasa ili usiudhike, fanya jitihada za kuondoka nyumbani. Soma shule, faulu, soma boarding, jifunze kurelax around issues na haswa ambazo hauwezi kuzicontrol. Muweke huyo dada karibu ili uweze ku-monitor issues zake na issues za baba. Kubali kwanza, mama hayupo tena na maisha yataendelea.
sijamkosea maana sikwenda chumbani kwake na wala huyu dada nilikuwa namhoji tu alikuwa wapi, sasa nitamwambia namuomba msamaha wa nini?
That's ok... at least kama hukumuuliza moja kwa moja uhusiano na baba. Sasa kama wanavyokyshauri wadau hapa (wengine ni watu wazima sana wanajua impacts zake), kaa mbali na hilo suala. Baba yako anahitaji upendo toka kwa familia na watu wa karibu. Ukilichukulia hili suala kwa hasira utajikuta umemchukia hadi baba na hiyo lazima itajionyesha wazi.
Hii ni dunia, kuna siku na wewe utajikuta umefanya makosa makubwa but baba yako atakuwa anakuonyesha upendo. Usisubiri hadi yatokee ndipo ulipe fadhila. Anza kulipa fadhila sasa kwa kumuonyesha baba upendo mkuu katikati ya makosa yake.
Usimfokee wala kumuuliza house maid chochote tena. Sawa mkuu?...
naomba kwanza nikuulize swali (jibu kwa PM ukipenda mamii! sawa eenh?? lol)you know am angry lakini hii comment yako imenifanya nicheke kidogo, sijamdharau kabisa huyo mdada na yeye kuwa mama yangu well its oky na iwe hivyo since my father is alone now. pia halikuwa lengo langu wajue kama mm nimejua kinachoendelea. ni hasira tu za kibinadamu.
lakini nyinyi wanaume hivi mnajisikiaje kutembea na mabinti wadogo kuliko hata watoto wenu?
naomba kwanza nikuulize swali (jibu kwa PM ukipenda mamii! sawa eenh?? lol)
hivi ulimaanisha nini kujiita romantic eyes?
usiku mwema! nalala mwenzio! naona mbu wa dengue na wa malaria wanashirikiana kuning'ata! lol! dar shida tupu!
kwa sababu nina mijicho mikubwa, and they are NOT romantic ila tu ni jina walilokuwa wanapenda sana watu kunitania ili nikasirike