Niwafanye nini watu hawa?

Ximena

JF-Expert Member
May 17, 2014
641
351
Ndugu zangu hata sijui nianzie wapi maana only God knows how I feel right now.

Na waliosema siku njema huonekana asubuhi hawakukosea maana siku nzima ya leo sijui ndo niseme jana nimeshinda na majonzi little did I know kuwa majonzi makubwa zaidi yanakuja.

This night I have just realized that my father is sleeping with our house maid, what hurts me the most is why did he have to do that in his room and its not even a year since my mum passed away?

Na kwa hasira nikaanza kumkaripia huyu dada na nilichoambulia ni kufokewa na baba kuwa nafuata nini vyumbani kwa watu usiku wote huu!

Natamani nifanye kitu kibaya sana lakini namuomba sana Mungu anisimamie nisifanye lolote ambalo nitajutia baadae.

Najua sitaweza kulala usiku huu.

I just have no one to tell this right now thats why I decided to post this here.

Nasubiri asubuhi ifike, lakini najiuliza hiyo asubuhi ikifika nichukue hatua gani?
 
baba yako sio mjinga
anajua anachofanya ni wrong ndo maana alifanya kwa siri

muache atalisahihisha mwenyewe...........

hupaswi kumkasrikia huyo housegirl......unamuonea....

na hupaswi kujifanya wewe ndo mlinzi wa 'heshima ya mama yako'...... utajipa stress za bure

nakushauri utafute boyfriend kama huna......the world is not perfect......soon you will realize that...
 
Kuna mentality moja umeweka kuwa house maid ni mtu duni. Sio sahihi. She is a woman, she deserves to love and to be loved, sawa na wewe sawa na baba yako.
Tukirudi kwenye mada, ni kweli inaweza kukuuma kugundua hilo. Lakini the way ulivyolihandle is totally wrong. Kama mtu mzima hukutakiwa kuparamia jambo emotional kama hilo kwa pupa. Ulipaswa utulie, ujifanye hujui kinachoendelea, with time may be in several days or even weeks akili yako ingetulia alafu ukaamua kwa busara zaidi. May be una mashangazi, bibi au jamaa wengine ambao ungewaeleza kiutaratibu mkashauriana mfanye nini...
Umemkosea baba yako heshima, kama una busara natarajia kesho umuombe msamaha...
 
Do not try to replace your mom...baba yako anahitaji kampani usilazimishe aendelee na huzuni forever..huose girl ni wrong but wewe sio wa kumfokea au kumuumbua
 
Pole sana. Ngoja nikuambie, hata kama mama yako angekuwa hai huwezi kuwa mlinzi wa ndoa yake. Jifunze hilo.

halafu nitakupa ushauri wa wazi. Mwanaume yeyote anahitaji mlinzi mwanamke. Mama yangu alifariki 10 yrs ago na tunatamani hata kumlengesha mshua kwa mwanamke ili aoe na atunzwe. Its a headache kula yake, usafi wa nyumba, afya yake na hata control ya vitu vya nyumbani. Mama yako ameshaondoka, huyo maid hajachukua nafasi ya mama. Na angeweza kuwa mwanamke mwingine asiwe maid. Hata nguo za marehemu zinarithiwa, hicho chumba as long as mama yako hatarudi hapo achana nacho.

sasa ili usiudhike, fanya jitihada za kuondoka nyumbani. Soma shule, faulu, soma boarding, jifunze kurelax around issues na haswa ambazo hauwezi kuzicontrol. Muweke huyo dada karibu ili uweze ku-monitor issues zake na issues za baba. Kubali kwanza, mama hayupo tena na maisha yataendelea.
 
angekuwa mwanamke mwingine wa nje kweli ungechukia kiasi hicho?

whats the difference now with the house maid?

watch yourself, utazidi kudharaulika kwa HG ukiendekeza hako karoho kako ka kwanini,

mwisho wa siku wewe utakuwa house maid, na house maid atakuwa mama yako!!!!

