Kiranja wa Kijiweni
JF-Expert Member
- Mar 9, 2023
- 582
- 1,045
Napenda kutoa mifano hai/halisi kwa lengo la kutoa hamasa na uvumilivu.Soma vizuri boss bandiko langu Sina lengo la kuua mtu na Sina roho hiyo.
Ni kweli Kuna kujisahau..lakini si tuambiane ndo ulete madharau??
Afu ukizungumzia MALI ...nikwambie tu hakuna kitu chochote tunachomiliki Cha kutishia kutoa uhai WA mtu...Sina shida hizo!! nikwambie tu ni Kati ya wale wanaume wabinafsi ,wachoyo,mwingi WA mipango utekelezaji ZERO... Huwa haoni makosa yake siku zote yeye ni malaika baada ya Kuona watoto wangu watakuja kuteseka nilimshawslishi kununua eneo kwa kutoa PESA yangu 90% na ,10% zilizobaki nilimwachia amalizie yeye.. na Bado Ada za watoto tunalipa pamoja na baadhi ya vitu vingine nanunua,sometimes Hadi matibabu ya watoto, wadada WA kazi nalipa mwenyewe..na Bado akikwama Mahali namsapoti... Haya unaongelea MALI GANI HAPO MKUU? Mambo ni mengi muda machache..!!
Tukio kama hili limetukumba Familia yetu.
Mimi ni mmoja ya Watoto sita kwa mama yetu ambaye ni mke mkubwa.
Enzi hizo Usukumani (Kahama) au hadisasa mwanaume akiwa na Ng'ombe ni fahari kubwa na jamii inamu term kama mtu aliyefanikiwa maishani.
Ni mtoto wa pili kati ya hao sita na wote tupo hai, Asante Mungu.
Mama yetu alipitia kipindi kigumu sana katika malezi yetu, Bibi mzaa mama RIP alimshauri asijaribu kuondoka kwenye Familia yake mbali apambane atulee na tupate elimu.
Mama ametufanya wote tukapata elimu, Brother (Mining Engineering by Professional) amejiajiri anamiliki maduka makubwa mjini DSM, ana mjengo Kigamboni safii kabisa.
Mimi second born nina kazi yangu safi Mkoani Dodoma tena ni moja ya Management team katika Taasisi ninayofanyia kazi at below 30YRS tu.
Third born ni a boy, ni Mining Engineering by Professional amejiajiri anafunga na analima mkoani Geita, dogo below 27 YRS ana minimum mtaji wa 200M.
Fourth born ni a boy, ni a Secondary Teacher by professional, yupo Handeni Tanga ana ajira yake safi serikalini.
Watano na wa mwisho bado wapo shule.
Tumekua tukiona mama ananyanyapaliwa, chozi la Mama limetupa Baraka na Neema sisi watoto wake.
Tunamshukuru tumeweza kujitegemea na tunashirikiana.
Mama angelikata tamaa may be tugelikuwa machokoraa, tugekuwa vijana wabaya.
Sipo hapa kujisifu natoa ushauri usijaribu kuacha watoto wako Dada yangu pambana hadi mwisho Mungu atakulipia chozi lako.