GO SLOWLY GIRL! JIFANYE HUONI.. WAKIYAKOROGA, JIFANYE HAUPO!
 
sijakataa kabisa kuwa baba yangu anahitaji mwenza by tha way umri wake unaruhusu vizuri sana, pia sijamdharau house maid since naishi nae kama mdogo wangu tu.... sasa ya nini kwenda kutembea na binti mdogo? haya basi awe nae ya nini kujiiba mtu mzima kama yeye? si angeweka wazi tu kwan sisi watoto wake tungekataa??
the situation is not the way you think maana sikwenda kumvamia chumbani kwake najua sio heshima kuingia chumbani kwa mzazi bila taarifa
 
baba yako sio mjinga
anajua anachofanya ni wrong ndo maana alifanya kwa siri

muache atalisahihisha mwenyewe...........

hupaswi kumkasrikia huyo housegirl......unamuonea....

na hupaswi kujifanya wewe ndo mlinzi wa 'heshima ya mama yako'...... utajipa stress za bure

nakushauri utafute boyfriend kama huna......the world is not perfect......soon you will realize that...

you said it well the world is not perfect and am not perfect too may be thats why i reacted in that manner in that yes i was wrong but i did not tell the girl that i know you were with my father i was just asking her where she was since i was looking for her and could not see her in her room...i was raised to respect house maids as though they are my own relatives.
 
angekuwa mwanamke mwingine wa nje kweli ungechukia kiasi hicho?

whats the difference now with the house maid?

watch yourself, utazidi kudharaulika kwa HG ukiendekeza hako karoho kako ka kwanini,

mwisho wa siku wewe utakuwa house maid, na house maid atakuwa mama yako!!!!

GO SLOWLY GIRL! JIFANYE HUONI.. WAKIYAKOROGA, JIFANYE HAUPO!

you know am angry lakini hii comment yako imenifanya nicheke kidogo, sijamdharau kabisa huyo mdada na yeye kuwa mama yangu well its oky na iwe hivyo since my father is alone now. pia halikuwa lengo langu wajue kama mm nimejua kinachoendelea. ni hasira tu za kibinadamu.
lakini nyinyi wanaume hivi mnajisikiaje kutembea na mabinti wadogo kuliko hata watoto wenu?
 
Kuna mentality moja umeweka kuwa house maid ni mtu duni. Sio sahihi. She is a woman, she deserves to love and to be loved, sawa na wewe sawa na baba yako.
Tukirudi kwenye mada, ni kweli inaweza kukuuma kugundua hilo. Lakini the way ulivyolihandle is totally wrong. Kama mtu mzima hukutakiwa kuparamia jambo emotional kama hilo kwa pupa. Ulipaswa utulie, ujifanye hujui kinachoendelea, with time may be in several days or even weeks akili yako ingetulia alafu ukaamua kwa busara zaidi. May be una mashangazi, bibi au jamaa wengine ambao ungewaeleza kiutaratibu mkashauriana mfanye nini...
Umemkosea baba yako heshima, kama una busara natarajia kesho umuombe msamaha...

sijamkosea maana sikwenda chumbani kwake na wala huyu dada nilikuwa namhoji tu alikuwa wapi, sasa nitamwambia namuomba msamaha wa nini?
 
Pole sana. Ngoja nikuambie, hata kama mama yako angekuwa hai huwezi kuwa mlinzi wa ndoa yake. Jifunze hilo.

halafu nitakupa ushauri wa wazi. Mwanaume yeyote anahitaji mlinzi mwanamke. Mama yangu alifariki 10 yrs ago na tunatamani hata kumlengesha mshua kwa mwanamke ili aoe na atunzwe. Its a headache kula yake, usafi wa nyumba, afya yake na hata control ya vitu vya nyumbani. Mama yako ameshaondoka, huyo maid hajachukua nafasi ya mama. Na angeweza kuwa mwanamke mwingine asiwe maid. Hata nguo za marehemu zinarithiwa, hicho chumba as long as mama yako hatarudi hapo achana nacho.

sasa ili usiudhike, fanya jitihada za kuondoka nyumbani. Soma shule, faulu, soma boarding, jifunze kurelax around issues na haswa ambazo hauwezi kuzicontrol. Muweke huyo dada karibu ili uweze ku-monitor issues zake na issues za baba. Kubali kwanza, mama hayupo tena na maisha yataendelea.

nashukuru dada yangu, si kwamba napenda kuingilia maisha ya baba yangu napenda awe na furaha ila natamani sana aoe mwanamke ambaye kidogo umri unaruhusu.
 
sijamkosea maana sikwenda chumbani kwake na wala huyu dada nilikuwa namhoji tu alikuwa wapi, sasa nitamwambia namuomba msamaha wa nini?

That's ok... at least kama hukumuuliza moja kwa moja uhusiano na baba. Sasa kama wanavyokyshauri wadau hapa (wengine ni watu wazima sana wanajua impacts zake), kaa mbali na hilo suala. Baba yako anahitaji upendo toka kwa familia na watu wa karibu. Ukilichukulia hili suala kwa hasira utajikuta umemchukia hadi baba na hiyo lazima itajionyesha wazi.
Hii ni dunia, kuna siku na wewe utajikuta umefanya makosa makubwa but baba yako atakuwa anakuonyesha upendo. Usisubiri hadi yatokee ndipo ulipe fadhila. Anza kulipa fadhila sasa kwa kumuonyesha baba upendo mkuu katikati ya makosa yake.

Usimfokee wala kumuuliza house maid chochote tena. Sawa mkuu?...
 
thanx alot, at least i know i wasnt wrong in asking for advice here.
sitauliza chochote
 
you know am angry lakini hii comment yako imenifanya nicheke kidogo, sijamdharau kabisa huyo mdada na yeye kuwa mama yangu well its oky na iwe hivyo since my father is alone now. pia halikuwa lengo langu wajue kama mm nimejua kinachoendelea. ni hasira tu za kibinadamu.
lakini nyinyi wanaume hivi mnajisikiaje kutembea na mabinti wadogo kuliko hata watoto wenu?
naomba kwanza nikuulize swali (jibu kwa PM ukipenda mamii! sawa eenh?? lol)

hivi ulimaanisha nini kujiita romantic eyes?

usiku mwema! nalala mwenzio! naona mbu wa dengue na wa malaria wanashirikiana kuning'ata! lol! dar shida tupu!
 
Last edited by a moderator:
naomba kwanza nikuulize swali (jibu kwa PM ukipenda mamii! sawa eenh?? lol)

hivi ulimaanisha nini kujiita romantic eyes?

usiku mwema! nalala mwenzio! naona mbu wa dengue na wa malaria wanashirikiana kuning'ata! lol! dar shida tupu!

kwa sababu nina mijicho mikubwa, and they are NOT romantic ila tu ni jina walilokuwa wanapenda sana watu kunitania ili nikasirike
 
Hakuna mwanamke mdogo kwa mwanaume ili mladi yuko above 18. My father married a girl who was agemate to his first daughter and this happen to be my moda. Ila kosa ni kwamba inawezekana walianza zamani kabra ya malehemu kufariki. Lakini kama ni baada leave it don't even bother.
 
kwa sababu nina mijicho mikubwa, and they are NOT romantic ila tu ni jina walilokuwa wanapenda sana watu kunitania ili nikasirike

Ooh I'm turned on with big eyes asee, back to the topic, sweetheart better stay away from it, kama wadau walivyokwishasema, don't judge things by the moral sense of right and wrong, baba ana reasons zake maybe in the end utaweza zijua, btw how old is the maid? Ila she is all what papa needs right now...someone by the side of his bed, one more word...walls keep secrets, esp the walls of your father's bedroom just don't go beyond 'em.
 
Jifunze kuwa mtu anayelala na baba yako ni mama pia haijalishi hata km umemzidi umri.

Huwezi kumpangia baba yako mwanamke wa kuoa au kuwa mpenzi wake cha muhimu kuwa kipofu tu au hama nyumbani.
 
Relax unajua Huyo ni mwanaume wapo wanaoweza kuvumilia upweke na wapo wasioweza.sasa usimfanye baba yako kuwa na mawazo zaid.la sivyo atakufa. Mapema kwa stress za ukiwa. anajitambua na anajua nini anataka.pakikucha usimwonyeshe binti kama ulimind just be friendly maana dingi anaweza akaamua kumuoa je utaendelea kupinga?
 
Back
Top Bottom